Seminari
Kitengo 2: Siku ya 3, 1 Nefi 3–4


Kitengo 2: Siku 3

1 Nefi 3–4

Utangulizi

Bwana alimwamuru Lehi kuwatuma wanawe kurudi Yerusalemu kuchukua mabamba ya shaba kutoka kwa Labani. Ingawa Lamani na Lemueli hawakuona jinsi wangeweza kutimiza hii amri, Nefi alikuwa na imani kwamba Bwana angepatiana njia ambayo kwayo wangetimiza kile Yeye alihitaji. Licha ya masumbuko mengi, Nefi kwa uaminifu alijizatiti katika kufanya kile Bwana aliuliza kutoka kwake. Kama matokeo, aliongozwa na Roho Mtakatifu na kufanikiwa kupata mabamba. Uzoefu wa Nefi unaonyesha kwamba utiifu wa kila mara unatuhitimisha kwa usaidizi wa Bwana katika hali ngumu.

1 Nefi 3:1–9, 19–20

Wana wa Lehi wanarudi Yerusalemu

Umewahi kukabiliwa na hali ngumu na kushangaa jinsi itakavyosuluhishwa? Somo la leo linaweza kusaidia kuimarisha imani na azimio lako la kuwa mtiifu unapopitia hali ngumu. Anza kwa kusoma 1 Nefi 3:1–6, na uweke alama katika maandiko yako amri ambayo Bwana alimpa Lehi ili kutimizwa na wanawe. Pia tambua tofauti kati ya majibu ya Lamani na Lemueli kwa amri ya Bwana kinyume na majibu ya Nefi.

Ili kuelewa ugumu wa kile Bwana ameamuru, ni muhimu kujua kwamba umbali kutoka Yerusalemu mpaka Bahari ya Shamu (Ghuba la Akaba) ni karibu maili 180 kupitia nchi ya joto na ukame, iliyojawa na wezi wengi. Lehi na familia yake walikuwa wamesafiri siku tatu kupitia sehemu hii (ona1 Nefi 2:5–6), na sasa Bwana alikuwa anasema wanawe wanapaswa kurudi Yerusalemu. Soma 1 Nefi 3:7–8, na utambue sababu ambayo Nefi alitoa kwa kuwa radhi kutii amri ya Bwana.

Nefi alishuhudia kuhusu kanuni kuwa ikiwa tutafanya kile Bwana ameamuru, hivyo atatutayarishia njia ya kuitimiza. Unapoendelea kusoma 1 Nefi 3, fikiria jinsi mfano wa Nefi wa ujasiri na azimio unaweza kukuongoza kuwa mtiifu zaidi na kudhihirisha imani kuu katika Bwana. Tilia maanani haswa kwa jinsi Nefi alivyofanya kuhusu changamoto. Ingawa Nefi angeona dhiki wakati yeye na ndugu zake walipojaribu kuchukua yale mabamba ya shaba, aliamua kutonung’unika (ona 1 Nefi 3:6).

Mabamba ya shaba yalikuwa na “maandishi ya Wayahudi” (1 Nefi 3:3), ambayo yalikuwa maandiko yao. Yalikuwa na maandishi mengine na habari ambazo zinapatikana sasa katika Agano la Kale vile vile maandishi mengine ya kinabii. Soma 1 Nefi 3:19–20, na upige mstari chini ya kile kilichokuwa katika bamba za shaba na kuyafanya kuwa muhimu sana kwa familia ya Lehi na uzao wake.

Picha
ikoni ya umahiri wa maandiko
Umahiri wa Maandiko—1 Nephi 3:7

Soma 1 Nefi 3:7 mara tatu (unaweza kubadilisha jinsi unavyoisoma: kwa sauti au kimya). Funga maandiko yako, na ujaribu kuandika majibu kwa maswali yafuatayo bila kuangalia kifungu:

  • Nefi alikuwa akiongea na nani?

  • Nefi aliazimia kufanya nini?

  • Nefi alijua Bwana atafanya nini?

Fungua maandiko yako, na rejea 1 Nefi 3:7 na majibu yako.

Nabii Joseph Smith alisema: “Nilifanya hii kuwa kanuni yangu: Bwana anapoamuru, Tenda” (katika History of the Church, 2:170). Fikiria kuandika taarifa hii katika maandiko yako kando ya 1 Nefi 3:7.

1 Nefi 3: 10–31

Labani anaiba mali ya Lehi na kujaribu kumua Nefi na nduguze.

Mungu hutubariki kwa njia tofauti tunapotii amri Zake. Uzoefu wa Nefi katika kuchukua mabamba ya shaba unahimili ushuhuda wake kwamba Mungu hutoa njia kwa watoto Wake kutimiza amri Zake (ona 1 Nefi 3:7). Tumia chati ifuatayo kusoma majaribio mawili ya kwanza ya wana wa Lehi kuchukua mabamba ya shaba. Andika majibu kwa maswali katika safu kwa kila jaribio, au unaweza kukamilisha kazi hii katika shajara yako ya kujifunza maandiko.

Tazama:Siku za Nefi, kupiga kura (ona1 Nefi 3:11) ulikuwa ni njia ya kawaida ya kufanya uamuzi. Kwa kupiga kura, Nefi na nduguze walikuwa wakitafuta uongozi wa Bwana katika kutimiza amri ya kupata mabamba ya shaba (ona Mithali 16:33; Bible Dictionary, “Lots, Casting of”).

Maswali

Jaribio la Kwanza
(1 Nefi 3:10–18)

Jaribio la Pili
(1 Nefi 3:21–31)

  1. Nani alienda?

  1. Walifanya nini?

  1. Nduguze walifanya nini baada ya jaribio kushindikana?

  1. Baada ya jaribio lao la kwanza la kupata mabamba ya shaba kushindikana, Nefi na nduguze walikuwa na “huzuni mkubwa sana” (1 Nefi 3:14). Rejelea 1 Nefi 3:15–16, na katika shajara yako ya kujifunza maandiko elezea jinsi matendo ya Nefi kuhusu kushindwa huku kwa mara ya kwanza kulivyokuwa tofauti upande wa ndugu zake.

  2. Baada ya kutafakari jaribio la pili (ona 1 Nefi 3:21–31), jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Ghadhabu, kunung’unika, na kutoamini hutuzuia vipi sisi kumsikia Mungu?

1 Nefi 4:1–26

Nefi anapata mabamba ya shaba

Tambua maswali ambayo Lamani na Lemueli waliuliza katika 1 Nefi 3:31. Kama ungekuwa Nefi, ungejibu vipi maswali yao? Soma1 Nefi 4:1–3, ukitafuta majibu ya Nefi kwa maswali ya ndugu zake. Kwa nini unafikiri Nefi alichagua mfano wa Musa na Bahari ya Shamu katika kujibu maswali yao? Andika kishazi kutoka kwa majibu ya Nefi kwa ndugu zake ambayo kinakuinua:

Musa alikumbwa na changamoto kama hiyo ngumu wakati alipomwamuru kuwatoa wana wa Israeli kutoka Misri. Licha ya majaribu mengi, Musa hakuweza kumshawishi Farao awaachilie wana wa Israeli kutoka utumwani. Hata hivyo, Musa alisisitiza katika kufanya kile Bwana alikuwa amemwamuru yeye, na Bwana alitengeneza njia ambayo kwayo yeye aliwafanya huru wana wa Israeli.

Picha
Kuvuka Bahari ya Shamu

Nefi alitumia mfano wa Musa katika hali yake binafsi na alikuwa na imani kwamba Mungu pia angetayarisha njia kwake kuweza kwa njia fulani kupata mabamba ya shaba. Unaposoma masimulizi yaliyosalia, tafuta matokeo ya uvulimivu wa Nefi na azimio la kuwa mtiifu licha ya changamoto za awali.

Umewahi kutaka kufanya kitu au kuvutiwa kufanya kitu na usijue kwa mara moja ni kwa nini, lini, na vipi? Rais Harold B. Lee alisema kwamba kila mara katika hali hizi “tunataka kuona mwisho kuanzia mwanzoni” kabla ya sisi kufuata maelekezo ya Bwana, na alitoa ushauri ufuatao: “Ni sharti wewe ujifunze kutembea kandoni mwa nuru, na kisha hatua chache katika giza; kisha nuru itatokeza na kwenda mbele zako” (quoted in Boyd K. Packer, “The Edge of the Light,” BYU Today, Mar. 1991, 23).

Soma 1 Nefi 4:4–7, na utambue jinsi Nefi alisonga kwa imani katika giza (kusikojulikana)

Ni nini umuhimu wa maneno “Walakini niliendelea mbele” (1 Nefi 4:7)?

  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, elezea hali ambayo kwayo kijana au msichana anaweza kuulizwa kufanya kitu fulani au anaweza kuongozwa na Roho Mtakatifu kufanya kitu na asijue mapema matokeo yake. Pengine kuna wakati uliposonga mbele kwa imani bila kujua mapema jinsi au lini Mungu atakusaidia. Ikiwa hivyo, andika tukio hili katika shajara yako. Unaweza pia kutaka kuishiriki katika darasa.

Nefi alijifunza ni kwa nini, lini, na jinsi Bwana angemsaidia kutimiza amri ya kupata mabamba ila tu baada ya kuruhusu Roho Mtakatifu kumwongoza na baada ya kuamua kusonga mbele kwa imani. Soma 1 Nefi 4:8–26, na uone jinsi Bwana alivyomsaidia kupata mabamba ya shaba.

  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, orodhesha sababu ambazo Roho alimpatia Nefi za kumuua Labani? (ona 1 Nefi 4:8–13).

  2. Jibu swali lifuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Umejifunza nini kutokana na jitihada za mwisho za Nefi za kupata mabamba ya shaba ambazo zinaweza kukusaidia kufaulu katika changamoto unazopitia au utakazopitia katika maisha?

Unapokabiliwa na hali katika maisha yako ya kutokujua ni vipi, kwa nini, na lini, kumbuka kanuni inayoonyeshwa na uzoefu wa Nefi: Tunapofanya imani katika Mungu na kutafuta kufanya kile Yeye ameamuru, hata kama hatuwezi kuona matokeo yake, Yeye atatuongoza kwa ushawishi wa Roho Mtakatifu.

Picha
Nefi na Labani

Tangazo na Habari za Usuli

Amri ya Kumuua Labani

Nabii Joseph Smith alifunza kwamba ni Bwana ambaye huweka viwango vya usahihi na kosa: “Mungu alisema, ‘Usiue,’ [Kutoka 20:13]; na wakati mwengine Yeye akasema “Utaangamiza kabisa.’[Kumbukumbu ya Torati 20:17]. Hii ndio kanuni ambayo kwayo serikali ya mbinguni hufanya kazi—kwa ufunuo uliotolewa kwa hali ambazo kwazo watoto wa ufalme wamewekwa. Chochote Mungu anachohitaji ni sahihi, bila kujali ni nini, ingawa hatuwezi kuona sababu yake hadi muda mrefu baada ya matukio kutokea” Tukitafuta kwanza ufalme wa Mungu, mambo yote mazuri yataongezwa” (in History of the Church, 5:135).

Inaweza kutusaidia kuelewa ni kwa nini Bwana alitaka Nefi kumuua Labani tunapokumbuka yafuatayo: Bwana alimpatia Labani angalao nafasi mbili za kupeana kwa hiari mabamba ya shaba, lakini Labani “hakusikiza amri za Bwana” (1 Nefi 4:11). Labani alikuwa mwongo na mnyanganyi, na yeye alijaribu kumuua Lamani na kutaka kuwauua wana wanne wote wa Lehi, ambayo, chini ya sheria ya Musa, yangeadhibiwa kwa kifo (ona Kutoka 21:14). Bwana alijua ni muhimu kwa Lehi na uzao wake kuwa na kumbukumbu za kimaandiko, hata kama “mtu mmoja ataangamia” (1 Nefi 4:13) ili itokee.

Mabamba ya shaba sio tu yalibariki watu na mataifa ya Kitabu cha Mormoni, pia yalihifadhi na kutoa mafundisho ya manabii wa zamani kwa siku zetu wakati baadhi ya maandiko yaliandikwa katika mabamba ya dhahabu ambayo kwayo Kitabu cha mormoni kilitafsriwa (kama dondoo kutoka kwa Isaya na istiari ya Zenusi). Kupitia Kitabu cha Mormoni, mafundisho hayo kutoka kwa mabamba ya shaba yamebariki na yataendelea kubariki maisha ya mamilioni ya watu na mataifa ya ulimwengu. Cha msingi, haya yote yalikuwa hatarini wakati Nefi alisimama juu ya Labani na kufuata maelekezo ya Roho.

Picha
Rais Ezra Taft Benson

Rais Ezra Taft Benson alipendekeza “majaribio matatu mafupi” ya kutusaidia kuepuka kudanganywa wakati wa hali ngumu:

“1. Maandiko ya Kanisa yanasema nini kuyahusu? ‘Kwa sheria na kwa ushuhuda: kama hayaongei kulingana na neno hili, ni kwa sababu hamna nuru ndani yake,’ alisema Isaya. ( Isa. 8:20.) …

“Ni sharti tujifunze maandiko kwa bidii. Ya muhimu mahususi kwetu ni Kitabu cha Mormoni na Mafundisho na Maagano. …

“2. Mwongozo wa pili ni: Marais wa Kanisa wa siku za mwisho wanasema nini juu ya mada hii —hasa Rais aliye hai? 

“Kuna mtu mmoja tu ulimwenguni leo ambaye huongea kwa niaba ya Kanisa. (Ona M&M 132:7; 21:4.) Huyu mtu ni Rais wa [Kanisa]. Kwa sababu yeye hutoa neno la Bwana kwetu leo, maneno yake yana hata umuhimu mwingi wa mara moja kuliko yale ya manabii waliofariki. Anapoongea chini ya ushawishi wa Roho Mtakatifu maneno yake ni andiko. (Ona M&M 68:4.) …

“Rais anaweza kuongea juu ya mada yoyote anayohisi ni muhimu kwa Watakatifu. …

“3. Jaribio la tatu na la mwisho ni Roho Mtakatifu—jaribio la Roho. Na kwa Roho hiyo sisi ‘… tutajua ukweli wa vitu vyote.’ Moroni 10:5. Hili jaribio linaweza kuwa na athari kamili kama mkondo wa mtu wa mawasiliano na Mungu ni safi na mwema na hauna vurugu la dhambi” (katika Conference Report, Oct. 1963, 16–17).

  1. Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza 1 Nefi 3–4 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha