Seminari
2 Nefi


Utangulizi wa2 Nefi

Kwa nini Kujifunza Kitabu Hiki?

Kitabu cha 2 Nefi kitakusaidia kuelewa mafundisho ya misingi ya injili, kama vile Kuanguka kwa Adamu na Hawa, Upatanisho wa Yesu Kristo, na wakala. Kwa kuongezea , kitabu hiki kimejazwa na unabii kutoka kwa Nefi na Yakobo, na Isaya, ambao walikuwa mashahidi maalum wa Mwokozi. Walitabiri juu ya Urejesho wa injili katika siku za mwisho, kukusanyika kwa watu wa agano wa Mungu, Ujio wa Pili wa Yesu Kristo, na Milenia. Kitabu cha 2 Nefi pia kina maelezo ya Nefi ya mafundisho ya Kristo na kinamalizia kwa ushahidi wa Nefi wa Mwokozi.

Nani Aliandika Kitabu Hiki?

Nefi, mwana wa Lehi, alikiandika 2 Nefi. Nefi alikuwa nabii na kiongozi mkuu wa kwanza wa Wanefi. Maandishi yake yanaonyesha kwamba aliona uwezo wa Bwana wa ukombozi(ona 2 Nefi 4:15–35; 33:6) na alitamani kwa nafsi yake yote kuleta wokovu kwa watu wake (ona 2 Nefi 33:3–4). Ili kutimiza madhumuni haya, alianzisha hekalu na kuwafunza watu wake kumuamini Yesu Kristo.

Kiliandikwa Lini na Wapi?

Nefi aliandika taarifa ambayo ilikuja kuwa 2 Nefi takribani mwaka wa 570Kabla Kristo—miaka 30 baada ya yeye na familia kuondoka Yerusalemu (ona 2 Nefi 5: 28–31). Alikiandika alipokuwa katika nchi ya Nefi (ona 2 Nefi 5:8, 28–34).

Chapisha