Kitengo cha 1: Siku ya 4
Maelezo ya Jumla ya Kitabu cha Mormoni
Utangulizi
Nabii Joseph Smith alieleza matokeo yaliyofuatia kuja kwa Kitabu cha Mormoni. Kwa kujifunza maelezo yake, ushuhuda wako wa wito wake wa kinabii na wa jukumu tukufu la Kitabu cha Mormoni katika Urejesho wa injili timilifu ya Yesu Kristo unaweza kuongezeka. Somo hili litakusaidia pia kuwa na uzoefu zaidi wa jinsi Kitabu cha Mormoni kiliandikwa zamani. Nabii Mormoni na Moroni walishuhudia kuhusu maongozi ya Bwana walipokuwa wakiandika na kukusanya maandishi ya manabii wengine wengi katika mabamba ya dhahabu. Unapojifunza, tafuta ushahidi wa mkono wa Bwana katika kuleta Kitabu cha Mormoni na jukumu ambalo Kitabu cha Mormoni kinaweza kuwa nayo kwa kuongoza maisha yako.
“Ushuhuda wa Nabii Joseph Smith”
Unawezaje kujibu swali : “ Ni jinsi gani Kanisa lako lilipata Kitabu cha Mormoni?”
“Ushuhuda wa Nabii Joseph Smith” unapatikana katika nyenzo za utangulizi mwanzoni mwa Kitabu cha Mormoni, ina sehemu kutoka kwa Joseph Smith — Historia, inayopatikana kaitika Lulu ya Thamani Kuu. Inaelezea kuja kwa Kitabu cha Mormoni kwa maneno ya Nabii mwenyewe. Unahimizwa kusoma maalezo yake yote kutoka Joseph Smith — Historia wakati wa masomo yako ya maandiko ya kila siku.
Kwa sababu “Ushuhuda wa Nabii Joseph Smith” haujumuishi nambari za mistari, somo hili litarejelea Joseph Smith — Historia ili kukurahisishia kupata kazi ya kusoma. Unapojifunza Ushuhuda wa Nabii Joseph Smith, tafuta ushahidi kuwa Kitabu cha Mormoni kilikuja kwa uwezo wa Mungu
Soma Joseph Smith—Historia 1:29–35, 42–43, na piga mstari maelezo ya ziara ya Moroni kwa Joseph Smith ambayo ungejumuisha kama ungekuwa unaelezea matokeo haya kwa mtu mwingine Katika Joseph Smith—Historia 1:34, ni nini Moroni alisema yalikuwa kwenye mabamba ya dhahabu ?
-
Jibu maswali yafuatayo katika jarida lako la masomo ya maandiko: Ni nini kitu kimoja katika Joseph Smith—Historia 1:29–35, 42–43 ungetaka kuhimiza kama ungekuwa unashiriki maelezo haya na mtu mwingine? Kwa nini kina umuhimu kwako?
-
SomaJoseph Smith—Historia 1:51–54, kisha nakili mawazo yako kuhusu maswali yafuatayo katika jarida lako la masomo ya maandiko: Ni nini Joseph Smith alijifunza wakati wa ziara zake za kila mwaka na Malaika Moroni? Unadhania ni kwa nini ilikuwa muhimu kwa Joseph Smith kuwa na msimu huo wa miaka nne ya mafunzo kabla ya kupokea na kutafsiri mabamba?
Baada ya msimu wa kutayarishwa na kufunzwa, Joseph Smith alipewa mabamba mnamo 1827 na jukumu la kuyatafsiri kwa kipawa na uwezo wa Mungu. Soma Joseph Smith—Historia 1:59–60, na utambue agizo aliyopewa kuhusu mabamba ya dhahabu.
“Maelezo Mafupi kuhusu Kitabu cha Mormoni”
Ili kuelewa jinsi Kitabu cha Mormoni kimepangwa, soma “Maelezo Mafupi kuhusu Kitabu cha Mormoni” ambayo inapatikana baada ya “Ushuhuda wa Nabii Joseph Smith” Linganisha kile unasoma na vielelezo vinavyopatikana mwishoni mwa somo hili, ambavyo vinaonyesha jinsi makundi ya mabamba yanapatana pamoja kutengeneza rekodi ya Kitabu cha Mormoni.
Watu wengi binafsi walihudumu kama walinzi wa rekodi katika historia ya Wanefi na Walamani, kuanzia Lehi na kukamilika zaidi ya miaka 1,000 baadaye na nabii-mwanahistoria Mormoni na na mwanae Moroni. Mormoni aliongozwa na Bwana kufupisha maandiko ya manabii hawa wa kale na historia ya miaka 1,000 ya watu wake. Ufupisho wake ulirekodiwa katika mabamba ya Mormoni, yanayojulikana pia kama mabamba ya dhahabu. Kufuatia kifo cha Mormoni, bi wake Moroni alimaliza rekodi na mabamba yalifichwa hadi wakati yalipewa kwa Nabii Joseph Smith.
Helamani 3:13–15 ni moja wapo wa baadhi ya vifungu ambavyo Moroni anaelezea kuhusu ufupisho wa rekodi ya Wanefi. Unapokisoma, fahamu kuwa kulikuwa na mengi zaidi yaliyoandikwa kushinda yale Mormoni na Moroni waliweza kujumuisha kwenye mabamba ya dhahabu.
Soma Maneno ya Mormoni na Mormoni 8:34–35. Tilia mkazo maneno na vishazi vinavyoeleza jinsi Bwana alisaidia na kuongoza Mormoni na Moroni walipokuwa wakikusanya rekodi ya Kitabu cha Mormoni.
-
Jibu swali lifuatalo katika jarida lako la masomo ya maandiko: Kama ungekuwa Mormoni au Moroni na ungekuwa na jukumu la kufupisha wingi wa maandiko ya kinabii kwa rekodi moja, ungeamua vipi ya kujumuisha katika ufupisho wako?
Kutoka kwa mistari hii tunaweza kuona kuwa waandishi wa Kitabu cha Mormoni waliona siku yetu na waliandika yale yangekuwa ya maana zaidi kwetu. Unaweza kutaka kuandika haya katika maandiko yako kando ya Mormoni 8:35.
Rais Ezra Taft Benson alishuhudia kuwa Kitabu cha Mormon “kiliandikiwa siku yetu” na alieleza jinsi kujua hii kunaweza kutusaidia tunapojifunza Kitabu cha Mormoni.
Wanefi hawakuwahi kuwa na kitabu hiki, wala hata Walamani wa kale. Kilikusudiwa kiwe chetu Mormoni aliandika karibu na hitimisho la ustaarabu wa Wanefi. Chini ya uongozi wa Mungu, ambaye anaona mambo yote kwanzia mwanzo, alifupisha karne za rekodi, akichagua hadithi, hotuba, na matokeo ambayo yangekuwa ya maana zaidi kwetu. …
“Kama waliona siku zetu, na wakachagua mambo yale ambayo yangekuwa ya thamani kuu kwetu, hivyo sivyo tunavyopaswa kujifunza Kitabu cha Mormoni? Tunapaswa kujiuliza wenyewe kila mara, Kwa nini Bwana alimpatia maongozi Mormoni (au Moroni au Alma) kujumuisha hayo katika rekodi yake? Ni somo gani ninaweza kujifunza kutoka kwa hayo ili yanisaidie kuishi katika siku hizi na nyakati? (The Book of Mormon—Keystone of Our Religion,” Ensign, Nov. 1986, 6).
Kuuliza aina hii ya maswali unapojifunza kutakusaidia kugundua kanuni na mafundisho ambayo Bwana alijua yangekuwa ya maana kuu katika maisha yako.
Fikiri kuhusu maisha yako sasa hivi. Tafakari maswali ambayo unayo au hali unazokumbana nazo ambazo ungetaka kupokea mwongozo kutoka kwa Mungu Andika moja au mawili kati ya hayo katika jarida lako la kibinafsi (si jarida lako la masomo ya maandiko ambalo unaonyesha mwalimu wako ) Wakati wa masomo yako ya Kitabu cha Mormoni kila siku, tafuta kanuni ambazo zinatoa mwongozo na ushauri unaohusiana na hali hizi.
Kuhusu masomo ya kila siku ya maandiko, Rais Gordon B. Hinckley alisema: “Unaweza kufikiria kuwa uko na shughuli nyingi sana”. Dakika kumi au kumi na tano kila siku na maandiko matakatifu, na hasa na Kitabu cha Mormoni, inaweza kukupatia ufahamu wa ajabu wa kweli kuu za milele ambazo zimehifadhiwa na uwezo wa Mwenyezi Mungu kwa kubariki watoto Wake. Unaposoma … , utamkaribia Yule ambaye ni mtunzi wa wokovu wetu (“Rise to the Stature of the Divine within You,” Ensign, Nov. 1989, 97).
-
Tafakari lengo ambalo unaweza kuweka ambalo lingekusaidia kupata ya ziada kutoka kwa kusoma kwako Kitabu cha Mormoni mwaka huu. Nakili lengo lako katika jarida lako la masomo ya maandiko. Unaweza kutaka kuanzisha nyakati ya mazoea kutathmini maendeleo yako.
-
Andika yafuatayo chini ya kazi ya leo katika jarida lako la masomo ya maandiko:
Nimejifunza somo la “Maelezo ya Jumla ya Kitabu cha Mormoni” na kulikamilisha (siku).
Maswali, fikira na mawazo zaidi ningependa kushiriki na mwalimu wangu: