Seminari
Kitengo cha 17: Siku ya 2, Alma 19–20


Kitengo cha 17: Siku ya 2

Alma 19–20

Utangulizi

Kama ilivyoandikwa katika Alma 19–20, Mfalme Lamoni alipata mabadiliko makuu ya moyo, ambayo yalisababisha uongofu wa wengi wa watu wake. Amoni na Mfalme Lamoni walisafiri hadi nchi ya Midoni ili kuwakombowa ndugu za Amoni waliofungwa. Njiani, walikutana na babake Lamoni, aliyekuwa mfalme juu Walamani wote. Ushuhuda imara wa Amoni na ulinzi wa upendo wa Lamoni uliongoza baba ya Mfalme Lamoni kunyenyekeza moyo wake na na kukubali kuachiliwa kwa ndugu za Amoni. Kwa sababu ya ushuhuda na mfano wa Amoni, watu wengi walihisi ushawishi wa Roho Mtakatifu na wakafunzwa injili na kuongoka.

Alma 19

Mfalme Lamoni na wengi wa watu wake watubu na kubatizwa.

Fikiria juu ya athari ya kiwimbi ambacho hutokea unaporusha jiwe katika bwawa la maji.

Vitendo vya mtu vinawezaje kuwa kama jiwe ambalo lililorushwa ndani ya maji?

Andika Amoni katikati mwa mchoro ufuatao.

Picha
mchoro wa kiwimbi

Soma Alma 19:1, 6 ili kujua ni nani alikuwa wa kwanza kushawishiwa na ushuhuda wa Amoni, na uandike jina juu ya duara ya kwanza ya mchoro. Chagua vishazi kutoka kwa mistari hii ambavyo unahisi vinaeleza vyema kile kilichokuwa kikimfanyikia Lamoni. Andika kishazi hicho na kile unafikiri kinamaanisha:

Pekua Alma 19:7–10 kwa mtu mwengine ambaye aliathirika na ushuhuda wa Amoni, kisha weka kitambulisho duara ya pili ya mchoro. Kulingana na Alma 19:10, ni nini kilikuwa cha ajabu kuhusu imani ya mke wa Lamoni?

Kama ilivyoandikwa katika Alma 19:11–13, mkewe Lamoni aliathirika vipi na ushuhuda wa mumewe?

  1. Soma Alma 19:13–14, na ujibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Unafikiri inamaanisha nini “kulemewa na Roho,” au “kulemewa na shangwe”? Ni lini ulihisi ushawishi wa Roho Mtakatifu kwa nguvu katika maisha yako?

Soma Alma 19:15, ukiangalia mtu mwengine ambaye aliathirika na ushuhuda wa Amoni, kisha weka kitambulisho duara ya tatu ya mchoro.

Soma Alma 19:16–17 ili upate mtu mwengine aliyeathirika, kisha uweke kitambulisho duara ya nne ya mchoro.

Fikiria jinsi watumishi wote wa mfalme waliathirika kutokana na matukio ya Amoni, Lamoni, na mke wa Lamoni. Katika Alma 19:15–17, sisitizia maneno yoyote na vishazi vinavyoonyesha kwamba watumishi wa Lamoni walikuwa wakimgekia Mungu.

  1. Jibu swali lifuatalo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Ni kwa jinsi gani uzoefu wa kiroho wa Lamoni na nyumba yake ulisababisha uamuzi wa Abishi wa kushiriki ushuhuda wake na wengine baada ya miaka mingi ya “kutowahi kumjulisha yeyote” (Alma 19:17)?

Soma Alma 19:18–22 ili kuona jinsi watu waliokusanyika katika nyumba ya mfalme walitafsiri kile walichokiona. Fikiria kuwa wewe ulikuwa Abishi. Ungefanya nini baada ya kuona ubishi kati ya watu? Ili kujifunza kile Abishi alifanya, somaAlma 19:23–29.

Soma Alma 19:30–36, na ufikirie athari ambayo ushahidi wa Amoni ulileta juu ya wengine. Weka kitambulisho duara ya tano ya mchoro “Walamani wengine wengi.”

  1. Fikiria watu wote waliovutiwa na ushuhuda wa Amoni, na kisha ukamilishe kishazi katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Kwa kushiriki ushuhuda wangu na kuweka mfano mwema, naweza …

Kupitia kwa ushuhuda na mfano wake, Amoni alimsaidia Lamoni na wengine kumgeukia Bwana. Fikiria wale ambao wamefanya kazi muhimu ya kiroho katika maisha yako Fikiria juu ya mtu ambaye mfano wa haki na ushuhuda wake umekuathiri. Je! Unaweza kufikiria juu ya njia ambazo mtu huyu ameathiri watu wengine kwa mema vile vile?

  1. Fikiria jinsi unavyoweza kutumia kile ambacho umejifunza kutoka kwa mfano wa Amoni kwa kujibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Jinsi gani wanafamilia na marafiki zako wanaweza kubarikiwa kama ungefuata mfano wa Amoni wa kuishi kwa haki, kuwahudumia wengine, na kushiriki ushuhuda wako?

    2. Ni kwa jinsi gani mfano na ushuhuda wako husababisha “viwimbi” zaidi ya kile ambacho unaweza kuona kinatokea wakati huu kwa familia, marafiki, na jamaa?

Alma 20

Baba ya mfalme Lamoni ana mabadiliko ya moyo na anatamani kujifunza juu ya injili.

Soma hali tatu zifuatazo, na utafakari jinsi utakavyojibu:

  • Katika mashindano ya michezo, refa au mwamuzi anafanya maamuzi mabaya na anaonekana kukutendea visivyo.

  • Mwalimu anakushtumu mbele ya darasa kwa kudanganya mtihani wakati haukufanya hivyo.

  • Wazazi wako wanakushtumu kwa kufanya kitu ambacho ndugu au dada yako kweli alifanya.

Kama ilivyoandikwa katika Alma 20, Amoni na Lamoni walijikuta katika hali ambayo wangeweza kujibu kwa hasira. Fikiria kuwa katika hali ya Amoni au Lamoni unapojifunza sura hii.

Soma Alma 20:1–7 ili kuona kile kilichotokea wakati Lamoni alipotaka kumjulisha Amoni kwa baba yake, aliyekuwa mfalme juu ya Walamani wote. Kisha soma kila moja ya makundi yafuatayo ya mistari na utafakari majibu yako kwa maswali yafuatayo.

Alma 20:8–13

Kama ungekuwa katika hali ya Amoni na mtu mwengine akushtumu kwa kudanganya na kuiba, ungejisikia vipi?

Alma 20:14–16

Ni nini kinachokuvutia juu ya majibu ya Lamoni kwa baba yake?

Alma 20:17–25

Amoni aliitikiaje hasira ya babake Lamoni? Ni kwa jinsi gani Amoni alionyesha upendo kwa Lamoni?

Soma Alma 20:26–27 ili kuona athari ya mwitikio wa Amoni. Ni nini ambacho babake Lamoni alitamani kujifunza baada ya kuona upendo ambao Amoni alionyesha?

Tunaweza kujifunza nini kutoka kwa mwitikio wa Amoni kwa hasira ya babake Lamoni?

Andika ukweli ufuatao katika maandiko yako karibu na Alma 20:26–27 au katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Tunapotenda kwa upendo, inaweza kufanya wengine kulainisha mioyo yao na kutafuta kujua ukweli. Fikiria ni wakati gani unaweza kuwa na fursa nyumbani kwako, na marafiki zako, au shuleni ili kujibu hasira za watu wengine kwa upendo.

  1. Andika lengo katika shajara yako ya kujifunza maandiko linaloelezea jinsi unaweza kujibu hasira kwa upendo, kama alivyofanya Amoni na mfalme wa Walamani.

  2. Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza Alma 19–20 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha