Seminari
Kitengo 26: Siku ya 1, 3 Nefi 17


Kitengo 26: Siku ya 1

3 Nefi 17

Utangulizi

Siku yake ya kwanza na Wanefi ilipokaribia kumalizika, Yesu Kristo alitambua kwamba watu wengi hawakufahamu kikamilifu kile ambacho alikuwa amewafundisha. Kwa hiyo, Aliwafundisha jinsi ya kupokea uelewa wa ziada. Watu walilia aliposema Anaondoka. Akijawa na huruma, Mwokozi alibakia nao kwa muda mrefu. Aliwaponya wagonjwa wao, kubariki watoto wao, na kuomba kwa ajili yao. Umati ulihisi furaha kubwa na upendo kwa ajili ya Mwokozi walipojumuika na Yeye.

3 Nefi 17:1–3

Yesu anaamuru watu kutafakari maneno Yake na kuomba kwa ajili ya uelewa

Unafanyaje unapokutana na mafundisho usioelewa katika maandiko au kutoka kwa kiongozi wa Kanisa? Weka mviringo kwa yote yanayofaa:

  • Mimi hupuuza tu mafundisho.

  • Mimi huuliza mtu mwingine kunisaidia kuelewa.

  • Mimi hufikiri kwa makini juu ya mafundisho.

  • Mimi humwomba Baba wa Mbinguni kunisaidia kuelewa.

Matukio yaliyoandikwa katika 3 Nefi 17yalitokea karibu na mwisho wa siku ya kwanza ya Yesu Kristo pamoja na umati wa Wanefi. Soma 3 Nefi 17:1–3, na uwekee alama kile Mwokozi aliwaambia Wanefi kufanya ili kuelewa vyema kile ambacho aliwafundisha. Fikiria jinsi kuenda nyumbani kwako kutafakari na kusali kunaweza kukusaidia kuelewa vyema ukweli wa injili.

Na Rais Henry B. Eyring

Rais Henry B. Eyring wa Urais wa Kwanza alielezea maana ya kutafakari. Soma taarifa ifuatayo na usisitize maneno au vishazi vinavyoonyesha maana ya kutafakari: “Kusoma, kujifunza, na kutafakari si sawa. Tunasoma maneno na tunaweza kupata mawazo. Tunajifunza na tunaweza kutambua ruwaza na uhusiano katika maandiko. Lakini tunapotafakari, tunaalika ufunuo kwa Roho. Kutafakari, kwangu, ni kule kufikiria na kuomba ninayofanya baada ya kusoma na kujifunza maandiko kwa umakini” (“Serve with the Spirit,” Ensign or Liahona, Nov. 2010, 60).

Angalia kwa makini katika 3 Nefi 17:3, na uone kwamba Mwokozi aliwaagiza watu “kutayarisha akili [zao]” kwa tukio lijalo pamoja Naye. Kabla ya kuendelea na masomo yako, tafakari jinsi utakavyojibu maswali yafuatayo: Ungefanya ili kuandaa akili yako kabla ya kuhudhuria kanisa? Kabla ya kuhudhuria seminari? Kabla ya kusikiliza mkutano mkuu? Kabla ya kusoma maandiko? Ni tofauti gani unafikiri kuandaa akili yako italeta katika kile unapata kutoka fursa hizo za kujifunza?

Moja ya kanuni tunayojifunza kutoka kwa mistari hizi ni: Kwa kutafakari na kuomba kwa Baba, tunaweza kupokea uelewa mkubwa.(Unaweza kutaka kuandika haya katika maandiko yako karibu na3 Nefi 17:1–3.)

  1. ikoni ya shajaraIli kukusaidia kutumia kanuni hii, chagua moja au mawili ya vitu hapa chini na ujumuishe hatua katika maisha yako wakati wa wiki ijayo. Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko kile ulichofanya. Pia andika jinsi hatua hii iliongezeka kile ulichojifunza katika kanisa, seminari, au mkutano mkuu au kutoka kwa maandiko. Kuwa tayari kushiriki shughuli hii ya shajara na mwalimu wako. Pia, fanya mpango ili kuendelea kuboreka katika mojawapo wa maeneo haya wakati wa wiki ijayo.

    1. Nitaandaa akili yangu kabla ya kuhudhuria kanisa au seminari.

    2. Nitatafakari na kusali kuhusu kile ninachosikia katika kanisa au seminari.

3 Nefi 17:4–25

Mwokozi anawaponya wagonjwa miongoni mwa Wanefi na kubariki watoto wao

Kristo anabariki Watoto Wanefi

Fikiria juu ya wakati ulipohisi kuvutiwa na kujawa na furaha kiasi kwamba haukutaka hisia hio kuisha. Soma 3 Nefi 17:4–5 ili kujua jinsi Wanefi walivyofanya wakati Mwokozi aliposema ya kwamba Atarudi kwa Baba Yake.

Mwokozi Aliitikia tamaa za haki za Wanefi kwa upendo mkubwa. Shughuli ifuatayo inaweza kukusaidia kuelewa kikamilifu zaidi upendo anao Yesu Kristo kwetu sote. Inaweza pia kukusaidia kugundua ukweli wa maandiko kuhusu tabia na asili ya Yesu Kristo.

  1. ikoni ya shajaraAndika marejeo ya maandiko yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko. Acha nafasi chini ya kila rejeo kwa habari zaidi: 3 Nefi 17:6–10; 3 Nefi 17:11–18; 3 Nefi 17:19–25. Jifunze kila moja ya vifungu hivi vya maandiko, ukitafuta ukweli juu ya tabia ya Mwokozi —Jinsi Alivyo. Pata angalau kweli tatu, ukweli mmoja kwa kila marejeo ya maandiko, na uyaandike chini ya rejeo sahihi.

Moja ya matukio yenye upendo na karimu iliyoelezwa katika Kitabu cha Mormoni ni Yesu akibariki watoto wadogo waliokuwepo katika tukio lile. Tukio hili linatusaidia kuelewa asili na tabia ya Yesu Kristo. Kabla ya kunukuwa maelezo ya Mwokozi na watoto kutoka 3 Nefi 17:11–12, 21–25, Rais Boyd K. Packer alisema, “Katika maelezo ya huduma ya Mwokozi miongoni mwa Wanefi, tunaweza kuona kindani katika nafsi Yake labda kuliko sehemu nyingine yoyote” (“Teach the Children,” Ensign, Feb. 2000, 16–17).

Tambua kwamba umati ulileta wale waliokuwa wagonjwa na waliosumbuka kwa Mwokozi, wakiwemo pamoja na wale “waliosumbuka kwa jinsi yoyote” (3 Nefi 17:9). Mateso haya yangeweza kuwa ya kimwili, kihisia au kiakili. Tafakari njia ambazo unaweza “kusumbuliwa.” Mwokozi Anawezaje kukusaidia kwa masumbuko yako kama Angekubariki binafsi?

  1. ikoni ya shajaraChambua kanuni kuhusu kutafakari ambayo ulijifunza katika mwanzo wa somo hili. Njia moja ya kutafakari ni kujiona mwenyewe katika hali sawa na ilivyoelezwa katika maelezo ya andiko. Chukua muda na upige taswira jinsi ingekuwa kama ungalikuwa mshiriki katika matukio yaliyoandikwa katika3 Nefi 17. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, elezea kile unadhani ungalisikia, kuona, na kuhisi wakati wa tukio hilo na kwamba ungejifunza kutoka kwa Mwokozi. Unaweza pia kutaka kuelezea baraka ambayo ungelitaka kutoka kwa Mwokozi.

Fikiria juu ya sentensi inayoelezea ukweli ulichojifunza kutoka3 Nefi 17:6–25. Andika sentensi ukiongoni mwa maandiko yako karibu na mistrari hizi au katika shajara yako ya kujifunza maandiko. Kweli moja kutoka kwa maandiko haya ni: Mwokozi anahisi huruma kubwa kwa ajili yetu. Ni kwa nini ni muhimu kwako kujua ukweli wa tabia ya Mwokozi ambayo umejifunza kutoka kwa mistari hizi?

Soma taarifa ifuatayo kuhusu imani: “Ili imani yako iweze kukuongoza kwa wokovu, ni lazima izingatie katika Bwana Yesu Kristo. Unaweza kutumia imani katika Kristo unapo kuwa na uhakika kwamba Yeye yuko, wazo sahihi la tabia yake, ufahamu kwamba unajitahidi kuishi kulingana na mapenzi Yake” (True to the Faith: A Gospel Reference [2004], 54).

  1. ikoni ya shajaraJibu swali lifuatalo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Jinsi gani kuelewa asili ya huruma ya Mwokozi kunakusaidia kutumia imani Kwake?

  2. ikoni ya shajaraShiriki na mtu mwingine kitu ulichojifunza kuhusu Mwokozi kutoka3 Nefi 17. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, rekodi jina la mtu huyu na muhtasari wa kile ulisema kwake.

Ingawa hatujakuwa na uzoefu ambayo Wanefi walikuwa nayo na Yesu Kristo, siku itakuja kwa kila mmoja wetu ambapo tutamwona na kumsikia Yeye. Kote katika siku ifuatayo au ya pili, tafakari somo hili. Fikiria juu ya huruma ya Mwokozi unaposali kuhusu tamaa zako, udhaifu, huzuni, na majaribu.

  1. ikoni ya shajaraAndika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza3 Nefi 17 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe)

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu: