Seminari
Kitengo cha 21: Siku ya 2, Alma 50–52, 54–55


Kitengo cha 21: Siku ya 2

Alma 50–52, 54–55

Utangulizi

Kapteni Moroni aliendelea kuwasaidia watu wake kujilinda kwa kuimarisha miji yao. Wanefi walikuwa na mafanikio dhidi ya Walamani mpaka uasi na uovu ulipoanza kuwadhoofisha. Licha ya jitihada za Moroni za kuunganisha na kutetea watu, Wanefi walipoteza miji mingi kwa sababu ya ubishi kati yao wenyewe. Hatimaye, Moroni, Teankumu, na Lehi waliteka tena mji wa Muleki na kushinda moja ya jeshi kubwa la Walamani. Amoroni, kiongozi mwovu wa Walamani, alijaribu kujadili ubadilishanaji wa wafungwa, lakini Moroni aliwaweka huru wafungwa wa Wanefi bila umwagikaji wa damu. Moroni alisimama imara na hakuwa na mapatano na Amoroni na wafuasi wake.

Alma 50–51

Wanefi wanaimarishwa na kufanikiwa wanapokuwa watiifu kwa Bwana na kuwa na umoja miongoni mwao.

Fikiria wakati katika maisha yako ulipojitahidi kuishinda changamoto, kama vile majaribu, tatizo la kiafya, tatizo katika shule, au tatizo la uhusiano na marafiki au wanafamilia. Je! Ulitaka uwe na uwezo mkuu wa kiroho kwa wakati huo?

Picha
Rais Henry B. Eyring

Rais Henry B. Eyring wa Urais wa Kwanza alisema: “Jinsi vikosi [vya dhambi] karibu nasi vinavyoongezeka kwa kiwango, uwezo wowote wa kiroho iliokuwa wa kutosha hautakuwa wa kutosha. Na ukuaji wowote katika uwezo wa kiroho tuliyowahi kudhani uliwezekana, ukuaji mkubwa zaidi utatolewa kwetu. Haja yote ya uwezo wa kiroho na fursa ya kuupata itaongezeka kwa viwango tutakavyodharau kwa hasara yetu” (“Always,” Ensign, Oct. 1999, 9).

Maandalizi yaliyofanywa na Wanefi kwa vita vyao yanaweza kutusaidia kujifunza ukweli huu: Tukijiandaa kiroho, tunaweza kuzishinda changamoto za maisha.

Kagua Alma 50:1–6. Wanefi walifanya nini ili kuweka ngome kuzunguka miji yao? Soma Alma 50:7. Ni nini kingine ambacho Wanefi walifanya ili kujiandaa kwa ajili ya vita?

Wanefi waliweka ulinzi uliowapa uwezo nyakati za shida kubwa. Tunaweza kufuata mfano wao kwa kujenga uwezo wetu wa kiroho sasa ili tuweze kuwa na uwezo tunaohitaji katika wakati wa shida. Uwezo wa kiroho unajengwa kwa ufanisi zaidi kwa juhudi thabiti, ya kila siku. Tunakuwa na uwezo kiroho kwa mambo kama vile masomo ya kila mara ya maandiko, sala, kuhudhuria mikutano ya Kanisa, kutimiza miito yetu, kuonyesha shukrani kwa Mungu, kuwahudumia wengine, na kusikiliza na kutii ushauri wa viongozi wetu wa Kanisa.

  1. Kamilisha kauli zifuatazo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Naweza kujenga uwezo mkubwa zaidi wa kiroho kwa (orodhesha vitu vingine unavyoweza kufanya).

    2. Nitazidi kufanya (chagua kitu kimoja kutoka kwa orodha uliyotengeneza) kila siku kujenga uwezo wangu wa kiroho.

Soma Alma 50:19–23, na uangalie jinsi Bwana aliwabariki Wanefi ambao walikuwa waaminifu Kwake licha ya hali ngumu ya siku zao. Unaweza kutaka kuandika kanuni hii karibu mistari hizi: Uaminifu kwa Mungu huleta baraka, hata kukiwa na mtikisiko. Angalia Alma 50:21 ili kuona kile Mormoni alisema kilisababisha Wanefi kupoteza baraka hizi.

Wakati huo ambapo Kapteni Moroni alikuwa akiongoza Wanefi katika vita yao dhidi ya Walamani, Pahorani alikuwa mwamuzi mkuu wa Wanefi. Alikuwa mtu wa haki, na alifanya kazi ili kuweka amani katika nchi. Hata hivyo, kundi la Wanefi lilitaka kubadili sheria za Wanefi ili waweze kutawaliwa na mfalme, si mfumo wa waamuzi. Jambo hilo lilipigiwa kura, na watu wakapigia kura mfumo wao wa waamuzi. Hata hivyo, “watu wa mfalme” hawangeunga mkono sauti ya watu na walikataa kupigana pamoja na Wanefi wengine wakati Walamani walipokuja vitani. Ilimbidi Moroni kuongoza majeshi yake dhidi ya watu wa mfalme ili kuwalazimisha kujiunga na Wanefi. Hii iliwadhoofisha Wanefi katika vita vyao dhidi ya Walamani (ona Alma 51:1–21).

Soma Alma 51:22–27, na uangalie ushahidi kwamba Walamani waliweza kupata mamlaka dhidi ya Wanefi kwa sababu ya ubishi na watu wa mfalme. Fikiria juu ya kanuni hii: Mgawanyiko na ubishi huharibu amani.

  1. Soma Alma 50:39–40 na Alma 51:22, na uone jinsi Pahorani na Kapteni Moroni walitaka kwa bidii kuanzisha amani miongoni mwa watu wao. Fikiria juu ya wakati katika maisha yako ulipoona ubishi, iwe ni kati ya marafiki, wanafamilia, washirika wa shule, au wengine. Pia fikiria juu ya tabia ya mtu ambaye anajitahidi kuanzisha amani. Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko kuhusu sifa ambazo mpatanishi anaweza kuwa nazo.

Alma 52

Moroni na Teankumu wanafanya kazi pamoja ili kushinda Walamani

Picha
Kapteni Moroni na Bendera ya Uhuru

Kama ilivyoandikwa katika Alma 51:33–34, Amalikia aliuawa na Teankumu, mmoja wa viongozi wakuu wa kijeshi wa Wanefi. Baada ya kifo cha Amalikia, ndugu yake Amoroni alichukua mamlaka ya majeshi ya Walamani. Moroni alimpa Teankumu maelekezo kuendelea kuimarisha na kulinda sehemu ya kaskazini ya nchi ya Bountiful na kuteka tena miji yoyote ya Wanefi iliyokaliwa na Walamani, ikiwezekana (ona Alma 52:1–10). Soma Alma 52:15–17, na uangalie ni kwa nini Teankumu aliamua kutoshambulia mji wa Muleki.

Teankumu alijua kwamba wakati adui alikuwa katika ngome yake, itakuwa vigumu kumshinda. Kutokana na uzoefu huu, tunaweza kujifunza kanuni hii: Tukiepuka ngome za adui, tunaweza zaidi kuepuka na kupinga majaribu.

  1. Ni sehemu gani ambazo zinaweza kuchukuliwa kama ngome za adui? (Hizi ni sehemu au hali ambapo unaweza kusukumwa kutenda dhambi unapoenda huko—kwa mfano, sherehe ambapo watu wanakunywa pombe au kutazama sinema isiyofaa.) Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko maeneo machache kama hayo. Pia andika ni kwa nini unafikiri unapaswa kuepuka kwenda maeneo haya.

Huu ulikuwa ni wakati mgumu kwa Wanefi kwa sababu Walamani waliteka miji mingi ya Wanefi wakati Wanefi walipokuwa wakipambana na watu wa mfalme. Walamani walikuwa wakitumia miji hiyo kama ngome, hivyo ilikuwa vigumu kwa Wanefi kuiteka tena. Moroni alitengeneza mpango wa kuwaondoa Walamani nje ya mji wa Muleki ili Wanefi waweze kuupata mji huo tena. Soma Alma 52:21–26 ili kuona kile Moroni na Teankumu walifanya.

  1. Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko kile Moroni na Teankumu walifanya ili kuteka mji wa Muleki (ona Alma 52:21–26). Pia andika kile unafikiri kuhusu Moroni kama jemedari. Ni kwa njia gani alikuwa jemedari mzuri kwa Wanefi?

Alma 54–55

Moroni anakataa kubadilisha wafungwa na Amoroni na kuteka upya mji wa Gidi

Kote katika vita kati ya Walamani na Wanefi, pande zote mbili ziliwateka nyara wafungwa wengi wa vita. Kiongozi wa Walamani Amoroni alituma barua kwa Moroni, akipendekeza kwamba pande hizo mbili zibadilishane wafungwa wao. Moroni alikuwa na furaha kwa kubadilishana wafungwa ili Wanefi waliotekwa nyara waweze kurudishwa na ili majeshi yake yasiweze kulisha na kutunza wafungwa wa Walamani. (ona Alma 54:1–2.)

Hata hivyo, wakati yeye na Amoroni walipobadilishana barua, Amoroni aliandika akidai kwamba Wanefi wajisalimishe na kuwaacha Walamani kuwatawala. Alisema kwamba Wanefi walikuwa wauaji na kwamba Walamani walikuwa na haki katika kupigana nao. Yeye pia alitangaza kwamba hapakuwa na Mungu. (Ona Alma 54:16–24.)

Wakati Moroni alipopokea barua hii, alijua kuwa Amoroni alikuwa akidang’anya. Amoroni alijua kwamba Walamani hawakuwa na sababu ya haki kwa kupigana na Wanefi. Moroni alisema kwamba hangebadilishana wafungwa na kuwapa Walamani nguvu zaidi. Angeweza kupata njia ya kuwaokoa wafungwa wa Wanefi bila kubadilishana. (Ona Alma 55:1–2.)

Soma Alma 55:3–24 ili kujua kile ambacho Moroni alifanya ili kuwaokoa wafungwa wa Wanefi.

Wakati Moroni alipokataa madai ya Amoroni na kupata njia ya kuwaokoa wafungwa wa Wanefi, aliwazuia Walamani kwa kupata faida kubwa juu ya Wanefi na badala yake kupata faida kubwa kwa Wanefi. Ukweli mmoja tunaoweza kujifunza kutoka kwa mfano wa Moroni ni huu: Tukiamini Bwana kumtii kwa usahihi, Yeye atatuunga mkono katika mapambano yetu.

Hadithi inayopatikana katika Alma 55:3–24 ni hadithi ya kusisimua sana ya uokoaji. Fikiria juu ya mwanafamilia au rafiki ambaye angefurahia kusikia hadithi hii, na upate muda wa kusimulia mtu huyu hadithi hiyo. Unaweza pia kutaka kushiriki na huyu mtu kanuni katika mstari hapo juu na ueleze jinsi Moroni ni mfano wa kanuni hii.

  1. Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    NimejifunzaAlma 50–52; 54–55 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha