Kitengo cha 6: Siku ya 4
2 Nefi 9–10
Utangulizi
Katika somo lililopita ulijifunza ushuhuda wa Yakobo wa kile Yesu Kristo angetufanyia kupitia Upatanisho Wake. Katika somo hili utakamilisha mafunzo yako ya 2 Nefi 9 na siku ya kwanza ya mahubiri ya Yakobo na kujifunza kile ambacho sharti tufanye ili kupokea baraka za Upatanisho. Yakobo alionya dhidi ya kufanya maamuzi ambayo yanatuelekeza kwenye kutengwa kutoka kwa Mungu, na aliwaalika wote waje kwa Kristo na kuokolewa. Pia utasoma 2 Nefi 10 na ujifunze kile Yakobo aliwaambia watu siku iliyofuata. Yakobo alifunza tena kwamba ingawa Israeli ingetawanyika kwa sababu ya dhambi, Bwana angekumbuka maagano Yake na wao, na Yeye angewakusanya wakati watatubu na kurudi Kwake. Yakobo alisema kwamba kulikuwa “hakuna taifa lingine duniani ambalo lingemsulubu Mungu wao” (2 Nefi 10:3). Alitabiri kwamba Amerika ingekuwa nchi ya uhuru, iliyolindwa dhidi ya mataifa yote, na hakutakuwa na wafalme juu yake. Yakobo alishuhudia kwamba mtu lazima ajiweke chini ya mapenzi ya Mungu na kukumbuka kwamba ni kwa kupitia tu neema ya Mungu wangeokolewa.
2 Nefi 9:28–54
Yakobo alionya juu ya matendo na mitazamo ambayo inatutenganisha na Mungu na anawaalika watu wote kuja kwa Kristo.
Kwa sababu ya Kuanguka na kwa sababu ya dhambi zetu za kibinafsi, kila mmoja wetu anahitaji Mwokozi. Yakobo alishuhudia kwamba kupitia Upatanisho tunafanywa kuwa huru kutokana na madhara ya Kuanguka na tunaweza kushinda dhambi zetu na kupokea uzima wa milele. Yakobo alitumia mfano wa lango na njia kuonyesha haya. Soma 2 Nefi 9:41, na uangalie jinsi Yakobo alivyoelezea njia sharti tutembelee ili tupate uzima wa milele. Tafakari maswali yafuatayo: Unafikiria inamaanisha nini “njooni kwa Bwana”? (Fikiria ikiwa wewe upo katika njia ambayo itakuleta karibu na Mwokozi.) Inamaanisha nini kwako kwamba “njia ya mwanadamu [hadi kwa Mwokozi] ni nyembamba, lakini imenyooka mbele yake”?
Yakobo pia alimwelezea Mwokozi kama “mlinzi wa lango.” Hii ni ishara ya wajibu wa Mwokozi kama mwamuzi wetu. Yeye ndiye anayetoa baraka za Upatanisho Wake kwetu kulingana na mitazamo na matendo yetu. Yakobo pia alitufunza kiustadi zaidi jinsi mitazamo na matendo yetu yanaathiri uwezo wetu wa kuja kwa Mwokozi.
-
Ili kukusaidia kutambua mitazamo, fikira, na matendo ambayo yanatuelekeza kwa Mwokozi, fanya yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
-
Chora mstari kutoka katikati ya ukurasa mzima katika shajara yako ya kujifunza maandiko, na uandike Kujitenganisha Wenyewe na Kristo kwenye upande mmoja na Kuja kwa Kristo upande mwingine.
-
Soma 2 Nefi 9:27–39, na utambue matendo au mitazamo yoyote ambayo Yakobo alionya inaweza kututenganisha na Mwokozi. Tengeneza orodha ya kile umepata ambacho ni cha rafu ya “Kujitenganisha Wenyewe na Kristo” katika shajara yako ya kujifunza maandiko. Pia unaweza kutaka kuweka alama kile umepata katika maandiko yako. (Kumbuka kwamba 2 Nefi 9:28–29ni kifungu cha umahiri wa maandiko. Unaweza kutaka kukiweka alama katika njia ya kipekee ili uweze kukipata siku zijazo.)
-
Chaguo mojawapo wa matendo au mitazamo ambayo uliitambua, na ujibu swali lifuatalo kwenye ukurasa uliotengwa katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Je! Tendo hili au mtazamo huu unaweza kutuzuia kuja kwa Kristo na kupokea baraka kamili za Upatanisho Wake?
-
Kama ziada ya onyo kuhusu matendo na mitazamo ambayo inatupeleka mbali kutoka kwa Bwana, Yakobo alifunza kuhusu matendo na mitazamo ambayo itatusaidia sisi kuja kwa Yesu Kristo. Soma 2 Nefi 9:23, 42, 45–46, 49–52, na tafuta kile Yakobo alifunza kingetuleta sisi kwa Bwana. Orodhesha kile umepata katika safu ya “Kuja wa Kristo” ya chati yako.
-
Kujifundisha 2 Nefi 9:28–54, ulijifunza kanuni: Kwa kuchagua kuja kwa Bwana na kuishi kulingana na mapenzi Yake, tunaweza kupokea baraka kamili za Upatanisho.
-
Ili kukusaidia wewe kutumia kile umejifunza, andika majibu yako ya maswali kati ya mawili au zaidi ya kazi zilizopo chini katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
-
Katika 2 Nefi 9:23 ulisoma kwamba Bwana alituamuru sisi tutubu na kubatizwa. Ingawa unaweza kuwa umebatizwa tayari, je, kufanya upya maagano ya ubatizo kupitia sakramenti kunakusaidia vipi kuja kwa Bwana na kupokea baraka za Upatanisho Wake?
-
Unafikiria inamaanisha nini kuwa na “imani kamili katika yule Mtakatifu wa Israeli” (2 Nefi 9:23)? Ni baadhi ya njia gani wewe kwa sasa unaonyesha imani katika Bwana?
-
Inamaanisha nini “kuacha dhambi zenu” (2 Nefi 9:45)? Ni kitu gani kinachoweza kukusaidia kuacha dhambi zako?
-
Ni baadhi ya mifano gani ya kutumia pesa “kwa yale yasiyo na thamani” wala kushughulikia “kwa yale yasiyotosheleza” (2 Nefi 9:51)? Je! Kuepuka shughuli za uovu au upuuzi kunakusaidia kuja kwa Bwana? Je! Unawezaje kusawazisha vyema jinsi ya kutumia wakati wako katika shughuli tofauti za shule, kujifundisha, Kanisa, burudani, na shughuli za kijamii?
-
Ni baadhi ya njia gani unaweza “mle yale yasiyoangamia” (2 Nefi 9:51)?
-
Yakobo aliwahimiza watu “washukuru” na “waache mioyo yao ishangilie” (2 Nefi 9:52). Kwa nini unafikiria ni muhimu kufuata ushauri huu unapojitahidi kuja kwa Mwokozi?
-
-
Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko jinsi moja au zaidi ya matendo na mitazamo uliyojifunza imekuleta karibu na Mwokozi.
Umahiri wa maandiko—2 Nefi 9:28–29
Je! Unafanya nini ili kutumia vyema nafasi zako za sasa za kielimu? Je! Mipango yako ya siku zijazo kwa masomo yako ni gani?
Soma kauli ifuatayo kutoka kwa Rais Gordon B. Hinckley, na uweke mstari chini ya baraka ambazo zinaweza kuja kutokana na kujifunza: “Unakabiliwa na changamoto kubwa ambazo zipo mbele. Unaingia katika ulimwengu wa mashindano makali. Ni lazima upate elimu yote unayoweza kupata. Bwana ametuelekeza sisi kuhusu umuhimu wa elimu. Inakuhitimisha kwa nafasi kuu sana. Inakupatia uwezo wa kufanya kitu cha maana katika ulimwengu mkuu kwa fursa zilizo mbele yako. Kama unaweza kwenda chuoni na hayo ni matakwa yako, basi fanya hivyo. Ikiwa hauna hamu ya kuhudhuria chuo, basi nenda kwa shule ya ufundi au biashara ili unoe ujuzi wako na uongeze uwezo wako” (“Converts and Young Men,” Ensign, May 1997, 49–50).
Soma 2 Nefi 9:28, na uweke alama kile Yakobo alisema vilikuwa vikwazo vya kujifunza na mtazamo usio sawa.
-
Jibu swali lifuatalo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
-
Je! Unafikiria kauli hii “wanapopata elimu wanafikiria kuwa wana hekima” inamaanisha nini?
-
Kuna hatari gani katika kufikiria tuna hekima kuliko wazazi wetu, askofu wetu au rais wa tawi, nabii, au Baba yetu wa Mbinguni?
-
Soma 2 Nefi 9:29, na utambue kile wewe unahitaji kukumbuka unapotafuta elimu.
-
Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, jibu swali lifuatalo: Je! Kujifunza maandiko kwa bidii kunaweza kusaidia vipi kuishi kulingana na kanuni katika 2 Nefi 9:29?
2 Nefi 10
Yakobo anawatia moyo watu wake kushangilia na kuja kwa Bwana
Katika siku ya pili ya ufunzaji wake, Yakobo tena alishuhudia uwezo wa Bwana wa ukombozi kutoka kwa matokeo ya dhambi. Yakobo pia alifundisha watu wake jinsi wanapaswa kupokea toleo la huruma la Upatanisho. Soma 2 Nefi 10:20, 23–25, na uweke alama vishazi ambavyo vinaonyesha kile Yakobo alitufunza tunapaswa kufanya katika kujibu dhabihu ya Mwokozi kwetu.
-
Jibu moja au zaidi ya maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
-
Ukifikiria kile wewe umejifunza kuhusu Mwokozi, kwa nini daima unataka “kumkumbuka yeye” (2 Nefi 10:20)?
-
Kwa nini unahisi kwamba kuweka kando au kutubu kitu fulani unachofanya kimakosa kingeonyesha shukrani zako na upendo wa Mwokozi?
-
Ni kitu gani umejifunza kuhusu Mwokozi ambacho hukusaidia kuhisi matumaini kuliko “kuinamisha” kichwa chako kwa kuvunjika moyo?
-
Kishazi muhimu katika sura hii ni “jipatanisheni na nia ya Mungu” (2 Nefi 10:24). Inamaanisha kwamba tunapaswa kuanzisha tena uhusiano wa karibu na Bwana ambao kwao sisi ni watiifu na tuko katika uwiano na mapenzi Yake. Rejea maandiko yoyote ulioweka alama katika 2 Nefi 9–10. Tafuta mwongozo wa Roho Mtakatifu unapotathimini kitu unachoweza kufanya ili kujipatanisha wenyewe na mapenzi ya Mungu.
-
Andika yafuatayo katika sehemu ya chini ya kazi za leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
Nimejifunza 2 Nefi 9–10 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).
Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningependa kushiriki na mwalimu wangu: