Seminari
Kitengo 16: Siku ya 2, Alma 12


Kitengo 16: Siku ya 2

Alma 12

Utangulizi

Maneno ya Amuleki katika Alma 11 yalimfanya Zeezromu kufahamu hatia yake kwa kusema uongo na kuwadanganya watu. Baada Amuleki kuzungumza na watu wa Amoniha, Alma alisimama mbele yao. Kwa sababu watu katika Amoniha walikuwa waovu, Alma alilenga kweli ambazo zingewasaidia kutubu kwa ugumu wa mioyo yao na dhambi nyinginezo. Alielezea mitego za Shetani, hukumu ambazo zitawapata waovu, na mpango wa ukombozi unaotolewa kwa njia ya Mwana wa Mungu inayowezesha wale wanaotubu kurudi kwa uwepo wa Mungu.

Alma 12:1–7

Alma anafichua nia mbaya ya Zeezromu

Fikiria jinsi mtego unafanya kazi ya kukamata mnyama: Kitanzi cha kamba kinawekwa kwa mzunguko wa kipande cha chakula. Kadri mnyama anavyopitia kitanzi kuchukua chakula, mtego unakazwa, na mnyama anakamatwa.

Picha
kamba imefungwa kwa mtego

Chambua jinsi Zeezromu alijaribu kumkamata Amuleki kwa mtego katikaAlma 11:21–25. Baada Amuleki kujua lengo la Zeezromu na kumjibu, Alma alisimama kumhutubia Zeezromu na umati uliokuwapo (ona Alma 12:1–2). Tazama katika Alma 12:3–6 kwa maneno na vishazi ambavyo Alma alitumia kuelezea mbinu za Zeezromu, ambazo Alma alisema zilitoka kwa iblisi (ona Alma 12:5).

Kulingana na Alma 12:3, Alma aliwezaje kujua mpango wa Zeezromu?

Alma alisema nia ya iblisi ilikuwa nini katika Alma 12:6?

Alma alifundisha kwamba Roho Mtakatifu anaweza kutusaidia kutambua majaribu ya adui. Katika somo juu ya Alma 11, ulijifunza kwamba tukitegemea Roho Mtakatifu, tunaweza kushinda majaribu. Kipengele muhimu ya kushinda majaribu ni kuacha Roho atusaidie kutambua majaribu na madhara yanayoweza kutuletea. Kisha tunaweza kuamua kubakia wasafi na waaminifu kwa kuepuka majaribu. Je, umewahi kuwa na tukio ambapo Roho Mtakatifu alikusaidia kutambua na kuepuka moja ya majaribu ya iblisi?

  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika kile unaweza na utafanya ili kuongeza uwezo wako wa kutambua na kuitikia minong’ono ya Roho Mtakatifu ili uweze kutambua na kuepuka “mitego” ya adui.

Alma 12:7–18

Alma anafundisha kuhusu hukumu ya mwisho ya watu wote

Fikiria juu ya kazi unaoyotaka kutafuta. Kadiria ni kiasi gani utaweza kulipa katika masomo (malipo kwa maelekezo) katika shule au ratiba ya mafunzo ili kupata ujuzi unaohitajika ili kufanikiwa katika kazi hiyo.

Picha
Mzee David A. Bednar

Soma dondoo ifuatayo, ukitafuta “masomo” ambayo Mzee David A. Bednar wa Akidi ya Wale Mitume kumi na Wawili alisema lazima yalipwe ili kupokea ujuzi wa kiroho: “Ufahamu wa kiroho ambao mimi na wewe tumebarikiwa kupokea, na ambao umethibitishwa kama kweli katika mioyo yetu, hauwezi kutolewa kwa [wengine]. Masomo ya bidii na ya kujifunza kwa utafiti na pia kwa imani lazima yalipwe ili kupata na ‘kumiliki’ kibinafsi ujuzi huo. Ni kwa njia hii tu ambapo kile kinachojulikana katika akili pia kiweze kuhisiwa katika moyo” (“Watching with All Perseverance,” Ensign or Liahona, May 2010, 43).

Angalia ushahidi katika Alma 12:7–8 kwamba Zeezromu alikuwa tayari kulipa “masomo” ya kiroho yaliyohitajika ili kupata ufahamu wa kiroho. Unaona nini ambayo inaonyesha Zeezromu aliaanza kubadili moyo wake ili aweze kujifunza kweli za kiroho?

Angalia kile ambacho Alma alifundisha Zeezromu kuhusu kupata ufahamu wa kiroho unaposoma Alma 12:9–11. Inaweza kusaidia kujua kwamba “siri za Mungu ni kweli za kiroho zinazojulikana tu kwa ufunuo. Mungu hufunua siri zake kwa wale ambao ni watiifu kwa Injili” (Guide to the Scriptures, “Mysteries of God,” scriptures.lds.org). Unaweza kutaka kuandika ufafanuzi huu katika maandiko yako karibu na Alma 12:9. Katika Alma 12:9, Alma alielezea kuwa Mungu atatoa sehemu ya neno Lake kwa mwanadamu kulingana na nini?

Kulingana na Alma 12:10–11, kuna uhusiano gani kati ya hali ya mioyo yetu na kupokea kweli za kiroho?

Ina maana gani “kushupaza” moyo wako (ona Alma 12:10–11), na unadhani hali kama hiyo inaoonekana vipi katika maisha ya mtu?

Ujumbe wa Alma kwa Zeezromu unafundisha kanuni zifuatazo: Bwana huonyesha kweli za kiroho kwetu kulingana na usikivu na bidii tunayoyapatia maneno Yake.

  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika kuhusu amri au ushauri kutoka kwa Bwana ambao umekuwa ukijitahidi kufuata kwa kuupa “usikivu na bidii.” Ni kwa njia gani Bwana amekubariki na uongozi wa ziada, ufahamu, au minong’ono ya Roho Wake kwa sababu umekuwa ukitimiza yale aliyokufunza?

Baada ya Alma kuelezea jinsi tunakuja kujua ukweli wa kiroho, aliendelea kujibu swali ambalo Zeezromu aliuliza katika Alma 12:8 kuhusu jinsi tutahukumiwa. Tazama kile ambacho Alma alimfundisha Zeezromu katika Alma 12:12–15 kuhusu ufufuo na hukumu. Jaza pengo zilifuatazo: Tutawajibishwa mbele za Mungu kwa ajili ya , ,na.

Tafakari swali lifuatalo: Ni tofauti gani italeta katika chaguo zako za kila siku ikiwa utakumbuka kwamba utawajibika kwa maneno, matendo, na mawazo yako?

Weka alama marejeo-mtambuko katika tanbihi 14a hadi kifungu cha umahiri wa maandiko Mosia 4:30, kisha soma au ukaririMosia 4:30.

  1. Rejea kile ulichoandika katika shajara yako ya kujifunza maandiko kwa zoezi la 1 katika somo la leo —kuhusu jinsi unaweza kuwa msikivu zaidi kwa Roho Mtakatifu. Ongeza mawazo yako kuhusu jinsi kuelewa uwajibikaji wako binafsi kwa Mungu kunaweza kuongeza hamu yako ya kutambua na kuepuka majaribu.

Alma 12:19–37

Alma anaelezea jinsi mwanadamu anaweza kushinda madhara ya Kuanguka kupitia kwa mpango wa ukombozi

Mtawala mkuu katika Amoniha aitwaye Antiona hakuamini mwanadamu anaweza kutokufa, akisema kuwa Kuanguka kuliifanya kuwa vigumu (ona Alma 12:20–21). Tafuta mistari kutoka Alma 12iliyoorodheshwa katika chati ifuatayo, na uandike kile Alma alifundisha katika safu chini ya vichwa:

Madhara ya Kuanguka (Alma 12:22, 24)

Kile ambacho Mungu alifanya ili kuleta ukombozi wetu (Alma 12:24–25, 28–33)

Kile ambacho lazima tufanye ili kukombolewa (Alma 12:24, 30, 34, 37)

Picha
Kuondoka katoka Bustani ya Edeni
  1. Baada ya kumaliza kujaza chati, jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Ni kwa jinsi gani Upatanisho wa Yesu Kristo unatusaidia kushinda madhara ya Kuanguka?

    2. Kulingana na Alma 12:24, Alma alifundisha nini ambacho kilikuwa madhumuni ya maisha kwa vile Mwokozi amewezesha kushinda madhara ya Kuanguka?

Picha
Mzee L. Tom Perry

Neno “hali ya kujaribiwa” katika Alma 12:24 ni kishazi kinachotumika tu na Alma katika Kitabu cha Mormoni (ona pia Alma 42:4, 10, 13). Mzee L. Tom Perry ya Akidi ya Wale Mitume kumi Wawili alielezea hali hii ya kujaribiwa: “lengo kuu la maisha ya duniani ni kuruhusu roho zetu, ambazo zilikuwepo kabla ya ulimwengu kuwepo, kuunganishwa na miili zetu kwa muda wa nafasi kubwa katika maisha ya duniani. Uhusiano wa hivi viwili pamoja umetupa fursa ya kukua, kuendeleza, na kukomaa kama tu tunaweza na roho na mwili vikiwa pamoja. Pamoja na miili yetu, tunapitia kiasi fulani ya majaribu katika kile kinachojulikana kama hali ya majaribio ya kuwepo kwetu. Huu ni wakati wa kujifunza na kupimwa ili kuthibitisha kuwa tunastahili fursa za milele. Yote ni sehemu ya mpango ambao Baba yetu anayo kwa watoto wake” (“Proclaim My Gospel from Land to Land,” Ensign, May 1989, 14).

Alma alishuhudia kwamba maisha ya dunia ni wakati wetu kujiandaa kukutana na Mungu. Unaweza kutaka kuviweka alama vishazi vinavyofundisha fundisho hili katikaAlma 12:24. Soma Alma 34:32, na ufanye rejeleo mtambuko na Alma 12:24.

  1. Ili kutumia ulichojifunza, jibu moja au wawili ya maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Ni kwa jinsi gani kujua lengo la maisha ya dunia kunasaidia kukuongoza katika maisha yako?

    2. Ni kwa jinsi gani imani yako katika Upatanisho wa Yesu Kristo inakusaidia katika hali yako ya kujariwa duniani?

Soma Alma 12:33–35, na utambue tofauti kwa kile kitatokea kwa wale wanaotubu na kwa wale wasiotubu. Inaweza kukusaidia kuelewa vyema mistari hii ili kujua kwamba kuingia katika pumziko la Bwana inahusisha kupokea ondoleo la dhambi zetu na hatimaye kuingia katika utukufu wa uwepo wa Bwana (ona M&M 84:24).

  1. Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza Alma 12 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha