Seminari
Kitengo cha 28: Siku ya 2, Mormoni 1–2


Kitengo cha 28: Siku ya 2

Mormoni 1–2

Utangulizi

Ingawa Mormoni aliishi wakati wa uovu mkubwa, alichagua kuwa mwaminifu. Kwa sababu ya uaminifu wake, aliitwa atunze kumbukumbu za Wanefi. Alipokuwa na umri wa miaka 15, Mormoni “alitembelewa na Bwana, na kuonja na kujua uzuri wa Yesu.”(Mormoni 1:15). Katika mwaka huo huo, Wanefi walimteua Mormoni kuongoza majeshi yao (ona Mormoni 2:1). Alitaka sana kuwasaidia Wanefi kutubu, lakini kwa sababu ya uasi wao wa makusudi, alikatazwa na Bwana kuwahubiria. Wanefi walipoteza karama ya Roho Mtakatifu na karama zingine za Mungu na waliachwa kwa uwezo wao wenyewe walipokuwa wanapigana na Walamani.

Mormoni 1:1–5

Mormoni anapewa umiliki wa kumbukumbu tukufu

Ni baadhi gani ya maneno ungependa watu watumie wanapokuelezea?

Je, umewahi kuelezwa kama Mmormoni? Inamaanisha nini kwako kuelezwa na mtu kama Mmormoni?

Rais Gordon B. Hinckley alizungumza juu ya jina la utaniMmormoni ambalo watu wengine hutumia wanapowataja waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho:

Picha
Rais Gordon B. Hinckley

“Ingawa wakati mwingine mimi hujuta kwamba watu hawaliiti kanisa hili kwa jina lake sahihi, ninafurahi kuwa jina la utani wanalolitumia ni moja la heshima kuu lililoletwa na mtu wa sifa na kitabu kinachotoa ushuhuda usiolinganishwa kumhusu Mkombozi wa dunia.

Mtu yeyote ambaye huja kumjua Mormoni, kupitia kwa kusoma na kuyatafakari maneno yake, mtu yeyote asomaye dafina hii ya thamani ya historia iliyokusanywa na kuhifadhiwa naye, atakuja kujua kuwa Mormoni si neno la dharau, bali linawakilisha wema mkuu —huo wema ambao ni wa Mungu. ” (“Mormoni Should Mean ‘More Good,’” Ensign, Nov. 1990, 52–53).

Mormoni, nabii, alizaliwa wakati karibu kila mtu nchini alikuwa anaishi katika uovu. Wakati huu nabii aliyeitwa Amaroni aliamuriwa kuficha rekodi zote tukufu (ona 4 Nefi 1:47–49). Amaroni alimtembelea Moroni aliyekuwa kijana wa umri wa miaka 10 wakati huo na kumpa maelezo kuhusu jukumu lake kwenye rekodi katika siku zake za usoni. Soma Mormoni 1:2, na utafute maneno na vishazi Amaroni alitumia ili kumwelezea kijana Mormoni.

Neno moja Amaroni alitumia kumwelezea Mormoni lilikuwa heshima.Neno heshima linamaanisha msikivu, mnyenyekevu, mwenye haki, ama uungu. Unaweza kuamua kuandika maelezo haya pembeni mwa maandiko yako. Ni mada gani ama hali gani za maisha unadhani unapaswa kuwa msikivu? Ni muhimu kuelewa kwamba watu wasikivu wanaweza kuwa na furaha na kucheka, lakini wanaelewa wakati ufaao wa kuwa na bashasha na wakati ufaao wa kuwa makini zaidi.

Amaroni pia alimweleza Mormoni kama kuwa “mwepesi wa kusoma” (Mormoni 1:2). Unafikiri inamaanisha nini kuwa mwepesi wa kusoma? Mzee David A. Bednar wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alieleza kwamba neno soma limetumiwa katika maandiko kwa njia mbili:

“Karama ya kiroho ambayo inaonekana kuwa rahisi na pengine kutothaminiwa— uwezo wa kuwa ‘mwepesi wa kusoma’ (Mormoni 1:2)— ni muhimu kabisa kwa ajili yako na kwa ajili yangu katika dunia ambapo tunaishi sasa na ambapo tutaendelea kuishi. …

“Tafadhali zingatia thamani ya karama hii muhimu ya kiroho. Kama linavyotumiwa katika maandiko, neno soma lina matumizi mawili ya msingi. Maana moja huaashiria ‘kutazama’ ama ‘kuona’ ama ‘kutambua’ — kama tunavyojifunza katika Isaya 42:20. …

“Maana ya pili ya neno somahupendekeza ‘kutii’ ama ‘kushika’— kama ilivyowazi katika [ Mafundisho na Maagano 54:6]. 

“Hivyo basi wakati tuko wepesi kusoma, tunatazama mara moja ama tunatambua na kutii. Vipengele hivi viwili vya msingi—kuona na kutii—vina muhimu katika kuwa wepesi wa kusoma. Na nabii Mormoni ni mfano mzuri wa utumizi wa karama hii” (“Quick to Observe,” Ensign, Dec. 2006, 31–32).

  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika mawazo yako kuhusu jinsi hulka na tabia hii ya kuwa mwepesi kusoma inaweza kukusaidia katika maisha yako ya kila siku.

Soma Mormoni 1:3–5, na utambue ushauri wa Amaroni kwake Mormoni. Hulka na tabia ya Mormoni ya kuwa mtulivu na mwepesi wa kusoma zinawezaje kumsaidia katika majukumu haya?

Mormoni 1:6–19

Mormoni akatazwa na Bwana kuhubiri kwa sababu ya uasi wa watu wa kimakusudi

Picha
Mormoni

Je, umewahi kupoteza kitu cha thamani sana? Akiwa bado kwenye ujana wake, Mormoni alishuhudia vita kadhaa kati ya Wanefi na Walamani na uenezi wa uovu mkubwa nchini (ona Mormoni 1:6–13). Kwa sababu uovu wa Wanefi ulikuwa mkubwa sana, Mormoni alirekodi kwamba walipoteza karama nyingi za thamani kutoka kwa Bwana.

  1. Chora safu mbili katika shajara yako ya kujifunza maandiko. Ita safu ya kwanza “Karama Wanefi Walipoteza.” Soma Mormoni 1:13–14, 18, na utafute ni karama gani Bwana alichukua kutoka kwa Wanefi. Andika uliyopata katika safu ya kwanza. Ita safu ya pili “Sababu ya Bwana Kuchukua Karama Zake.” SomaMormoni 1:14, 16–17, 19, na utafute sababu za Bwana kuchukua karama Zake kutoka kwa Wanefi. Andika yale uliyoyapata kwenye safu ya pili.

Kutoka kwa mistari hii tunaweza kujifunza kwamba uovu na kutoamini huzuia karama za Bwana na ushawishi wa Roho Mtakatifu. Ingawa uasi wa Wanefi ulikuwa wa hali ya juu sana, kanuni hii inatumika pia kwetu kibinafsi tunapokosa kutii amri za Mungu.

Ikiwa ungekuwa unaishi wakati wa Mormoni, ni karama zipi za Mungu zilizotajwa katika Mormoni 1:13–14, 18 ungejuta kupoteza?

Soma Mormoni 1:15, na utafute kile ambacho Mormoni alikuwa anapitia wakati Wanefi wengine wote walikuwa wakipoteza karama ya Roho Mtakatifu na karama zingine za Mungu. Je, unafikiri Mormoni aliwezaje kuwa na matukio ya kiroho hata ingawa alikuwa miongoni mwa uovu mwingi?

Mormoni 2:1–15

Mormoni awaongoza majeshi ya Kinefi na kuomboleza juu ya uovu wao.

Zingatia tukio lifuatalo: Mwanaume mwenye umri wa miaka 30 anaishi nyumbani na wazazi wake na kuchagua kutotafuta ajira. Badala yake, anategemea kazi ya wazazi wake na kupoteza wakati wake katika shughuli zisizosaidia kama vile kutumia wingi wa wakati wake akicheza michezo ya video. Linganisha tukio hili na maelezo ya kijana Mormoni unaposoma Mormoni 2.

SomaMormoni 2:1–2, na utafute ni jukumu gani Mormoni alipewa na alikuwa na umri gani alipolipokea.

Si muda mrefu kufuatia kuteuliwa kwa Mormoni kama kiongozi wa majeshi ya Wanefi, jeshi la Walamani liliwashambulia Wanefi na ukali mkubwa hadi kwamba Wanefi waliogopa na kukimbia Walamani waliwafukuza kutoka jiji moja hadi lingine hadi Wanefi walipokusanyika mahali pamoja. Hatimaye, jeshi la Mormoni liliwashinda Walamani na kuwafanya watoroke (ona Mormoni 2:3–9).

  1. Soma Mormoni 2:10–15, na utafute hali ya kiroho ya Wanefi baada ya vita hivi. Kisha jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Kwa nini Wanefi walikuwa wakihuzunika?

    2. Kulingana na Mormoni 2:14, ni vipi Mormoni alijua kwamba huzuni wao haukuwa ishara ya toba ya kweli?

    3. Ni tofauti gani unaweza kuona katika Mormoni 2:13–14 kati ya wale waliohuzunika hadi kwenye toba na wale ambao huzuni yao ilielekeza katika hukumu (kukatizwa kwa maendeleo yao)?

Mistari hii inafundisha kwamba ikiwa huzuni yetu kwa ajili ya dhambi inaelekeza hadi toba, itatuongoza kumjia Kristo kwa moyo mnyenyekevu.Inaonyesha pia kanuni kwamba huzuni pekee kwa ajili ya matokeo ya dhambi huelekeza kwa hukumu (ama kukatizwa kwa maendeleo yetu kuelekea uzima wa milele).

  1. Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Ni kwa jinsi gani mtu ambaye ametenda dhambi anaweza kuonyesha huzuni ya kidunia—aina ya huzuni ambayo huelekeza kwa hukumu?

    2. Ni kwa jinsi gani mtu ambaye ametenda dhambi anaweza kuonyesha aina hii ya huzuni inayoelekeza kwenye toba?

Tafakari jinsi wewe hutenda wakati umetambua kuwa umefanya makosa au umetenda dhambi. Ukimjia Mwokozi na moyo mnyenyekevu na utubu, unaweza kupata amani na kupatanishwa na Mungu.

Mormoni 2:16–29

Mormoni anapokea mabamba na anaandika rekodi ya uovu wa watu wake.

Vita na Walamani vilipoendelea, Mormoni alijikuta karibu na kilima ambako Amaroni alikuwa ameficha kumbukumbu za Wanefi. Alitoa mabamba ya Nefi na kuanza kuandika kile alichokuwa ameona miongoni mwa watu tangu alipokuwa mtoto (ona Mormoni 2:16–18). Soma Mormoni 2:18–19, na uweke alama kwa baadhi ya vishazi vinavyoeleza hali ya kiroho ambayo Mormoni alilelewa.

Kutoka yale uliyojifunza kuhusu Mormoni, kwa nini unadhani alikuwa na uhakika kwamba “angeinuliwa juu katika siku za mwisho”? (Mormoni 2:19). (Katika muktadha huu, “kuinuliwa juu katika siku za mwisho” kunamaanisha kuinuliwa —kufufuka na mwili wa kiselestia na kuletwa katika uwepo wa Mungu kubaki Naye milele.)

Maisha ya Mormoni ni ushuhuda kwamba tunaweza kuchagua kuishi tukiwa wenye haki hata katika jamii yenye uovu.

Zingatia ushauri ufuatao: “Una wajibu kwa ajili ya chaguo unazofanya. Mungu anakujali na atakusaidia kufanya chaguo nzuri, hata ikiwa familia yako na marafiki wanatumia wakala wao kwa njia ambazo sio nzuri. Kuwa na ujasiri wa kimaadili wa kusimama imara katika kutii mapenzi ya Mungu, hata ikiwa unalazimika kusimama peke yako. Unapofanya hivi, unatoa mfano kwa wengine kufuata” (For the Strength of Youth [booklet, 2011], 2).

  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika kuhusu wakati ulipoona rafiki ama mwana familia akisimama imara katika kutii mapenzi ya Mungu hata wakati wengine hawakuwa wanatii. Pia andika fikra zako kuhusu jinsi mfano wa mtu huyo na mfano wa Mormoni unakusaidia wewe.

Wito wa Wasichana ni “Simama katika Ukweli na Haki.” Bila kujali kama wewe ni msichana ama mvulana, fikiria juu ya sehemu maalum ya maisha yako ambapo unaweza kujitahidi zaidi kusimama kwa kile kilicho cha haki. Bwana atakusaidia unapojitahidi kusimama kwa kile kilicho cha haki hata wakati wengine waliokaribu nawe hawafanyi hivyo.

  1. Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza Mormoni 1–2 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningetaka kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha