Seminari
Kitengo cha 20: Siku ya 2, Alma 40–41


Kitengo cha 20: Siku ya 2

Alma 40–41

Utangulizi

Kama ilivyoandikwa katika Alma 40–41, Alma alifundisha mwanawe Koriantoni mafundisho muhimu yanayohusiana na maisha baada ya kifo. Alma alifafanua kwamba kupitia kwa Upatanisho waYesu Kristo, wanadamu wote watafufuliwa. Alma pia alimfundisha Koriantoni kuhusu ulimwengu wa kiroho ambapo wafu, kulingana na chaguo zao katika maisha, wanasubiri katika paradiso au katika gereza ya kiroho hadi ufufuo. Koriantoni alijifunza kutoka kwa Alma kwamba mpango wa urejesho ulijumuisha si tu ufufuo wa kimwili, lakini pia urejesho wa kiroho ambapo pia tunapokea madhara ya matendo yetu na tamaa. Hatimaye, Alma alisisitiza kuwa muhimu katika mpango huu wa urejesho ni ukweli kwamba uovu kamwe hauwezi kuleta furaha halisi.

Alma 40

Alma anamfundisha Koriantoni kuhusu ulimwengu wa kiroho na ufufuo

Picha
mama na watoto kando ya jiwe la kaburini

Fikiria kwamba una rafiki ambaye hivi juzi alipitia kifo cha mpendwa wake. Rafiki yako, akijua kwamba wewe ni mcha Mungu, amekuja kwako na maswali yafuatayo:

  • Ni nini kinachotuwezesha kuishi tena? Ni nani atakayefufuliwa?

  • Tutaenda wapi baada ya kufa, na itakuaje?

  • Ufufuo ni nini? Kuna tofauti gani kati ya miili yetu inayokufa na miili yetu inayofufuliwa? Ni nini kinatokea baada ya sisi kufufuka?

Habari katika Alma 40 inaweza kusaidia kujibu maswali haya. Sura hii ni muendelezo wa mafundisho ya Alma kwa mwanawe Koriantoni. Koriantoni alikuwa na wasiwasi kuhusu ufufuo wa wafu.

  1. Soma vifungu vyote vitatu vifuatavyo vya maandiko. Chagua kifungu kimoja au zaidi , na ueleze katika shajara yako ya kujifunza maandiko jinsi kile ambacho Alma alifundisha kinajibu swali husika. (Kama una muda mwishoni mwa somo, unaweza kutaka kurudi nyuma na kutathmini kile Alma alifundisha katika mistari ingine.)

    1. Soma Alma 40:1–5. Ni nini kinachotuwezesha kuishi tena? Ni nani atakayefufuliwa?

    2. Soma Alma 40:6–7, 11–14. Tutaenda wapi baada ya kufa, na itakuaje? (Wakati Alma alifundisha kwamba roho za watu wote “zinachukuliwa nyumbani kwa yule Mungu ambaye alizipatia uhai” (Alma 40:11), alikuwa akifundisha kwamba baada ya kifo chetu, lakini kabla ya ufufuo wetu, roho zetu zitarudi katika ulimwengu wa kiroho, si kwa hatima ya mwisho baada ya hukumu ya Mungu. Inaweza kuwa muhimu kuangalia tanbihi katika mstari 13 ili kuelewa kile ambacho Alma alimaanisha kwa “gizani nje.” Alma 40:14 pia inatusaidia kuelewa kwamba mtajo wa gizani nje inamaanisha hali kabla ya ufufuo ambao sisi huita gereza ya roho wala si mahali pa mwisho au pa kudumu pa wale waliolaaniwa.)

    3. Soma Alma 40:21–26. Ufufuo ni nini? Kuna tofauti gani kati ya miili yetu inayokufa na miili yetu ya kufufuliwa? Nini kinatokea baada ya sisi kufufuka?

Akirejea Alma 40:11–12, Rais George Q. Cannon wa Urais wa Kwanza alielezea kuwa Alma “hakukusudia kuonyesha wazo kwamba tayari wanapelekwa katika uwepo binafsi wa Mungu. Ni dhahiri kwamba anatumia kishazi hicho katika hali ifaayo” (Gospel Truth: Discourses and Writings of President George Q. Cannon, sel. Jerreld L. Newquist, 2 vols. [1957–74], 1:73).

Mzee Neal A. Maxwell wa Akidi ya Wale Mitume Kumi na Wawili alielezea baadhi ya yale tutakayopata baada ya sisi kufufuliwa:

“Wakati wa Siku ya Hukumu kutakuwa na umoja wa usawa. Si tu kwamba tutakuwa na kile ambacho Kitabu cha Mormoni kinaita ‘kukumbuka hatia zetu zote’ na ‘ufahamu kamilifu’ wa makosa yetu, lakini mambo ya shangwe yataletwa mbele na kurejeshwa pia. Tutajua ‘kama vile tujuavyojua sasa.’ (Alma 5:18; 11:43; ona pia M&M 93:33.) Tutaona ‘jicho kwa jicho’ (Mosia 12:22; 15:29) kwa sababu ya kumbukumbu moja.

Miongoni mwa ‘vitu vyote [ambavyo] vitarudishwa’ (Alma 40:23) itakuwa ni kumbukumbu, ikiwemo ni, hatimaye, kumbukumbu zetu kabla ya dunia…Fikiria furaha ya kuunganishwa pamoja akilini na moyoni kwa kumbukumbu muhimu za hali yote ya kwanza na ya pili.

“Ni gharika kiasi gani ya hisia itakayokuja kwetu wakati huo, wakati Mungu mwenye upendo atakapoona ni busara kwamba kumbukumbu zirejeshwe kikamilifu! Gharika hii ya kuburudisha ya ukweli itazidisha shukrani zetu kwa kiasi gani nyuma uvumilivu wa Mungu huenda na kwa fadhili ya upatanisho wa hiari wa Yesu!” (Lord Increase Our Faith [1994], 103).

Ufufuo ni kuungana kwa roho na mwili, na vitu vyote vikirejeshwa katika hali yake na sehemu zake kamili. Baada ya ufufuo tutasimama kila mmoja katika uwepo wa Mungu ili kuhukumiwa. Soma Alma 40:25–26, na upate maelezo ya Alma ya hali ya mwisho ya wale ambao wanachagua haki katika maisha haya kama ikilinganishwa na hali ya mwisho ya wale ambao huchagua uovu. Fikiria jinsi fungu hili linaweza kuathiri hamu yako kuwa msafi mbele ya Mungu.

Kama ilivyoandikwa katika Alma 40:16–22, ufufuo ambao Alma alizungumza kuhusu ulikuwa unahusiana na muda wa kidunia. Yesu Kristo alikuwa wa kwanza kufufuliwa, akifuatwa baada ya muda mfupi na wenye haki ambao waliishi na kufa tangu wakati wa Adamu mpaka wakati wa ufufuo wa Kristo (onaAlma 40:16, 20; D&C 133:54–55). Ufufuo huu ndio kile Alma alieleza kama “ufufuo wa kwanza.”

Alma 41

Alma anafundisha Koriantoni kuhusu mpango wa urejesho

Kuzingatia kweli ambazo Alma alifundisha juu ya ufufuo, ulimwengu wa kiroho, na hukumu, fikiria jinsi inaweza kuathiri vitendo vya mtu ikiwa aliamini kwa yafuatayo:

  • Hakuna maisha baada ya kifo.

  • Baada ya sisi kufa, tutafanywa kamilifu bila kujali kama matendo yetu yalikuwa mazuri au mabaya juu ya nchi.

  • Katika hukumu tutalipwa kwa matendo yetu mema na kuadhibiwa kwa ajili ya matendo yetu mabaya.

Picha
Yeye Anaishi

Katika Alma 41 tunajifunza kwamba Koriantoni alichanganyikiwa na kile watu walikuwa wakifundisha juu ya ufufuo. Fikiria kuweka alama kishazi “wamepotelea mbali” katika Alma 41:1, na kisha usome mstari huu ukiangalia kile kilichosababisha watu wengine kupotea. Ili kukusaidia kuelewa mstari huu, inaweza kuwa na manufaa kwako kujua kwamba geuza maandiko inamaanisha kupinda, kupotosha, au kubadilisha maana ya maandiko.

Ni dhana gani ambayo Alma alisema anataka kufafanua kwa Koriantoni?

Urejesho inamaanisha kurudisha tena. Alma alitaka Koriantoni kuelewa kwamba kuna hali ya kimwili na ya kiroho kwa kile alichokiita “mpango wa ufufuo” (Alma 41:2). Pekua Alma 41:2–5, na uweke alama kile kitakachorejeshwa kwetu baada ya kifo na kile kitakachorejeshwa kiroho. (Lazima katika mistari hizi inamaanisha kinachohitajika au muhimu.)

Ni nini hali ya kimwili ya mpango wa ufufuo iliotajwa katika Alma 41:2?

Hali ya kiroho ya mpango wa ufufuo kama ilivyoelezwa katika Alma 40:3–5 ni: Sisi tutarejeshwa kwa aidha furaha au huzuni kulingana na matendo yetu na tamaa katika maisha haya.

  1. Tuseme kwamba umetakiwa kufundisha Alma 40:3–5kwa darasa la Msingi. Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko jinsi utakavyoelezea mafundisho ya urejesho wa kiroho kwa njia rahisi ili watoto waweze kuelewa kile ambacho Alma alifundisha.

Tafakari jinsi uelewa wa mafundisho ya urejesho unaweza na unapaswa kushawishi matendo na tamaa yako.

Tunapokuja kuelewa mafundisho ya urejesho, kwa kawaida tunaanza kuwa na wasiwasi kuhusu madhara ambayo yatakuja kwa sababu ya dhambi zetu na chaguo mbaya. Je! Kuna njia ya kubadilisha matokeo mabaya ya tamaa na vitendo vyetu vibaya? Alma alimpa Koriantoni sababu ya kuwa na matumaini. Soma Alma 41:6–9, na uangalie kile ambacho tunaweza kufanya ili kuweza kuwa na wema na furaha kurejeshwa kwetu hata wakati tumefanya dhambi. Unaweza kutaka kuweka alama maneno au vishazi katika Alma 41:6–7 vinavyoonyesha kwamba tunawajibika kwa kile tunachopokea katika ufufuo. Fikiria kuhusu swali lifuatalo: Kulingana na mistari hizi, ni kwa namna gani tunakuwa mwamuzi wetu wenyewe?

Kuna wale ambao wanafikiri wanaweza kurudi kwa Mungu bila ya kuchukua jukumu la binafsi kwa vitendo vyao. Wao mara nyingi hudai kwamba chaguo zao za dhambi ni raha. Wakati mwingine wale wanaoshiriki katika dhambi wanaweza hata kuonekana kuwa furaha. Lakini soma Alma 41:10, na uangalie kile Alma alifundisha kuhusu uovu. Alma 41:10 ni kifungu cha umahiri wa maandiko. Unaweza kutaka kukiweka alama katika njia tofauti ili uweze kukipata katika siku zijazo.)

  1. Katika Alma 41:10, Alma alishuhudia kwa mwanawe kwamba “uovu haujapata kuwa furaha.” Kamilisha kazi ifuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Andika ni kwa nini unaamini kauli ya Alma ni ya kweli.

    2. Andika mfano wa jinsi Shetani anaweza kujaribu kutushawishi kuamini kwamba tunaweza kuvunja amri za Mungu na bado kuwa na furaha.

Fikiria kuandika maelezo yafuatayo kutoka kwa Rais Ezra Taft Benson katika maandiko yako karibu na Alma 41:10: “Huwezi kufanya makosa na kujisikia sawa. Haiwezekani kabisa!” (“A Message to the Rising Generation,” Ensign, Nov. 1977, 30).

Alma 41:11 inaelezea ni kwa nini ni vigumu kuwa furaha ya kweli wakati wa kuchagua mabaya. Ili kukusaidia kuelewa mstari huu, kamilisha chati ifuatayo kwa kulinganisha kila kishazi cha maandiko na maana yake. (Unapomaliza, kagua majibu yako na yale mwishoni mwa somo.)

Maneno au vishazi kutoka Alma 41:11 ambavyo vinavyoelezea kuwa katika “hali ya asili”

Maana

  1. “Kwenye hali ya kimwili”

  1. Kuzuiwa na kulemewa na dhambi zetu

  1. “Kwenye masumbuko ya uchungu na kwenye kifungo cha uovu”

  1. Kukosa urafiki wa Roho Mtakatifu

  1. “Bila Mungu ulimwenguni”

  1. Kutawaliwa na mapenzi ya mwili

Sasa kwa kuwa umefafanua maneno haya, soma Alma 41:11 tena ili kutambua ni kwa nini ni vigumu kuwa na furaha wakati unapochagua mabaya. Wengine wanaochagua uovu wanaweza kufikiri kuwa wana furaha kwa wakati huo, lakini chaguo zao hatimaye zitawaletea masikitiko na huzuni.

  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, jibu maswali yafuatayo:

    1. Kwa nini unafikiri kwamba kuwa katika “hali ya asili,” au hali ya dhambi au “kimwili,” ni kinyume na hali ya furaha?

    2. Ni mifano gani mingine ya sababu ya vijana kujikuta kukosa urafiki wa Roho Mtakatifu, kuzuiwa au kulemewa na dhambi zao, au kutawaliwa na mwili?

Soma Alma 41:12, na uangalie lile swali ambalo Alma alimuuliza Koriantoni kuhusu urejesho. Sasa soma Alma 41:13, na uweke alama jinsi Alma alivyojibu swali hili.

  1. Fikiria kuzungumza na rafiki anayetaka kuwa na furaha lakini anachagua kutenda kwa njia ambayo ni kinyume na amri ya Bwana. Kutumia mafundisho ya urejesho ambayo umejifunza leo, elezea katika shajara yako ya kujifunza maandiko ni kwa nini huyu rafiki hana furaha na kile kinachopaswa kufanywa ili kuwa na furaha ya kweli.

Picha
bumarengi

Bumarengi ni chombo kilichotumika awali kwa uwindaji. Kwa sababu ya umbo lake, kinapotupwa kwa usahihi, kinarudi kwa mtu ambaye alikitupa. Soma Alma 41:14–15, ukiangalia jinsi bumarengi inaweza kuashiria kweli zilizofundishwa katika mistari hizi. Unaweza kutaka kuweka alama kishazi “unapeleka” katika mstari 15. Fikiria wakati ulipotuma nje wema au rehema au fadhili na kuipokea tena…

Ni kitendo gani cha haki ungependa kutuma nje kwa wengine au tabia ya haki ambayo ungependa wengine kuona kwako ambayo ungependa kupokea tena kutoka kwa watu wengine? Ni lengo gani unaloweza kuweka ili “kupeleka nje” moja ya mitazamo au vitendo hivi?

Picha
alama ya umahiri wa maandiko
Umahiri wa Maandiko—Alma 41:10

  1. Soma Alma 41:10, na uandike yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Kama uovu haujapata kuwa furaha, basi daima italeta furaha. Andika neno katika sehemu tupu ambayo inakamilisha sentensi vilivyo. Sasa orodhesha idadi ya matendo mahususi ya haki ambayo unahisi pia yatajaza sehemu tupu (kwa mfano, kuwahudumia wengine ). Andika ushuhuda wako wa jinsi umeona baadhi ya matendo haya ya haki yakielekeza kwa furaha.

Ni muhimu kuelewa kwamba furaha inayokuja kutoka kwa haki daima si mara moja, mara kwa mara, au ya kuendelea hapa katika maisha. Hata hivyo, amani na furaha daima itakuja katika njia na wakati wa Bwana kwa mtu ambaye yuko katika uwiano na mafundisho na amri Zake.

  1. Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    NimejifunzaAlma 40–41 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu:

  • Majibu kwa shughuli inayooana: (1) c, (2) a, (3) b.

Chapisha