Seminari
Kitengo ya 16: Siku ya 1, Alma 11


Kitengo ya 16: Siku ya 1

Alma 11

Utangulizi

Amuleki alibishana na wakili Zeezromu, aliyejaribu kumlazimisha kukana Mungu wa kweli na aliye hai. Alipokuwa akitetea imani yake dhidi ya majaribio ya Zeezromu ya kumtega, Amuleki alishuhudia kwamba wokovu kutoka kwa dhambi huja tu kupitia kwa Yesu Kristo. Amuleki alitoa ushahuda wa nguvu kwamba wanadamu wote watafufuliwa na kuhukumiwa na Mungu. Kwa sababu ya Upatanisho wa Mwokozi, utafufuliwa na siku moja utasimama mbele ya Mungu na kutoa hesabu ya maisha yako ya hapa duniani.

Alma 11:1–25

Amuleki anakataa majaribu ya Zeezromu ya kukana uwepo wa Mungu

Fikiria juu ya kitu unachomiliki ambacho ni cha thamani kwako ambacho kamwe huwezi kuuza. Fikiria ni kwa nini ni cha thamani kubwa vile kwako. Katika Alma 11, wakati Alma na Amuleki walipoendelea kufundisha watu wa Amoniha, wakili mwovu aitwaye Zeezromu alimkabili Amuleki na kumpa pesa ili kubadilishana kitu ambacho kilikuwa muhimu sana kwa Amuleki. Maandiko yanaelezea Zeezromu kama “Mtu aliyekuwa na ujuzi katika mipango ya ibilisi” (Alma 11:21), kumaanisha kwamba alikuwa amejifunza jinsi ya kutumia mbinu sawa, mipango, udanganyifu, na hila ambazo Shetani hutumia ili kuwashawishi wengine kutokana na haki na ukweli.

Pekua Alma 11:21–22, na ugundue ni kiasi gani cha fedha Zeezromu alimtolea Amuleki na kile alichotaka Amuleki kufanya kwa ajili yake. Fedha za “onti” zilikuwa zenye thamani zaidi kwa sarafu za Wanefi (ona Alma 11:6, 11–13). Onti moja ilikuwa sawa na takriban mshahara wa wiki moja kwa mwamuzi (ona Alma 11:3).

Jibu maswali yafuatayo:

  • Ni lini uliwahi kuona mtu akikataa ushawishi wa dunia, kama ule uliotolewa kwa Amuleki?

  • Jinsi gani kuona hivi kulikuvutia kuwa mwaminifu?

SomaAlma 11:23–25 ili uone jinsi Amuleki alivyojibu toleo la Zeezromu. Kisha jibu maswali yafuatayo katika kitabu cha kiada chako:

  • Kwa nini unafikiri Amuleki hakupendezwa na toleo la Zeezromu?

  • Kulingana na Alma 11:25, mpango wa Zeezromu ulikuwa gani katika kutoa onti sita kwa Amuleki?

  • Je! Hii inafananaje na kile Shetani hufanya wakati watu wanapokubali majaribu yake?

  1. Kamilisha mazoezi yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Ili kubainisha vilivyo jinsi Amuleki aliweza kukataa toleo la Zeezromu, soma Alma 11:22 na ukamilishe kauli ifuatayo: “kwani chochote ambacho ni kinyume cha Roho wa Bwana.” Kisha andika maneno matatu au manne mengine ambayo unaweza kuweka katika pengo ambalo pia linaweza kutoa taarifa ya kweli (fikiria, kwa mfano, kufanya, kusoma, kuvaa, kuangalia, na kuandika ).

    2. Andika taarifa kulingana na Alma 11:22 ambayo inaweza kukusaidia kukumbuka jinsi unaweza kushinda majaribu kwa usaidizi wa Roho Mtakatifu. Kile utaandika kinapaswa kueleza kwa maneno yako mwenyewe ukweli kwamba tunapotegemea Roho Mtakatifu, tunaweza kushinda majaribu.

Tua katika masomo yako kwa muda, na utafakari swali lifuatalo: Ni kwa jinsi gani kuishi ili nitambue Roho Mtakatifu na kufuata ushawishi Wake kunanisaidia kushinda majaribu?

Soma shauri ufuatao kutoka kwa Rais Boyd K. Packer, Rais wa Akidi ya Wale Mitume Kumi na Wawili, ili kuona jinsi kutegemea Roho Mtakatifu kunaweza kukusaidia kushinda majaribu

Picha
Rais Boyd K. Packer

“Kama unajiingiza ndani ya mambo ambayo haupaswi kujiingiza ndani au kama unajihusisha na watu ambao wanakuvuta mbali katika njia mbaya, hiyo ndio wakati wa kudai uhuru wako, wakala wako. Sikiliza sauti ya Roho, na hautapotea. …

“… Kama mtumishi wa Bwana, naahidi kwamba utalindwa na kukukingwa kutokana na mashambulizi ya adui ikiwa utatii maongozi kutoka kwa Roho Mtakatifu” (“Counsel to Youth,” Ensign or Liahona, Nov. 2011, 18).

  1. Ili kufikiria matumizi yafaayo ya yale uliyojifunza, jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Ni baadhi ya hali gani ambazo vijana hujaribiwa ili kulegeza shuhuda zao au kuzipuuza kwa mambo ya dunia?

    2. Ni mapendekezo gani ungeweza kutoa kwa mwanafunzi mwengine ambayo yatamsaidia kutegemea Roho Mtakatifu anapokabiliwa na majaribu ya aina hii?

Tumia kile ulichojifunza kwa kukumbuka mfano wa Amuleki wakati ujao unapojaribiwa kulegeza imani yako au maadili. Kumbuka kwamba unaweza kupata matumaini makubwa na uhakika unapoishi kwa utakatifu na kufuata maongozi ya Roho Mtakatifu.

Alma 11:26–40

Amuleki anashuhudia juu ya Mwana wa Mungu na kushinda majaribio ya Zeezromu ya kupuuza neno lake

Zeezromu anashambulia imani ya Amuleki katika Yesu Kristo. Ili kuhusisha kibinafsi kile kilichotokea baada ya Zeezromu kushindwa kumfanya Amuleki kukana uwepo wa Mungu, fikiria kuhusu wakati labda mtu alipopinga imani yako. Soma mazungumzo ya Amuleki na Zeezromu katika Alma 11:26–34, na kisha uangalie jinsi Zeezromu alibadilisha maneno ya Amuleki katika Alma 11:35.

Soma jinsi Amuleki alivyorekebisha uwongo huu katika Alma 11:36–37. Unaweza kutaka kuweka alama tanbihi ya 34a katika maandiko yako, na kusoma Helamani 5:10–11. Kisha elezea kwa maneno yako mwenyewe tofauti kati ya kuokoka “katika dhambi zetu” na kuokoka “kutoka kwa dhambi zetu”

Soma Alma 11:40, na ubaini hatua ya kwanza ambayo Amuleki alisema watu ni lazima wachukue ili kuokolewa kutoka kwa dhambi zao. Kuna baadhi ya watu wanaodai kuamini katika Yesu Kristo ilhali hawataki kubadili tabia zao. Kuamini katika jina la Yesu Kristo inamaanisha kuwa na imani katika Yeye.

Picha
Rais Dieter F. Uchtdorf

Ili kuelewa vizuri jinsi “kuamini katika jina lake” (kuwa na imani katika Yesu Kristo) huelekeza kwenye toba, soma dondoo ifuatayo kutoka kwa Rais Dieter F. Uchtdorf wa Urais wa Kwanza: “Tunahitaji imani thabiti katika Kristo ili kuweza kutubu. Imani yetu inafaa kujumuisha ‘wazo sahihi la tabia [ya Mungu], ukamilifu, na sifa’ (Lectures on Faith [1985], 38). Ikiwa tunaamini kwamba Mungu anajua mambo yote, ni mwenye upendo, na ni Mwenye huruma, tutaweza kuweka matumaini yetu Kwake kwa ajili ya wokovu wetu bila kusita. Imani katika Kristo utabadili mawazo yetu, imani, na tabia isiyowiana na mapenzi ya Mungu” (“Point of Safe Return,” Ensign or Liahona, May 2007, 100).

Picha
Yesu Kristo

Jinsi gani imani yako katika Yesu Kristo imekupa motisha ya kubadilisha mawazo, imani, na tabia yako?

  1. Kwa nini mtu anahitaji imani katika Yesu Kristo ili kutubu? Ukitumia yale uliyojifunza kutoka kwa Amuleki na Rais Uchtdorf, andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko jinsi utakavyoeleza kanuni zifuatazo: Imani ya kweli katika Yesu Kristo ni mwanzo wa mchakato wa ukombozi kutoka kwa dhambi zetu.

Alma 11:41–46

Amuleki anafundisha juu ya ufufuo na hukumu ya watu wote

Kabla ya kusoma hitimisho la ushuhuda wa Amuleki kwa Zeezromu, tafakari juu ya swali lifuatalo: Ni jinsi gani matendo ya mtu yanaweza kuathirika kwa kutoamini katika maisha baada ya kifo?

  1. Andika maneno Ufufuko na Hukumu kama safu mbili tofauti za vichwa katika shajara yako ya kujifunza maandiko. Kisha tafuta Alma 11:41–45, ukitafuta habari nyingi uwezavyo kuhusu ufufuo na hukumu, na uandike kile ulichojifunza chini ya kila kichwa. Unaweza kutaka kuandika juu ya ukurasa katika maandiko yako au katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Kupitia kwa Upatanisho wa Yesu Kristo, wote watafufuliwa na kuhukumiwa kulingana na matendo yao. Aya hizi pia zinafundisha kwamba ufufuo ina maana kuungana kwa miili yetu na roho zetu katika “hali yake kamilifu” na “sehemu zao kamili,” kamwe tena kutengana (ona Alma 11:43, 45).

  2. Jibu swali moja au yote ya yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Ni mawazo gani na hisia unazo unapofikiri juu ya kufufuliwa na kuhukumiwa?

    2. Jinsi gani imani yako kwamba utafufuliwa na kuhukumiwa kunaathiri jinsi unavyochagua kuishi kila siku?

  3. Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza Alma 11 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha