Seminari
Kitengo cha 19: Siku ya 3, Alma 37


Kitengo cha 19: Siku ya 3

Alma 37

Utangulizi

Kama ilivyoandikwa katika Alma 37, Alma aliendelea na ushauri wake kwa mwanawe Helamani na akampa umiliki wa kumbukumbu takatifu. Alimkumbusha Helamani kwamba maandiko yalikuwa tayari ndio njia ya kuwaleta maelfu ya Walamani kwa Bwana, na akatoa unabii kwamba Bwana alikuwa na madhumuni mengine makubwa kwa ajili ya kumbukumbu hizo katika siku zijazo. Alma alimwelekeza mwanawe katika kile alichopaswa kufundisha watu, na akamfundisha Helamani umuhimu wa kutegemea maneno ya Yesu Kristo kwa ajili ya uongozi kwa kulinganisha maneno ya Mwokozi na Liahona.

Alma 37

Alma anamkabidhi Helamani kumbukumbu, anamshauri kuweka amri, na kumkumbusha jinsi Liahona ilivyofanya kazi kulingana na imani.

Fikiria kuhusu mchoro ufuatao:

mshale

Fikiria juu ya vitu viwili au vitatu vidogo na rahisi ambavyo vimeleta mageuzi ulimwenguni, kama vile taa ya globu. Fikiria juu ya vitu vingine vidogo ambavyo vimeleta tofauti kubwa kwa mema katika maisha yako. Andika mambo mawili ya vitu hivi vidogo upande wa kushoto wa mchoro hapo juu. Upande wa kulia, andika maneno machache yanayoelezea athari kubwa vitu hivi vidogo vimeleta katika maisha yako.

Kama ilivyoandikwa katika Alma 37, Alma alikuwa akimwandaa mwanawe Helamani kuwa mweka kumbukumbu takatifu aliyefuata. Alma alifundisha Helamani kanuni juu ya jukumu la vitu vidogo na rahisi katika mpango wa Bwana. Soma Alma 37:6–7, na kisha ukamilishe kanuni ifuatayo: Ili kutimiza kusudi Lake kuu na la milele, Bwana hufanya kazi kwa.

Soma Alma 37:1–7, na uangalie kile Alma alieleza kama kitu kidogo na rahisi. Pia pekua Alma 37:8–10, ukitafuta njia kwa ambayo mabamba ya shaba (ambayo yana maandiko) yalielekeza kwa vitu vikubwa kwa watu wa Kitabu cha Mormoni. Unaposoma, weka alama katika maandiko yako ni gani kati ya baraka hizi ulizopokea pia kupitia kwa masomo yako ya maandiko mwenyewe.

  1. ikoni ya shajaraJibu swali lifuatalo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Ni njia gani mbili au tatu maandiko yamesababisha vitu vikubwa kutokea katika maisha yako?

Alma 37:13–16 imeandikwa ushauri ambao Alma alimpa Helamani alipokuwa akimkabidhi mwanawe kumbukumbu. Jifunze aya hizi, na uangalie kanuni ambazo Alma alifundisha. Moja ya kanuni hizi ni: Tukitii amri za Bwana, tutafanikiwa.Tafakari jinsi kanuni hii inahusiana na mchoro mwanzoni mwa somo hili.

Kama ilivyoandikwa katika Alma 37:35–47, Alma alimwelekeza Helamani kufundisha watu kuepukana na uovu na majaribu kupitia kwa imani katika Bwana Yesu Kristo. Yafuatayo ni muhtasari miwili ya masomo yanayojumuisha mafundisho haya. Jifunze kila somo na maandiko yanayoambatana nayo. Kisha jiandae kufundisha mojawapo ya masomo kwa mwanafamilia, familia yako yote (labda kama sehemu ya masomo ya jioni ya familia nyumbani), au rafiki. Unaweza kufanya marekebisho kadha kwa somo kulingana na nani na wapi unakofundisha. Panga wakati, na ufundishe somo wakati wa siku iliyopangiwa. Pia, leta muhtasari wa somo lako kwa darasa lako lijalo la masomo ya nyumbani na uwe tayari, ukiitwa kufundisha somo lako kwa darasa.

Somo 1—Alma 37:35–37

Elezea wale unaofundisha kwamba ni kawaida kwa wale wanaopanda miti kufunga au kufunganisha mti mdogo kwenye kigingi na kisha kuondoa kigingi baadaye wakati mti umekomaa. Uliza: Kwa nini unafikiri mti utahitaji kuwa na kigingi kwa msaada wakati ni mdogo na unakua?

Soma tukio lifuatalo kutoka kwa maisha ya Rais Gordon B. Hinckley:

mti mwebamba

Rais Gordon B. Hinckley alipanda mti mdogo karibu na nyumba yake mara tu baada ya kuowa. Hakuitilia maanani sana miaka ilivyopita. Siku moja aligundua mti kuwa mti ulijipinda na kuning’inia upande wa magharibi kwa sababu upepo kutoka mashariki uliukunja ulipokuwa mdogo na nyepesi. Alitoka na kujaribu kuisimamisha, lakini shina kilikuwa nene sana. Alijaribu kutumia kamba na maroda ili kuunyoosha, lakini haungejikunja. Hatimaye, alichukua msumeno wake na kukata tawi zito upande wa magharibi, ambalo iliacha kovu la kutisha. Baadaye alisema kuhusu mti:

mti uliopogolewa

“Zaidi ya nusu karne umepita tangu nilipopanda ule mti. Binti yangu na familia yake wanaishi huko sasa. Siku ingine niliuangalia tena ule mti. Ni mkubwa. Sura yake ni bora. Ni mali kubwa ya nyumbani. Lakini jinsi gani ilikuwa maumivu ya ujana wake na jinsi gani nilivyounyoosha kikatili.

mti wa shina lenye kovu

“Ulipopandwa mara ya kwanza, kipande cha kamba kingeushikilia dhidi ya nguvu za upepo. Ningeweza na ningeweka ile kamba kwa nguvu kidogo ya ajabu. Lakini sikufanya hivyo, na Ulijipinda kulingana na nguvu zilizokuja juu yake (“Bring up a Child in the Way He Should Go,” Ensign, Nov. 1993, 59).

mti mdogo wenye mhimili

Acha mtu asome ushauri wa Alma kwake Helamani katika Alma 37:35, na ujadili jinsi mstari huu unavyohusiana na uzoefu wa Rais Hinckley na mti. (Alma 37:35 ni kifungu cha umahiri wa maandiko. Unaweza kutaka kuweka alama kwa njia tofauti ili uweze kukipata katika siku zijazo.)

Waalike wale unaofundisha waseme kanuni ambayo ni muhtasari wa Alma 37:35. (Inaweza kuwa kitu kama yafuatayo: Tunapaswa kujifunza katika ujana wetu kuweka amri za Mungu. Unaweza kutaka kuuliza moja au zaidi ya maswali yafuatayo:

  • Ni tofauti gani unadhani inaweza kuleta katika maisha ya watu ikiwa wamejifunza kuweka amri za Mungu, wanapokuwa vijana?

  • Ni kwa jinsi gani kushika amri wakati ukiwa katika ujana wako umeleta tofauti kwako?

  • Unaweza kufikiria juu ya mtu aliyebarikiwa katika maisha yake yote kwa sababu ya kujifunza kutii amri akiwa kijana? Huyu mtu alibarikiwa vipi?

Uliza mtu asome Alma 37:36–37 kwa sauti na uangalie ushauri mahususi ambayo unaweza kukusaidia mtu kuweka amri. Uliza maswali kama yafuatayo:

  • Ni kwa jinsi gani kufuata ushauri huu kila siku kumekusaidia kuweka amri?

  • Ni katika njia gani unaweza kujaribu kumweka Bwana kwanza katika mawazo na vitendo vyako? Ni kwa jinsi gani unaweza kuboreka?

  • Ni ahadi gani zinatolewa kwa wale ambao ni wazoefu wa kuomba?

Shiriki ushuhuda wako juu ya jinsi kushauriana na Bwana kumekusaidia kuweka amri. Waalike wale unaowafundisha kufuata maneno ya Alma juu ya kushauriana na Bwana.

Somo 2—Alma 37:38–45

Liahona

Waulize wale unaofundisha ikiwa wanajua jina la dira ambayo Bwana aliwapa familia ya Lehi ambayo iliyowasaidia kusafiri hadi nchi ya ahadi. Kisha uliza mtu kusomaAlma 37:38. Eleza kuwa Alma alirejea Liahona kwa kufundisha Helamani kanuni muhimu kuhusu jinsi Bwana anaongoza watoto Wake.

Acha wale unaofundisha kujibu maswali yafuatayo kwa kusoma mistari iliyotajwa na kutafuta majibu:

  • Kulingana na Alma 37:38–40, Liahona ilifanya kazi kivipi?

  • Kulingana na Alma 37:41–42, ni kwa nini Liahona iliwacha kufanya kazi mara kwa mara?

  • Kulingana na Alma 37:43–45, ni kwa jinsi gani Liahona ni kama maneno ya Kristo?

Eleza kwamba maneno mfano na mfano (Alma 37:43, 45) inamaanisha kwamba kitu kinatumika kama ishara ya wazo kubwa. Kwa mfano, kutii au kutotii kwa familia ya Lehi kwa maelekezo ya Liahona ni ishara ya chaguo zetu ya kutii au kutotii maneno ya Kristo. Kama vile familia ya Lehi ilivyofika nchi ya ahadi kwa kufuata Liahona, tutapata uzima wa milele tunapofuata maneno ya Kristo.

Uliza mtu aelezee ni wapi tunaweza kupata maneno ya Yesu Kristo katika maisha yetu. (Majibu mengine yanayowezekana ni kama maandiko, maneno ya manabii wa kisasa, baraka ya baba, na uvuvio wa Roho.)

Uliza: Ni kanuni gani ambazo Alma alikuwa akifundisha Helamani kwa kutumia mfano wa Liahona? (Majibu yanaweza kuwa kitu kama kanuni zifuatazo: Tukitii maneno ya Yesu Kristo, yatatuelekeza kupokea uzima wa milele.) Unaweza kutaka kushiriki ushuhuda wako kwamba kusikiliza na kutii maneno ya Bwana kutaleta baraka kubwa katika maisha yetu.

  1. ikoni ya shajaraKatika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika sentensi chache zinazoelezea yale uliyojifunza kwa kusoma somo ulilochagua kufundisha.

  2. ikoni ya shajaraAndika yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: nimeamua kufundisha somo langu juu ya Alma 37: (andika ni mistari gani utakayofundisha). Nitafundisha (andika ni nani uliyechagua kufundisha) mnamo (andika tarehe uliyopanga kufundisha somo hili).

ikoni ya umahiri wa maandiko
Umahiri wa Maandiko—Alma 37:35

Weka alama Alma 37:35. Jaribu kukariri mstari huu. Kisha usimulie au uusome kwa mzazi au mtu mwingine mzima wakuaminiwa. Uliza mtu huyu maswali yafuatayo:

  • Ni kwa jinsi gani utii kwa amri ya Mungu umekusaidia katika maisha yako?

  • Ni ushauri gani uliyonayo kwangu ambao utanisaidia kuwa na hekima katika ujana wangu?

  1. ikoni ya shajaraAndika katika shajara yako ya kujifunza maandiko yale uliyojifunza kutoka kwa yule mtu uliyeongea naye kuhusu Alma 37:35.

  2. ikoni ya shajaraAndika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza Alma 37 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu: