Kitengo cha 10: Siku ya 2
Yakobo 7
Utangulizi
Yakobo alitegemea ushuhuda wake na Bwana kushinda mawazo ya uongo na ubishi wa Sheremu, mpinga Kristo. Mpinga Kristo ni mtu ambaye kwa nguvu sana au kwa ukali humpinga Kristo na hujaribu kuangamiza imani za watu wengine Kwake, Kanisa Lake la kweli, injili Yake, au mpango wa wokovu.
Ili kuzuia juhudi za Sheremu, Yakobo alipata nguvu kutoka kwa uzoefu wa siku zilizopita ambao uliongeza imani yake katika Yesu Kristo. Pia alitegemea mwongozo wa Roho Mtakatifu, elimu yake ya maandiko na maneno ya manabii, na ushuhuda wake wa Yesu Kristo. Wakati Sheremu alidai ishara ambayo ingethibitisha maneno ya Yakobo yalikuwa kweli, aliangamizwa na Mungu. Yakobo alihitimisha kumbukumbu yake kwa kuelezea jinsi Nefi aliamini katika Bwana walipokuwa wanajikinga wenyewe dhidi ya Walamani. Kabla ya Yakobo kufa, alimkabidhi mabamba madogo Enoshi mwanawe.
Yakobo:1–14
Yakobo anamtegemea Bwana anapokabiliana na Sheremu, mpinga Kristo
Mzee Robert D. Hales wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alifunza: “Mojawapo wa majaribio makuu ya maisha ya muda huja wakati imani zetu zinatiliwa shaka au kukosolewa. Katika nyakati kama hizo, tunaweza kutaka kujibu kwa ukali sana. Lakini hizi ni nafasi muhimu za kusimama kando, kuomba, na kufuata mfano wa Mwokozi. Kumbuka kwamba Yesu Mwenyewe alidhiakiwa na kukataliwa na ulimwengu. Wakati tunawajibu wanaotuhukumu sisi kama Mwokozi alivyofanya, sisi hatuwi tu kama Kristo, tunawaalika wengine kuhisi upendo Wake na kumfuata Yeye pia” (“Christian Courage: The Price of Discipleship,” Ensign or Liahona, Nov. 2008, 72).
Fikiria wakati ambapo imani yako ilitiliwa shaka au kukosolewa. Unapojifunza Yakobo 7 utajifunza jinsi Yakobo alipata ukosoaji wa imani yake kutoka kwa mtu aliyeitwa Sheremu na jinsi alivyofanikiwa kujibu changamoto hii.
Soma Yakobo 7:1–5, na utafute maneno na vishazi ambavyo vinaonyesha (1) kile Sheremu alikuwa anajaribu kufanya na (2) jinsi alivyotafuta kutimiza malengo yake. Unaweza kutaka kuweka alama hizi katika maandiko yako.
Kulingana na Yakobo 7:3, Sheremu alikuwa na athari gani kwa watu?
-
Tazama katika Yakobo 7:4 kwamba Sheremu “alikuwa ameelimika” na alikuwa na “uwezo wa kuzungumza sana.” Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko kwa nini wakati mwingine ni vigumu kutetea imani yako dhidi ya mtu kama Sheremu.
Kumbuka kwamba si watu wote ambao hutilia shaka au hukosoa imani yetu ana nia hizo hizo kama Sheremu. Hali baadhi ya watu, kama Sheremu, kwa makusudi wanatafuta kuangamiza imani, wengine wanaweza kutilia shaka imani yetu kwa sababu wao wana udadisi, au labda wana habari ambazo si sahihi kuhusu imani yetu.
Unaposoma Yakobo 7:5–14, tafakari jinsi ungeweza kujibu mtu kama Sheremu. Unapojifunza majibu ya Yakobo, utaona kwamba tunapomtegemea Bwana tunaweza kushinda changamoto kwa imani yetu.Unaweza kutaka kuandika kanuni hii pembezoni mwa maandiko yako karibu na aya hizi. Tafuta njia Yakobo alionyesha kanuni hii katika makabiliano yake na Sheremu.
Katika chati iliyopo chini, soma aya kutoka kwa Yakobo 7:5–14 katika safu ya kwanza na uoanishe rejeleo hilo na kauli katika safu ya pili ambayo inaelezea vyema jinsi Yakobo alimtegemea Bwana katika rejeleo hilo. Andika herufi ya kauli kwenye mstari karibu na rejeleo la maandiko.
Ni nini Yakobo Alifanya ili Kumtegemea Bwana | |
---|---|
|
Unaweza kuangalia majibu yako kwa hili zoezi la kuoanisha kwa kurejea kwa majibu sahihi yanayopatikana mwisho wa somo hili.
Unaweza kuimarisha vipi ushuhuda wako ili kwamba usitingishwe wakati kile unachoamini kinatiliwa shaka au kukosolewa? Kumbuka katika Yakobo 7:5 kwamba Yakobo alionyesha ukweli ufuatao:Hatuwezi kutingishwa katika imani yetu kama ushuhuda wetu upo chini ya ufunuo na uzoefu wa kiroho wa kweli.Tafakari juu ya nguvu ya ushuhuda wako wa Yesu Kristo na kile unaweza kufanya ili kuuimarisha.
Jibu la Yakobo kwa Sheremu hutoa mfano kwetu wa kufuata tunapojibu watu ambao wanatilia shaka au kukosoa imani yetu.
-
Jibu matatu ya maswali yaliyopo chini katika shajara yako ya kujifunza maandiko ili kukusaidia kufikiria kuhusu mambo Yakobo alifanya ili kumtegemea Bwana na jinsi matendo haya haya yamekusaidia au yanaweza kukusaidia wewe wakati watu wengine wanashambulia imani yako:
-
Tazama katika Yakobo 7:5 kwamba kwa sababu ya uzoefu wa kiroho wa Yakobo wa mapema imani yake ikawa haitingisiki. Ni gani baadhi ya uzoefu ambao umeimarisha imani yako? Je! Kukumbuka au kuandika uzoefu huu kunakusaidia vipi wakati mtu anatilia shaka au anakosoa imani yako?
-
Katika Yakobo 7:8, Yakobo alisema kwamba “Bwana Mungu alinishushia Roho wake katika nafsi yangu.” Unahitaji kufanya nini ili uweze kuwa na Roho kushushwa katika nafsi yako? Ni kwa jinsi gani Roho Mtakatifu amekusaidia unaposhughulikia maswali au ukosoaji kuhusu imani yako?
-
Ni kwa jinsi gani tabia za kila siku za kujifunza maandiko na maneno ya manabii wa siku za mwisho inakukusaidia katika mazingira ambapo wengine wanatilia shaka au wanakosoa imani yako? (ona Yakobo 7:10–11).
-
Ni lini ulishiriki ushuhuda wako na mtu ambaye amenatilia shaka au amekosoa imani yako? (ona Yakobo 7:12). Matokeo yalikuwa ni nini?
-
Badala ya kutafuta kuthibitisha ukweli wa ushuhuda wake wakati Sheremu alitafuta ishara,Yakobo aliacha matokeo hayo katika mikono ya Bwana (ona Yakobo 7:14). Ni kwa jinsi gani inaweza kukusaidia kujua kwamba hauhitaji kutibitisha ukweli wa ushuhuda wako kwa wale wanashambilia imani yako?
-
Yakobo 7:15–23
Sheremu anapingwa, anaungama, na kufa, kusababisha umati wa Wanefi kumgeukia Bwana
Mzee Robert D. Hales alifunza:
Wakati tusipolipiza kisasi—wakati tunageuza lile shavu lingine na kuzuia hisia za hasira—sisi tunasimama pamoja na Mwokozi. Tunaonyesha upendo Wake, ambao ndiyo nguvu pekee ambayo inaweza kumdhibiti adui na kuwajibu wakosoaji wetu bila kuwatuhumu wao pia. Huo si udhaifu. Huo ni ujasiri wa Kikristo.
“Kupitia miaka tunajifunza kwamba changamoto kwa imani yetu si mpya, na haielekei kupotea hivi karibuni. Lakini wafuasi wa kweli wa Kristo wanaona nafasi katikati ya upinzani. …
Kwa bahati nzuri, Bwana anajua mioyo ya wakosoaji wetu na jinsi tunavyoweza kuwajibu kwa njia ya kufaa. Kama wafuasi wa kweli tunatafuta mwongozo kutoka kwa Roho, wanapokea maongozi yaliyojengwa kwa kila kabiliano. Na katika kila pambano, wafuasi wa kweli hujibu katika njia ambayo inamwalika Roho wa Bwana” (“Christian Courage: The Price of Discipleship,” 72–73).
Unafikiria inamaanisha nini “kuona nafasi katikati ya upinzani”?
Kunaweza kuwa na matokeo mema tunapowajibu wale wanaoshambulia imani yetu katika njia ambayo inamwalika Roho wa Bwana. Soma Yakobo 7:15–23, na utafute mema ambayo yalitokea kutoka pambano la Yakobo na Sheremu.
Ni ushahidi gani unaouona katika Yakobo 7:21–22 ambao Yakobo alitamani uzoefu wake na Sheremu uwasaidie wengine?
Kulingana na Yakobo 7:23, ni kwa jinsi gani pambano la Yakobo na Sheremu liliathiri umati hatimaye?
-
Kanuni moja tunayojifunza kutoka kwa pambano la Yakobo na Sheremu ni kwamba tunapojibu maswali au ukosoaji wa imani yetu katika njia ambayo inamwalika Roho, tunaweza kuwasaidia wengine kumgeukia Bwana. Andika majibu ya maswali yafuatayo kuhusu kanuni hii katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
-
Ni kwa jinsi gani kujua kanuni hii kunakuruhusu wewe kuwasaidia wengine kumgeukia Bwana?
-
Unaweza kujaribu vipi kutumia kanuni hii?
-
Yakobo 7:24–27
Yakobo anaelezea mchangamano wa Wanefi na Walamani na anahitimisha kumbukumbu yake.
Soma Yakobo 7:24–27. Angazia kishazi katika Yakobo 7:25 ambacho huhimili ujumbe wa Yakobo kuhusu umuhimu wa kumtegemea Bwana tunapokabiliana na changamoto.
-
Jibu swali lifuatalo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Ni kitu gani kimoja utafanya ili kujitayarisha kwa wakati ambapo mtu atashambulia imani yako?
Kama una wasi wasi kuhusu jinsi ya kushughulikia maswali mahususi au ukosoaji wa imani yako, jifunze kitabu cha kiada Kweli kwa Imani: Rejea la Injili, Hutoba ya Mzee Robert D. Hales ya mkutano mkuu “Christian Courage: The Price of Discipleship” (Ensign or Liahona, Nov. 2008, 72–75), na nyenzo zingine zinazopatikana katika LDS.org na youth.lds.org.
-
Andika yafuatayo mwisho wa kazi za leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
NimejifunzaYakobo 7 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).
Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningependa kushiriki na mwalimu wangu:
Majibu ya shughuli ya kuoanisha hapo mwanzoni mwa somo hili: 1) d, 2) c, 3) a, 4) e, 5) b.