Seminari
Kitengo 4: Siku 1, 1 Nefi 15


Kitengo 4: Siku ya 2

1 Nefi 15

Utangulizi

Katika 1 Nefi 15 utaona tofauti kati ya juhudi za Nefi za kupokea ufunuo wa kibinafsi na juhudi zisizo na imani za ndugu zake. Unapojifunza sura hii, tafakari juhudi unayofanya ili kupokea majibu na maongozi kutoka kwa Bwana.

1 Nefi 15:1–11

Ndugu za Nefi walilalamika kwamba hawakuweza kuelewa ono la Lehi.

Shughuli nyingi zinahitaji juhudi katika upande wetu kabla ya kuweza kupata matokeo. Fikiria juu ya shughuli ulizo wahi kushiriki—kama vile kazi za shule, kucheza chombo cha muziki, au riadha— na utafakari uhusiano kati ya juhudi unayoweka katika kila shughuli na matokeo ambayo yatafuata…Tafuta mfumo sawa unapojifunza1 Nefi 15. Tazama jinsi kuweka juhudi inahusiana na kujifunza kweli za kiroho na kupokea ufunuo kutoka kwa Bwana.

Baada ya kutafuta kwa bidii ili kuelewa ono la baba yake na mafundisho na baadaye kupokea ono lake mwenyewe, Nefi alirudi katika hema la baba yake. Pale aliwapata ndugu zake wakibishana wenyewe. Tafuta 1 Nefi 15:1–3, na utambue kile walikuwa wakijadili.

Katika 1 Nefi 15:6–7, weka mstari kile kiliwatatiza ndugu za Nefi na kusababisha mabishano. Kulingana na 1 Nefi 15:3, kwa nini ilikuwa ni vigumu kwao kuelewa mafundisho ya Lehi?

Soma 1 Nefi 15:8, na upige mstari chini ya swali ambalo Nefi aliwauliza ndugu zake. Kwa nini hili ni swali muhimu kwa Nefi kuuliza baada ya kile alichopitia?

Piga mstari chini ya majibu ya ndugu zake katika 1 Nefi 15:9. Neno kwani katika mstari huu unamaanisha kwa sababu. Kwa maneno menginie, Ndugu zake Nefi walieleza, “Sisi hatujauliza, kwa sababu Bwana haongei nasi.”

  1. Fikiria kuwa una rafiki ambaye haulizi Bwana kwa maelekezo kwa sababu yeye haamini kuwa Atajibu. Soma 1 Nefi 15:11, na utafakari ushauri ambao Nefi aliwapatia ndugu zake kuhusu kupokea majibu kutoka kwa Bwana. Kisha, katika shajara yako ya kujifunza maadiko, andika barua ukihimiza rafiki yako kuomba Mungu kwa imani. Shiriki ushauri wa Nefi na hisia zako mwenyewe kuhusu maombi katika barua.

Kanuni moja ya injili ambayo tunaweza kujifunza kutoka kwa matendo na uzoefu wa Nefi na ndugu zake ni kwamba kama tutamwomba Bwana kwa imani na kutii amri Zake, basi tutakuwa tayari kupokea ufunuo na mwongozo kutoka Kwake.

  1. Chagua moja ya maswali yafuatayo, na ulijibu katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Unaweza kusema nini ili kusaidia mshiriki mgeni wa Kanisa kuelewa kinachohitajika kutoka kwetu ili kufundishwa na kuongozwa na Bwana?

    2. Jinsi gani juhudi zako za kujifunza kweli za kiroho na kutafuta mwongozo wa Bwana kumeathiri uwezo wako wa kuhisi Roho na kuelewa injili?

Wakati mwingine katika siku ifuatayo, shiriki jibu lako kwa zoezi hilo na mzazi, mwanafamilia mwengine, kiongozi wa Kanisa, au mwalimu. Unapofanya hivyo , kumwalika mtu huyo kushiriki uzoefu pamoja nawe wakati alipoweka bidii na imani katika kutafuta usaidizi na mwongozo wa Baba wa Mbinguni.

1 Nefi 15:12–20

Nefi alielezea kutawanyika na kukusanyika kwa Israeli.

Ndugu za Nefi walichanganikiwa kuhusu unabii wa Lehi na mafundisho ya mti wa mzeituni na Wayunani (ona 1 Nefi 15:7; ona pia 1 Nefi 10:12–15). Nefi alieleza kuwa kutawanyika kwa matawi asili ya mti wa mzeituni kunaashiria kutawanyika kimwili na kiroho kwa nyumba ya Israeli (Watu wa agano wa Mungu) kwa sababu ya kutotii kwako. Katika hali yao ya kutawanyika walipoteza elimu ya injili, vile vile utambulisho wao kama washiriki wa nyumba ya Israeli. Kama sehemu ya kukusanyika kwa nyumba ya Israeli katika siku za mwisho, watu duniani kote watakubali injili iliorejeshwa na kutambua kwamba wao ni watu wa agano wa Bwana (ona 1 Nefi 15:14–15).

Soma 1 Nefi 15:14, na uweke alama kile Israeli iliotawanyika itaelewa katika siku za mwisho.

Nefi alifundisha kwamba wale wanaojiunga na Kanisa ni kama wamepandikizwa “kwenye mti wa mzeituni wa kweli” (1 Nefi 15:16). Alisema pia kwamba, kama vile kutawanyika kwa nyumba ya Israeli, kupandikizwa huku au kukusanyika kutatimizwa “na Wayunani” (1 Nefi 15:17). Itakuwa muhimu kuelewa kwamba “katika maandiko, Wayunani ina maana nyingi. Wakati mwengine inamaanisha watu wasio wa uzao wa Israeli, wakati mwengine wasio wa uzao wa Wayahudi, na wakati mwengine mataifa yasiokuwa na injili, hata kama kunaweza kuwa na damu ya Muisraeli miongoni mwa watu. Matumizi haya ya sasa ni sifa bainifu ya neno kama linavyotumika katika Kitabu cha Mormoni” (Guide to the Scriptures, “Gentiles,” scriptures.lds.org).

Picha
msichana anaomba

Bwana anaweka ahadi Zake na kukumbuka maagano Yake na watoto Wake. Ana hamu ya watoto Wake wote kupokea baraka za injili ya milele (ona 1 Nefi 15:18). Juhudi zako za kushiriki injili na marafiki na familia na azimio lako la kuhudumu misheni yenye heshima itasaidia kutimiza unabii wa Lehi.

1 Nefi 15:21–36

Nefi anajibu maswali ya ndugu zake kuhusu ono la Lehi kutoka kwa uzoefu wake mwenyewe

Salio la 1 Nefi 15 linahusisha maswali ambayo ndugu zake Nefi walimuuliza kuhusu ndoto ya Lehi. Waliuliza, “Nini maana ya fimbo ya chuma ambayo baba aliona, ikielekeza kwenye ule mti? 1 Nefi 15:23.) Soma jibu la Nefi katika 1 Nefi 15:24–25, na utambue Baraka zilizoahidiwa wale wanaotii kwa bidii neno la Mungu. Katika taarifa zifuatazo kutoka kwa Rais Ezra Taft Benson kuhusu uwezo wa neno la Mungu, piga mstari chini ya vishazi vinavyofanana na kile Nefi alifundisha:

  • “Sio tu neno la Mungu litatuelekeza sisi kwenye tunda ambalo ni la kutamanika juu yale mengine, lakini katika neno la Mungu na kulipitia tunaweza kupata nguvu za kushinda majaribu, uwezo kuzima uwezo wa Shetani na wajumbe wake.”

  • “Neno la Mungu … lina nguvu za kuimarisha Watakatifu na kuwaami wao kwa Roho ili waweze kushinda uovu, kushikilia kwa nguvu wema, na kupata shangwe katika maisha haya”

  • “Ufanisi katika utakatifu, nguvu ya kuzuia uwongo na kukataa majaribu, uongozi katika maisha yetu ya kila siku, uponyaji wa nafsi—haya ni mojawapo wa chache kati ya ahadi ambazo Bwana amewapatia wale ambao watakuja kwa neno Lake. … Kwa vyovyote tunavyoweza kujitahidi katika hali mbalimbali, Baraka nyingine ziyanapatikana tu katika maandiko, ni kwa kuja tu kwa neno la Bwana na kulishikilia kwa nguvu tunapotengeneza njia yetu kupitia ukungu wa giza kufikia mti wa uzima” (“The Power of the Word,” Ensign, May 1986, 80, 82).

Ni muhimu kwamba tushikilie neno la Mungu kupitia kwa masomo ya maandiko, maombi, na kusikiliza viongozi wenye maongozi.

  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, tengeneza kitini kinachotangaza neno la Mungu. Hakikisha kujumuisha baraka ambazo Nefi aliahidi kwa wale watakaoshikilia kwa nguvu neno la Mungu. Pia ungetaka kuorodhesha marejeo ya kupata neno la Mungu.

Picha
kijana anasoma

Fikiria kuandika kanuni ifuatayo katika maandiko yako karibu na1 Nefi 15:24–25: Kujifunza na kufuata neno la Mungu kila siku hutuimarisha dhidi ya majaribu ya Shetani.

  1. Ili kusaidia kuimarisha ushuhuda wako wa kanuni hili, jibu moja au yote ya maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Ni uzoefu gani inayohusiana na masomo yako ya kibinafsi ya maandiko imekusaidia kujua kwamba kanuni hii ni ya kweli?

    2. Unawezaje kugundua ikiwa kanuni hii ni kweli?

Katika ndoto ya Lehi, wale walioshikilia kwa nguvu fimbo ya chuma waliongozwa kwa usalama kupitia ukungu wa giza hadi kwa mti wa uzima. Katika 1 Nefi 15:26, Ndugu za Nefi walimuuliza yeye aelezee maana ya mto uliokuwa karibu na mti wa uzima. Angalia katika 1 Nefi 15:27–29, na utambue kile mto uliwakilisha.

Soma 1 Nefi 15:32–36. Kwa nini ndugu za Nefi walifadhaishwa na mafundisho haya?

  1. Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Ni sehemu gani ya ndoto ya Lehi na maelezo ya Nefi ya ndoto inaonyesha upendo wa Mungu na usikivu kwa ndugu za Nefi?

    2. Unauonaje upendo wa Mungu na usikivu kwako katika 1 Nefi 15?

  2. Andika yafuatayo mwisho wa kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza1 Nefi 15 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha