Kitengo 26: Siku ya 3
3 Nefi 19
Utangulizi
Matukio yaliyoandikwa katika 3 Nefi 11–18 yalifanyika yote katika siku moja. Mwisho wa siku hiyo, habari ya ziara ya Mwokozi na kurudi Kwake siku ya pili ulivuma miongoni mwa watu, na “walitembea sana usiku, ili wawe mahali ambapo Yesu atajionyesha mwenyewe kwa umati (3 Nefi 19:3). Asubuhi, wanafunzi kumi na wawili waliwafundisha watu na kuomba pamoja nao. Kisha Nefi akawabatiza wanafunzi kumi na wawili, na wakapokea Roho Mtakatifu na wakazingirwa na malaika. Wakati wa onyesho hili, Yesu Kristo alijitokeza na kuwaamuru wanafunzi kuomba, na Yeye pia akamwomba Baba kwa niaba ya umati. Kwa sababu ya imani yao, wafuasi walijazwa na Roho Mtakatifu. Walitakaswa, na wakawa wamoja na Baba na Mwana.
3 Nefi 19:1–14
Wanafunzi kumi na wawili wahudumia watu kama vile Mwokozi alivyoaamuru
Fikiria jinsi unavyoweza kuhisi na kile unaweza kufanya ukijua kwamba kesho Yesu Kristo atakuja kwa hekalu umbali kiasi kutoka kwako. Utajitahidi vipi kujaribu kufika huko? Je, ungetaka kuleta watu wengine pamoja na wewe? Ni nini unaweza kufanya ili kujiandaa kwa ajili ya tukio hili?
Soma 3 Nefi 19:1–3, ukiangalia majibu ya Wanefi kwa ahadi ya Mwokozi kwamba Atarudi siku ya pili. Baada ya umati kukusanyika, wale wanafunzi kumi na wawili wakagawa umati kwa vikundi kumi na mbili na kuanza kuwafundisha. Waliwaagiza umati kupiga magoti katika sala na kuwafundisha ukweli sawa ambao Mwokozi alikuwa Amewafundisha siku iliyopita. (Ona 3 Nefi 19:4–7.)
-
Soma 3 Nefi 19:8–9, na ujibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
-
Ni nini wafuasi wengi walitamani? Kutokana na uzoefu wako, ni kwa nini karama ya Roho Mtakatifu inatamanika sana?
-
Wanafunzi kumi na wawili walipaswa kusimamia mambo ya Kanisa huko Amerika baada ya Mwokozi kutoka. Kwa nini ilikuwa muhimu kwamba wawe na Roho Mtakatifu kuwaongoza?
-
Baada ya kukamilisha zoezi lako la kujifunza maandiko, tafakari maswali haya: Ni mambo gani machache ambayo unatamani sana unapoomba? Ni mara ngapi unaomba kwa ajili ya Roho Mtakatifu?
Soma 3 Nefi 19:10–12, na uangalie kile Wanafunzi walifanya baada ya kuomba. Ubatizo ulioelezwa katika mistari ya 10 –12 ulikuwa ni ubatizo wa pili kwa wanafunzi kumi na wawili. Kanisa lilikuwa limetengezwa kwa miaka mingi miongoni mwa Wanefi, na ndugu hawa wa ukuhani hizi wangebatizwa hapo awali, ingawa ubatizo wao wa kwanza haijaandikwa katika maandiko. Ubatizo huu wa pili ulikuwa wa hali maalum, kama ilivyoelezwa na Rais Joseph Fielding Smith: “Mwokozi alimwamuru Nefi na watu kubatizwa tena, kwa sababu alikuwa Ametengeneza upya Kanisa chini ya injili. Kabla ya hiyo ilikuwa imetengenezwa chini sheria [ya Musa] (Doctrines of Salvation, ed. Bruce R. McConkie, 3 vols. [1954–56], 2:336).
Kumbuka kwamba wanafunzi na Wanefi wengine walistahili kuwa katika uwepo wa Mwokozi. Soma 3 Nefi 19:13, ukiangalia kile wanafunzi kumi na wawili walipewa kwa kuwa na tamaa za haki.
-
Tengeneza orodha katika shajara yako ya kujifunza maandiko ya baraka zinazokuja katika maisha ya mtu mwenye karama ya Roho Mtakatifu na anayeishi kuustahili. Kisha linganisha orodha yako na dondoo ifuatayo na Mzee Robert D. Hales wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, na uongeza katika orodha yako mawazo yoyote mpya unayopata:
“Roho Mtakatifu anatupa nguvu na ujasiri wa kuendesha maisha yetu kwa njia ya ufalme wa Mungu na ndiye chanzo cha ushuhuda wetu wa Baba na Mwana. …
“Tunahitaji Roho Mtakatifu kama rafiki yetu wa kila mara ili kutusaidia kufanya maamuzi bora katika maamuzi zinazotukabili kila siku. Vijana wetu na wasichana wanakabiliwa na mambo mabaya ya ulimwengu. Urafiki na Roho utawapa nguvu ya kushindana na uovu, na panapohitajika, kutubu na kurudi kwa njia iliyosonga na nyembamba. Hakuna yeyote kati yetu aliye na kinga dhidi ya majaribu ya adui. Sisi sote tunahitaji uimarisho unaopatikana kupitia kwa Roho Mtakatifu. Kuwa na karama ya Roho Mtakatifu husaidia wanafamilia kufanya maamuzi yenye hekima — maamuzi yatakayowasaidia kurudi pamoja na familia zao kwa Baba yao wa Mbinguni na Mwanawe, Yesu Kristo, kuishi Nao milele” (“The Covenant of Baptism: To Be in the Kingdom and of the Kingdom,” Ensign, Nov. 2000, 8).
Kulingana na mafunzo yako ya 3 Nefi 19:1–14, tafakari ni baraka gani unataka zaidi katika maisha yako na kwa nini unaitaka.
Kamilisha kauli ya kanuni ifuatayo kulingana na 3 Nefi 19:9, 13: Kupitia kwa tamaa ya dhati na maombi, tunaweza kuwa.
3 Nefi 19:14–36
Mwokozi Anatokea na kuombea watu ili kutakaswa kupitia kwa imani yao
Soma 3 Nefi 19:14–16 ili kujifunza kilichotokea baada ya wanafunzi kumi na wawili kubatizwa na kujazwa na Roho Mtakatifu.
Baada ya wafuasi na umati kupiga magoti chini, Mwokozi aliwaamuru wanafunzi Wake kumi na wawili kuomba. Soma maelezo ya maombi yao katika3 Nefi 19:17–18, 24–26, 30. Hii ndio sehemu pekee katika maandiko ya kumbukumbu ambapo watu waliomba moja kwa moja kwa Yesu Kristo. Katika maombi yetu tunaomba kwa Mungu Baba katika jina la Mwanawe, Yesu Kristo. Hakuna mahali katika maandiko ambapo tunafundishwa kuomba kwa Yesu.
Mzee Bruce R. McConkie wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alipendekeza sababu ya wanafunzi kuweza kuomba kwa Yesu kwa mfano huu wa kipekee: “Yesu alikuwa tayari amewafundisha kuomba katika jina lake kwa Baba, ambayo walifanya mwanzo [ona 3 Nefi 19:8–9]. Lakini wakati huu ‘waliomba kwa Yesu, wakimwita Bwana wao na Mungu wao.’ 3 Nefi 19:18.] Yesu alikuwepo mbele yao kama ishara ya Baba. Kumwona Yesu, ilikuwa ni kana kwamba waliona Baba; kuomba kwake, ilikuwa ni kana kwamba waliomba kwa Baba. Ilikuwa ni hali maalum na ya kipekee”(The Promised Messiah: The First Coming of Christ [1978], 560–61). Mwokozi Mwenyewe alisema, “Wanaomba kwangu kwa sababu niko nao” (3 Nefi 19:22).
-
Wakati watu walikuwa wamepiga magoti, walishuhudia Yesu Kristo akitoa maombi matatu tofauti kwa wanafunzi Wake na kwa ajili yao. Nakili chati ifuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko. Soma marejeo yaliyotolewa ya maandiko na ukamilishe chati.
Kifungu cha Maandiko |
Ni kwa nini Mwokozi aliomba? |
Unawezaje kutumia yale uliyojifunza kutoka kwa sala ya Mwokozi katika maisha yako? |
---|---|---|
Soma 3 Nefi 19:24. Unafikiri inamaanisha nini “hawakuzidisha maneno”? Kuhusu maombi ambapo maneno yanapeanwa kwetu ili kujua cha kuombea, Mzee Bruce R. McConkie alifundisha, “Sala kamili ni zile zenye maongozi, ambazo Roho hufunua maneno yanayopaswa kutumika” (Mormon Doctrine, 2nd ed. [1966], 586).
Ili kukusaidia kuelewa vyema baadhi ya kanuni ambazo Mwokozi alifundisha katika maombi Yake, chambua 3 Nefi 19:28 na uwekee alama maneno au vishazi vinavyofundisha kanuni hii: Tunapotekeleza imani katika Yesu Kristo, tunaweza kutakaswa. Tafakari njia ambazo wanafunzi walitekeleza imani kote katika matukio yalioonyeshwa katika3 Nefi 19. Kama matokeo ya imani yao, wanafunzi walijazwa na Roho Mtakatifu (ona 3 Nefi 19:13), na kupokea Roho Mtakatifu ni muhimu ili kutakaswa.
Soma taarifa ifuatayo kutoka kwa Rais Marion G. Romney wa Urais wa Kwanza, na uangalie kinachomaanisha kutakaswa: “Kisha ubatizo wa moto na Roho Mtakatifu unakuja.’ 2 Nefi 31:13.] Huu ubatizo wa moto na wa Roho Mtakatifu ulionenwa hapa na Nefi huathiri mabadiliko makubwa katika mioyo ya watu iliotajwa na Alma [ona Alma 5:14]. Inawabadilisha kutoka kwa ubinadamu hadi kwa kiroho. Unatakasa, kuponya, na kutakasa nafsi. Imani katika Bwana Yesu Kristo, toba, na ubatizo wa maji yote ni tangulizi na muhimu kwalo, lakini ndilo ukamilisho [wa mwisho]. Kuipokea ni kuweza kuosha mavazi ya mtu katika damu ya upatanisho wa Yesu Kristo” (Learning for the Eternities, comp. George J. Romney [1977], 133).
-
Tafakari kinachomaanisha kutakaswa, na ujibu swali lifuatalo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Jinsi gani kutekeleza imani katika Yesu Kristo kunatusaidia kuwa weupe na wasafi?
Yesu alitoa sala kubwa usiku wa dhabihu Yake ya upatanisho ambao ulifanana na sala Alizotoa mingoni mwa Wanefi siku ya pili ya ziara Yake pamoja nao. Soma 3 Nefi 19:23, 29 na Yohana 17:9, 11, 21–22. Wekea alama kishazi “ili tuwe kitu kimoja.” Tafakari jinsi Yesu Kristo na Baba, ni kitu kimoja. Tunajifunza nini kutoka kwa mistari hizi kuhusu jinsi tunavyoweza kuwa kitu kimoja na Yesu Kristo?
Moja ya kanuni zinazofundishwa katika mistari hizi ni: Kwa imani tunaweza kutakaswa na kuwa kitu kimoja na Yesu Kristo, kama Yeye alivyo kitu kimoja na Baba. Soma taarifa ifuatayo kutoka kwa Mzee D. Todd Christofferson wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili juu ya jinsi tunavyoweza kuwa kitu kimoja na Baba na Mwana: “Hakika hatutakuwa kitu kimoja na Mungu na Kristo mpaka tutakapofanya mapenzi Yao na maslahi “kuwa” nia yetu kubwa. Unyenyekevu kama vile haufikiwi kwa siku moja, lakini kupitia kwa Roho Mtakatifu, Bwana atatufundisha kama tuko tayari mpaka, katika harakati ya muda, inaweza kusemekana kwa usahihi kwamba Yuko ndani yetu kama vile Baba alivyo ndani Yake. Wakati mwingine mimi hutetemeka nikifikiria kile kinahitajika, lakini najua kwamba ni katika muungano huu kamili ndipo utimilifu wa furaha unaweza kupatikana” (“That They May Be One In Us,” Ensign, Nov. 2002, 73).
Hitimisha masomo ya leo kwa kusoma na kutafakari3 Nefi 19:35–36.
-
Andika yafuatayo mwisho wa kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
Nimejifunza 3 Nefi 19na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).
Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu: