Utangulizi kwa Moroni
Kwa nini ujifunze Kitabu Hiki?
Unapojifunza kitabu cha Moroni, unaweza kupata nguvu kutoka kwa mfano wa ajabu wa Moroni na ushuhuda. Zaidi ya hayo, kutoka kwa mafundisho ya Moroni na babake, Mormoni, utajifunza kuhusu ibada tukufu za msingi na desturi za Kanisa la Yesu Kristo, umuhimu wa kufanya matendo ya haki kwa nia ya kweli, njia ya kuhukumu kati ya mema na mabaya, na uhusiano kati ya imani, tumaini na hisani. Utasoma pia himizo la Moroni la kuomba ili kujijulia mwenyewe kwamba Kitabu cha Mormoni ni cha kweli na “mje kwa Kristo na mkamililishwe ndani yake” (Moroni 10:32).
Nani Aliandika Kitabu Hiki?
Moroni aliandika kitabu hiki, kinachojumuisha maneno yake, maneno ya Yesu Kristo kwa wanafunzi Wake kumi na wawili (ona Moroni 2), na maneno ya babake, Mormoni (ona Moroni 7–9). Kabla ya maangamizo ya Wanefi, Moroni alihudumu kama kiongozi wa kijeshi na wa Kanisa miongoni mwao (ona Mormoni 6:12; Moroni 8:1). Kama waandishi wengine wakuu na wakusanyaji wa Kitabu cha Mormoni, Moroni alikuwa shahidi wa Mwokozi. Alishuhudia: “Nimemwona Yesu, na.amenizungumzia uso kwa uso” (Etheri 12:39). Moroni alikuwa mwaminifu kwa ushuhuda wake na alihimiza kukubali kwake kuuliwa badala ya kumkataa Kristo (ona Moroni 1:1–3).
Mnamo 1823, takribani miaka 1,400 baada ya kukamilisha kumbukumbu ya Kitabu cha Mormoni, Moroni alimjia Nabii Joseph Smith kama kiumbe kilichofufuka na akamujuza kwamba kumbukumbu ilikuwa imezikwa katika mlima karibu na nyumbani kwa Joseph Smith. Wakati huo na kupitia miaka michache iliyofuata, Moroni pia aliamwamuru Joseph Smith “juu ya yale Bwana atakayoyafanya, na namna gani na kwa jinsi gani ufalme wake utaendeshwa katika siku za mwisho” (Joseph Smith—Historia 1:54).
Kiliandikwa Lini na Wapi?
Moroni huenda aliandika na kutunga kitabu hiki kati ya miaka 401 Baada ya Kristo na 421 Baada ya Kristo (ona Mormoni 8:4–6; Moroni 10:1), alipokuwa anatanga kwa ajili ya usalama wa maisha yake (ona Mormoni 1:1–3).