Seminari
Kitengo cha 29: Siku ya 3, Etheri 1–2


Kitengo cha 29: Siku ya 3

Etheri 1–2

Utangulizi

Kitabu cha Etheri ni ufupisho wa Moroni wa historia ya Wayaredi. Wayaredi walikuwa ni watu waliokuja katika Ulimwengu wa Magharibi karne nyingi kabla ya watu wa Lehi. Kufuatia Mafuriko katika siku za Nuhu, wengi wa uzao wa wale waliokuwa wameachwa walikuwa waovu. Kikundi kimoja cha watu walijaribu kujenga mnara “kilele chake kifike mbinguni” (Mwanzo 11:4). Rekodi ya nchi ya Wayaredi ilianza na kujenga kwa Mnara wa Babeli. Bwana alikumbana na uenezi mkubwa wa uovu kwa kukanganya lugha yao moja na kwa kutawanya watu kwenye uso wa dunia. (ona Mwanzo 11:5–8; Etheri 1:33). Rekodi hii katika kitabu cha Etheri inaanza na Yaredi na nduguye wakitafuta usaidizi wa Bwana alipokanganya lugha ya watu kwenye Mnara wa Babeli. Bwana alihifadhi lugha ya Yaredi, nduguye, na familia zao na marafiki na akawaongoza katika jangwa kuelekea nchi ya ahadi. Bwana kisha alimwamuru kaka ya Yaredi ajenge mashua nane ili kuwabeba watu wake kwenye bahari.

Picha
watu wakizungumza chini ya Mnara wa Babeli.

Etheri 1:1–33

Moroni anaandika nasaba ya Etheri hadi kwa Yaredi kwenye Mnara wa Babeli.

Ili kukusaidia uelewe kule kitabu cha Etheri kilitoka, rejelea “Maelezo ya jumla ya Mosia 7–24” kutoka kwa Kitengo cha 12: Siku ya 1 somo (ukurasa wa 116). rejea safari ya 4, na tambua kile watu wa Limhi walipata kwenye safari hii.

Angalia mwanzoni mwa kitabu cha Etheri, na pata maelezo mafupi ya kitabu chini ya anuani. Elezo hili linaelezea kwamba kumbukumbu ya Wayaredi ilichukuliwa kutoka mabamba 24 ya dhahabu yaliyopatikana na watu wa Limhi.

Baada ya Moroni kukamilisha kumbukumbu ya babake, alichukua kumbukumbu ya Wayaredi na akaunda toleo lake fupi ili kujumuisha katika Kitabu cha Mormoni. Soma Etheri 1:1–4, na utafute kile Moroni alisema hakujumuisha katika toleo lake la kumbukumbu ya Wayaredi. Kisha soma Etheri 1:5, na utafute kipande cha rekodi ambayo Moroni alijumuisha katika kumubukumbu yake. Mnara ulio ongelewa katika Etheri 1:5 ni Mnara wa Babeli. Kama ilivyoelezewa katika Etheri 1:33, Bwana “alichanganya” (alikanganya ama kuchanganyisha) lugha ya watu waliotaka kujenga mnara ili wasiweze kuelewana, na aliwatawanya watu ulimwenguni kote.

Kama ilivyoandikwa katika Etheri 1:6–33, mwanaume aliyeitwa Etheri alikuwa ameandika kumbukumbu ya Wayaredi. Moroni aliandika ukoo wa Etheri hadi kwa mwanume aliyeitwa Yaredi, aliyeishi wakati wa Mnara wa Babeli.

Etheri 1:33–43

Kaka ya Yaredi anaomba usaidizi, na wana familia wake na marafiki wapokea huruma na mwongozo

Je, umewahi kuwa katika nchi ama eneo ambapo watu waliongea lugha ambayo haukuelewa? Unafikiri ungehisi vipi kama haungeweza kuelewa lugha ambayo wengine karibu nawe wanazungumza? Kama ungeweza kuchagua watu wachache kuzungumza nao katika hali hiyo, ungechagua nani? Hali hii ilikuwa kwa mwanaume aliyeitwa Yaredi na kaka yake, pamoja na familia zao, walioishi wakati wa Mnara wa Babeli. Soma Etheri 1:33–37, na utafute watu ambao Yaredi alitaka aweze kuzungumza nao. Baada kaka ya Yaredi kupokea ahadi kutoka kwa Bwana kwamba lugha yao haingekanganywa (ona Etheri 1:34–35), aliwaombea marafiki zake (ona Etheri 1:36–37). Kama ilivyoonyeshwa na kaka ya Yaredi, sifa moja ya watu waaminifu ni kuwaombea marafiki zao ili wapokee baraka za Bwana.

Bwana aliwabariki familia za Yaredi na kaka yake na marafiki zao ili kwamba lugha yao haikukanganywa. Kisha Yaredi alimuuliza kaka yake aombe Mungu, akimuuliza mahali ambapo familia zao zilipaswa kwenda. (Ona Etheri 1:38–40.)

Soma Etheri 1:40–43, na utambue mashauri Bwana aliwapa Wayaredi kuwaongoza katika safari yao. Kwa nini unafikiri ilikuwa muhimu kwa Yaredi na kaka yake kufuata mashauri haya kutoka kwa Bwana?

Etheri 2:1–12

Wayaredi waanza safari yao kuelekea nchi ya ahadi.

SomaEtheri 2:1–3 ili kugundua jinsi Wayaredi walichukulia vyema mashauri ambayo Bwana aliwapa kuhusu kujitayarisha kusafiri kwa nchi ya ahadi (ona Etheri 1:41–42). Kisha soma Etheri 2:4–6, na utafute kile kilichotendeka baadaye. Tazama kwamba kwa sababu Wayaredi walitii mashauri ya Bwana, aliwapa maelekezo zaidi. Tafakari baraka na mwongozo Wayaredi walipokea kwa sababu walifuata mashauri ya Bwana.

Kutoka kwa yale Wayaredi walipitia tunajifunza kanuni hii: Tunapotenda kwa imani kwenye mwongozo Bwana ametupa, tunaweza kupokea maongozi zaidi kutoka Kwake.Unaweza amua uandika kanuni hii katika maandiko yako karibu na Etheri 2:6.

Je, unaweza kufikiria juu ya msukumo ama ushawishi umepokea kutoka kwa Bwana ukiomba, ukijifunza maandiko, ama ukihudhuria mkutano wa Kanisa? Weka msukumo ama ushawishi huo akilini unaposoma kauli ifuatayo kutoka kwa Richard G. Scott wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili kuhusu jinsi mara nyingi sisi hupokea majibu kwa maombi: “Mara chache utapokea jibu kamilifu [kwa maombi] mara moja. Litakuja kipande kimoja baada ya kingine, katika pakiti, ili kwamba utakuwa kiuwezo. Kila kipande kinapofuatwa katika imani, utaongozwa kwa migao mingine hadi uwe na jibu lote. Mfuatilio huo unakuhitaji uweke imani katika uwezo wa Baba kujibu. Ingawa wakati mwingine huwa ni vigumu sana, huelekeza katika kukuwa kabisa kibinafsi” (“Using the Supernal Gift of Prayer,” Ensign ama Liahona, Mei 2007, 9).

  1. Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko jinsi ulichukulia (ama unaweza kuchukulia) ushawishi wa kiroho uliofikiria kuhusu hapo awali. Unaweza kujumuisha pia baraka ulizopokea (ama unaweza kupokea) kutoka kwa kufuata ushawishi huo.

Kama ilivyoandikwa katika Etheri 2:7–12, Bwana alimwambia kaka ya Yaredi kwamba wakati yeye na watu wake watafika katika nchi ya ahadi, watahitaji “wamtumikie, yule Mungu wa kweli na wa pekee, au waangamizwe” (Etheri 2:8).

Etheri 2:13–15

Bwana amrudi kaka ya Yaredi kwa kutomwita Yeye katika maombi.

Soma Etheri 2:13–15, na utafute kile kilichotendeka wakati Yaredi alipokuja kwenye bahari kuu iliyogawanya ardhi. Walikuwa wameongozwa kupitia jangwa na Bwana kwa sababu walimsikiliza Bwana na kutii amri Zake. Lakini, baada ya kupiga kambi kando ya bahari kuu kwa miaka minne, Bwana alimjia kaka ya Yaredi na kumrudi kwa kutosali.

Etheri 2:14–15 Inatusaidia tujifunze kanuni hizi: Bwana hapendezwi tunapokosa kumwita Yeye katika maombi. Bwana anatutaka tumwite Yeye kila mara katika maombi.

Unaposoma kauli ifuatayo kutoka kwa Mzee Donald L. Staheli, aliyehudumu kama mshiriki wa Wale Sabini, fikiria kuhusu mara ngapi wewe huomba: “Maombi ya kila siku ya kina tukiomba msamaha na usaidizi maalum na mwongozo yana maana sana kwa maisha yetu na kukuzwa kwa ushuhuda wetu. Tunapokuwa na haraka, kurudiarudia, kuwa kawaida, ama kusahausahau katika maombi yetu, sisi huelekea kupoteza ukaribu wa Roho, ambao ni muhimu katika mwongozo wa kila mara ambao tunahitaji ili kukumbana kwa ufanisi na changamoto za maisha yetu ya kila siku” (“Securing Our Testimonies” Ensign ama Liahona, Nov. 2004, 39).

Katika shajara yako ya kibinafsi ama kwenye kipande tofauti cha karatasi, jibu maswali yafuatayo:

  • Unahisi vipi kuhusu kurudia rudia maombi yako?

  • Unahisi vipi kuhusu uaminifu wa maombi yako ya kibinafsi?

  • Katika maombi yako ya kibinafsi, je, unahisi kwamba unawasiliana kwa dhati na Baba wa Mbinguni? Kwa nini, kama sio ni kwa nini?

  • Kama ungeweza kufanya badiliko moja ambalo lingeimarisha maombi yako ya kibinafsi, lingekuwa nini?

Kama ilivyoandikwa katika Etheri 2:16, kaka ya Yaredi alitubu dhambi zake na akaomba kwake Bwana kwa ajili ya wana familia wake na marafiki. Bwana alimwambia kwamba alikuwa amesamehewa lakini kwamba ilimbidi aendelee katika haki ili aongozwe hadi kwa nchi ya ahadi.

Etheri 2:16–25

Wayaredi wanajenga mashua ili kuvuka bahari hadi nchi ya ahadi.

Picha
Mashua ya Wayaredi

Fikiria kuhusu uamuzi muhimu wa kibinafsi unaokumbana nao ama huenda utakumbana nao katika siku za usoni, kama vile jinsi ya kushughulika na hali ngumu ya kifamilia ama kijamii, jinsi ya kufuzu shuleni, kumuoa nani, ama uweledi upi wa kufuata. Umefikiria kuhusu jinsi Bwana angeweza kupatia maelekezo ama kukusaidia katika hali hiyo? Unaposoma yaliyobaki ya Etheri 2, tafakari uamuzi uliotambua na utafute kanuni ambazo zitakusaidia kupokea usaidizi wa Bwana.

Soma Etheri 2:16–17, na utafute kile Bwana aliwauliza Wayaredi wafanye ili kuendelea kuelekea nchi ya ahadi. Kaka ya Yaredi alikumbana na shida tatu zilizotokana na umbo wa mashua. Soma Etheri 2:18–19, na tia alama kwenye shida tatu ambazo kaka ya Yaredi alimtajia Bwana.

  1. Ili kukusaidia kuchora picha akilini ya kile ulichosoma katika Etheri 2:16–19, chora kile unachofikiria mashua huenda yalionekana kuwa katika shajara yako ya kujifunza maandiko.

Chati ifuatayo itakusaidia kugundua jinsi Bwana alimsaidia kaka ya Yaredi na shida za mashua. Soma mistari ya maandiko katika chati, na kisha tumia maarifa kujaza sehemu ya “Suluhisho kwa ajili ya Shida” safu ya chati.

Mistari ya Maandiko

Shida ya Mashua

Suluhisho la Shida

Etheri 2:20–21

Hakuna hewa

Etheri 6:4–9

Hakuna usukani

Etheri 2:22–3:6

Hakuna mwangaza

Kile ambacho Bwana alifanya na kile alimhitaji kakake Yaredi afanye vilikuwa tofauti kwa kila shida. Kutoka kwa kila shida na suluhisho, tunaweza kujifunza ukweli tofauti kuhusu jinsi Bwana hutusaidia tunapohitaji usaidizi. Linganisha suluhisho ulizoandika katika chati na yale katika orodha ifuatayo:

Hakuna hewa (Etheri 2:20–21). Ili kutatua shida hii, Bwana alimwambia kaka ya Yaredi kile alipaswa afanye. Kaka ya Yaredi kisha alikuwa na imani kufuata maelezo ya Bwana.

Hakuna usukani (Etheri 6:4–9). Ili kutatua shida hii, Bwana alitoa suluhisho kwa shida Mwenyewe.

Hakuna mwangaza (Etheri 2:22–3:6). Ili kutatua shida hii, Bwana alimpa kaka ya Yaredi mwelekeo. Kaka ya Yaredi kisha alilazimika afikirie suluhisho kwa shida —kulingana na maarifa aliyokuwa nayo— na kuuliza idhini ya Bwana na usaidizi katika kuitekeleza.

Kutoka kwa kaka yake naYaredi aliyopitia, tunajifunza kanuni hii: Tunapojitahidi kutekeleza wajibu wetu ili kusuluhisha shida zetu, tunaweza kupokea usaidizi wa Bwana.Ukifikiria kuhusu uamuzi wa kibinafsi uliofikiria awali, kujua kanuni hii kunawezaje kukusaidia kupokea usaidizi ama mwongozo kuhusu uamuzi huu? Unafikiri Bwana angetarajia ufanye nini katika kufanya uamuzi wako?

  1. Andika aya katika shajara yako ya kujifunza maandiko ukielezea kile umejifunza kutoka kwa yale kaka ya Yaredi alipitia kuhusu maombi na kuhusu kupokea usaidizi wa Bwana na mwongozo katika maisha yako.

  2. Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimesoma Etheri 1–2 na kukamisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningetaka kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha