Kitengo 1: Siku 1
Kujifunza Maandiko
Utangulizi
Madhumuni ya somo hili ni kukusaidia ujifunze jinsi ya kujifunza maandiko na kumukaribisha Roho Mtakatifu kukuvutia na kukufundisha unapofanya hivyo. Somo hili pia litakufundisha umahiri ambao utakusaidia kuelewa maandiko zaidi na kutumia mafunzo yake katika maisha yako. Unapojifunza somo hili, tafuta njia unayoweza kumualika Roho Mtakatifu katika kujifunza injili
Jifunze Kwa Kusoma na Kwa Imani
Fikiria kuwa unataka kuimarisha afya yako ya kimwili, basi utamwomba rafiki afanye mazoezi kwa niaba yako. Ni kwa kiwango kipi mazoezi ya rafiki yako yataathiri afya yako ya kimwili? Kuhusisha mfano huu na ukuaji wetu wa kiroho, kama vile mtu mmoja hawezi kufanya mazoezi kwa niaba ya mwingine, mtu mmoja hawezi kujifunza injili kwa niaba ya mwingine. Kila mmoja wetu anawajibika mwenyewe kujifunza injili na kujikuza kiroho.
Katika Mafundisho na Maagano 88:118 , Bwana anaelezea jinsi ya kujifunza injili. Unapoisoma, tambua yale unahitaji kufanya ili kujifunza injili na kamilisha kauli ifuatayo “ tafuteni maarifa, hata kwa na pia kwa .”
Kutafuta maarifa kwa kujifunza na kwa imani kunahitaji bidii binafsi. Bidii zako za kujifunza injili kwa maombi kutaalika Roho Mtakatifu katika mpangilio wa kusoma. Baadhi ya njia za kutia bidii katika kujifunza injili kwako mwaka huu ni kuomba ufahamu, kutimiza kazi zako za ziada za seminari, kushiriki ushuhuda wako na uzoefu wako wa kuishi injili na wengine, na kutumia vitu unavyojifunza maishani mwako.
Juhudi moja muhimu unayoweza kufanya katika kumwalika Roho Mtakatifu kuwa sehemu ya kujifunza kwako kiroho ni kujifunza maandiko kila siku. Masomo ya kila siku ya kibinafsi ya maandiko yanakusaidia kusikia sauti ya Bwana ikikuzungumzia (ona D&C 18:34–36). Mzee Robert D. Hales wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili aliahidi: “Tunapotaka Mungu azungumze nasi, tunasoma maandiko, kwa vile maneno Yake husemwa kupitia manabii Wake. Kisha atatufunza tunaposikiliza ushawishi wa Roho Mtakatifu” (“Holy Scriptures: The Power of God unto Our Salvation,” Ensign or Liahona, Nov. 2006, 26–27).
Unaposoma maandiko na kualika Roho Mtakatifu katika masomo yako, utapokea baraka za , kuwa karibu na Mungu, ufunuo zaidi katika maisha yako, nguvu zaidi ya kujikinga na majaribu, na ushuhuda mkuu wa injili ya Yesu Kristo.
Kusoma Maandiko
Rais Marion G. Romney wa Urais wa Kwanza alitambulisha mojawapo ya Kitabu ya maandiko aliposema, “ Maandiko yameandikwa kuhifadhi kanuni kwa manufaa yetu” (“Records of Great Worth,” Ensign, Sept. 1980, 4). Tunajifunza kanuni na mafundisho ya injili tunapojifunza maandiko. Kanuni na mafundisho haya yatatuongoza tunapoyaweka maanani katika maisha yetu.
Kupata kanuni na mafundisho ya thamani sana yaliyo katika maandiko kunahitaji bidii na mazoezi. Mzee Richard G. Scott wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alilinganisha kujifunza maandiko na kazi ya kuchimbua vito vya thamani: “ Pata almasi za ukweli ambazo wakati mwingine ni lazima zichimbuliwe kwa makini kutoka katika kurasa za [maandiko] (“Four Fundamentals for Those Who Teach and Inspire Youth,” in Old Testament Symposium Speeches, 1987 [1988], 1). Mpangilio wa kujifunza, au kuchimbua, maandiko una sehemu tatu muhimu: (1) lazima tuelewe usuli na mazingira ya maandiko, (2) lazima tutambue kanuni na mafundisho yanayofundishwa na (3) lazima tutumia ukweli hizo katika maisha yetu.
-
Katika jarida lako la masomo ya maandiko, jibu maswali yafuatayo: Ni nini mfanano kati ya mchimba madini anayetafuta almasi na mtu ambaye anatafuta kanuni za injili katika maandiko na kuzitumia katika maisha yake?
Kuelewa Usuli na Mazingira ya Maandiko
Kuelewa usuli na mazingira ya fungu la maandiko kunakutayarisha kutambua ujumbe wa injili uliomo katika fungu hilo. Rais Thomas S. Monson aliamuru: “ Jijulishe na mafunzo yanayofunzwa na maandiko” Jifunze usuli na mazingira Jifunze juu yake kama vile wanaongea na wewe, kwani hivyo ni kweli” (“Be Your Best Self,” Ensign au Liahona, Mei 2009, 68).
Unaposoma maandiko, ni ni vyema kujiuliza maswali kama vile: “Ni nani aliyeandika mistari hii?” “Ziliandikwa kwa ajili ya nani?” “Ni nini kinafanyika katika tukio hili?” na “ kwa nini mwandishi aliandika mistari hii?” Mada ya sura ( mafupisho yaliochapishwa kwa herufi ya mlazo katika mwanzo wa kila sura ) yanapeana maelezo ya jumla ya matokeo makuu katika sura na mara nyingi hujibu maswali haya.
Ni muhimu pia kuangalia maneno magumu au yasiyo ya kawaida katika kamusi Wakati kishazi au fungu la maandiko si wazi, kurejea tanbihi zozote zilizoko kunaweza kukusaidia kulielewa.
Ili kufanya zoezi katika kutumia vifaa hivi, soma 3 Nefi 17:1–10,:1 na tafuta majibu ya maswali yafuatayo: Nani aliyekuwa msemaji?” Alikuwa akizungumuzia nani? Nini kilikuwa kikitendeka? Kumbuka kuangalia mada ya sura ili kupata maelezo kwa haraka ya jumla ya matukio yanayotendeka.
-
Ukitumia tanbihi katika 3 Nefi 17:1, jibu maswali yafuatayo katika jarida lako la masomo ya maandiko: Yesu alimaanisha nini aliposema : “Muda wangu umewadia”
-
Katika jarida lako la masomo ya maandiko, andika kwa maneno yako kilichotendeka Mwokozi alipokuwa akijitayarisha kuwacha umati Kwa nini alibaki? Ni nini aliwafanyia watu?
Tambua Mafundisho na Kanuni
Mafundisho na kanuni ni kweli za injili za milele, zisizobadilika ambazo hutoa mwongozo wa maisha yetu. Manabii wa kale wanatufunza ukweli hizi kupitia matokeo, hadithi, au mahubiri waliyorekodi katika maandiko.
Mara unapoelewa usuli na mazingira ya fungu la maandiko, uko tayari kutambua mafundisho na kanuni linalofundisha. Mzee Richard G. Scott alielezea njia nzuri ya kuelewa kanuni: “ Kanuni ni ukweli zilizokolea, zilizowekwa pamoja kwa ajili ya kutumiwa katika hali nyingi tofauti. Kanuni ya kweli hufanya uamuzi kuwa wazi hata katika hali ya kukanganya kabisa na ya kushurutisha. Inahitaji bidii kuu kupanga ukweli tunazokusanya katika kauli rahisi ya kanuni” (“Acquiring Spiritual Knowledge,” Ensign Nov. 1993, 86).
Baadhi ya kanuni za injili hufanywa kuwa wazi kwa matumizi ya vifungu kama vile “basi tunaona” au “hata hivyo” Kanuni nyingi, hata hivyo, huwa hazielezwi moja kwa moja. Badala yake huwa zinaashiriwa na maisha ya watu katika maandiko. Mafundisho na kanuni hizi zinaweza kugunduliwa kwa kujiuliza maswai kama vile: “Ni nini madhumuni na lengo la maelezo haya?” Kwa nini mwandishi aliyajumuisha maelezo au matokeo haya ?” “Je, mwandishi alitaka tujifunze nini?” na ni “ Kweli gani zinazofunzwa katika aya hii ya maandiko?”
-
Ili kufanya zoezi ya kutambua baadhi ya kanuni na mafundisho yaliofundishwa katika 3 Nefi 17:1–10 , andika jibu ya shughuli a au b Katika jarida lako la masomo ya maandiko Kumbuka kusoma mada ili kupata maelezo ya jumla ya sura kwa haraka
-
Ni nani anayeongea katika vifungu hivi? Anazungumzia nani? Ni nini madhumuni au lengo la 3 Nefi 17:1–10?
-
Ni nini baadhi ya vitu ambavyo mwandishi wa mistari 1, 5–6, na 9–10 , alinuiya sisi tujifunze kutoka kwa maelezo haya? Ni kweli zipi muhimu ambazo umejifunza kutoka kwa mistari hii?
-
Mojawapo ya kweli za injili unaoweza kuwa umetambua kutoka kwenye mistari hizi: Bwana hushawishika na matakwa yetu ya kweli ya kumukaribia.
Tumia Mafundisho na Kanuni.
Baada ya kutambua mafundisho na kanuni za injili, uko tayari ku tenda na fanya kitu kuihusu. Unapotumia yale ambayo umejifunza, utahisi Roho Mtakatifu akishuhudia ukweli wa kanuni (ona Moroni 10:4–5). Kila somo linalofundishwa nyumbani, katika seminari na kanisani, na katika kila shughuli ya Jukumu Kwa Mungu na uzoefu wa Mipango ya kibinafsi linalenga kutusaidai kutumia yale ambayo tumefunzwa.
Rais Thomas S. Monson alisema: “Lengo la kufundisha injili si ku “mimina habari” katika akili ya [wanafunzi] … Lengo ni kushawishi mtu binafsi kufikiria juu ya, kuhisi juu ya, na kisha kufanya kitu juu ya kuishi kanuni za Injili.” (katika Conference Report, Oct. 1970, 107).
Ili kukusaidia kutumia kanuni unazojifunza, uliza maswali kama vile: “ Je, Bwana anataka nifanye nini na elimu hii? “Je, ni vutio gani ya kiroho nilipata kunisaidia kufanya vyema zaidi?” “Kanuni hii inaweza kuleta tofauti gani katika maisha yangu?” “Je, ni nini ninaweza kuanza kufanya au kuwacha kufanya sasa ili niweze kuishi kulingana na ukweli huu?” “Ni vipi maisha yangu itakuwa mzuri zaidi nikifanya vile maandiko haya yanafundisha?”
-
Katika jarida lako la masomo ya maandiko, andika anuani fupi ukielezea jinsi unaweza kutumia kanuni au fundisho umejifunza kutoka 3 Nephi 17:1–10.
Ujuzi na Mbimu za Kujifunza Maandiko
Kutumia ujuzi na mbinu zifuatazo za kujifunza kutakusaidia kuelewa usuli na mazingira ya maandiko na kutambua na kutumia mafundisho na kanuni zinazofundishwa ndani yake. Mbinu hizi zitatajwa kote katika kitabu hiki cha mwongozo. Soma kila ujuzi, na chagua moja au mbili unahisi unahitaji kutumia kwa zaidi katika masomo yako ya kibinafsi ya maandiko.
Chanzo na athari Tafuta kama-basi na sababu-kwa hiyo uhusiano Mifano: 2 Nefi 13:16–26; Alma 34:33.
Marejeo-mtambuko, Panga, unganisha au kusanya maandiko pamoja ili kuweka wazi maana na kufungulia ufahamu Kwa mfano, fananisha Mosia 11:2–6, 14 na Kumbukumbu la Torati 17:14–20. Unaweza pia kutumia tanbihi kupata marejeo-mtambuko ya maandiko Mfano: 3 Nefi 12:28–29, tanbihi 29a, marejeo Mafundisho na Maagano 42:23.
Amua Mazingira Fasili nani, nini, lini na wapi ya matokeo ya maandiko. Mfano: Alma 31:1, 6–11; 32:1–6 inatoa mazingira ya Alma 32:21–43.
Maneno Makuu. maneno na vifungu kama vile “hata hivyo” au “hivyo tunaona” ni mwaliko wa kusimama na kutafuta maelezo ya kile kilichoandikwa hapo awali. Mifano: Alma 30:60; Helamani 6:35–36; 3 Nefi 18:30–32.
Kuweka alama Kwenye Maandiko. Sisitizia kwa kupaka rangi, kuweka duara, au kupigia mstari maneno na vifungu muhimu katika maandiko yako ambayo yanapatia mstari huo maana maalum. Pia andika fikra fupi, hisia, mawazo au kanuni za muhimu kwenye pambizo Hii itakusaidia kukumbuka kile kilichofanya andiko liwe muhimu kwako.
Kubadili Jina Badili jina lako na lile katika maandiko Mfano: Badili jina lako na lile la Nefi katika 1 Nefi 3:7.
Kutafakari. Kutafakari kunamaanisha kufikiria kwa undani kuhusu jambo fulani. Kutafakari kunahusisha kuuliza maswali na kutathmini kile unachojua na kile umejifunza. Kutafakari kwa mara nyingi huishia katika kujua jinsi ya kutumia kanuni katika maisha yako.
Maneno Yaliyorudiwa. Maneno au vifungu vilivyorudiwa vinaweza kuwa muhimu kwa msomaji kuweka maanani Ni vidokezo kwa yale mwandishi alihisi kuwa muhimu. Mifano: Neno mwovu katika 2 Nefi 9:10, 19, 26–27, 39, 46–47; neno kumbuka katika Helamani 5:6–14.
Malinganisho ya Maandiko Wakati mwingine, manabii huweka maelezo ya watu, mawazo au matokeo tofauti karibu na kila moja katika maandiko. Tofauti kati yao huifanya rahisi kutambua na kuelewa kanuni za injili muhimu zinazofundishwa. Tafuta tofauti katika mistari iliyo ya kipekee, vipande vikubwa vya maandiko, au sura. Mifano: 2 Nefi 2:27; Alma 47–48.
Orodha ya Maandiko Kupata orodha zilizomo katika maandiko kunaweza kukusaidia kuelewa zaidi kile Bwana na manabii Wake wanafundisha. Unapopata orodha, unaweza kutaka kuzipa nambari kila kipengele. Mfano: orodha ya mazoea maovu miongoni mwa Wanefi inayopatikana Helamani 4:11–13.
Taashira ya MaandikoManeno kama vile kama, vile, au fananisha na husaidia kutambua ishara. Jaribu kubainisha kile ambacho kiashiria kinasimamia. Tumia tanbihi, Kamusi ya Bibilia, na Mwongozo wa Mada kusaidia kwa kupata maana ya kiashiria. Mfano ; Fananisha Yakobo 5:3, 75–77 na Yakobo 6:1–7.
Kupiga Taswira Kichwani Piga taswira kichwani ya kile kinachotendeka unaposoma. Uliza maswali kuhusu tokeo, na jidhanie kuwa pale lilipokuwa likitendeka. Mfano: Jaribu kupiga taswira kichwani ya kile kinachotendeka katikaEnoshi1:1–8.
Ufafanuzi wa ManenoMaandiko kwa mara nyingi hutumia maneno ambayo si ya kawaida kwetu. Unapokumbana na neno lisilo la kawaida, tumia Kamusi ya Bibilia, tanbihi au Kamusi ya kawaida kupata maana yake.
-
Chagua na utumie moja ya ujuzi kutoka sehemu iliotangulia ya “Ujuzi na Mbimu za Kujifunza Maandiko” Katika jarida lako la masomo ya maandiko, andika kuhusu jinsi ujuzi huo ulikusaidia katika masomo yako ya kibinafsi ya maandiko.
-
Andika zifuatazo chini ya kazi ya leo katika jarida lako la masomo ya maandiko
Nimejifunza somo la “Kijifunza Maandiko” na kulikamilisha (siku).
Maswali, mawzo, na utambuzi zaidi ambazo ningetaka kushiriki na mwalimu wangu: