Seminari
Kitengo cha 8: Siku ya 1, 2 Nefi 26–27


Kitengo cha 8: Siku ya 1

2 Nefi 26–27

Utangulizi

Nefi aliona mapema matembezi ya Yesu Kristo katika Amerika na maangamizo ambayo baadaye yangekuja kwa watu wake. Nefi pia aliona mbele wale wanaishi katika siku za mwisho na kuwaonya dhidi ya kiburi, makundi ya siri, na ukuhani wa uongo. Ili kuonyesha jinsi Bwana angetoa njia kwetu ya kushinda madhara ya uovu na ukengeufu, Nefi alijumuisha unabii wa Isaya kuhusu Urejesho wa injili ya Yesu Kristo katika siku za mwisho.

2 Nefi 26

Nefi alitoa unabii kuhusu siku za mwisho na anawaalika wote kuja kwa Kristo

Je! Wewe umeshapata kuwa katika tetemeko la ardhi, tufani ya radi kali, au tukio lingine la uharibifu au kuona picha au video ya hayo? Nefi aliona kwamba katika siku za mwisho wakazi wa duniani “wataadhibiwa kwa radi, na umeme, na matetemeko ya ardhi, na kila aina ya maangamizo” (2 Nefi 26:6). Ni nini kinachokuja akilini mwako unaposoma kuhusu “hasira ya Bwana” (2 Nephi 26:6) au “hukumu za Mungu” (2 Nephi 25:3)? Hukumu za Mungu zinadhamiriwa kubariki watoto Wake—ili kuwaleta waovu kwenye toba na kuwalinda wenye haki. Katika 2 Nefi 26:1–11, Nefi alitoa unabii wa maangamizo ambayo yatatangulia matembezi ya Yesu Kristo katika Amerika na hatimaye maangamizo ya watu wake kwa sababu ya uovu wao. Soma 2 Nefi 26:8–9, na utafute baraka ambazo Nefi alisema zingekuja kwa uzao wake wenye haki. Kisha soma 2 Nefi 26:12–13, na utafute kile tulichoahidiwa sisi tunapofanya imani katika Yesu Kristo.

  1. Yesu Kristo anajionyesha Mwenyewe kwa wale waofanya imani katika Yeye na kuvumilia katika haki. Andika majibu yako kwa maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Je! Yesu Kristo ujionyesha Mwenyewe vipi kwa wale ambao wanafanya imani katika Yeye? (Ona 2 Nefi 26:13.)

    2. Je! Wewe umeshashuhudia au kupata uzoefu wa baadhi ya maonyesho haya ya Yesu Kristo?

Katika 2 Nefi 26:14–19, Nefi alitoa unabii kwamba katika siku za mwisho, baada ya watu wake na mbegu ya kaka zake kudhoofishwa na kutoamini, Kitabu cha Mormoni kingetokea. Katika 2 Nefi 26:20–22, yeye alielezea jinsi watu wengi katika siku za mwisho watajawa na kiburi, kukataa miujiza ya Mungu, na kutegemea hekima yao wenyewe na kujifunza. Ni kwa njia gani umeona mifano ya unabii wa Nefi ukitimia?

Nefi alituonya sisi kwamba ibilisi hutumia kiburi, ulafi, na kazi za siri kutuharibu au kutuangamiza. Katika maandiko yako karibu na 2 Nefi 26:22, weka alama jinsi Shetani hutafuta kutufunga sisi. Kamba ya kitani ni uzi mwembamba ambao unaweza kukatika kwa urahisi. Hata hivyo, wakati nyuzi nyingi zinaposukwa pamoja zinakuwa kamba thabiti. Soma 2 Nefi 26:32, na uone mifano ya “kazi za gizani” ambazo Bwana hutuamuru tuepukane nazo. Tafakari jinsi uzi mmoja unaweza kuwa “kamba thabiti” katika 2 Nefi 26:32.

  1. Fikiria unamfundisha rafiki jinsi ya kuepuka mitego ya ibilisi (Shetani). Ukitumia 2 Nefi 26:20–22, 32, andika aya katika shajara yako ya kujifunza maandiko ambayo inaelezea mchakato ambao kwake ibilisi hutafuta kutufunga sisi. Angalia kimahususi katika 2 Nefi 26:22 jinsi adui hutumia kamba za kitani mpaka mwadhiriwa wake anafungwa na kamba thabiti, na utoe mfano.

Nefi aliona maangamizo yaliyosababishwa na adui na kuonya juu ya mitego na ushawishi wa Shetani katika siku za mwisho. Kinyume na kazi za giza za Shetani, Nefi alifunza kwamba upendo wa Mungu umetawanywa kwa wote na kwamba kusudi Lake ni kuwaokoa wengi wanaokuja Kwake. Soma 2 Nefi 26:23–24, na uangazie maneno na vishazi ambavyo vinaelezea jinsi Mungu hufanya kazi na watoto Wake. Kuligana na 2 Nefi 26:24, kusudi la Mungu ni nini katika kila kitu anachofanya? Unaweza kutaka kuangazia kishazi ambacho hufunza fundisho hili: Kila kitu Bwana anachofanya ni kwa manufaa ya ulimwengu

  1. Jibu swali lifuatalo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Je! Kuelewa kwamba kila kitu Bwana anachofanya ni kwa manufaa ya ulimwengu kunakusaidia vipi kuongeza imani yako katika Baba yetu wa Mbinguni na kukupatia imani na hakikisho katika maisha haya?

Pitia haraka 2 Nefi 26:25–28, 33, na uweke alama kila wakati maneno yote, chochote, na hamna yanatokea. Kisha rudi nyuma na usome tena mistari hii, ukiwa makini kwa maneno haya na jinsi Nefi alifunza kwamba Bwana anawapenda watu wote na anawaalika wote waje Kwake na kupokea wokovu Wake.Tafakari jinsi kanuni hii inaathiri jinsi wewe unavyoona amri, viwango, na watu wengine.

  1. Soma 2 Nefi 26:29–31. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, orodhesha sifa mbili au tatu za ukuhani wa uongo zilizoorodheshwa katika mstari wa 29, na kisha ujibu maswali yafuatayo:

    1. Kwa nini unafikiri kuhani za uongo zinaleta sifa mbaya kwa Kanisa?

    2. Kulingana na 2 Nefi 26:30, kuhani za uongo zinazuiliwa vipi?

2 Nefi 27:1–23

Nefi anatoa unabii wa kuja kwa Kitabu cha Mormoni

Picha
Biblia katika lugha nyingi
  1. Jibu swali lifuatalo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Wewe unajuaje (au kwa nini unaamini) kwamba Kitabu cha Mormoni ni neno la Mungu?

Bwana alifunua kwa nabii Isaya utondoti kuhusu kuja kwa Kitabu cha Mormoni, ambavyo Nefi aliandika katika 2 Nefi 27. Baada ya Isaya kutoa unabii kwamba katika siku za mwisho watu wengi watajawa na uovu na kuwakataa manabii, alifunza kwamba Mungu angefunua kitabu kilichoandikwa maandishi ya kale (ona 2 Nefi 27:1–7). Soma 2 Nefi 27:12–14, na utafute kile inachofundisha Bwana angefanya ili kuthibitisha ukweli wa kitabu hiki ambacho kingekuja katika siku za mwisho.

Njia moja Bwana alithibitisha ukweli wa Kitabu cha Mormoni ilikuwa ni kuwaruhusu watu wengine kushuhudia mabamba ya dhahabu. Oliver Cowdery, David Whitmer, na Martin Harris walichaguliwa kama Mashahidi Watatu waliotajwa katika 2 Nefi 27:12. (Ona “Ushuhuda wa Mashahidi Watatu” hapo mwanzoni wa Kitabu cha Mormoni.)

“Wachache” waliotajwa katika 2 Nefi 27:13 inajumuisha Mashahidi Wanane (ona “Ushuhuda wa Mashahidi Wanane” hapo mwanzoni wa Kitabu cha Mormoni). Fikiria kuweka alama kishazi “mashahidi wengi kama apendavyo” katika 2 Nefi 27:14. Unapopokea na kushiriki ushuhuda wako wa Kitabu cha Mormoni, wewe pia unakuwa shahidi wa ukweli wa kitabu hiki. Unaweza kutaka kuandika jina lako karibu na 2 Nefi 27:14 kama mmoja wa mashahidi hawa wa ziada wa ukweli wa Kitabu cha Mormoni.

Mzee Jeffrey R. Holland wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alisema kuhusu ushuhuda wake mwenyewe wa Kitabu cha Mormoni:

Picha
Mzee Jeffrey R. Holland

“Mimi nashuhudia kwamba mtu hawezi kufikia imani kamili katika kazi hii ya siku za mwisho— na kwa hivyo kupata kipimo kamili cha imani na faraja katika hizi, nyakati zetu— mpaka yeye akumbatie utakatifu wa Kitabu cha Mormoni na Bwana Yesu Kristo, ambaye kinamshuhudia. …

“Naomba kwamba ushuhuda wangu wa Kitabu cha Mormoni na mambo yote ambayo kinahusu, umetolewa leo chini ya kiapo changu mwenyewe na ofisi, yaandikwe na watu wa duniani na malaika wa mbinguni. … Mimi nataka iwe wazi kabisa ninaposimama mbele ya baraza la hukumu ya Mungu kwamba mimi nautangazia ulimwengu, katika lugha ya wazi kabisa ninayoweza kupata, kwamba Kitabu cha Mormoni ni cha kweli, kwamba kilikuja kwa njia ambayo Joseph alisema kilikuja na kilitolewa ili kuleta furaha na matumaini kwa waaminifu katika taabu za siku za mwisho” (“Safety for the Soul,” Ensign, Nov. 2009, 89–90).

Tafakari juu ya kile unaweza kufanya ili kuimarisha kusadiki kwako kwa ukweli wa Kitabu cha Mormoni.

  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika kile wewe utafanya mwaka huu ili kuimarisha ushahidi wako wa ukweli wa Kitabu cha Mormoni.

Ili kukamilisha shughuli ifuatayo, utahitaji kurejea kwa Joseph Smith—Historia, ambayo iko katika Lulu ya Thamani Kuu. Soma Joseph Smith—Historia 1:63–65, na utambue watu katika tukio hili. Kisha soma vifungu vilivyopangiwa kutoka 2 Nefi 27 katika chati iliyopo chini, na uoanishe jina na kila seti ya mistari.

  1. Charles Anthon

  2. Joseph Smith

  3. Martin Harris

Picha
Kitabu cha Mormoni na maandishi ya kale

Neno maandishi katika Joseph Smith—Historia 1:63–65 linamaanisha maandishi ya Kimisri yaliyorekebishwa ambayo Joseph Smith alikuwa amenakili na kutafsiri kutoka kwenye mabamba ya dhahabu ambayo Martin Harris aliwasilisha kwa Profesa Charles Anthon. Charles Anthon alikuwa mwalimu katika Chuo cha Columbia na mtu aliyekuwa na sifa za kuelewa lugha za kale. Baada ya kutangaza na kuthibitisha kwa maandishi kwamba tafsiri ya Joseph Smith ya maandishi yalikuwa sahihi, Profesa Anthon alipasua idhinisho lake la tafsiri wakati alipoambiwa kuhusu njia ya miujiza mabamba hayo yalivyopatikana. Aliomba atafsiri kumbukumbu hizo mwenyewe. Wakati Martin Harris alielezea kwamba baadhi ya mabamba hayo yalikuwa yamefungwa, Profesa Anthon alisema kwamba yeye hawezi kusoma kitabu kilichofungwa. Kulingana na 2 Nefi 27:16, tunajifunza nini kuhusu nia ya Charles Anthon ya kutaka kutafsiri mabamba hayo?

Soma 2 Nefi 27:20–23, na uweke alama kishazi ambacho kimerudiwa katika aya ya 20 na {nb 21.

  1. Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko jinsi kile umejifunza kufikia hapo katika 2 Nefi 27:1–23 kinathibitisha kwamba Mungu anaweza kufanya kazi Yake. (Ikiwa unahitaji habari za ziada kuhusu kuja kwa Kitabu cha Mormoni, ona M&M 20:8–12.)

Unaweza kutaka kuandika ukweli ufuatao katika maandiko yako: Kuja kwa Kitabu cha Mormoni ni mojawapo ya njia ambazo Mungu atakamilisha kazi Yake katika siku za mwisho.

  1. Jibu swali lifuatalo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Kutimizwa kwa unabii wa kale kuhusu Kitabu cha Mormoni kunaimarisha ushuhuda wako wa kitabu hiki vipi na nafasi yake katika Urejesho wa Kanisa la Bwana?

2 Nefi 27:24–35

Nefi anatoa unabii wa adhira chanya ya injili iliyorejeshwa ya Yesu Kristo

Picha
Joseph Smith katika Kichaka Kitakatifu

Mungu alimchagua mvulana aliyeitwa Joseph Smith kuwa nabii wa Urejesho na kuleta kazi Yake ya ajabu katika siku za mwisho. “Kazi ya kushangaza” inayotajwa katika maandiko ni Urejesho wa injili ya Yesu Kristo, ambayo inajumuisha kuja kwa Kitabu cha Mormoni. Soma 2 Nefi 27:25–26, uweke alama kishazi “kazi ya kushangaza na maajabu,” na utambue baadhi ya hali ambazo zingekuwapo wakati Bwana alipoanza hii kazi ya kushangaza. Tafakari jinsi Kitabu cha Mormoni na Urejesho umekusaidia wewe kuepukana na hali hizi.

Soma 2 Nefi 27:29–30, 34–35, na uweke alama baraka ambazo zinakuja kwa sababu ya kuja kwa Kitabu cha Mormoni na Urejesho wa injili. Kitabu cha Mormoni na injili iliyorejeshwa italeta furaha na uelewa kwa wale ambao watajifunza na kukipokea.

  1. Andika jibu la swali lifuatalo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Urejesho wa injili, ambao unajumuisha kuja kwa Kitabu cha Mormoni, imekuwa “kazi ya kushangaza” katika maisha yako vipi?

  2. Andika yafuatayo katika sehemu ya chini ya kazi za leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza2 Nefi 26–27 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningependa kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha