Kitengo cha 17: Siku ya 4
Alma 23–24
Utangulizi
Kufuatia uongofu wake, mfalme wa Walamani alitangaza uhuru wa kidini miongoni mwa watu wake. Tangazo hili lilimruhusu Haruni na ndugu zake kuhubiri injili na kuanzisha makanisa katika miji mingi ya Walamani. Maelfu ya Walamani waliongoka na kamwe hawakuanguka. Wale Walamani walioongoka kwa Bwana walifanya agano wa kuweka chini silaha zao za vita. Walijichukulia juu yao jina la Waanti-Nefi-Lehi. Wakati Walamani wasioongoka walipowashambulia, wengi wa Waanti-Nefi-Lehi walijitolea maisha yao badala ya kuvunja agano lao.
Alma 23
Maelfu ya Walamani waliongelewa kwa Bwana na kubadili jina yao kuwa Waanti-Nefi-Lehi
-
Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, chora picha ya sura ya furaha na sura ya huzuni. Weka kitambulisho sura yenye furaha Mwaminifu na sura yenye huzuni asiyefuata utaratibu. Unaposoma maelezo yafuatayo kutoka kwa Mzee Richard G. Scott wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, tafuta maneno au vishazi vinavyoelezea aina hizi mbili tofauti za watu. Andika maneno haya au vishazi chini ya picha ifaayo.
“Kila mmoja wetu ameona jinsi watu wengine wanapitia maisha kila siku kwa kufanya mambo ya haki. Wanaonekana wenye furaha, hata wachangamfu kuhusu maisha. Wakati chaguo ngumu zinatakiwa kufanywa, wanaonekana kufanya chaguo sahihi kila wakati, hata kama kulikuwa na vivutia mbadala kwao. Tunajua kwamba wanaweza kujaribiwa, lakini walionekana kutotambua hayo. Vile vile, tumeona jinsi wengine si hodari katika maamuzi wanazofanya. Katika mazingira ya kiroho yenye nguvu, wanaamua kufanya vizuri, ili kubadilisha mwelekeo wa maisha yao, kwa kuweka kando tabia za kudhoofisha. Ni waaminifu sana katika uamuzi wao wa kubadilika, lakini kwa haraka wanarudia tena yale mambo waliyoamua kutofanya.
“Ni nini ambacho huleta tofauti katika maisha ya makundi haya mawili? Ni kwa jinsi gani unaweza kufanya chaguo sahihi kila wakati?” (“Full Conversion Brings Happiness,” Ensign, May 2002, 24).
Tafakari jinsi utayajibu maswali mawili ambayo Mzee Scott aliuliza. Unapojifunza Alma 23–24, fikiria ni kwa nini washiriki wengi wa Kanisa hubakia waaminifu kwa injili ya Yesu Kristo katika maisha yao yote.
Baada ya mfalme wa Walamani kuongoka kwa injili ya Yesu Kristo, alituma tangazo miongoni mwa watu wake wote, na muujiza ulitokea. Maelfu ya Walamani pia walioongoka. Soma Alma 23:1–5 ili kuona tangazo lilikuwa gani na jinsi muujiza ulitokea.
Soma Alma 23:6–7. Ni maelfu mangapi ambao “walimgeukia Bwana” walibakia waongofu katika maisha yao?
Baada ya Walamani hawa kuongoka, walitaka kuitwa kwa jina jipya ili wasiweze tena kujulikana kama Walamani. Soma Alma 23:16–18, na utambue jina walilochagua na baraka ambazo ziliwajia kwa sababu ya uaminifu wao.
-
Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, chini ya mchoro uitwao “Mwaminifu,” andika kile ulichojifunza kutokana na Waanti-Nefi-Lehi kuhusu kuwa mwaminifu kwa Bwana katika maisha yako yote.
Andika ukweli ufuatao katika maandiko yako au shajara ya kujifunza maandiko: Uongofu unamaanisha kubadilika kiroho na kuwa mtu mpya kwa uwezo wa Mungu.} Kama vile Waanti-Nefi-Lehi walivyobadilika, ikiwa u tayari kupokea uwezo wa Upatanisho katika maisha yako kwa imani yako na toba, unaweza kuwa mtu mpya kwa uwezo wa Mungu na kubakia mwongofu maisha yako yote.
Angalia tena maswali ya mawili ya Mzee Scott, na kisha usome jibu lake: “Uongofu wa kweli ni matunda ya imani, toba, na utii thabiti. … Uongofu wa kweli utaimarisha uwezo wako wa kufanya kile unajua ni lazima ufanye, unapopaswa kukifanya, bila kujali hali” (“Full Conversion Brings Happiness,” 25).
-
Jibu swali lifuatalo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Kulingana na Alma 23:18, Walamani waongofu waliaanza kuwa wachapakazi na marafiki na Wanefi. Wakati watu wapojaribu kutubu na kubadilisha maisha yao, kwa nini ni muhimu kwao kushirikiana na wengine ambao pia wanajitahidi kuishi kwa haki?
-
Chunguza maneno uliyoorodhesha chini ya mchoro wa “Mwaminifu” katika shajara yako ya kujifunza maandiko. Fikiria jinsi maneno haya yanaweza kuelezea vyema kiwango chako cha uongofu. Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko yale utakayofanya ili kuongoka kikamilifu zaidi kwa Bwana.
Alma 24
Waanti-Nefi-Lehi wanaapa kutochukua silaha tena.
Kama ilivyoandikwa katika Alma 24:3, mfalme wa Walamani alikabithi ufalme juu ya mwanawe kabla ya kifo chake, na akampa mwanawe jina Anti-Nefi-Lehi. Soma Alma 24:1–5 ili kuona ni tatizo gani lililotokea kwa haraka ambalo liliwafanya Amoni na ndugu zake kufanya baraza pamoja na mfalme. Wakati ilipojulikana kwamba Walamani wasioongoka walikuwa wakienda vita dhidi ya wa Waanti-Nefi-Lehi, watu hawa wema waliamua kutofanya maandalizi ili kujitetea (ona Alma 24:6 ). Soma Alma 24:7–14, na utambue ni kwa nini wa Waanti-Nefi-Lehi walifanya uamuzi huu.
-
Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika kile ulichojifunza kutoka kwa Waanti-Nefi-Lehi kuhusu maana ya kuacha dhambi zetu tunapotubu.
Soma Alma 24:15–18, ukiangalia kile Waanti-Nefi-Lehi walifanya ili kuonyesha Bwana kwamba walikuwa wametubu kwa kweli. Kwa nini watu walizika panga zao na silaha zingine chini katika ardhi? (Ona Alma 24:17–18.)
Katika maisha yetu wenyewe tunapotubu dhambi, tunapaswa kujitahidi ili kamwe tusitende dhambi hizo tena. Soma kile Rais Spencer W. Kimball alifundisha kuhusu kuacha dhambi kama kipengele muhimu ya toba: “Katika kuacha dhambi mtu hawezi tu kutamani hali bora zaidi. Lazima azitengeneze. … Lazima awe na hakika si tu kwamba ameacha dhambi bali kwamba amebadilisha hali inayo sababisha dhambi. Anapaswa kuepuka maeneo na hali na mazingira ambapo dhambi ilitokea, kwani hizi zinaweza kuzieneza tena. Ni lazima aachane na watu waliohusishwa na dhambi hiyo. Pengine hatawachukia watu wanaohusika lakini ni lazima aepukana nao na kila kitu kinachohusishwa na dhambi. Ni lazima ajenge maisha mapya. Ni lazima aondoe kitu chochote ambacho kinaweza kuamsha mawazo ya zamani” (The Miracle of Forgiveness [1969], 171–72).
Katika Alma 24:10–12, weka alama kwa maneno au vishazi vinavyoonyesha toba ya Waanti-Nefi-Lehi na msamaha wa Mungu kwa dhambi zao. Andika kanuni ifuatayo katika pambizo karibu na mistari hii: Tukifanya yote tunayoweza ili kutubu, Mungu ataondoa hatia yetu na kutusaidia kubakia wasafi. Rejea maelezo ya Waanti-Nefi-Lehi wakizika silaha zao chini ya ardhi. Katika siku zetu, bado tunahitaji “kuzika” dhambi zetu ili kuonyesha Bwana kwamba tunafanya yote tunayoweza ili kutubu na kutotenda dhambi hiyo tena.
-
Fikiria jinsi watu katika hali zifuatazo wanaweza kuhakikisha kwamba hawatatenda dhambi kama hizo tena. Andika mapendekezo yako kwa kila hali katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
-
Mtu mwengine alitazama picha za ngono katika sinema kwa sababu marafiki zake walimhimiza kutazama sinema hiyo pamoja nao.
-
Mtu mwengine alivunja kisiri Neno la Hekima pamoja na marafiki wakati kikundi kilipotembea pamoja wakati wa usiku.
-
Mtu fulani alishiriki majibu kutoka kwa mtihani uliokamilika na rafiki aliyekuwa akijiandaa kufanya mtihani huo huo siku hiyo.
-
Tafakari swali lifuatalo: Ni nini unahitaji “kuzika” katika maisha yako ili usijaribiwe kutenda dhambi ambazo ulizotubu?
Soma Alma 24:19–22 ili uone kile Waanti-Nefi-Lehi walifanya wakati Walamani walipokuja kupigana dhidi yao. Watu hawa walionyesha kujitolea kwao kwa Bwana kwa kuwa tayari kufa kuliko kuvunja ahadi waliyoifanya kwa Bwana. Walikuwa wametoa maisha yao kabisa kwa Bwana, na walibakia kabisa waaminifu Kwake katika maisha yao yote.
Soma kile Rais Ezra Taft Benson alifundisha kuhusu kutoa maisha yetu kwa Bwana;
“Watu waliobadilika kwa ajili ya Kristo wataongozwa na Kristo. Kama Paulo watakuwa wakimuuliza, ‘Bwana, yanipasa nifanye nini? ( Matendo ya Mitume 9:6.) …
“Mapenzi yao yamemezwa katika mapenzi Yake. (Ona Yohana 5:30.)
“Wao hufanya mambo yanayompendeza Bwana. (Ona Yohana 8:29.)
“Siyo tu kwamba watakufa kwa Bwana, lakini muhimu zaidi wanataka kuishi kwa ajili Yake.
“Ingieni majumbani mwao, na picha kwenye kuta zao, vitabu juu ya rafu zao, muziki hewani, maneno yao na matendo yanawaonyesha wao kama Wakristo.
“Wanasimama kama mashahidi wa Mungu nyakati zote, na katika vitu vyote, na katika mahali popote. (OnaMosia 18:9.)
“Wana Kristo katika mawazo yao, wanapomtazamia Yeye katika kila wazo. (Ona M&M 6:36.)
“Wana Kristo katika mioyo yao kwani mapenzi yao yameelekezwa Kwake milele. (Ona Alma 37:36.)” (“Born of God,” Ensign, Nov. 1985, 6–7).
-
Jibu swali lifuatalo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Wakati wa wiki hii, ni kwa njia gani unaweza kuonyesha kwamba umetoa maisha yako kabisa kwa Bwana?
SomaAlma 24:23–27, ambayo inaeleza majibu ya Walamani walipoona kwamba Waanti-Nefi-Lehi hawakuwa wakienda kupigana. Unaposoma, tafuta maneno au vishazi vinavyofundisha kanuni hii: Kwa kuwa mwaminifu kwa Bwana, tunaweza kuwasaidia wengine kuwa waongofu. Fikiria jinsi washiriki wengine wa familia zao au marafiki wengine wanaweza kushawishiwa na uamuzi wako wa kuwa mwaminifu kwa Bwana.
-
Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
NimejifunzaAlma 23–24 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).
Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu: