Kitengo cha 11: Siku ya 2
Mosia 3
Utangulizi
Akiendelea na hotuba yake kwa watu wake, Mfalme Benyamini aliwaambia wao kwamba malaika ameongea naye kuhusu huduma ya Yesu Kristo. Mfalme Benyamini alishuhudia kwamba kupitia imani katika Yesu Kristo na toba, wale ambao wametenda dhambi wanaweza kupokea wokovu. Pia alifunza kwamba kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo mtu anaweza kushinda mtu wa kawaida kwa kujiweka chini ya ushawishi wa Roho Mtakatifu.
Mosia 3:1–10
Mfalme Benyamini anatoa hutoa maneno ya malaika kuhusu Upatanisho
Unapojifunza Mosia 3, tafuta chanzo cha “habari njema ya shangwe kuu” (Mosia 3:3).
Soma Mosia 3:1–5, na utafute kile malaika alimwambia Mfalme Benyamini. Malaika alitangaza kwamba watu wa Mfalme Benyamini walikuwa na sababu ya kufurahia na kujawa na shangwe.
Ni kitu gani katika ujumbe wa malaika ambacho kingewajaza Wanefi na shangwe?
Soma Mosia 3:5–10, na uweke alama maneno au vishazi kuhusu Mwokozi na huduma Yake ambavyo vinakusaidia kufahamu vyema huduma ya Mwokozi duniani.
-
Chagua vishazi viwili ulivyoweka alama, na uandike maelezo katika shajara yako ya kujifunza maandiko kuhusu kile vinakufunza ili kukusaidia uelewe vyema na kuthamini huduma ya Mwokozi.
Kuna mafundisho mengi na kanuni nyingi zilizofunzwa katika Mosia 3:5–10. Moja ya zile muhimu ni hii: Yesu Kristo aliteseka ili sisi tuweze kuokolewa kutoka kwenye dhambi zetu. Fikiria kuandika fundisho hili katika maandiko yako karibu na Mosia 3:7–9.
Baada ya kusoma Mosia 3:7–9, soma Luka 22:44 na Mafundisho na Maagano 19:16–18. Ni umaizi gani wa ziada unatolewa na Mosia 3? Ni kwa jinsi gani Mosia 3 inatusaidia kufahamu kile kilichomtokea Mwokozi?
Soma kauli ifuatayo ya Mzee James E. Talmage wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili kuhusu kuteseka kwa Mwokozi katika Bustani ya Gethsemane:
“Masumbuko makali ya Kristo katika bustani ile hayawezi kueleweka na akili yenye kikomo, yote kwa uzito na jinsi. Yeye alisumbuka na kugumia chini ya mzigo ambao hakuna mtu mwingine ambaye aliishi ulimwenguni angeweza hata kuelewa kabisa. Haikuwa uchungu kwa kimwili, wala mateso ya kiakili peke yake, ambayo yalimsababishia yeye kuteseka kwa mateso yaliyopelekea kutokwa na damu kutoka kwa kila kinyweleo; lakini masumbuko ya kiroho ya nafsi ambayo tu Mungu ndiye aliyeweza kupitia. Katika saa ile ya masumbuko Kristo alikutana na kushinda hofu zote ambazo Shetani, ‘mkuu wa ulimwengu huu’ [John 14:30] anazoweza kutenda.
Kwa jinsi fulani, kikweli na vibaya sana ingawa kwa mtu haiwezi kueleweka, Mwokozi alijichukulia juu Yake Mwenyewe mzigo wa dhambi za wanadamu kutoka kwa Adamu hadi mwisho wa dunia” (Jesus the Christ, 3rd ed. [1916], 613).
-
Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika kuhusu uzoefu ambao umekusaidia kujua kwamba Yesu Kristo ndiye Mwokozi. Ni kwa jinsi gani kukumbuka uzoefu huu kunaongezea shangwe katika maisha yako?
Mosia 3:11–27
Mfalme Benyamini anaelezea jinsi ya kumshinda mtu wa kawaida
Mfalme Benyamini anapoendelea kuwafunza watu wake, aliwafundisha jinsi Upatanisho hubariki watoto wa Mungu. Pia alifundisha jinsi tunavyoweza kumshinda mtu wa kawaida na kuwa Watakatifu kupitia Upatanisho wa Mwokozi.
Ili kuelewa vyema jinsi Upatanisho hubariki watoto wa Mungu, soma vifungu vya maandiko vifuatavyo na uandike maelezo ya kundi la watu ambalo aya hii husuhudia watabarikiwa kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo:
Ni muhimu kujua kwamba ingawa Yesu Kristo alipatanisha kwa ajili ya dhambi za wale wasiojua injili—wale wanaokufa katika ujinga —sharti bado watubu na kufanya imani katika Yesu Kristo katika ulimwengu wa roho ili waokolewe (ona M&M 131:6; 138:31–34). Pia, Bwana amefunua kwamba watoto huzaliwa wakiwa mausumu katika macho ya Mungu na kwamba Shetani hana uwezo wa kuwajaribu. Mpaka wanapofikia uwajibikaji katika umri wa miaka nane, watoto wadogo wanaokolewa kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo bila haja ya kutubu au kubatizwa (ona Moroni 8:8–15; M&M 29:46–47; 137:10).
Ni sharti tuitendee kazi elimu tuliyonayo ya injili ya Yesu Kristo. Soma Mosia 3:12–13, na uweke mstari maneno na vishazi ambavyo vinafunza kwamba tunaweza kuokolewa kutoka kwenye dhambi zetu na kufurahia tunapofanya imani katika Yesu Kristo na kutubu.
Kumbuka picha ya kikombe ambacho kilijazwa na “furaha.” Kumbuka maneno ya malaika akitangaza kwamba shangwe hutokana na kuelewa huduma na Upatanisho wa Mwokozi (ona Mosia 3:4–5). Ili kuelewa kinyume cha picha hii, soma Mosia 3:24–27. Weka mstari kile wale ambao wanachagua kutotubu watakunywa siku ya hukumu.
Ni nini kitatokea kwa wale ambao wanachagua kutofanya imani katika Yesu Kristo na kutubu?
Baada ya kuwafundisha watu wake kuhusu Upatanisho wa Mwokozi ana haja ya kutubu na kuwa na imani katika Mwokozi, Mfalme Benyamini aliwafundisha watu wake jinsi ya kuvua sehemu ya dhambi ya uhalisi wao na kuwa Watakatifu kupitia Upatanisho.
Soma Mosia 3:19, na utambue maneno au vishazi vyovyote usivyovielewa. Inaweza kusaidia kuandika maelezo matatu katika maandiko yako karibu na aya hii. “Mtu wa kawaida” ni mtu ambaye huchagua kushawishiwa na tamaa, hamu, na njaa za kimwili badala ya minong’ono ya Roho Mtakatifu. “Kujitoa” humaanisha kujiweka chini ya mtu au kitu. “Vishawishi” ni mialiko ya kuvutia au kupendeza. Mosia 3:19 ni kifungu cha umahiri wa maandiko. Unaweza kutaka kukiweka alama kwa njia ya kipekee ili uweze kukipata hapo baadaye.
-
Andika kichwa “Kumvua Mtu wa Kawaida” katika shajara yako ya kujifunza maandiko. Chini ya kichwa hiki, orodhesha kile Mosia 3:19 anafundisha ni sharti tufanye ili kumshinda “mtu wa kawaida.” Weka mviringo kitendo ambacho unahisi kingekuwa muhimu sana kwako kukishughulikia wakati huu. Weka mpango wa kutumia kitendo hiki.
Moja ya kanuni Mosia 3:19 anafundisha ni kwamba kama tukikubali vishawishi vya Roho Mtakatifu, tunaweza kumshinda mtu wa kawaida kupitia Upatanisho wa Kristo.
Kwa maneno yako mwenyewe, inamaanisha nini kukubali “ushawishi wa Roho Mtakatifu”?
Soma kauli ifuatayo kutoka kwa Mzee Neal A. Maxwell wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili kuhusu kumvua mtu wa kawaida: “Wema wa kibinafsi, wema, kuabudu, maombi, na kujifunza maandiko ni muhimu sana ili “kumvua mtu wa kawaida’ (Mosia 3:19)” (“The Tugs and Pulls of the World,” Ensign, Nov. 2000, 36).
-
Jibu swali lifuatalo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Ni kwa njia gani unatafuta kukubali ushawishi wa Roho Mtakatifu katika maisha yako?
-
Unaweza kufanya nini ili kukubali kabisa zaidi “ushawishi wa Roho Mtakatifu” katika maisha yako mwenyewe? Andika lengo katika shajara yako ya kujifunza maandiko ili kukusaidia kuboreka katika sehemu hii wiki hii. Unaweza kufikiria kushughulikia moja ya sifa ambazo zinatusaidia kuwa kama mtoto, zilizoorodheshwa katikaMosia 3:19—kwa mfano, kuwa mtiifu, mpole, mnyenyekevu, mvumilivu, mwenye upendo tele, au kuwa tayari kukubali vitu vyote ambavyo Bwana anaona “sawa akupatie” wewe.
-
Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko baadhi ya vikwazo katika maisha yako ambavyo vinakuzuia kukubali ushawishi wa Roho.
Umahiri wa Maandiko—Mosia 3:19
-
Ili kukusaidia kukumbuka au kukariri Mosia 3:19, unaweza kutaka kukisoma chote mara tatu. Kurudiarudia kutakusaidia kuwa na mazoea na maudhui ya aya hii. Baada ya kufanya hivi, jaribu kuandika mengi ya aya hii, ua mawazo katika haya hii, kama unavyoweza katika shajara yako ya kujifunza maandiko bila kuangalia maandiko yako. Jaribu kurudia aya hii kwa sauti mara nyingi, kama unapotembea, unapofanya mazoezi, au unapojitayarisha kulala. Kufanya hivi kwa siku kadhaa mfululizo kunaweza kukusaidia kukariri na kukumbuka kanuni muhimu katika haya hii.
-
Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi za leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
Nimejifunza Mosia 3 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).
Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningependa kushiriki na mwalimu wangu: