Seminari
Mosia


Utangulizi wa Mosia

Kwa nini Ujifunze Kitabu Hiki?

Katika kujifunza kwako kwa kitabu cha Mosia, utasoma shuhuda za nguvu za misheni ya Yesu Kristo. Pia utajifunza kuhusu watu ambao Bwana aliwakomboa kutoka utumwani wa dhambi au kutoka kwa udhalimu wa kimwili. Zaidi ya hayo, utajifunza jinsi juhudi za wema za watu kama vile Mfalme Benyamini, Abinadi, na Alma zilileta baraka nyingi sana kwa wengine. Kinyume chake , utaona jinsi chaguo mbaya za watu kama vile Zenifu na mwanawe, Mfalme Nuhu, zilileta matokeo hasi juu yao wenyewe na watu wao .

Nani Aliandika Kitabu Hiki?

Mormoni alikusanya na kufupisha kumbukumbu za waandishi kadha wengine ili kuunda kitabu cha Mosia. Kitabu hiki kinaitwa jina la Mosia, ambaye alikuwa mwana wa Mfalme Benyamini. Mosia alikuwa nabii, mwonaji, mfunuaji, na mfalme ambaye alitawala Zarahemla kutoka takriban miaka 124 hadi 91 Kabla Kristo Aliitwa kama babu yake Mosia, ambaye pia alikuwa mfalme wa Zarahemla (ona Omni 1:12–13, 19).

Mormoni alichukua kutoka kwa kumbukumbu kadhaa ili kutengeneza kitabu cha Mosia. Alifupisha na kunukuu kutoka kwa kumbukumbu zilizowekwa na Mosia kwenye mabamba makubwa ya Nefi, ambayo yalikuwa na utondoti wa historia ya Nefi katika nchi ya Zarahemla (ona Mosia 1–7; 25–29). Pia alichukua kutoka kwa kumbukumbu ya Zenifu, ambayo inasimulia historia ya watu wa Zenifu kutoka wakati walipoondoka Zarahemla mpaka waliporudi (ona Mosia 7–22). Kwa nyongeza, Mormoni alidondoa kutoka kwa na sehemu zilizofupishwa za maandishi ya Alma, ambaye alihifadhi maneno ya Abinadi (ona Mosia 17:4) na kuweka kumbukumbu za watu wake mwenyewe (ona Mosia 18; 23–24).

Kiliandikwa Lini na Wapi?

Kumbukumbu za asili zilizotumiwa kama vyanzo vya kitabu cha Mosia yawezekana kuwa ziliandikwa kati ya miaka 200 Kabla ya Kristo na 91 Kabla ya Kristo Mormoni alizifupisha kumbukumbu hizo wakati fulani kati ya miaka 345 na 385Baada ya Kristo. Mormoni hakuandika mahali alipokuwa wakati alipokusanya kitabu hiki.

Chapisha