Kitengo cha 8: Siku ya 4
2 Nefi 31
Utangulizi
Nefi alifundisha fundisho la Kristo: ni sharti sisi tufanye imani katika Yesu Kristo, tutubu dhambi zetu, tubatizwe, tupokee Roho Mtakatifu, na tuvumilie hadi mwisho. Yeye pia alishuhudia kwamba tunavyotumia mafundisho haya, Mungu atatubariki na uenzi wa Roho Mtakatifu na kutuongoza hadi uzima wa milele.
2 Nefi 31:1–21
Nefi anafundisha kwamba Mwokozi aliweka mfano kamili kwa ajili yetu
Yesu alimwendea Yohana Mbatizaji ili abatizwe. Kwa vile Yesu hakuwa ametenda dhambi zozote, kwa nini unafikiri Yeye alibatizwa? Kwa nini wewe ulibatizwa? Kutafakari maswali haya kutakusaidia wewe kujitayarisha kwa somo hili.
Soma 2 Nefi 31:2, 21, na uweke alama kishazi “fundisho la Kristo.” Kumbuka kwamba katika aya ya 2, Nefi alisema kwamba yeye “lazima aseme kuhusu fundisho la Kristo.” Kisha katika aya ya 21 alisema kwamba yeye aliongea juu ya “fundisho la Kristo.” Katika 2 Nefi 31:3–20 tunajifunza kuhusu zile kweli ambazo Nefi aliziita “fundisho la Kristo.” Kweli mbili tunazojifunza ni: Yesu Kristo alitimiza haki yote kwa kutii amri zote za Baba, na sisi lazima tufuate mfano wa utiifu wa Yesu Kristo kwa kubatizwa na kupokea Roho Mtakatifu.
-
Andika vichwa vifuatavyo katika safu sambamba katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Sababu za Kwa Nini Yesu Alibatizwa na Sababu za Kwa Nini Tunabatizwa. Kisha soma 2 Nefi 31:4–12, na orodhesha kile unajifunza chini ya kila moja ya vichwa hivyo.
Kulingana na 2 Nefi 31:11, ni nini sharti kitangulie ubatizo?
Ili kukusaidia kueleza kwa nini ubatizo wa maji unahitajika, soma kauli ifuatayo ya Nabii Joseph Smith: “Ubatizo ni ishara kwa Mungu, kwa malaika, na mbinguni kwamba sisi tutafanya mapenzi ya Mungu, na hakuna njia ingine yoyote chini ya mbingu ambayo kwayo Mungu aliitawaza kwa mtu kuja Kwake ili kuokolewa, na kuingia katika ufalme wa Mungu, isipokuwa imani katika Yesu Kristo, toba, na ubatizo kwa ondoleo la dhambi, na njia ingine yoyote ni bure; ndipo una ahadi ya kipawa cha Roho Mtakatifu” (Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith [2007], 91).
-
Fikiria kwamba rafiki ambaye si mshiriki wa Kanisa amekuuliza wewe kwa nini ubatizo ni muhimu sana. Andika jinsi wewe ungeweza kujibu katika shajara yako ya kujifunza maandiko.
-
Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko jinsi kufuata mfano wa Yesu Kristo kwa kubatizwa kumeathiri na kubariki maisha yako.
Kuna mengi ya sisi kufanya baada ya kubatizwa. Soma 2 Nefi 31:13, na uweke alama vishazi ambavyo vinaelezea mtazamo mtu anafaa kuwa nao wanapofuata mfano wa Mwokozi.
Kulingana na 2 Nefi 31:13, tunapotimiza agano letu kwa madhumuni kamili ya moyo na kwa nia halisi, ni nini Baba yetu wa Mbinguni ametuahidi baada ya hayo? (Unaweza kutaka kuweka alama haya katika maandiko yako.) Soma kishazi cha mwisho katika 2 Nefi 31:17, na utambue kwa nini tunahitaji kupokea Roho Mtakatifu. Katika nafasi iliyotolewa, andika kauli ya kimafundisho au kanuni iliyo na msingi wa maandiko ambayo yanaelezea kile Roho Mtakatifu atatufanyia sisi.
Moto unatumika kusafisha vitu kama vile metali. Huchoma uchafu, na kuwacha kitu kisafi. Hii ni sawa na kile kinachotokea kwetu kiroho wakati tunapopokea kipawa cha Roho Mtakatifu. Inajulikana pia kama “ubatizo wa moto” (ona 2 Nefi 31:13). Roho Mtakatifu hushuhudia kuhusu Baba na Mwana na huleta ondoleo la dhambi. Rais Marion G. Romney wa Urais wa Kwanza alifunza, “Ubatizo huu wa moto na Roho Mtakatifu … hutakasa, huponya, na husafisha nafsi” (Learning for the Eternities, comp. George J. Romney [1977], 133).
Ili kupata kitu kingine cha “fundisho la Kristo,” soma 2 Nefi 31:15–16, na uangazie kile unachopata. Fananisha vishazi ulivyogundua katika 2 Nefi 31:13 na maelekezo yaliyotolewa katika 2 Nefi 31:15–16, na ufikirie kuhusu jinsi unaweza kuvumilia hadi mwisho kwa “nia halisi” na “madhumuni kamili ya moyo.”
-
Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
-
Je! Maneno “kwa madhumuni kamili ya moyo,” “kutenda bila unafiki,” na “kwa nia halisi” yanatumika vipi kwa shughuli kama vile masomo ya kila siku ya maandiko au mahudhurio ya Kanisa?
-
Nini tofauti kati ya mtu ambaye “husema maombi yao” na mtu ambaye huomba kwa “madhumuni kamili ya moyo”
-
Kuna tofauti gani kati ya mtu ambaye “hupokea sakramenti” na mtu ambaye hupokea sakramenti “kwa nia halisi”?
-
Soma 2 Nefi 31:18, na utafute pale tupo baada ya kupita lango la toba na ubatizo. Tunapofanya imani, kutubu, na kubatizwa, na kupokea Roho Mtakatifu, tunaingia katika “njia iliyosonga na nyembamba.” Iliyosonga humaanisha nyembamba, kali, barabara, na hairuhusu kuchepuka hata kidogo. Kulingana na 2 Nefi 31:18, tunawezaje kujua kama tuko kwenye njia iliyosonga na nyembamba?
Kupata uzoefu wa kipawa cha Roho Mtakatifu si tu hisia nzuri tunayopokea kutoka wakati mpaka wakati. Wenzi wa Roho Mtakatifu ni ushahidi kutoka kwa Mungu kwamba tuko kwenye njia inayoelekea kwenye uzima wa milele.
-
Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
-
Je! Uenzi wa Roho Mtakatifu umekusaidia vipi kukaa katika njia iliyosonga na nyembamba?
-
Ni kwa njia zingine zipi ambapo Roho Mtakatifu amebariki maisha yako?
-
Soma 2 Nefi 31:19–21, na utengeneze orodha kwa kuweka nambari katika maandiko yako vitu vingine ambavyo ni sharti tufanye ili tukae katika njia hii. (Kumbuka kwamba2 Nefi 31:19–20 ni kifungu cha umahiri wa maandiko. Unaweza kutaka kuweka alama kwa njia ya kipekee ili uweze kukipata hapo baadaye.)
-
Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika sentensi moja inayoelezea kile inamaanisha kwako “msonge mbele mkiwa na imani imara katika Kristo” (2 Nefi 31:20).
Katika nafasi zilizotolewa, fanya muhtasari wa 2 Nefi 31:19–20 kwa kauli ya kanuni:
Ikiwa sisi , basi sisi . (Unaweza kutaka kuiandika katika maandiko yako.)
Mzee Russell M. Nelson wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alitoa ushauri huu wa matumaini kwa wale ambao wanahisi wamepotoka kutoka kwa njia ilisonga na nyembamba: “Katika safari yako katika maisha, utakutana na vikwazo vingi na utafanya makosa fulani. Mwongozo wa kiroho hukusaidia wewe kutambua kosa na kufanya marekebisho yanayofaa. Unakoma kwenda katika njia isiyo sahihi. Kwa makini unasoma ramani ya kiroho ya barabara. Kisha unaendelea na toba na kulipia kunakohitajika ili kwenda kwenye “njia iliyosonga na nyembamba inayoelekea kwa uzima wa milele’ [2 Nefi 31:18]” (“Living by Scriptural Guidance,” Ensign, Nov. 2000, 17).
Tafakari jinsi kauli hii na maandiko uliyojifunza leo yatakuletea “mng’aro mkamilifu wa tumaini” (2 Nefi 31:20).
Umahiri wa Maandiko—2 Nefi 31:19–20
-
Tumia dakika tano ukifanya zoezi la kukariri 2 Nephi 31:20. Acha mwana familia au rafiki akufanyie jaribio la elimu yako ya maandiko, au unaweza kuchagua kufunika aya kwa mkono wako na ujaribu kuinukuu bila kuiangalia. Jaribu kuandika aya hiyo kutoka akilini katika shajara yako ya kujifunza maandiko.
-
Ukitumia 2 Nefi 31:20, chagua mojawapo ya vitu sharti tufanye ili tukae kwenye njia sahihi ambao unafanya vyema. Kisha andika maelezo katika shajara yako ya kujifunza maandiko kuhusu jinsi unavyofanya. Kisha chagua eneo moja unalotaka kuboreka, na uandike jinsi utakavyofanya hivyo.
Tangazo na Habari za Usuli
Tunaweza kuepuka unafiki vipi?
Nefi alionya dhidi ya unafiki katika2 Nefi 31:13. Unafiki humaanisha kujifanya au kutenda sehemu kwa wengine ili waone, ambayo haiakisi utambulisho wetu halisi. Mzee Joseph B. Wirthlin wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alizungumza juu ya kutenda bila unafiki:
“Je! Sisi, kweli, kwa hakika tunaishi injili, au tunaonyesha tumuonekano wa haki ili watu walio karibu nasi wadhanisisi ni waaminifu ambapo, kwa hali halisi, mioyo yetu na matendo ya siri si kweli kwa mafundisho ya Bwana?
“Je! Sisi tunachukua tu ‘aina ya uchamungu’ hali twazikana ‘nguvu zake’ [ona Joseph Smith—Historia 1:19]?
“Je, hakika sisi ni wenye haki, au tunafanya maigizo [tunajifanya] utiifu tu wakati tunafikiri wengine wanatuzama?
“Bwana ameiweka bayana kwamba Yeye hatapumbazwa na sura, na Ametuonya tusiwe waongo Kwake au kwa wengine. Yeye ametuonya sisi tujihadhari na wale wanaofanya maigizo ya uongo, ambao wanafanya ulaghai ambao unaficha uhalisi wa kiza. Tunajua kwamba Bwana ‘huutazama moyo’ na si ‘sura ya nje’ [ona 1 Samweli 16:7]” (“True to the Truth,” Ensign, May 1997, 15–16).
Je! Sisi “tutavumiliaje hadi mwisho” i?
Neno “kuvumilia hadi mwisho” (2 Nefi 31:16) hutumika mara nyingi kupendekeza haja ya kuteseka matatizo kwa uvumilivu katika maisha yetu. Mzee Joseph B. Wirthlin alielezea kwamba kuvumilia hadi mwisho pia humaanisha kuendelea kwa uaminifu kwa Kristo mpaka mwisho wa maisha yetu:
“Kuvumilia hadi mwisho ni mafundisho ya kuendelea katika njia inayoelekeza kwenye uzima wa milele baada ya mmoja kuingia katika njia hii kupitia imani, toba, ubatizo, na kupokea Roho Mtakatifu. Kuvumilia hadi mwisho huhitaji moyo wetu wote. …
“Kuvumilia hadi mwisho humaanisha kwamba tumepanda maisha yetu imara juu ya udongo wa injili, tukibakia katika mkondo mkuu wa Kanisa, tukiwatumikia wenzetu kwa unyenyekevu, kuishi maisha ya kama Kristo, na kuweka maagano yetu. Wale wanaovumilia ni bora, thabiti, wanyenyekevu, wakiboreka daima, na bila ya hila. Ushuhuda wao haukujengwa juu ya sababu za kidunia —umejengwa kwenye ukweli, ujuzi, uzoefu, na Roho” (“Press On,” Ensign, Nov. 2004, 101).
-
Andika yafuatayo chini ya kazi za leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
Nimejifunza 2 Nefi 31na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).
Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningependa kushiriki na mwalimu wangu: