Seminari
Kitengo cha 15: Siku ya 3, Alma 6–7


Kitengo cha 15: Siku ya 3

Alma 6–7

Utangulizi

Baada ya kufundisha watu katika Zarahemla na kuweka Kanisa vilivyo, Alma alikwenda katika mji wa Gideoni. Alikuta wenyeji pale wakiwa waaminifu zaidi kuliko wale wa Zarahemla walivyokuwa. Kwa hiyo, aliwahimiza watu katika Gideoni kuendelea kumtegemea Bwana na kutafuta kutumia Upatanisho Wake katika maisha yao. Ushuhuda wa Alma wa Yesu Kristo unaweza kukusaidia kuelewa upana wa Upatanisho wa Yesu Kristo na kukufundisha jinsi ya kupokea baraka za Upatanisho Wake kila siku unapoendelea katika njia ya ufalme wa Mungu.

Alma 6

Alma anaimarisha Kanisa katika Zarahemla na anaenda kuhubiri katika Gideoni

Kamilisha sentensi ifuatayo: Nahudhuria kanisa kwa sababu .

Unapojifunza Alma 6, fikiria kuhusu jinsi kuelewa madhumuni ya mikutano ya kanisa kunaweza kufanya mikutano kuwa na maana zaidi kwenu.

Kabla ya Alma kutoka Zarahemla, aliimarisha Kanisa huko. Read Alma 6:1–4, na utambue vishazi viwili au vitatu vinavyoeleza majukumu ya viongozi wa ukuhani katika Kanisa.

Kanuni muhimu tunayojifunza kutokana na uzoefu wa Alma ni hii: Katika siku zetu, vile vile katika siku za Kitabu cha Mormoni, Kanisa limeundwa kwa maslahi ya watu wote. Soma Alma 6:5–6, na uweke alama kwenye vishazi viwili vifuatavyo: “ili kusikia neno la Mungu” na “waungane katika kufunga na sala kuu kwa niaba ya ustawi wa nafsi ambazo hazikumjua Mungu.” Hivi vishazi vinabaini njia ambazo Kanisa hutoa fursa kwa watu wote kukua na kuwasaidia wengine. Fikiria jinsi washiriki wa Kanisa katika Zarahemla wangekamilisha sentensi uliyokamilisha hapo juu.

  1. Andika mawazo machache katika shajara yako ya kujifunza maandiko jinsi kwenda kanisani kwa sababu zilizoelezwa katika Alma 6:5–6 kunaweza kuleta tofauti katika uzoefu wako kanisani.

Baraka za ushiriki Kanisani zinakusudiwa kwa watoto wote wa Mungu. Mzee Jeffrey R. Holland wa Akidi ya Wale Mitume Kumi na Wawili alieleza:

Picha
(Mzee Jeffrey R. Holland)

Kila mtu huwaombea wamisionari. Na iwe hivyo hata milele. Katika roho hiyo hiyo, tunapaswa pia kuwaombea wale ambao wanaokutana (au ambao wanahitaji kukutana) na wamisionari. Katika Zarahemla, waumini waliagizwa ‘waungane katika kufunga na sala kuu’[Alma 6:6] kwa wale ambao hawakuwa wamejiunga na Kanisa la Mungu. Tunaweza kufanya vivyo hivyo.

“Tunaweza pia kuomba kila siku kwa uzoefu wetu binafsi wa kimisionari. Omba kwamba chini ya usimamizi mtakatifu wa mambo kama hayo, nafasi ya umisionari unayotaka tayari inatayarishwa ndani ya moyo wa mtu anayetamani na kutafuta kile ulichonacho. ‘Kwani bado wako wengi duniani… ambao huzuiliwa kuupata ukweli kwa sababu tu hawajui mahali pa kuupata’ [M&M 123:12]. Omba ili kwamba wapate! Na kisha uwe macho, kwa sababu kuna umati katika maisha yako wanaohisi njaa katika maisha yao, si njaa ya chakula, si kiu cha maji, bali ya kusikia neno la Bwana [ona Amos 8:11]” (“Witnesses unto Me,” Ensign, Mei 2001, 15).

Ili kufuata ushauri wa Mzee Holland, fikiria kuomba kwa Baba wa Mbinguni ili akusaidie kutambua na kutenda juu ya fursa za kimisionari ambazo zinatayarishwa kwa ajili yako. Tafuta fursa za kuwaalika wengine kushiriki baraka unazofurahia kama mshiriki wa Kanisa.

Alma 7:1–13

Alma anafundisha watu wa Gideoni kuhusu Upatanisho wa Yesu Kristo

Fikiria kuwa unafanya mazungumzo kuhusu toba na marafiki ambao ni washiriki hai wa Kanisa Marafiki zako hawadhani kuwa wametenda dhambi yoyote kubwa na wanashangaa jinsi gani wanaweza kweli kupata uzoefu wa nguvu za Upatanisho. Fikiria juu ya kile unachoweza kushiriki na marafiki hawa. Kumbuka mawazo haya unapojifunzaAlma 7:1–13.

Baada ya kuondoka Zarahemla, Alma aliongea na watu katika mji wa Gideoni. Soma Alma 7:3–6 ili kuona ni hali gani ya kiroho ambayo Alma alitumaini kuipata kati ya watu katika Gideoni. Kisha soma Alma 7:17–19 ili kujua kama matumaini ya Alma yalithibitishwa. Katika mistari ifuatayo, elezea hali ya kiroho ya watu wa Gideoni:

Soma Alma 7:7–10, na uangalie tukio ambalo Alma alihisi lilikuwa muhimu zaidi kwa watu kujua kuhusu na kile watu walihitajika kufanya ili kujiandaa kwa ajili yake.

  1. Jibu swali lifuatalo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Kwa nini unafikiri Alma angewaambia watu ambao tayari walikuwa na imani imara (ona Alma 7:17) kwamba walihitaji kutubu ili kujiandaa kwa ajili ya ujio wa Mwokozi? (Ona Warumi 3:23.)

Alma alifundisha watu wa Gideoni kanuni hii muhimu: Yesu Kristo aliteseka ili kutuokoa kutoka kwa dhambi na kifo na kutusaidia kupitia changamoto ya maisha. Soma Alma 7:11–13, na uweke alama katika maandiko yako kwa hali ambazo Mwokozi alikuwa tayari “kubeba” Mwenyewe kwa manufaa yetu.

Ni muhimu kujua kuwa unyonge ni udhaifu, ulemavu, au magonjwa —neno linajumuisha aina nyingi za matatizo. Neno kuwasaidia lina maana kusaidia wakati wa mahitaji au shida. Mzizi wake wa Kilatini unamaana kukimbilia msaada wa mtu, ambayo inaonyesha mapenzi makuu ya Mungu ya kutusaidia.

Karibu na Alma 7:11–13 katika maandiko yako au katika shajara yako ya kujifunza maandiko, ungetaka kuandika maelezo yafuatayo kutoka kwa Mzee Bruce C. Hafen, aliyehudumu kama mshiriki wa Wale Sabini: “Upatanisho sio tu kwa ajili ya wenye dhambi” (“Beauty for Ashes: The Atonement of Jesus Christ,” Ensign, Apr. 1990, 7). (Alma 7:11–13 ni kifungu cha umahiri wa maandiko. Unaweza kutaka kukiweka alama kwa njia tofauti ili uweze kukipata siku zijazo.)

  1. Chati ifuatayo ina maneno kutoka Alma 7:11–13 ambayo inaelezea hali ambazo Mwokozi alibeba juu yake mwenyewe. Chora chati katika shajara yako ya kujifunza maandiko, na kisha uchague baadhi ya maneno haya na uandike mifano ya jinsi wewe au watu unaowajua wamepitia hali hizi. Fikiria kuhusu maana ya Yesu Kristo kuchukua mambo haya juu Yake Mwenyewe.

Maumivu

Mateso

Majaribu

Magonjwa

Kifo

Unyonge

Dhambi

Mzee Jeffrey R. Holland alishiriki ushuhuda ufuatao kwamba Upatanisho unaweza kuinua mizigo yetu kutoka kwetu:

“Je! Unakabiliana na pepo wa ulevi wa —tumbaku au madawa au kamari, au ugonjwa hatari wa kisasa wa picha za ngono? Je! Ndoa yako imo hatarini au mtoto wako yumo hatarini? Je! Umechanganyikiwa na utambulisho wa jinsia au utafutaji wa kijithamini? Je! Wewe—au mtu unayempenda —anakabiliwa na ugonjwa au msononeko au kifo? Hatua zozote unazohitaji kuchukua ili kutatua matatizo haya, njoo kwanza kwa injili ya Yesu Kristo. Amini katika ahadi za mbinguni. Katika suala hilo ushuhuda wa Alma ni ushuhuda wangu: ‘Mimi najua,’ anasema, ‘kwamba wote watakaoweka imani yao katika Mungu watasaidiwa kwa majaribio yao, na taabu zao, na mateso yao’[Alma 36:3].

“Kutegemea utu karimu wa Mungu umo katika kitovu cha injili ambayo Kristo alifundisha. Nashuhudia kwamba Upatanisho wa Mwokozi huinua kutoka kwetu si tu mzigo wa dhambi zetu lakini pia mzigo wa kukatishwa tamaa zetu na huzuni, huzuni zetu nzito na kufa moyo. [ona Alma 7:11–12]. Tangu mwanzo, uaminifu katika msaada huo ulipaswa kutupatia sababu na njia ya kuboresha, motisha ya kutoa mizigo yetu na kuchukua wokovu wetu” (“Broken Things to Mend,” Ensign or Liahona, May 2006, 70–71).

  1. Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko kuhusu hisia zako kwa Yesu Kristo na yale amekufanyia kwa njia ya Upatanisho. Kisha jibu moja au zote mbili za seti zifuatazo za maswali:

    1. Ni lini Upatanisho ulikusaidia katika mojawapo ya njia ambazo Alma alieleza katikaAlma 7:11–13? Jinsi gani Upatanisho ilikusaidia wakati huo?

    2. Jinsi gani ya Upatanisho wa Mwokozi imekusaidia na changamoto unazopitia sasa? Utafanya nini ili kutegemea Upatanisho unapopitia changamoto hii?

Picha
ikoni ya umahiri wa maandiko
Umahiri wa maandiko—Alma 7:11–13

Ilhali Alma 7:11–13 ni kifungu cha umahiri wa maandiko kirefu, kina maneno maalum ambayo yanaweza kukusaidia kukumbuka ukuu na nguvu za Upatanisho katika maisha yako yote. Ili kukusaidia kukariri maneno haya muhimu, andika upya{Alma 7:11–13 kwenye karatasi tofauti, ukiacha nje maneno yanayopatikana katika chati mapema katika somo hili. Soma toleo lako lilioandikwa la andiko hili hadi utakapojaza maneno yaliyokosekana bila kuangalia maandiko yako. Unaweza kutaka kurejea mistari hii kwa siku chache zijazo ili kukusaidia kukumbuka yale Mwokozi anaweza kukufanyia wewe na wengine katika maisha yako yote. Fanya jaribio la umahiri wako wa maandiko kwa Alma 7:11–13kwa kuikariri kwa sauti kwako mwenyewe au kwa mwanafamilia au rafiki au kwa kuuandika katika shajara yako ya kujifunza maandiko.

Picha
Kuu juu ya Yote

Alma 7:14–27

Alma anawahimiza watu kuendelea katika njia ya ufalme wa Mungu

Soma Alma 7:19 ili kukumbuka jinsi Alma alivyoeleza hali ya kiroho ya watu katika Gideoni. Alma alikuwa akifundisha kanuni hii muhimu: Kwa kuishi kanuni za injili, tunafuata njia ya ufalme wa Mungu.(Ufalme wa Mungu ni ufalme wa selestia.) Pekua Alma 7:14–16, na uweke mstari chini ya maneno na vishazi vinavyoonyesha yale tunayohitaji kufanya ili kufuata njia ambayo itatuongoza hata kwa Ufalme wa Mungu. Kisha pekua Alma 7:22–25, na uweke mstari chini ya maneno na vishazi vinavyoonyesha yale tunayohitaji kuwa ili kufuata njia hii.

  1. Chora njia katika shajara yako ya kujifunza maandiko kutoka kona ya chini kushoto mwa ukurasa hadi kwa kona ya juu kulia mwa ukurasa. Andika Maisha ya muda chini ya njia, na uandike Ufalme wa Mungu sehemu ya juu ya njia. Njiani, andika kile unapaswa kufanya na kile unapaswa kuwa ambayo itakuongoza kwa ufalme wa Mungu.

  2. Chagua kitendo kimoja kutoka kwa njia, na uandike jinsi umeona mtuakifanyahaya. Kisha uchague sifa moja kutoka kwa njia, na uandike kuhusu jinsi umeona mtu akiwa hivi. Weka lengo ambalo litakusaidia kuboreka katika maeneo haya mawili ili uweze siku moja kuingia katika ufalme wa Mungu.

Soma Alma 7:27, na uangalie baraka ambazo Alma alijua watu watapewa ikiwa wataendelea katika imani na matendo mema. Kumbuka kwamba unapofuata njia kwa uaminifu inayoelekeza kwa ufalme wa Mungu, unaweza pia kupokea baraka hizi.

  1. Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    NimejifunzaAlma 6–7 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha