Seminari
Kitengo cha 2: Siku ya 2, 1Nefi 2


Kitengo cha 2: Siku ya 2

1 Nefi 2

Utangulizi

Watu hujibu maono kutoka kwa Mungu kwa njia tofauti. Bwana alimwamuru Lehi katika ndoto kuongoza familia yake hadi nyikani. Lamani na Lemueli walinung’unika dhidi ya amri ya Mungu wakati ambapo Nefi alitafuta ushahidi thibitishi. Kulinganisha majibu yao mbalimbali kutakusaidia kuamua jinsi ya kutumia haki yako ya kujiamulia wako unapofuata maelekezo ya Bwana.

1 Nefi 2:1–7

Mungu alimwamuru Lehi aondoke kwenda nyikani.

Fikiria kuwa wewe ni Lehi na Bwana amekuamuru wewe na familia yako kuiacha nyumbani yako pamoja na mali yako yote. Ingekubidi kutembea kwa siku nyingi na ukichukua tu vitu vinavyohitajika kusaidia mahitaji ya familia yako tu. Fikiri jinsi ambavyo ungefanya kulingana na ombi hilo.

Msafara wa familia ya Lehi

Soma 1 Nefi 2:1–6, na utafute sababu zilizosababisha Lehi na familia yake kuenda hadi nyikani

Kwa nini watu “wanatafuta kutoa uhai wa [Lehi]”? (ona 1 Nefi 2:1).

Bwana alimwamuru Lehi kufanya nini? (ona 1 Nefi 2:2).

Lehi ni kielelezo cha kanuni ya injili kwambatunapokuwa waaminifu na watiifu, Bwana atatusaidia nyakati za majaribu.

  1. ikoni ya shajaraKatika shajara yako ya kujifunza maandiko, jibu swali lifuatalo kuhusu1 Nefi 2:4:Unaweza kujifunza nini kutokana na uamuzi wa Lehi kuhusu kile angechukua na kile cha kuuacha nyuma?

Ili kukusaidia kuelewa jiografia ya safari ya Lehi vyema, rejea ramani kufikia mwisho wa somo.

Soma 1 Nefi 2:7, na utambue kile Lehi alifanya baada ya kuondoka pamoja na familia yake ili kuelekea nyikani. Ni neno gani ungetumia ili kuelezea sifa bainishi ambayo Lehi alionyesha?

1 Nefi 2:8–14

Lamani na Lemueli walinung’unika dhidi ya baba yao

Wana wote wanne wa Lehi walikuwa katika safari moja, lakini walifanya hivyo kwa mitazamo tofauti kwa amri za Mungu.

Soma 1 Nefi 2:8–10, na uvingire manenomto na bonde.

  1. ikoni ya shajaraKatika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika mawazo yako kuhusu swali lifuatalo: Unafikiri ni nini Lehi alikuwa anajaribu kufundisha Lamani na Lemueli kwa kuwalinganisha na mto na bonde?

Soma 1 Nefi 2:11–14, na utambue sababu za Lamani na Lemueli za kunung’unika dhidi ya baba yao. (Tazama: Nenoukaidi linamaanisha usugu na kiburi.)

Sababu moja Shetani huhimiza kunung’unika ni kwamba inazuia watu kufuata manabii hai, na wale viongozi wenye maongozi na wazazi. Mzee H. Ross Workman wa Wale Sabini aliongea juu ya kunung’unika. Alisema kwamba “Kunung’unika kuna hatua tatu, kila moja ikielekeza kwenye ile ifuatayo katika mapito ya mteremko hadi kutotii.”

Mzee H. Ross Workman

Kwanza, watu wanapo nung’unika, wanatumia maamuzi yao wenyewe na kuanza kutilia shaka mafundisho ya manabii hai. “Wanatilia [shaka] kwanza katika akili zao wenyewe na kisha [wanapanda] maswali katika akili za wengine.

Pili, wale wanaonung’unika huuanza “kufanya urazini na kujiondoa kutokana na kufanya kile wameelekezwa kufanya. Basi, [wanatoa] kisingizio cha kutotii.’

“Hatua ya tatu lazima ifuate: uzembe katika kufuata amri ya Bwana. [ona M&M 58:29]. …

“Nawaalika mlenge juu ya amri kutoka kwa manabii hai ambao wanakukera sana. Je! Unatilia shaka kama amri inafaa kwako? Je! Unapata visingizio tayari kwa nini hauwezi kufuata amri hii. Je! Unahisi kusumbuliwa au kuhudhiwa na wale wanaokukumbusha juu ya amri hii? Je! Wewe ni mzembe katika kuiweka? Jihadhari na udanganyifu wa adui. Jihadhari na kunung’unika” (“Beware of Murmuring,” Ensign, Nov. 2001, 85–86).

Lehi na familia yake
  1. ikoni ya shajaraJibu swali lifuatalo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Je! Unaweza kufanya nini kama unajipata ukinung’unika (kulalamika) kuhusu amri au kanuni ya Kanisa?

1 Nefi 2:16–19

Nefi anatafuta uelewa kutoka kwa Bwana

Soma 1 Nefi 2:16, 19, uweke alama kile Nefi alitaka na kile alifanya ambacho kilimfanya kukubali amri za Bwana zilizotolewa kupitia kwa baba yake. Ingawa Nefi hakunung’unika, tafakari jinsi kile aliandika katika 1 Nefi 2:16 kuhusu Bwana kulainisha moyo wake kinaonyesha kuwa kuondoka Yerusalemu pengine ilikuwa vigumu kwake pia.

  1. ikoni ya shajaraKatika shajara yako ya kujifunza maandiko, shiriki mfano wa nyakati ambapo, kama Nefi, ulimwita Baba yako wa Mbinguni na kuona ulainisho wa moyo wako kupitia kwa Roho au nyakati ambapo ulipokea ushuhuda wa kitu ambacho Bwana alisema.

Uzoefu wa Nefi hutufunza kanuni ya injili ifuatayo: Tunapomwomba Mungu, Yeye atalainisha mioyo yetu hata kuamini katika maneno Yake.

Soma 1 Nefi 2:17–18, na utambue hamu na matendo ya Nefi baada ya Bwana kulainisha moyo wake. Fikiria juu ya kile unaweza kujifunza kutokana na majibu tofauti ya Nefi, Samu, Lamani, na Lemueli. Ifuatayo ni kweli moja muhimu: Tunaposhiriki tulichojifunza kupitia kwa Roho Mtakatifu, wengine wanaweza kuamini maneno yetu.

  1. ikoni ya shajaraAndika katika shajara yako ya kujifunza maandiko juu ya lini maneno ya mtu mwengine yalikufanya kuamini neno la Mungu, kama vile Samu alivyomwamini Nefi.

Fikiria juu ya mtu mwengine ambaye unaweza kushiriki kitu ambacho Roho amekusaidia kujifunza na kuhisi ni kweli. Inaweza kuwa ni rafiki, mwana familia yako, kiongozi wa Kanisa, au mwalimu. Chukua fursa wiki hii kuongea na mtu huyo na kushiriki ushuhuda huo.

1 Nefi 2: 20–24

Bwana anamhakikishia Nefi kwamba atafanikiwa kupitia utii wake.

Tambua na uweke alama ahadi ilioko katika1 Nefi 2:20–21. Ahadi hii inatokea mara 34 kote katika Kitabu cha Mormoni. Wakati wa kujifunza kwako kwa Kitabu cha Mormoni utaona jinsi maneno ya Bwana kwa Nefi yalivyotimizwa yote. Hitimisha somo la leo kwa kusoma 1 Nefi 2:22–24.

Mungu huwabariki wale walio watiifu na waaminifu. Tafakari kiwango chako cha utiifu katika kutii amri za Mungu. Ni njia gani moja ambayo unaweza kuwa mtiifu zaidi? Fuatilia uvutio unaopokea kupitia kwa Roho.

  1. ikoni ya shajaraAndika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza 1 Nefi 2 na kukamisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu: