Seminari
Kitengo cha 7: Siku ya 3, 2 Nefi 21–24


Kitengo cha 7: Siku ya 3

2 Nefi 21–24

Utangulizi

Mengi ya unabii wa Isaya katika Kitabu cha Mormoni yanahusu siku za mwisho. Alitoa unabii kuhusu Urejesho wa injili, Nabii Joseph Smith, Ujio wa Pili, na maangamizo ya waovu. Aliona mapema kwamba Bwana “atawatwekea mataifa bendera” ili kuwakusanya watu Wake katika siku za mwisho (ona 2 Nefi 21:11–12). Isaya pia alishuhudia kwamba Bwana angepata ushindi juu ya Shetani na kukaribisha Milenia, kipindi cha amani na furaha.

2 Nefi 21:1–4, 10–12

Isaya anaona Urejesho wa injili ya Yesu Kristo katika siku za mwisho

Tua kwa dakika, na ufikirie mwanga ukianza kutokeza mbele yako. Mwanga unakuwa angavu na angavu zaidi. Ghafula mjumbe aliyetumwa kutoka uwepo wa Mungu anasimama mbele yako. Anakuambia kwamba unabii wa kale u karibu kutimia na kwamba wewe utasaidia katika utimilifu wake. Mjibizo, fikira, na maswali yako ya kwanza yangukuwa gani?

Picha
Moroni Anamtokea Joseph Smith katika Chumba Chake

Usiku ambao Moroni alijitokeza kwanza kwa Joseph Smith—Septemba 21, 1823—alinukuu Isaya 11, ambayo pia inapatikana katika 2 Nefi 21. Moroni alimwambia Joseph Smith kwamba unabii katika sura hiyo ulikuwa karibu “kutimia ” (Joseph Smith—Historia 1:40). Unapojifunza unabii huu kutoka kwa Isaya, tafakari juu ya kwa nini Nefi aliuandika kwenye mabamba madogo na pia kwa nini Moroni aliunukuu kwa Joseph Smith.

Nabii Joseph Smith alipokea ufunuo ambao unafafanua maana ya unabii ulioandikwa katika 2 Nefi 21. Wasomi kwa muda mrefu wamevutiwa katika kujaribu kuelewa maana ya ishara zilizotumika katika sura hii. Kitabu cha Mormoni na manabii wa kisasa wametusaidia kuelewa vyema maana yake. Kwa mfano, Isaya alitumia mfano wa mti au mmea. Soma 2 Nefi 21:1, 10, na utambue sehemu mahususi za mti au mmea Isaya alitaja. Kisha usome Mafundisho na Maagano 113:1–6 ili kukusaidia kuelewa kile hizi ishara zinamaanisha. Inaweza kuwa msaada kuandika ufafanuzi wa ishara katika maandiko yako.

Shina la Yese—Yesu Kristo

Chipukizi katika shina la Yese —Mtumishi wa Yesu Kristo

Mzizi wa Yese—Mtu ambaye anashikilia funguo za ukuhani

Fikiria kauli ifuatayo ya Mzee Bruce R. McConkie, ambaye alielezea kwamba “Mzizi wa Yese” na “Chipukizi kutoka shina la Yese” yote yanamlenga Nabii Joseph Smith: “Je, tunakosea tunaposema kwamba nabii aliyetajwa hapa [katika M&M 113:5–6] ni Joseph Smith, ambaye kwake ukuhani ulikuja, ambaye alipokea funguo za ufalme, na ambaye aliinua bendera kwa ajili ya kukusanyika kwa watu wa Bwana katika kipindi chetu? Na yeye si pia ni ‘mtumishi katika mikono ya Kristo, ambaye ni wa sehemu ya uzao wa Yese na vile vile wa Efraimu, au wa nyumba ya Yusufu, ambaye juu yake umewekwa uwezo mwingi’? [M&M 113:3–4]” (Millennial Messiah [1982], 339–40).

Soma 2 Nefi 21:10, 12, na utafute kile Isaya alitoa unabii Bwana angefanya kupitia “mzizi wa Yese” (Joseph Smith). Neno bendera linamaanisha “beramu” ambapo watu hukusanyika.

Mistari hii inafundisha ukweli ufuatao Bwana amerejesha injili Yake na Kanisa Lake kupitia kwa Nabii Joseph Smith na sasa anawakusanya watu Wake katika siku za mwisho.

  1. Jibu swali lifuatalo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Ni kwa jinsi gani Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho ni bendera kwa ulimwengu ?

2 Nefi 21:6–9; 22:1–6

Isaya anaelezea Milenia

Mojawapo wa mada inayojadiliwa sana miongoni mwa Wakristo ni utawala wa milenia wa Mwokozi. Je! Umeshafikiria juu yake sana? Fikiria kwamba rafiki amekuuliza kile unachoamini kuhusu Milenia. Ungesema nini?

Picha
Bila Hasira Yoyote

Isaya alitoa unabii kwamba baada ya Ujio wa Pili wa Mwokozi, kungekuwa na mabadiliko juu ya ulimwengu ambayo yangedumu kwa miaka elfu moja. Tunaita kipindi hiki cha amani Milenia. Soma 2 Nefi 21:6–9, ukitafuta hali gani zitakuwepo juu ya ulimwengu wakati wa Milenia

Kulingana na 2 Nefi 21:9, unabii mmoja kuhusu Milenia ni kwamba “dunia yote itajaa elimu ya Bwana.” Tafakari jinsi utimilifu wa unabii huu utaathiri watu kote ulimwenguni. Soma 2 Nefi 22:1–6, na utambue roho ya ibada ambayo watu watakuwa nayo wakati wa Milenia. Tunawezaje kuendeleza mtazamo huo hivi leo?

Mistari uliyojifunza inafundisha ukweli huu Wakati wa Milenia, duniani itakuwa ni mahali pa amani kwa sababu itakuwa imejaa elimu ya Bwana.Ni hali gani ya Milenia ungependa kuwa nayo katika maisha yako sasa hivi? Tafakari kwa dakika kile ungefanya ili kupokea baadhi ya baraka hizi.

Unaweza kutaka kuimba, kusikiliza, au kusoma “The Lord Is My Light” (Wimbo, no. 89) kushamirisha kujifunza kwako kwa 2 Nefi 22.

2 Nefi 23–24

Isaya anaelezea kuanguka kwa Babeli, kuanguka kwa waovu, na kuanguka kwa Lusiferi

Kama ilivyoandikwa katika 2 Nefi 23–24, Isaya alishutmu uovu wa nyumba ya Israeli na kulinganisha maangamizo ya waovu katika siku za mwisho na maangamizo ya Babeli ya kale. Babeli lilikuwa taifa ovu sana katika siku za Isaya na kutoka hapo limekuja kuashiria uovu wa dunia (ona M&M 133:14).

Jifunze kile Isaya alitoa unabii kingetokea kwa wale waovu katika siku za mwisho kwa kusoma 2 Nefi 23:1, 4–9, 11, 15, 19, na 22.

Isaya pia alifananisha maangamizo ya Babeli ya kale na kuanguka kwa Lusiferi (Shetani) kutoka mbinguni. Alizungumza juu ya Lusiferi kwa istairi kama mfalme wa Babeli, kumaanisha ulimwengu ovu wote. Isaya alitumia kuanguka kwa Lusiferi katika dunia kabla ya kuzaliwa kama onyesho la jinsi waovu wangeshindwa na kuanguka. Jifunze 2 Nefi 24:12–14, na uweke alama vishazi ambavyo vinaangazia ujeuri na kiburi cha Shetani.

Je! Umeona matumizi ya neno hilo Mimi katika mistari hii? Unaweza kutaka kuzungushia Mimikatika maandiko yako. Rais N. Eldon Tanner wa Urais wa Kwanza wakati mmoja alisema kwamba Shetani “alikuwa anajishughulisha na sifa kuliko matokeo; utukufu na sifa zilikuwa ni mwisho wa kila kitu” (“For They Loved the Praise of Men More Than the Praise of God,” Ensign, Nov. 1975, 76).

Pekua 2 Nefi 24:15–16 kwa kile hatimaye kitatokea kwa Shetani na jinsi watu watahisi kumhusu yeye wakati watamwona kwa kile alicho.

Soma kauli ifuatayo ya Rais Ezra Taft Benson: “Katika baraza la maisha kabla ya duniani, ilikuwa ni kiburi kilichomwangusha Lusiferi, ‘mwana wa asubuhi.’ (2 Ne. 24:12–15; ona pia M&M 76:25–27; Musa 4:3.) Lusiferi aliweka mapendekezo yake kushindana na mpango wa Baba kama ulivyotetewa na Yesu Kristo. (Ona Musa 4:1–3.) Alitaka kuheshimiwa juu ya wengine wote. (Ona 2 Ne. 24:13.) Kwa ufupi, nia yake yenye kiburi ilikuwa kumwondoa Mungu kwenye ufalme. (Ona M&M 29:36; 76:28.)” (“Beware of Pride,” Ensign, Mei 1989, 4–5).

Katika 2 Nefi 23:22, tunajifunza kwamba unaweza kuwa na faraja kama wewe ni mwema. Mungu atakurehemu wewe, lakini waovu watangamizwa.

  1. Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Ninaweza kubadilisha nini katika maisha yangu leo ili kuwa mtiifu zaidi?

    2. Ninaweza kuazimia vipi kukaa mtiifu?

Omba nafasi za kushiriki ushuhuda wako kuhusu kweli ulizojifunza katika 2 Nefi 23.

  1. Andika yafuatayo katika sehemu ya chini ya kazi za leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza2 Nefi 21–24 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningependa kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha