Seminari
Kitengo cha 1: Siku ya 3, Ukurasa wa Jina, Utangulizi, na Ushuhuda wa Mashahidi


Kitengo cha 1: Siku ya 3

Ukurasa wa Jina, Utangulizi, na Ushuhuda wa Mashahidi

Utangulizi

Fikiria kuwa rafiki alikuuliza kwa nini washiriki wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho wanahitaji Kitabu cha Mormoni kama tayari tuna Bibilia. (Pengine tayari umekuwa na uzoefu huu!) Ungemwambia nini rafiki yako?

Kitabu cha Mormoni kinaanza na ukurasa wa jina, na utangulizi zinazo elezea madhumuni ya kitabu hiki kitakatifu, pamoja na kinachoweza kufanyia ushuhuda wetu na uhusiano na Mungu. Kurasa za kwanza za Kitabu cha Mormoni pia zina ushuhuda wa mashahidi ambao waliona mabamba ya dhahabu ambako kitabu kilitafsiriwa na wakatoa ushuhuda wa chanzo chake kitukufu.

Unapokamilisha somo hili, fikiria kuhusu jinsi unaweza kupokea zaidi kutoka kwa kujifunza kwako Kitabu cha Mormoni mwaka huu na jinsi Kitabu cha Mormoni kinaweza kukusaidia kukuza ushuhuda mkuu wa Mwokozi Yesu Kristo na injili Yake rejesho.

Ukurasa wa Jina

Picha
Joseph Smith na mabamba

Nabii Joseph Smith alieleza kuwa nabii wa kale Moroni alijumuisha ukurasa wa jina wa Kitabu cha Mormoni katika mabamba ya dhahabu: “ Ukurasa wa jina wa Kitabu cha Mormoni ni tafsiri halisi, iliochukuliwa kutoka kurasa ya mwisho kabisa, katika mkono wa kulia wa mkusanyiko au kitabu cha mabamba, ambacho kina rekodi ambayo imetafsiriwa, na huo ukurasa wa jina kwa njia yoyote ile si utunzi wa kisasa, ama wangu au wa binadamu mwingine yeyote ambaye ameishi ama anaishi katika uzao huu” (Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith [2007], 60–61).

Unaposoma aya ya kwanza kwenye ukurasa wa jina, tafuta maneno na vishazi ambavyo Moroni alitumia kushuhudia juu ya kuhusika kwa Bwana katika kuja kwa Kitabu cha Mormoni.

  1. Katika jarida lako la masomo ya maandiko, eleza kwa nini ni muhimu kwako kujua jinsi Bwana alivyohusika katika uandishi na utafsiri wa Kitabu cha Mormoni.

Unaposoma aya ya pili kwenye ukurasa wa jina, tafuta ni yapi malengo matatu ambayo Moroni alitoa ya kuandikwa kwa Kitabu cha Mormoni. Unaweza kutaka kuyawekea alama haya katika maandiko yako. “Nyumba ya Israeli” inarejea wale ambao ni wa uzazi wa Yakobu pamoja na wale ambao ni washiriki wa agano wa Kanisa la Bwana (Ona Kamusi ya Bibilia, Israeli). Zaidi ya hayo, Kishazi “ Wayahudi na Wayunani” inajumuisha watoto wote wa Baba wa Mbinguni. Katika aya ya pili, fanya ujumbe wa ukurasa wa jina uwe wa kibinafsi kwa kubadilisha jina lako na “ sazo la Nyumba ya Israeli” na “Wayahudi na Wayunani”

  1. Katika jarida lako la masomo ya maandiko, eleza jinsi kujua madhumuni haya ya Kitabu cha Mormoni kunakusaidia kuelewa umuhimu wake.

Rais Exra Taft Benson alisema yafuatayo kuhusu “madhumuni makuu” ama lengo la Kitabu cha Mormoni:

“Madhumuni makuu ya Kitabu cha Mormoni, kama ilivyoandikwa katika ukurasa wake wa jina, ni ‘kuwathibitishia Wayahudi na Wayunani kwamba Yesu ndiye Kristo, Mungu wa milele, anayejidhihirisha kwa mataifa yote”

“Mtafutaji wa ukweli mwaminifu anaweza kupata ushuhuda kwamba Yesu ndiye Kristo kama kwa maombi atatafakari maneno ya maongozi ya Kitabu cha Mormoni.

“Zaidi ya nusu ya aya zote katika Kitabu cha Mormoni zinamtaja Bwana wetu. Aina fulani ya jina ya Kristo imetajwa mara nyingi zaidi katika kila mstari katika Kitabu cha Mormoni kuliko hata katika Agano Jipya (“Come unto Christ,” Ensign, Nov. 1987, 83).

Kama ukurasa wake wa jina unavyotangaza, Kitabu cha Mormoni ni ushuhuda mwingine wa Yesu Kristo Unapojifunza Kitabu cha Mormoni mwaka huu,zingatia yale unayojifunza kuhusu Yesu Kristo kisha uliza Baba wa Mbinguni katika maombi kuthibitisha yale unajifunza kupitia uwezo wa Roho Mtakatifu.

Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni

Je, umewahi fikiria jinsi teo katika daraja au jengo linaweza kubaki bila kuanguka bila mihimili chini yake? Tao linapojengwa, pande mbili hujengwa kwa mihimili ya kuzishikilia. Nafasi juu ya teo hupimwa kwa makini, na jiwe la kiungo la tao hukatwa ili ingie barabara. Jiwe la kiungo la teo likiwekwa, teo husimama bila mihimili. Fikiria ni nini kingetokea kwa teo kama jiwe la kiungo lingetolewa.

Picha
tao

Fungua utangulizi wa Kitabu cha Mormoni kisha usome aya ya sita, inayoanza “Kuhusu maandishi haya …” Unaposoma aya hii, tafuta kanuni tatu muhimu ambazo Nabii Joseph Smith alifundisha kuhusu Kitabu cha Mormoni.

Rais Ezra Taft Benson alieleza zaidi kuhusu jinsi Kitabu cha Mormoni huwa kama jiwe la kiungo la teo la dini yetu. Unaposoma nukuu, weka mstari kwenye vishazi ama kauli zinazoweza kukusaidia kuelezea mtu mwingine jukumu la msingi ambalo Kitabu cha Mormoni kinatimiza katika dini yetu.

“Kuna njia tatu ambazo Kitabu cha Mormoni ni jiwe la kiungo la tao la dini yetu. Ni jiwe la kiungo la teo katika ushahidi wetu wa Kristo. Ni jiwe la kiungo la teo la mafundisho yetu. Ni jiwe la kiungo la teo la ushuhuda wetu.

“Kitabu cha Mormoni ni jiwe la kiungo la tao katika ushahidi wetu wa Yesu Kristo, ambaye Yeye mwenyewe ndiye jiwe la pembeni la kila kitu tunachofanya. Hushuhudia uasili Wake kwa uwezo na uwazi. …

“Bwana Mwenyewe amenena kwamba Kitabu cha Mormoni kina “utimilifu wa injili ya Yesu Kristo’ ( M&M 20:9). Hii haimaanishi kina kila mafunzo, kila mafundisho ambayo yameshawahi kufunuliwa. Bali, inamaanisha kwamba katika Kitabu cha Mormoni tutapata utimilifu wa yale mafundisho yanayohitajika kwa wokovu wetu. Na yanafunzwa kwa uwazi na urahisi ili kwamba hata watoto waweza kujifunza njia za wokovu na kuinuliwa. …

“Mwishowe, Kitabu cha Mormoni ni jiwe la kiungo la tao la ushuhuda. Kama vile tao inavyobomoka jiwe la kiungo la tao likiondolewa, vivyo hivyo Kanisa lote litasimama au kuanguka na ukweli wa Kitabu cha Mormoni. Adui wa Kanisa wanaelewa hii kabisa. Kwa sababu hiyo wao hujitahidi kabisa kujaribu kukikanusha Kitabu cha Mormoni, kwa sababu kama kinaweza kukoseshwa thamani, Nabii Joseph Smith anaenda nayo. Hivyo pia madai yetu ya funguo za ukuhani, na ufunuo, na kanisa la urejesho. Lakini vile vile, kama Kitabu cha Mormoni ni cha Kweli —na mamilioni sasa wameshuhudia kuwa wanaushuhuda wa Roho kuwa hasa ni cha kweli —basi mtu ni lazima akubali madai ya Urejesho na yale yote yanayo kuja nayo” (“The Book of Mormon—Keystone of Our Religion,” Ensign, Nov. 1986, 5–6).

  1. Soma aya ya nane ya utangulizi wa Kitabu cha Mormoni, inayoanza “ Tunawakaribisha watu wote kila mahali … ,” na utabue jinsi unaweza kujua Kitabu cha Mormoni ni cha kweli. Baada ya kusoma aya, kamilisha sentensi ifuatayo katika jarida lako la masomo ya maandiko: Tunaposoma, tafakari, na kuomba, Roho Mtakatifu ata …

Kama vile jiwe la kiungo la tao linahimili mawe hayo mengine katika tao, ushuhuda wa Kitabu cha Mormoni unahimili ushuhuda wetu wa kanuni zingine muhimu za injili. Soma aya ya tisa ya utangulizi, inayoanza : “ Wale ambao wanapata ushuhuda huu mtakatifu … ,” kisha weka mstari kweli zingine tatu ambazo utapokea ushuhuda kuhusu unapofuata agizo katika aya ya tisa. Tunaposoma, tunapotafakari, na kuomba juu ya Kitabu cha Maandiko, Roho Mtakatifu atashuhudia kwamba ni kweli, kwamba Yesu ndiye Kristo, kwamba Joseph Smith alikuwa nabii wa Mungu, na kwamba Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho ni ufalme wa Bwana ulimwenguni.

  1. Katika jarida lako la masomo ya maandiko, eleza ni kwa nini Kitabu che Mormoni kinaitwa jiwe la kiungo la tao la dini yetu.

Ushuhuda wa Mashahidi

Fikiria kuwa wewe ni jaji anayejaribu kudhihirisha ukweli kuhusu kilichotendeka katika malumbano kati ya wahusika wawili Ni ya manufaa gani kuwa na shahidi wa kile kiliochotendeka? Ni ya manufaa gani zaidi kuwa na mashahidi wengi?

Picha
Oliver Cowdery

Oliver Cowdery

Picha
David Whitmer

David Whitmer

Picha
Martin Harris

Martin Harris

Bwana aliwaonyesha mashahidi kadha mabamba ya dhahabu ambako Joseph Smith alitafsiri Kitabu cha Mormoni. Soma “ Ushuhuda wa Mashahidi Watatu” kisha weka alama vifungu vitatu au vinne ambavyo walitumia kushuhudia kuhusu mabamba na kukuja kwa Kitabu cha mormoni. Kisha soma “Ushuhuda wa Mashahidi Wanane.” Fahamu tofauti katika matokeo waliopitia vikundi hivi viwili, kama ilivyoonyeshwa kwenye jedwali lifuatalo.

Mashahidi Watatu

Mashahidi Wanane

  1. Malaika aliwaonyesha mabamba, Urimu na Thumimu, dirii, Liahona na upanga wa Laban.

  1. Joseph Smith aliwaonyesha mabamba

  1. Sauti ya Mungu ilitangaza utukufu wa rekodi.

  1. Walishika (inua) mabamba ya dhahabu.

  1. Jibu swali lifuatalo katika jarida lako la masomo ya maandiko: Kwa nini ni muhimu kuwa kulikuwa na mashahidi wengine wa mabamba ya dhahabu pamoja na Joseph Smith?

  2. Katika jarida lako la masomo ya maandiko, andika ushuhuda wako kuhusu Kitabu cha Mormoni, Joseph Smith, na injili ya urejesho ya Yesu Kristo. Kama unahisi bado huna ushuhuda wako mwenyewe, andika kile utafanya ili kukuza ushuhuda wa Kitabu cha Mormoni mwaka huu. Ili kuimarisha ushuhuda, shiriki hisia zako kuhusu kile ulichoandika na mmoja wa wazazi wako au mwana familia mwingine au rafiki.

  1. Andika ifuatayo chini ya kazi ya leo katika jarida lako la masomo ya maandiko

    Nimejifunza somo la “Nyenzo za Utangulizi katika Kitabu cha Mormoni” na kulikamilisha (siku)

    Maswali, fikra na mawazo ya ziada ambazo ningependa kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha