Seminari
Utangulizi wa mpango wa mafunzo ya seminari nyumbani.


Utangulizi wa mpango wa mafunzo ya seminari nyumbani

Mpango wa mafunzo ya seminari nyumbani umebuniwa kukusaidia kuimarisha uelewa wako wa injili ya Yesu Kristo na kutumia mafundisho yake katika maisha yako ya kila siku kupitia mafunzo ya maandiko. Kwa mafunzo yako mwaka huu,utatakiwa kwanza umalize mazoezi ya kusoma kutoka kifungu cha maandiko ya kozi hii—kitabu cha Mormoni—na ndipo utamaliza somo mojamoja. Mara moja kwa wiki, utakutana na mwalimu wa seminari ili uwasilishe kazi yako na ushiriki katika somo la wiki.

Seminari ni mpango wa kila siku wa elimu ya kidini. Kujifunza maandiko yako kwa maombi iwe ni desturi yako kila siku. Itakuhitaji ufanye mazoezi yako ya seminari kila siku ya shule, hata kama hutahudhuria darasa la seminari kila siku. Kuna vitengo 32 vya kumalizwa wakati wa kozi. Chati cha kusoma kwenye kurasa Viii kinaonesha nini unatakiwa kujifunzae kutoka kila kitengo. Mwalimu wako atakusaidia uelewe wakati kila kitengo kinapokuwa tayari Masomo katika mwongozo huu wa kujifunza kila moja yanatakiwa kuchukuwa takribani dakika 30 kumalizika, ukijumuisha mafunzo yako ya maandiko ya kila siku.

Huna budi uwe na mashajara mawili ya mafunzo ya maandiko (au madaftari mawili), tenganisha kutoka mashajara yako binafsi, ambamo utaandika mazoezi kutoka shughuli za muongozo wa mafunzo. Kila wiki ambayo unakutana na mwalimu wako, huna budi kukabithi shajara la mafunzo ya maandiko lililo na mazoezi yaliyokamilika kutoka shughuli za muongozo wa mafunzo uliyokamilisha wiki ile. Mwalimu wako atasoma na kujibu mazoezi na kukurudishia shajara lile la mafunzo ya maandiko kwako wiki inayofuata. Unaweza pia kuandika majibu yako kwenye karatasi katika daftari lisilounganishwa na upatiane kurasa ulizozifanya wiki ile. Kisha,wakati mwalimu wako anarudisha zile kurasa, unaweza kuzirudisha katika dafutari.

Kutumia shajara hili katika mpango wa seminari wa kila siku

Kitabu hiki cha kiada kinaweza kutumika na waalimu na wanafunzi katika mpango wa seminari wa kila siku kuongeza ubora wa masomo au kwa kazi ya fidia. Hata hivyo, hakikusudiwi kupewa kila mwanafunzi waseminari wa kila siku. Kama mwanafunzi anataka kufidia somo alilolikosa, mwalimu anaweza kumpangia amalize somo la mafunzo nyumbani ambalo linafanana na somo ambalo alilikosa.

Kutumia kitabu cha kiada cha mwanafunzi wa mafunzo nyumbani.

Picha
Mwongozo wa kujifunza ukurasa wa 17

Chati ya Kusoma Kitabu cha Mormoni

Picha
Book of Mormon Reading

Karibu kwenye Kitabu cha Mormoni

Kitabu cha Mormoni ni nini?

Kitabu cha Mormoni ni ushuhuda mwingine wa Yesu Kristo. Kina maandiko ya manabii wa zamani, wakitoa maelezo ya shughuli za Mungu na tawi moja la Nyumba ya Israel kwenye kontinenti la merikani. Kwa Watakatifu wa siku za mwisho kitabu cha Mormoni kinasimama ubavuni mwa Biblia, Mafundisho na maagano,na Lulu ya thamani kuu kama maandiko matakatifu. Kitabu cha Mormoni ni kumbukumbu ya ustaarabu mkubwa wa zamani - Merikani.

Tangu kilipochapishwa kwa lugha ya Kiingereza mnamo 1830, kitabu cha Mormoni kimetafsiriwa katika lugha nyingi, na nakala zilizo chapishwa ni zaidi ya milioni 150. Kimeelezwa na Manabii wa Mungu kama jiwe la “msingi” la Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa siku za mwisho.

Ni kwa nini mafunzo ya kitabu cha Mormoni ni muhimu kwangu?

Rais Ezra Taft Benson alifundisha kwamba baraka za kuwa karibu zaidi na mungu zinakusubiri wewe unapojifunza Kitabu cha Mormoni kwa moyo wa dhati:

“Je, Si kuna kitu ndani ya mioyo yetu ambacho kina shauku ya kumsogelea Mungu zaidi, kuwa zaidi kama Yeye katika matembezi yetu ya kila siku,kuhisi uwepo wake pamoja nasi daima? Kama ndivyo, basi kitabu cha Mormoni kitatusaidia kufanya hivyo kuliko kitabu kingine chochote.

Sio tu kwamba kitabu cha Mormoni kinafundisha ukweli, ingawa kweli kinafanya hivyo. Sio tu kwamba Kitabu cha Mormoni kinatoa ushuhuda wa Kristo, ingawa kweli kinafanya hivyo, pia. Lakini kuna kitu kingine zaidi. Kuna nguvu katika kitabu ambayo inaanza kutiririka katika maisha yenu wakati unapoanzaMafunzo ya dhati ya kitabu. Utapata nguvu kubwa ya kujizuia na majaribu.Utapata nguvu ya kuepuka undanganyifu. Utapata nguvu ya kubaki kwenye njia ndefu na nyembamba. Maandiko yanaitwa ‘maneno ya uzima’(ona MM 84:85), na hakuna popote palipo na kweli nyingi kuliko ilivyo katika Kitabu cha Mormoni. Utapoanza kuwa na njaa na kiu ya maneno haya, utapata uzima kwa wingi mkuu na mkuu sana” (“The Book of Mormon—Keystone of Our Religion,” 7).

:Kitabu cha Mormoni kiliandikwa kwa ajili yetu leo. Mormoni, nabii wa zamani ambaye kitabu kimeitwa kwa jina lake, na mwanae wa kiume Moroni walifupisha kumbukumbu za karne walipo kuwa wanakusanya mabamba ya dhahabu ambayo kutokana nayo, Nabii Joseph Smith alitafsiri Kitabu cha Mormoni. Mungu, ajuaye mwisho kutoka mwanzo, aliwapatia mwongozo manabii Wake juu ya kile watajumuisha katika ufupisho ambao tungehitaji kwa siku zetu. Moroni, ambaye alikuwa wa mwisho wa manabii kuandika katika Kitabu cha Mormoni, alitabiri wakati wetu: “Tazama, nasema kwenu kama vile mpo,na lakini hampo. Lakini tazama,Yesu Kristo amewaonesheni nyie kwangu,na ninajua mnachofanya” (Mormoni 8:35).

Rais Benson alifundisha pia kwamba kujifunza kitabu cha Mormoni kutawasaidia kutambua kati ya mazuri na maovu:

Kitabu cha Mormoni huleta watu kwa Kristo kupitia njia mbili za msingi. Kwanza, kinatueleza katika njia ya wazi kuhusu Kristo na injili yake. Kina shuhudia juu ya Uungu wake na ya ulazima wa mkombozi na haja ya kuweka matumaini yetu kwake. Kina toa ushahidi wa anguko na upatanisho na kanuni za kwanza za injili, pamoja na haja yetu ya Moyo uliovunjika na roho iliyopondeka. Kinatangaza kwamba hatuna budi kuvumilia mpaka mwisho katika uadilifu na kuishi maisha mema ya mtakatifu.

“Pili, Kitabu cha Mormoni kinawafunua maadui wa Kristo. Kina duwaza mafundisho ya uongo na kinaondoa mabishano.(ona2 Ni.3:12. Kina waimarisha wafuasi wanyenyekevu wa Kristo dhidi ya mipango miovu, mikakati, na mafunzo ya ibilisi katika siku yetu. Aina za ukengeufu katika Kitabu cha Mormoni zinafanana na zile tulizonazo leo. Mungu, pamoja na uwezo wake usio na kikomo wa kujua kitu kabla hakijatokea, basi akakiunda Kitabu cha Mormoni ili tuweze kuona makosa na kujua jinsi ya kupambana na falsafa za uongo, kisiasa, kidini,na fikra za kifalsafa za wakati wetu”(“Kitabu cha Mormoni ni Neno la Mungu,”Ensign,May1975, 64).

Kuhusu Kitabu cha Mormoni

Kitabu cha Mormoni kimetengenezwa kutokana na vitabu 15 vidogo. Nane kati ya vitabu hivi vinaanza na vichwa vya habari ambayo iliandikwa kwenye mabamba asilia ya dhahabu yaliyotafsiriwa na Nabii Joseph Smith:1 Nefi,Yakobo,Alma,Helamani,3 Nefi,4 Nefi,na Etheri. Sura zingine katika kitabu cha Mormoni zimetanguliwa pia na kichwa cha habari ambacho kiliwekwa pamoja kwenye mabamba asilia ya dhahabu(isipokuwa kwa sentensi zinazohusu sura zilizo wekwa ndani): Mosia 9,Mosia 23,,Alma 5,Alma 7,Alma 9,Alma 17,,Alma 21,Alma 36,,Alma 38,Alma 39,Alma 45,Helamani 7,Helamani 13,,3 Nefi{11,na Moroni 9

Mwanzoni mwa kila sura katika kitabu cha Mormoni, kuna muhutasari mfupi wa sura uliochapishwa katika italiki. Mihutasari hii ya sura iliandikwa na kujumuishwa chini ya maelekezo ya Urais wa Kwanza na haikuwa sehemu ya maandiko ya asili ya Kitabu cha Mormoni kutoka mabamba ya dhahabu.

Chapisha