Seminari
Kitengo cha 12: Siku ya 3, Mosia 11–14


Kitengo cha 12: Siku ya 3

Mosia 11–14

Utangulizi

Mfalme Nuhu alifurahia sana katika kuishi kwa anasa na kukapelekea wengi wa watu wake katika uovu. Bwana alimtuma nabii Abinadi kuwaita watu wa Nuhu kwenye toba na kuwaonya juu ya utumwa uliokaribia. Watu walichagua kutokusikia maonyo, na Abinadi alitiwa gerezani kwa sababu ya unabii wake. Wakati makuhani wa Mfalme Nuhu walipomhoji Abinadi, nabii aliwakemea kwa kutoishi au kutofundisha amri. Mungu alimlinda Abinadi na kumpa nguvu za kukamilisha ujumbe wake kwa Mfalme Nuhu na makuhani wake. Akimnukuu Isaya, Abinadi alishuhudia juu ya haja ya watu wote ya kumtegemea Yesu Kristo na Upatanisho Wake.

Mosia 11:1–19

Mfalme Nuhu anaongoza watu wake katika uovu

Fikiria maswali yafuatayo:

  • Ungefanya nini kama mzazi wako, mlezi, au kiongozi alipendekeza kwamba baadhi ya marafiki zako walikuwa na ushawishi mbaya juu yako?

  • Ungefanya nini kama mmoja wa wazazi wako au kiongozi wa Kanisa alikuomba wewe uvalie inavyofaa kwa ibada za kuabudu za Jumapili na shughuli zingine za Kanisa?

  • Ungefanya nini kama nabii angesema kwamba wewe ulihitaji kubadilisha viwango vya burudani?

Watu wanaweza kujibu kwa njia tofauti maswali hapo juu. Unapojifunza somo hili, tazama jinsi Bwana angekutaka ujibu watu Yeye amewatuma kukusaidia wewe kuishi kwa haki.

Unapojitayarisha kujifunza Mosia 11, inaweza kukusaidia kujua kwamba baada ya Zenifu kufa, mwanae Nuhu aliwatawala Wanefi ambao walikuwa katika nchi ya Nefi. Soma Mosia 11:1–2, 5–7, 14–19, na uweke alama maneno na vishazi ambavyo vinaelezea matendo ya Nuhu na kile yeye alitaka baada ya kuwa mfalme. Kisha soma Mosia 11:2, 6–7, 15, 19, na uweke alama kwa rangi tofauti (kama unaweza) ushawishi wa matendo ya Nuhu ambao alikuwa nao juu ya watu wa ufalme.

Aya hizi zinaonyesha jinsi watu tunaingiliana nao wanaweza kushawishi matendo yetu. Fikiria jinsi wenzi wako wanashawishi chaguo unazofanya. Tafakari kwa dakika kile watu katika ulimwengu wa leo wakati mwingine wanafanya ambacho kinaweza kufananishwa na kufanya kazi ya “kuchosha sana kusaidia uovu” (Mosia 11:6).

Mosia 11:20–12:17

Abinadi aliwahimiza watu watubu na kuwaonya juu ya utumwa

Ingawa Mfalme Nuhu na watu wake walikuwa wanachagua uovu, Bwana bado aliwapenda na alitaka kuwasaidia. Pitia mistari minne ya kwanza ya Mosia 11:20, na utambue kile Bwana alifanya ili kusaidia watu wa Nuhu.

Andika ukweli ufuatayo katika maandiko yako karibu na Mosia 11:20: Mungu hutuma manabii kutusaidia sisi kutubu na kuepuka dhiki.

Bwana alimwamuru Abinadi mara mbili tofauti kuwaonya watu.

  1. ikoni ya shajaraNakili chati ifuatayo katika shajara yako ya maandiko, ukiacha nafasi ya kutosha chini ya kila rejeo la maandiko ya kuandika muhtasari. Jifunze aya zinazoonyeshwa, na uandike muhtasari wa maonyo ya Abinadi na majibizo ya watu.

Ujumbe wa Abinadi

Majibizo ya Watu

Onyo la Kwanza

Mosia 11:20–25

Mosia 11:26–29

Onyo la Pili

Mosia 12:1–8

Mosia 12:9–10, 13–17

  1. ikoni ya shajaraKatika shajara yako ya maandiko, jibu maswali yafuatayo kuhusu majibizo ya watu kwa maonyo ya Abinadi:

    1. Kwa nini unafikiria watu walimjibu kwa hasira Abinadi, ambaye alikuwa anajaribu kuwasaidia? Kwa nini unafikiria walimtetea Mfalme Nuhu, ambaye alikuwa anawaelekeza kwenye dhiki?

    2. Tazama kishazi “macho ya watu yalikuwa yamepofuka” katika Mosia 11:29. Ni baadhi ya mifano gani ya tabia na ushawishi unaamini Shetani anashughulikia kwa bidii ili kuwafanya watu wema “kupofuka” katika dunia ya leo?

    3. Unaweza kufanya nini ili kuonyesha unyenyekevu wakati wana familia, viongozi wa Kanisa, na manabii wanakuhimiza wewe kufuata neno la Mungu?

Mosia 12:18–13:26

Mungu anamlinda Abinadi anapomkemea Mfalme Nuhu na makuhani wake kwa kushindwa kwao kushika na kufundisha amri.

Kabla ya kuendelea na kujifunza kwako kwa Mosia 12, jipime mwenyewe katika ratili ya 1 hadi 10 (10 ikiwa ni kukubaliana kabisa) juu ya jinsi kauli zifuatazo zinakuelezea vyema sasa hivi:

Najua kile ninapaswa kufanya ili kuishi injili ya Yesu Kristo.

Mimi naishi injili ya Yesu Kristo.

Unapojifunza kuhusu Mfalme Nuhu na makuhani wake, fikiria jinsi wao walijua na jinsi wao waliishi amri vyema. Baada ya Nuhu kumtoa Abinadi gerezani, makuhani walianza kumhoji kuhusu maandiko. Soma Mosia 12:26–30, na uweke alama kile Abinadi alisema kumkemea Nuhu na makuhani wake.

Unafikiria Nuhu na makuhani wake wangekadiriwa vipi katika ratili ya 1 hadi 10 ya kujua na kuishi amri? Unafikiria inamaanisha nini kutumia “moyo wetu wa kuelewa”? (ona Mosia 12:27). Angalia katika Mosia 12:33, na uweke mstari kanuni ambayo inaonyesha kwa nini ni muhimu kuishi amri.

Abinadi Mbele ya Mfalme Nuhu

Abinadi alitangaza ukweli huu: Ikiwa kushika amri za Mungu, tutaokolewa. Kwa nini kujua njia ya kuishi hakutoshi sisi kuhitimu kwa wokovu?

Abinadi alimwambia Mfalme Nuhu na makuhani wake kwamba hawakuwa wanaishi au kufundisha amri, na alianza kuorodhesha zile Amri Kumi. Hii ilimkasirisha mfalme, na akaamuru kwamba Abinadi auawe. Mungu alimlinda Abinadi na kumpa nguvu za kuendelea kufundisha kuhusu Amri Kumi. Unaweza kutaka kuziweka alama na nambari katikaMosia 12:35–36 naMosia 13:12–24. Chati ifuatayo itakusaidia kutambua kila moja ya Amri Kumi:

Abinadi Alifundisha Amri Kumi

  1. Mosia 12:35

  1. Mosia 12:36; 13:12–13

  1. Mosia 13:15

  1. Mosia 13:16–19

  1. Mosia 13:20

  1. Mosia 13:21

  1. Mosia 13:22

  1. Mosia 13:22

  1. Mosia 13:23

  1. Mosia 13:24

Abinadi kwa ujasiri alimkemea Nuhu na makuhani wake kwa kutoweka Amri Kumi, akisema “Nahisi kwamba hazijaandikwa mioyoni yenu” (Mosia 13:11). Ili kukusaidia kufikiria kuhusu jinsi wewe unavyoishi vyema Amri Kumi, jaza utathimini –wa kibinafsi ufuatayo:

Kauli zilizopo chini zinaweza kuonyesha jinsi Amri Kumi zimeandikwa vyema katika moyo wako. Weka alama jinsi kauli hizi ni kweli kwako.

Sivyo Kamwe

Wakati mwingine

Wakati mwingi

Karibu daima

Mimi nampenda Baba yangu wa Mbinguni.

Mimi namweka Mungu kwanza katika maisha yangu (kabla ya marafiki, uraibu, mali, hamu zangu mwenyewe, na vitu vingine).

Mimi husema jina la Bwana kwa staha.

Mimi huiweka siku ya Sabato kuwa takatifu kwa kushiriki katika shughuli ambazo zinanileta karibu na Bwana; Mimi naitambua kama siku Yake, si yangu.

Mimi nawaheshimu wazazi wangu kwa kuwa mtiifu na mwenye heshima.

Mimi hudhibiti hasira zangu na siwatendei wengine kwa ukatili.

Mimi ni msafi kimaandili Mimi naepukana na picha, lugha, na matendo ya ashiki.

Mimi najiepusha na kuiba na kudanganya.

Mimi husema ukweli.

Mimi hujiepushana na tamaa (ambayo inamaanisha hamu zisizofaa za kitu ambacho ni cha mtu mwingine).

  1. ikoni ya shajaraTazama nyuma katika majibu yako na uweke lengo la kuishi vyema moja ya Amri Kumi. Andika lengo lako katika shajara yako ya maandiko.

Mosia 13:27–14:12

Abinadi anafunza kuhusu ujio wa Yesu Kristo

Soma Mosia 13:28, 32–35, na uweke alama maneno au vishazi vyovyote ambavyo vinaweza kukamilisha dondoo ifuatayo ya Mzee Dallin H. Oaks wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili: “Baada ya utiifu wetu wote na kazi njema, hatuwezi kuokolewa kutoka kwa kifo au madhara ya dhambi zetu kibinafsi bila .”

Dondoo kamili ya Mzee Oaks inasema “Baada ya utiifu wetu wote na kazi njema, hatuwezi kuokolewa kutoka kwa kifo au madhara ya dhambi zetu kibinafsi bila ya neema inayotolewa kwa upatanisho wa Yesu Kristo” (“Another Testament of Jesus Christ,” Ensign, Mar. 1994, 67).

Unaweza kutaka kuandika ukweli huu karibu na Mosia 13:28: Hakuna mtu anayeweza kuokolewa isipokuwa kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo.

Tumia dakika chache kujifunza Mosia 14:1–12, na uweke alama maneno na vishazi ambavyo vinaelezea kile Yesu Kristo alifanya katika maisha ya duniani ili kukusaidia kurudi nyumbani kwa Baba yetu aliye Mbinguni. Fikiria kuhusu ghamu, huzuni, na dhambi ambazo Yesu Kristo alizibeba kwa ajili yako. Aya hizi zinalinnga na Isaya 53:1–12. Abinadi alikuwa ananukuu kile Isaya alikuwa ameandika (ona Mosia 14:1).

  1. ikoni ya shajaraKatika shajara yako ya maandiko, andika jinsi ungeweza kuelezea kile Mosia 14:4–5 anafundisha kuhusu Yesu Kristo kwa rafiki.

  2. ikoni ya shajaraAndika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi za leo katika shajara yako ya maandiko:

    Nimejifunza Mosia 11–14 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningependa kushiriki na mwalimu wangu: