Seminari
4 Nefi


Utangulizi wa4 Nefi

Unajifunza Kitabu hiki kwa nini?

Katika mafunzo yako ya 4 Nefi, utashuhudia baraka zinazowajia watu wanoungana katika kuishi injili ya Yesu Kristo. Kitabu hiki kinafunua kwamba watu wote, nchini kote, waliongoka wakati wa huduma ya Mwokozi miongoni mwao. Kwa kutii amri, walifurahia amani, ustawi na baraka kuu za kiroho. Mormoni alitangaza, “Na kwa kweli hakujakuwa na watu ambao wangekuwa na furaha zaidi miongoni mwa watu wote ambao waliumbwa na mkono wa Mungu” (4 Nefi 1:16). Utajifunza pia mafunzo muhimu kutokana na kudidimia taratibu kwa watu hawa hadi katika hali ya uovu mkubwa.

Nani Alikiandika Kitabu Hiki?

Mormoni alikusanya na kufupisha kumbukumbu za waandishi wanne ili kuunda kitabu cha 4 Nefi. Wa kwanza wa hawa alikuwa Nefi, ambaye kwake kitabu kilipewa jina. Nefi alikuwa mwana wa Nefi aliyekuwa mmoja wa wanafunzi 12 waliochaguliwa na Bwana wakati wa huduma Yake miongoni mwa uzao wa Lehi (ona 3 Nefi 11:18–22; 12:1). Waandishi wale wengine watatu walikuwa Amosi mwana wa Nefi, Amosi mwana wa Amosi, na Amoroni kaka ya Amosi (ona 4 Nefi 1:19, 21, 47).

Kiliandikwa Lini na kiliandiki Wapi?

Kumbukumbu za asili zilizotumika kama vyanzo vya kitabu cha 4 Nefi huenda ziliandikwa kati ya miaka 34Baada ya Kristo na miaka 321 Baada ya Kristo. Mormoni alifupisha kumbukumbu hizo wakati fulani kati ya miaka 345 Baada ya Kristo.na miaka 385 Baada ya Kristo. Mormoni hakuandika pale alipokuwa alipotunga kitabu hiki.

Chapisha