Kitengo cha 16: Siku ya 4
Alma 14–16
Utangulizi
Baada ya kusikia Alma na Amuleki wakihubiri, baadhi ya watu katika Amoniha waliamini na kutubu, ikiwa ni pamoja na Zeezromu. Wengine walikuwa na hasira na kufanya Alma Amuleki wafungwe jela. Watu waovu katika Amoniha waliwafukuza watu ambao waliamini na kuchoma wake na watoto wao. Baada ya siku nyingi, Bwana aliwakomboa Alma na Amuleki kutoka gerezani na kuwaangamiza viongozi waovu wa Amoniha. Katika Sidomu, Zeezromu alikuwa akiteseka kimwili na kiroho. Alikiri imani yake katika Yesu Kristo kwa Alma na akapona. Katika kutimiza unabii, jeshi la Walamani liliangamiza mji wa Amoniha. Mwongozo wa kinabii wa Alma uliruhusu majeshi ya Wanefi kusitisha uchokozi ya Walamani. Alma, Amuleki, na wengine wengi waliimarisha Kanisa kote katika nchi ya Wanefi.
Alma 14
Alma na Amulek wanatiwa gerezani na waumini ni kutupwa nje au kuchomwa na moto.
Fikiria nyakati ulipoona au kusikia kuhusu mtu ambaye hakuwa na hatia akiteseka katika mikono ya mtu mwingine —tukio la mtu kuteswa kwa ajili ya imani yake, kwa mfano. Tafakari maswali yafuatayo:
-
Ni hisia gani ulikuwa nayo kwa mtu aliyekuwa akiteseka?
-
Ulijihisi vipi juu ya yule aliyekuwa akisababisha mateso?
-
Kwa nini unafikiri mambo mabaya wakati mwingine hutokea watu wasio na hatia na wenye haki?
Unaposoma Alma 14, husisha maswali haya kwa uzoefu wa Alma na Amuleki.
Soma Alma 14:1–10, ukitafuta wale walioteseka na jinsi walivyoteseka. Kisha ikamilishe chati ifuatayo:
Ni kina nani Walioteseka? |
Waliteseka vipi? |
---|---|
Kama ilivyoandikwa katika Alma 14:10, Amuleki alitaka kufanya nini? Soma Alma 14:11, na utambue ukweli ambao unaweza kusaidia mtu ambaye anashindwa kuelewa ni kwa nini waovu wakati mwingine huruhusiwa kuwadhuru wale wasiokuwa na hatia au wenye haki.
Njia moja ya kueleza ukweli kutoka Alma 14:11 ni: Bwana huruhusu mwenye haki kuteseka katika mikono ya waovu ili hukumu Yake iweze kuwa ya haki. Kumbuka kwamba ilifunuliwa kwa Alma kwamba wale waliokufa walikaribishwa na Bwana “kwa utukufu” (Alma 14:11). Akifundisha juu ya tukio hili na mtazamo wa milele, Rais Henry B. Eyring wa Urais wa Kwanza alisema: “Amuleki alipewa baraka ili kuona wema na haki ya Mungu katika janga hata la kutisha” (“Amulek: The Blessings of Obedience,” in Heroes from the Book of Mormon [1995], 110).
Soma Alma 60:12–13, na ufanye rejeleo mtambuko na Alma 14:10–11. Tunajifunza kwamba miongoni mwa sababu wenye haki wanaruhusiwa kuteseka ni kutia muhuri ushahidi wao kwa maisha yao (ona M&M 135:3) na kusimama kama mashahidi dhidi ya waovu.
Kuelewa ni kwa nini Mungu anaruhusu wenye haki kuteseka inaweza kuwa kanuni gumu kwetu kuelewa. Tafakari juu ya taarifa ifuatayo kutoka kwa Rais Spencer W. Kimball ili kuelewa zaidi ni kwa nini Mungu anawaruhusu watu kutumia wakala wao, hata kama wanafanya maamuzi mbaya:
“Tukiangalia maisha haya kama maisha yote, basi maumivu, huzuni, kushindwa, na maisha mafupi yatakuwa msiba. Lakini tukiangalia maisha kama kitu cha milele yanayoenea kutoka maisha kabla ya maisha ya dunia hadi maisha ya milele baada ya kifo, kisha matukio yote yanaweza kuwekwa katika mtazamo sahihi. …
“… Kama wenye haki wote wangelindwa na waovu kuangamizwa, mpango mzima wa Baba ungefutiliwa mbali na kanuni ya msingi ya injili, wakala wa bure, ungemalizika. Hakuna mtu angelazimika kuishi kwa imani” (Teachings of Presidents of the Church: Spencer W. Kimball [2006], 15).
-
Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika jinsi kweli ulizojifunza katika Alma 14:11 na taarifa ya Rais wa Kimball zitakusaidia kuelewa ni kwa nini Mungu wakati mwingine huruhusu wenye haki kuteseka katika mikono ya waovu.
Soma Alma 14:12–13, na uangalie kile Alma alifundisha Amuleki ili kumsaidia kuvumilia majaribu waliyokuwa wakipitia. Kwa nini unafikiri Alma aliweza kujibu kwa ukakamavu kama huo?
Soma taarifa ifuatayo na Mzee Richard G. Scott wa Akidi ya Wale Mitume Kumi na Wawili ili kukusaidia kuelewa kile ambacho Alma alikuwa akimfundisha Amuleki kuhusu kuamini katika Bwana: “Maisha haya ni uzoefu katika uaminifu mkubwa —uaminifu katika Yesu Kristo, uaminifu katika mafundisho Yake, uaminifu katika uwezo wetu kama tunavyoongozwa na Roho Mtakatifu kutii mafundisho hayo kwa furaha sasa na kwa maisha yenye malengo, yenye furaha halisi ya milele. Kuamini kunamaanisha kutii kwa hiari bila kujua mwisho kutoka kwa mwanzo (onaMithali. 3:5–7). Ili kuzalisha matunda, uaminifu wako katika Bwana lazima uwe na nguvu zaidi na ya kudumu kuliko ujasiri wako katika hisia yako binafsi na uzoefu” (“Trust in the Lord,” Ensign, Nov. 1995, 17).
Inaweza kuwa na manufaa kwa kusisitiza ukweli huu kwa kuandika karibu na Alma 14:12–13 katika shajara yako ya kujifunza maandiko. Tunapomtumainia Bwana, Yeye hutuimarisha wakati wa majaribu yetu.
-
Chagua moja au zaidi ya hali zifuatazo na, katika shajara yako ya kujifunza maandiko, elezea jinsi kanuni ulioandika katika maandiko yako inaweza kuwasaidia watu walioelezwa:
-
Wachezaji kadhaa katika timu ya michezo ya kijana wanampuuza na kumkejeli wazi wazi au kumtania kuhusu uzingatiaji wake kwa viwango vya injili. Wanaonekana kupanga shughuli kwa makusudi pamoja nje ya mazoezi ambayo wanajua hatahudhuria kwa sababu ya imani yake.
-
Msicahana anaomba kazi katika duka ambapo rafiki yake wa dhati anafanya kazi. Hapati kazi hiyo, na rafiki yake anamwambia baadaye kuwa mmiliki wa duka alisema kamwe hataajiri Mmormoni.
-
Wakati kijana anauliza kundi la watu wengine vijana shuleni kukoma kutumia lugha chafu karibu naye, wanamsukuma kando na kutishia kumdhuru zaidi ikiwa atawaambia tena jinsi ya kuzungumza.
-
SomaAlma 14:14–17, na ufikirie jinsi imani ya Alma na Amuleki iliwasaidia walipoendelea kuteseka katika mikono ya viongozi waovu katika Amoniha. Kwa nini unafikiri kutotoa jibu katika hali kama hiyo ilikuwa majibu bora? (Ona pia Mathayo 27:11–14.)
Alma 14:18–28 inaelezea jinsi Alma na Amuleki waliteseka mambo mengi kabla ya Mungu kuwakomboa na kuangamiza wengi wa viongozi waovu wa Amoniha. Kishazi “wakiwasaga meno” (mstari 21) ina maana kukereza meno yao pamoja katika hasira au chuki.
-
Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika mambo ambayo Alma na Amuleki waliteseka katika Alma 14:18–25 ambayo yangekuwa magumu zaidi kwako, na ueleze ni kwa nini. Kisha andika kuhusu uzoefu wa kibinafsi au uzoefu wa mtu unayemjua ambaye alikuwa akijitahidi kuishi kwa haki lakini bado alikabiliwa na majaribio.
Kama ilivyoandikwa katika Alma 14:25, ni nini kilichowezesha Alma na Amuleki kusimama kwa miguu yao? SomaAlma 14:26–29,na uweke alama kwenye vishazi na maneno ambayo unahisi yanathibitisha vilivyo ukweli huu: Tukimwita Bwana kwa imani, Atatuimarisha katika taabu zetu na kutukombowa katika njia Yake na wakati Wake.
Bwana anaweza kupanua uwezo Wake na kukukombowa kutoka kwa majaribu na mateso katika njia Yake mwenyewe na wakati Wake. Tunapojifunza kuamini katika mapenzi ya Bwana, tutapata nguvu kuu zaidi na uwezo wa kuvumilia matatizo katika maisha yetu yote.
Alma 15–16
Zeezromu anaponywa, jeshi la Walamani laangamiza Amoniha, na Alma na Amuleki waendelea kuhubiri kwa Wanefi.
Baada ya kuondoka Amoniha, Alma na Amuleki walienda kwa mji wa karibu wa Sidomu, walipokutana na waumini kutoka Amoniha, wakiwemo pamoja na Zeezromu. Soma Alma 15:3–5 ili kugundua hali ya Zeezromu.
Fikiria yafuatayo: Ni nini kilichosababisha ugonjwa wa Zeezromu? Ni nini ambacho Zeezromu alifanya ili kupata nafuu na amani?
Kwa makini soma Alma 15:6–10, na uweke mstari chini ya vishazi viwili au vitatu vinavyoonyesha kwamba Alma alimsaidia Zeezromu kuzingatia Yesu Kristo na Upatanisho Wake. Ili kuelewa njia moja ambayo viongozi wa ukuhani wanaweza kuwasaidia watu kupokea huruma kupitia Upatanisho, soma uzoefu ufuatao kutoka kwa Mzee Jay E. Jensen wa Urais wa Wale Sabini na:
“Wakati nilipokuwa nikihudumu kama Askofu, nilishuhudia baraka za Upatanisho katika maisha ya waumini wa Kanisa waliofanya makosa mazito. …
“Kijana mzima katika kata yetu alikuwa akifanya miadi na msichana. Waliruhusu hisia zao kupita kiasi cha kudhibiti. Alikuja kwangu kwa ushauri na msaada. Kulinagana na kile kilichoungamwa na hisia za Roho kwangu, miongoni mwa mambo mengine, hakuruhusiwi kushiriki sakramenti kwa wakati. Tulikutana mara kwa mara ili kuhakikisha kwamba toba ilitendeka, na baada ya muda muafaka, nilimruhusu kushiriki tena sakramenti.
“Nilivyoketi pale jukwani katika mkutano huo wa sakramenti, macho yangu yalimwangazia alivyokuwa sasa akishiriki sakramenti kwa ustahiki. Nilishuhudia mikono ya huruma, upendo, na usalama ikimzunguka wakati uponyaji wa Upatanisho ulipopasha nafsi yake na kuinua mzigo wake, kuleta msamaha ulioahidiwa, amani, na furaha” (“Arms of Safety,” Ensign or Liahona, Nov. 2008, 49).
Maaskofu na viongozi wengine wa ukuhani wanaweza kutusaidia kupokea rehema na nguvu tunayohitaji kupitia kwa Upatanisho wa Yesu Kristo. Ni ushahidi gani unapata katika Alma 15:11–12 kwamba Zeezromu alitubu na kupokea huruma ya Bwana?
Kanuni moja ambayo unaweza kuandika katika maandiko yako au shajara yako ya kujifunza maandiko kwa Alma 15:6–12 ni: Kupitia kwa imani yetu katika Yesu Kristo, tunaweza kuponywa na kuimarishwa. Kulingana na Alma 15:16, 18, ni jinsi gani kanuni hii inadhihirika katika maisha Amuleki?
Alma na Amuleki walianzisha Kanisa miongoni mwa watu wa Sidomu na kisha wakarudi Zarahemla.
KatikaAlma 16 tunasoma kwamba jeshi la Walamani llivamia nchi ya Wanefi na kuangamiza mji wa Amoniha, kutimiza unabii wa Alma na Amuleki kwamba kama watu hawatatubu wataangamizwa (onaAlma 9:12). Unaposoma Alma 16, angalia wale ambao Wanefi waligeukia kwa msaada ili waweze kuwashinda jeshi la Walamani. Fananisha uzoefu huu kwa vita vyako mwenyewe na maadui unaokabiliana nao.
-
Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
Nimejifunza Alma 14–16 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).
Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu: