Seminari
Kitengo cha 5: Siku ya 4, 2 Nefi 3


Kitengo cha 5: Siku ya 4

2 Nefi 3

Utangulizi

Katika 2 Nefi 3, Lehi alitoa maneno ya ushauri na baraka kwa mwanawe mdogo, Yusufu. Katika kufanya hivyo, Lehi alisimulia unabii wa Yusufu wa Misri kuhusu kazi ya mwonaji mteule Joseph Smith Mdogo. katika kukileta Kitabu cha Mormoni. Katika somo hili utaweza kuwa na nafasi ya kuona thamani kuu ya Nabii Joseph Smith na ushuhuda wa nguvu wa kazi yake tukufu teule katika Urejesho wa injili.

2 Nefi 3:1–25

Lehi anasimulia unabii wa Yusufu wa Misri kuhusu Nabii Joseph Smith.

Lehi aliendelea na ushauri wake wa mwisho kwa familia yake kwa kumfundisha mwanawe Yusufu kuhusu watu watatu wengine ambao pia waliitwa jina la Yusufu. Chora mstari kutoka kwenye marejeo ya maandiko katika 2 Nefi 3 hadi kwa Yusufu au akina Yusufu unaojifunza kuwahusu katika aya hii.

Joseph Stick Figures

Somo hili litalenga unabii wa Yusufu wa Misri kuhusu Nabii Joseph Smith—uliotolewa zaidi ya miaka 3,000 kabla ya Joseph Smith kuzaliwa!

  1. ikoni ya shajaraAnzisha orodha katika shajara yako ya maandiko ya matukio na mafundisho ambayo yanakuja akilini unapofikiria kuhusu Nabii Joseph Smith na wajibu wake katika Urejesho wa injili. Utaendelea kuongezea katika orodha hii unapoendelea kugundua habari zaidi kote katika somo hili, kwa hivyo acha nafasi ya kuandikia zaidi.

Soma 2 Nefi 3:6–8, na utambue maneno na vishazi ambavyo Yusufu wa Misri alitumia kuelezea kuhusu Nabii Joseph Smith na kazi ambayo yeye atakamilisha. Ongeza yoyote ya maneno haya na vishazi hivi ambavyo unahisi ni muhimu kwa orodha yako kuhusu Nabii katika shajara yako ya maandiko. Katika aya hizi Yusufu wa Misri alishuhudia kwamba Bwana atamwinua Nabii Joseph Smith ili kusaidia kuleta Urejesho wa injili. Unapoendelea kujifunza 2 Nefi 3, tafuta kweli za ziada kuhusu Nabii Joseph Smith ambazo zinaweza kuimarisha ushuhuda wako wa ujumbe wake mtakatifu na ziongeze katika orodha yako.

Ili kukusaidia kuelewa unabii wa Yusufu wa Misri vyema, tazama jinsi neno mwonaji linatokeza katika 2 Nefi 3:6–7, 11, na 14. Unaweza kutaka kutengeneza muhtasari katika pambizo yako kando ya mojawapo wa aya hizi kwamba mwonaji ni mtu ambaye anaweza kujua mambo ya kale, ya sasa, na ya siku zijazo (ona Mosia 8:13–17).

Yusufu wa Misri akiandika ono

Katika 2 Nefi 3:7, Yusufu wa Misri alisema kwamba Bwana alimwambia Joseph Smith “angefanya kazi ambayo itakuwa ya thamani kuu” kwa uzao wake. Pekua 2 Nefi 3:11–15, 19–21 ukitafuta ni kazi gani “yenye thamani kuu” ambayo Bwana atakamilisha kupitia Nabii Joseph. Visaidizi vya kujifunza ambavyo vinapatikana kwako (muhtasari wa sura, tanbihi, Mwongozo wa Maandiko na vinginevyo) vinaweza kukusaidia kuelewa utondoti mwingi ambao Yusufu wa Misri alitaja. Unapopata habari mpya kuhusu wajibu wa Nabii Joseph Smith, iongeze katika orodha katika shajara yako ya maandiko.

Wakati maandiko yanataja “tunda la kiuno [cha mtu],” yanalenga uzao wa mtu huyo. Yusufu wa Misri alitoa unabii kwamba Nabii Joseph Smith, mmoja wa uzao wake, angeleta Kitabu cha Mormoni katika siku za mwisho.

Katika 2 Nefi 3:12, kishazi “uzao wa viuno vyako [uzao wa Yusufu wa Misri] Utaandika” inalenga maandishi ya kumbukumbu za maandiko—Kitabu cha Mormoni—yaliyoandikwa na uzao wa Yusufu (ona 2 Nefi 3:4). Kulitolewa unabii kwamba Kitabu cha Mormoni kitaweza “kukua pamoja” na Biblia, kumbukumbu takatifu zilizoandikwa na “uzao wa viuno vya Yuda.” Pekua 2 Nefi 3:12 kwa vishazi ambavyo vinaelezea athari ambazo Kitabu cha Mormoni na Biblia vingekuwa navyo kwa ulimwengu vinapokua pamoja.

Yusufu wa Misri pia alitoa unabii kwamba Nabii Joseph Smith angechukua nafasi muhimu katika mpango wa Baba wa Mbinguni katika “kuwaleta watu wangu katika uongofu” (2 Nefi 3:15).

  1. ikoni ya shajaraJibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya maandiko ili kukusaidia kuendelea kupanua uthamini wako kwa wajibu wa Joseph Smith katika mpango wa wokovu wa Baba wa Mbinguni.

    1. Ni baadhi ya mifano gani ya maagano, mamlaka, au maagizo ambayo yalirejeshwa kupitia Nabii Joseph Smith ambayo yanaweza kusaidia kuwaletea watu uokovu?

    2. Ni tofauti gani hizi baraka zimeleta katika maisha yako?

Tafuta maneno au vishazi ambavyo vinaelezea Nabii Joseph Smith katika 2 Nefi 3:24, na uviongeze katika orodha kwenye shajara yako ya maandiko. Unaposoma dondoo ifuatayo kutoka kwa Rais Gordon B. Hinckley, ongeza katika orodha yako mafundisho yoyote ya ziada ya Nabii Joseph Smith ambayo yanathibitisha kwamba yeye alikuwa “chombo katika mikono ya Mungu”:

“Niruhusu mimi nitaje machache ya mafundisho na desturi nyingi ambazo zinatutofautisha sisi na makanisa mengine yote, na yote ambayo yamekuja kutokana na ufunuo kwa kijana Nabii [Joseph Smith]. …

“Cha kwanza kati ya hayo, kwa kweli, ni maonyesho ya Mungu Mwenyewe na Mwanawe Mpendwa, Yesu Kristo aliyefufuka. …

“Elimu hii ya Uungu, iliyofichwa kwa ulimwengu kwa karne nyingi, ilikuwa kitu cha kwanza na kikuu ambacho Mungu alimfunulia mtumishi wake mteule. …

“Kitabu cha Mormoni kimetokea kwa kipawa na nguvu za Mungu. …

Ndugu Joseph

“[Mchango mwingine wa Nabii Joseph Smith] ni urejesho wa ukuhani. …

“Ufunuo mwingine mkuu na wa kipekee uliotolewa kwa Nabii ulikuwa ni mpango wa uzima wa milele kwa familia. …

“Umaasumu wa watoto wadogo ni ufunuo mwingine ambao Mungu aliutoa kupitia utumishi wa Nabii Joseph. 

 Fundisho kuu la wokovu wa wafu ni la kipekee kwa Kanisa hili. …

Uhalisi wa milele wa mtu umefunuliwa. …

“… Kuna kitu kimoja zaidi ambacho lazima nikitaje. Hii ni kanuni ya ufunuo wa kisasa. …

 Katika mda mfupi wa miaka 38 na nusu wa maisha yake, kulikuja kupitia kwake [Joseph Smith] mtiririko usio na kifani wa elimu, karama, na mafundisho” (“The Great Things Which God Has Revealed,” Ensign au Liahona, Mei 2005, 80–83).

Baada ya kifo cha kishahidi cha Nabii Joseph Smith, Rais John Taylor aliandika kile kilikuja kuwa Mafundisho na Maagano 135. Soma Mafundisho na Maagano 135:3, na utafakari kile umejifunza katika somo hili kuhusu wajibu wa Joseph Smith katika mpango wa Baba wa Mbinguni kwa Urejesho wa injili.

  1. ikoni ya shajaraAndika majibu ya mojawapo wa maswali yafuatayo katika shajara yako ya maandiko:

    1. Je! Umejifunza au kuhisi nini leo ulipokuwa unasoma 2 Nefi 3 ambacho kinaimarisha ushuhuda wako wa Nabii Joseph Smith?

    2. Je! Ni nini ambacho Joseph Smith alifanya, alifundisha, au kurejesha ambacho unahisi ni cha “thamani kuu” (2 Nefi 3:7) kwako?

Kwa maombi tafuta njia za kushiriki ushuhuda wako wa Nabii Joseph Smith pamoja na marafiki zako na familia ili kuwasaidia kutambua vitu vingi vya thamani kuu ambavyo vilirejeshwa kupitia kwake.

  1. ikoni ya shajaraAndika yafuatayo katika sehemu ya chini ya kazi za leo katika shajara yako ya maandiko:

    Nimejifunza 2 Nefi 3na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningependa kushiriki na mwalimu wangu: