Seminari
Kitengo cha 8: Siku ya 3, 2 Nefi 29–30


Kitengo cha 8: Siku ya 3

2 Nefi 29–30

Utangulizi

Ujumbe wa Nefi kuhusu kazi ya kushangaza ya Urejesho wa injili inaendelea katika 2 Nefi 29–30. Alishuhudia kwamba katika siku za mwisho maandiko yote yatafanya kazi pamoja kuonyesha mataifa yote, koo, ndimi, na watu kwamba Bwana huwakumbuka watoto Wake. Kumbukumbu hizi ni ushahidi na ushuhuda kwamba Yesu Kristo ni Mwokozi wetu. Alitoa unabii kwamba wengi watakataa Kitabu cha Mormoni lakini wale watakaoamini watakusanywa katika Kanisa. Kwa kuongezea , Nefi alifundisha kwamba watu wa Mungu wa agano ni wale wanaotubu, na kuamini katika Mwana wa Mungu.

Picha
nusu tufe ya mashariki ikiwa na Biblia, magharini ikiwa na Kitabu cha Mormoni

2 Nefi 29:1–14

Bwana anamwambia Nefi kwamba katika siku za mwisho wengi watakikataa Kitabu cha Mormoni.

Nefi aliona kwamba watu wengi katika siku za mwisho wangeamini Biblia kuwa tu kitabu cha maandiko peke yake kilichofunuliwa kutoka kwa Mungu na wangekataa Kitabu cha Mormoni. Je! Ungejibu vipi kama ungelikuwa na rafiki aliyeuliza, “Kwa nini Wamormoni wana Biblia ingine?”

Nefi alitoa baadhi ya majibu kwa swali hili kwa kuandika maneno ya Bwana kuhusu jukumu la Kitabu cha Mormoni katika Urejesho wa siku za mwisho wa injili, ambao Bwana aliita “kazi ya kushangaza.” (2 Nefi 29:1). Soma 2 Nefi 29:1–2, na utambue nini maneno ya Bwana yangefanya katika siku za mwisho. (“Yatatoka” hadi kwa mbegu, au uzao wa Nefi, na pia “yatapigwa miunzi hadi miisho ya dunia.”) “Kupiga muunzi’ humaanisha “kupiga mbinja,” ambayo ni ishara ya kukusanyika (ona Isaya 5:26, tanbihi b).

Neno bendera katika 2 Nefi 29:2 linamaanisha kitu kinachotumika kukusanya na kuunganisha watu. Bendera mara nyingi huitwa viwango. Kulingana na 2 Nefi 29:2, ni “bendera” gani ambayo itaenda mbele “hadi miisho wa dunia” ili kuwakusanya watu wa Bwana? (Unaweza kutaka kuandika kitu kama Kitabu cha Mormoni—maneno ya mbegu au uzao wa Nefi karibu na 2 Nefi 29:2.)

  1. Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko kile, kulingana na 2 Nefi 29:1–2, ndiyo madhumuni ya Bwana ya kutoa maandiko ya ziada kama vile Kitabu cha Mormoni.

Picha
Mzee Jeffrey R. Holland

Mzee Jeffrey R. Holland wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alishiriki umaizi ufuatao kuhusu Kitabu cha Mormoni: “Kitabu cha Mormoni ni kauli yenye kushinda zote ya agano la Mungu pamoja na upendo Wake kwa watoto Wake hapa ulimwenguni” (Christ and the New Covenant: The Messianic Message of the Book of Mormon [1997], 4).

Katika 2 Nefi 29, neno Wayunanilinamaanisha watu wasiokuwa wa nyumba ya Israeli. Neno Wayahudi linamaanisha watu ambao ni wa nyumba ya Israeli, ikijumuisha familia ya Lehi na uzao wake. Soma 2 Nefi 29:3–6ukitafuta mjibizo wa baadhi ya Wayunani wangekuwa nayo kwa maandiko ya ziada. Andika majibu yako kwa maswali yafuatayo katika sehemu iliyotolewa.

Baadhi watajibu vipi kuhusu maandiko ya ziada?

Bwana alisema nini kuhusu watu wanaojibu kwa njia hii?

Nefi alitabiri kinabii katika maelezo yake ya mjibizo wa watu kwa Kitabu cha Mormoni. Watu hivi leo mara nyingi huonyesha shaka kuhusu Kitabu cha Mormoni kwa sababu tayari wana Biblia. Angazia maneno au vishazi katika 2 Nefi 29:7–11 ambavyo vinaelezea madhumuni ya Bwana ya kutoa maandiko ya ziada. Fikiria kuhusu jinsi unaweza kuelezea madhumuni haya kwa mtu mwingine ambaye haelewi haja au thamani ya kupokea ufunuo wa ziada kutoka kwa Mungu.

  1. Ukitumia kile ulichoweka alama katika 2 Nefi 29:7–11, andika jibu katika shajara yako ya kujifunza maandiko kwa swali lililowasilishwa mwanzoni mwa somo hili: “Kwa nini Wamormoni wana Biblia ingine?”

Bwana hutoa maandiko kama ushuhuda wa pili na ili kukusanya watu kwenye agano Lake. Soma 2 Nefi 29:13–14, na utafute baraka zinazokuja wakati maandiko— “maneno ya Wanefi”(Kitabu cha Mormoni), “maneno ya Wayahudi (Biblia), na “maneno ya makabila yaliyopotea ya Israeli” — ni miongoni mwa watu.

2 Nefi 30:1–8

Nefi anatoa unabii juu ya jukumu la Kitabu cha Mormoni katika siku za mwisho

Picha
wavulana wawili

Baada ya kufundisha kwamba Mungu angekumbuka nyumba ya Israeli, Nefi alionya watu wake wasifikiri walikuwa wenye haki zaidi kuliko vile Wayunani wangekuwa. Pia aliwakumbusha kwamba watu wote wanaweza kuwa watu wa agano wa Mungu. Soma 2 Nefi 30:2, na katika nafasi iliyotolewa andika mambo mawili watu wanahitaji kufanya kabla Bwana kufanya maagano nao.

Chukua dakika na utafakari athari Kitabu cha Mormoni kinayo kwako au mtu mwingine uliye karibu nawe. Kisha soma 2 Nefi 30:3–8, na ukamilishe shughuli ifuatayo kwa vishazi vinavyoeleza matokeo ya Kitabu cha Mormoni kwa wale wanaokipokea.

Makundi ya Watu

Matokeo ya Kitabu cha Mormoni

Uzao wa Lehi (2 Nefi 30:3–6)

Wayahudi (2 Nefi 30:7)

Wayunani, au mataifa yote (2 Nefi 30:8)

Soma kauli ifuatayo kutoka kwa Rais Henry B. Eyring wa Urais wa Kwanza na uangazie sababu za kwa nini Kitabu cha Mormoni ni chombo chenye nguvu cha umisionari:

Picha
Rais Henry B. Eyring

“Kitabu cha Mormoni kimekuwa kitovu cha kazi umisionari tangu injili iliporejeshwa kupitia Nabii Joseph. Sisi tunakitumia kila siku katika kazi ya umisionari. Jambo moja kuhusu Kitabu cha Mormoni kuwa ni ufunguo wa nguvu katika kila sehemu ya kazi ya umisionari ni: Kitabu cha Mormoni ni ushuhuda wa Yesu Kristo. Ukurasa wa kichwa unatuambia kwamba. Unasema kwamba madhumuni ya kitabu hiki ni kuonyesha yale mambo makuu Bwana amewafanyia watu Wake ili kuwasaidia kujua kwamba maagano Bwana amefanya na watu Wake bado yanadumu, na kuwashawishi watu wote kwamba Yesu ndiye Kristo” (“Why the Book of Mormon?” New Era, May 2008, 6, 8).

Kujifunza 2 Nefi 30:1–8 huonyesha kwamba Kitabu cha Mormoni kinaweza kuwasaidia watu wote kupata kumjua Yesu Kristo na kuishi injili Yake.

  1. Chagua mojawapo wa maswali yafuatayo ili kujibu katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Kitabu cha Mormoni kimekusaidia vipi kumjua Mwokozi?

    2. Utatumia Kitabu cha Mormoni vipi kuwasidia wengine kuja kumjua Mwokozi?

2 Nefi 30:9–18

Nefi anatoa unabii wa hali ya dunia wakati wa Milenia

Soma 2 Nefi 30:9–10, na utafute kile kitakachotokea miongoni mwa watu kabla ya Milenia— miaka 1,000 ya haki na amani kufuatia Ujio wa Pili wa Mwokozi, wakati Yesu Kristo “atatawala binafsi juu ya Ulimwengu” (Makala ya Imani 1:10). Je! Umeshaona “mgawanyiko mkuu” (2 Nefi 30:10) unaowatenganisha wenye haki kutoka kwa waovu? Ni nini hatimaye kitakachowatokea waovu?

Soma 2 Nefi 30:12–18, ukitafuta vile maisha yatakuwa wakati wa Milenia.

  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika kichwa cha gazeti (angazia au fanya muhtasari katika maneno machache) ukielezea hali ya milenia unayotazamia sana. Baada ya kuandika kichwa cha habari, elezea jinsi kichwa hicho cha habari ni onyesho la amani ambayo itaenea juu ya ulimwengu wakati wa Milenia.

Fikiria vile itakuwa wakati Shetani hatakuwa na uwezo juu ya mioyo ya watu wakati wa Milenia, na haki na amani itaenea. Fikiria kuhusu jinsi shule au jamii yako ingekuwa tofauti kama hali hizo zingeenea leo.

  1. Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko kuhusu kile unaweza kufanya ili kujisaidia wewe mwenyewe, familia yako, na wengine kujitayarisha kwa kipindi hiki cha amani na haki.

Tangazo na Habari za Usuli

Je! Kumbukumbu za Maandiko ya Ziada Yatakuja Vipi?

Picha
Mzee Bruce R. McConkie

Mzee Bruce R. McConkie wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alipendekeza kwamba kumbukumbu zilizoongelewa katika 2 Nefi 29:12–14 zingeweza kuja kwa njia ya kushangaza, kwa maelekezo ya rais wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, ambaye mfunuaji na mfasiri na ambaye anashikilia funguo za ufalme wa Mungu” (The Millennial Messiah [1982], 217). Tunajua kwamba Mwokozi alitembelea baadhi ya makabila yaliyopotea ya Israeli baada ya Ufufuo Wake na kuwatembelea Wanefi na kwamba wao pia wangeandika matukio ya huduma Yake miongoni mwao baada ya ufufuo Wake (ona 3 Nefi 16:1–3; 17:4).

Ni Lini “Wayahudi Wataanza Kuamini katika Kristo”?

Mzee Bruce R. McConkie pia alijadili uongofu uliotabiriwa wa Wayahudi:

Na itakuja kuwa kwamba Wayahudi ambao wametawanyika pia wataanza kuamini katika Kristo; na wataanza kukusanyika juu ya uso wa nchi.’ 2 Ne. 30:7. Wingi wa chuki za Wayahudi wa zamani dhidi ya Kristo umekoma; wengi sasa wanamkubali yeye kama Rabi mkuu, ingawa si Mwana wa Mungu. Wachache wamemkubali yeye katika hali kamili, wakija katika Kanisa la kweli pamoja na kusanyiko la masazo ya Efraimu na wenzake.

“Lakini uongofu mkuu wa Wayahudi, kurudi kwao kwenye ukweli kama taifa, yamekusudiwa kutangulia Ujio wa Pili wa Masiya wao. Wale watakaoweza kuishi siku hio, katika upeo wa mateso yao na kuomboleza kwao, watauliza: ‘Haya makovu katika mikono yako na katika miguu yako yamesababishwa na nini? Kisha watajua kwamba mimi ndimi Bwana; kwani mimi nitasema kwa wao: Makovu haya ni makovu ambayo kwayo nilijeruhiwa katika nyumba ya marafiki zangu. Mimi ndiye yule aliyeinuliwa juu. Mimi ndimi Yesu ambaye alisulubiwa. Mimi ndimi Mwana wa Mungu.’ (M. & M. 45:51–52; Zekaria. 12:8–14; 13:6.)” (Mormon Doctrine, 2nd ed. [1966], 722–23).

  1. Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi za leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza2 Nefi 29–30 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningependa kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha