Kitengo cha 28: Siku ya 3
Mormoni 3–6
Utangulizi
Baada ya kuchukua tena nchi zao kutoka kwa Walamani, Wanefi walijitayarisha tena kwa ajili ya vita. Mormoni aliwasihi Wanefi watubu; badala yake, walijivunia uwezo wao wenyewe na kuapa kulipizia kisasi ndugu zao ambao walikuwa wameuawa. Kwa sababu Bwana alikuwa amewakataza watu Wake kutafuta kulipiza kisasi, Mormoni alikataa kuongoza jeshi lao, na walishindwa. Wanefi walipoendelea katika uovu, Mungu alimwaga hukumu Yake juu yao na Walamani wakaanza kuwaangamiza kutoka duniani. Hatimaye, Mormoni alirudi kuwaongoza Wanefi katika vita, lakini kwa sababu walikataa kutubu, waliangamizwa na Walamani. Mormoni aliombolezea kuanguka kwao na kukataa kwao kumrudia Yesu Kristo. Alitoa unabii kwamba kumbukumbu za watu hao zingechipuka katika siku za mwisho, na aliwahimiza wale ambao wangezisoma watubu na kujitayarisha kwa ajili ya hukumu yao wenyewe mbele ya Mungu.
Mormoni 3–4
Kwa sababu Wanefi wanaendelea zaidi katika uovu, Mormoni akataa kuongoza majeshi yao, na Walamani waanza kuwaangamiza Wanefi kutoka duniani.
Je, umewahi kuhisi kwamba Bwana alitaka ubadilishe kitu fulani katika maisha yako? Je, unadhani amekuhimiza ama kukusaidia kubadilisha kitu fulani katika maisha yako bila wewe kukigundua?
Wakati wa Mormoni, Wanefi mara nyingi walishindwa kutambua ama kushukuru jinsi Bwana alikuwa akielekeza vita vyao na Walamani. Baada ya Wanefi kufanya maagano na Walamani na wezi wa Gadiantoni, Bwana aliwaacha wawe na miaka 10 bila vurugu. Katika miaka hiyo walijitayarisha kimwili kwa ajili ya mashambulizi yajayo (ona Mormoni 2:28; 3:1).
Soma Mormoni 3:2–3, na utafute njia muhimu zaidi ambayo Bwana aliwataka Wanefi wajitayarishe kwa ajili ya mashambuzi ya Walamani. Wanefi walijibu vipi? Kulingana na Mormoni 3:3, kwa nini Bwana alikuwa amewalinda Wanefi katika vita vyao vya hivi karibuni licha ya uovu wao?
Kama ilivyoandikwa katika Mormoni 3:4–8, Bwana aliwalinda Wanefi mara mbili zaidi katika vita. Ukweli mmoja wa mafundisho tunaweza kujifunza kutoka kwa uhusiano wa Bwana na taifa ovu la Wanefi ni kwamba katika huruma yake, Bwana hutupatia fursa za kutosha ili kutubu dhambi zetu. Fursa hizi ni ishara ya uvumilivu na upole wa Mungu na nia Yake kwamba watoto Wake wote waishi kwa njia fulani ili wastahili kwa ajili ya baraka kamilifu za Upatanisho.
-
Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko (unaweza kuyajibu katika shajara yako ya kibinafsi ikiwa majibu ni matukufu ama ya siri):
-
Bwana amekuhimiza kwa njia gani kutubu na kukupatia fursa ya kufanya hivyo? Hii inakufunza nini kuhusu sifa Yake?
-
Unaweza kufanya nini ili kujikinga kutoka kwa kupuuza ama kufunga moyo wako dhidi ya himizo hilo, kama vile Wanefi walivyofanya katika Mormoni 3:3?
-
Fursa na maaliko kutoka kwa Bwana ili kufanya mabadiliko katika maisha yako yanaweza kuja mara nyingi kuliko vile unaweza kutambua. Kwa mfano, yanaweza kuja unapokula sakramenti ama unapohisi ushawishi kutoka kwa Roho Mtakatifu ili kujiboresha ama kuhudumia wengine. Unapotafuta fursa hizo na kutenda kwa kufanya mabadiliko kwa haraka, utaalika uwezo wa ukombozi wa Bwana katika maisha yako. Ili kukusaidia kuelewa uasi wa Wanefi kwa majaribu ya Bwana kuwafikia, soma Mormoni 3:9–10 na uangalie jinsi walivyotenda kwa mjibu wa ushindi wao mwingi dhidi ya Walamani. (Unaposoma, inaweza kukusaidia kujua kwamba neno lipiza katika mstari wa 9 linamaanisha kulipiza kisasi kwa ajili ya majeruhi.)
Wanefi walitenda vipi kufuatia ushindi wao dhidi ya Walamani? Soma Mormoni 3:11–13, na upate jibu la Mormoni kwa agano la jeshi kutafuta kulipiza kisasi (lipiza)
Mormoni alikuwa akiongoza majeshi ya Wanefi kwa zaidi ya miaka 30, licha ya uovu wao wa wazi. Ni nini kukataa kwa Mormoni kuongoza jeshi wakati huo kunatufunza kuhusu hatari ya kutaka kulipiza kisasi?
Soma Mormoni 3:14–16, na utie alama vishazi vinavyoelezea kile ambacho Bwana alimfundisha Mormoni kuhusu kulipiza kisasi (ama kutaka kulipiza). Ukweli mmoja tunaojifunza kutoka kwa mistari hii ni kwamba Bwana anatukataza kutafuta kulipiza kisasi.
-
Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
-
Je, umewahi kutaka kulipiza kisasi ama kumfanyia mabaya mtu yeyote kwa sababu ya kitu ambacho mtu huyo alikufanyia? Kwa nini unafikiria hiki ni kitendo hatari ama duni? Ni nani unafikiria atahadhirika zaidi na kutaka kwako kulipiza kisasi?
-
Kwa nini tunapaswa kuwacha hukumu na kulipiza katika mikono ya Bwana badala ya kujichukulia wenyewe?
-
Ingawa tunajua kuwa tunapaswa tuweke kando hisia za kulipiza na kuwa na nia ya kufanya hivyo, mara nyingi inaweza kuwa changamoto kushinda hisia hizi zinapotujia. Unaposoma ushauri ufuatao kutoka kwa Rais James E. Faust wa Urais wa Kwanza, tia mstari vishazi vinavyokusaidia kujua kile unaweza kufanya ili kushinda hisia za kulipiza unapokumbana nazo:
“Tunahitaji kutambua na kukiri hisia za kukasirika. Itachukua unyenyekevu kufanya hivi, lakini ikiwa tutapiga magoti na kumuuliza Baba wa Mbinguni atupe hisia ya kusamehe, atatusaidia. Bwana anahitaji ‘tusamehe kila mtu’ [M&M 64:10] kwa ajili yetu wenyewe kwa sababu ‘chuki hupuuza kukua kiroho’[Orson F. Whitney, Gospel Themes (1914), 144]. Tukijiondolea wenyewe chuki na hasira tu ndipo Bwana anaweza kuweka faraja katika mioyo yetu . …
“… Taharuki inapotanda, hatupaswi tutende kwa kutaka kulipiza kisasi kibinafsi lakini badala yake tuwache hukumu ichukue hatua yake na kisha tuachilie yote. Si rahisi kuwachilia vitu vipite na kutoa katika mioyo yetu chuki ya usaha. Bwana ametoa kwa kila mmoja wetu amani ya thamani kupitia Upatanisho Wake, lakini inaweza tu kuja tunapokuwa tayari kutupa mbali hisia mbaya za hasira, chuki, ama kulipiza kisasi. Kwa kila mmoja wetu anayesamehe ‘wale wanaowakosea’ [Tafsiri ya Joseph Smith, Mathayo 6:13] hata wale waliotenda uhalifu mkubwa, Upatanisho huleta kipimo cha amani na faraja” (“The Healing Power of Forgiveness,” Ensign ama Liahona, Mei 2007, 69).
Tafakari jinsi unaweza kutumia ushauri huu ili kuachilia kinyongo, hasira, ama hisia zisizo njema ambazo huenda ukawa nazo kwa ajili ya wengine.
Baada ya kukataa kuongoza majeshi ya Wanefi, Mormoni alielekeza malengo yake kuwaandikia wale ambao wangesoma maneno yake katika siku za mwisho. Alitaka kila mmoja wetu atubu na kujitayarisha “kusimama mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo” (onaMormoni 3:18–22).
Soma Mormoni 4:1–2, na utafute kile kilichotokea kwa jeshi la Wanefi walipotafuta kuwalipiza kisasi Walamani. Soma Mormoni 4:4, na utafute ni kwa nini majeshi ya Wanefi hayakushinda. Soma Mormoni 4:5, na ubainishe kweli zozote kuhusu matokeo ya kukithiri katika uovu. Ulipata nini?
Mmoja wa kweli ambazo huenda uliziona ni kwamba hukumu za Mungu zitawashinda waovu.Mara nyingi “ni kwa kupitia waovu kwamba waovu huadhibiwa” (Mormoni 4:5). Waovu wakataa usaidizi wa Mungu na wakataa kupata ulinzi Wake mtukufu. SomaMormoni 4:11–14, 18, na utafute jinsi hukumu za Mungu zilimwagwa juu ya Wanefi.
-
Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, jibu maswali yafuatayo:
-
Kwa maoni yako, ni sehemu gani ya kuhuzunisha zaidi ya hali ya Wanefi katika Mormoni 3–4?
-
Je! Mafundisho au kweli ulizojifunza hadi hapa siku ya leo zinaweza kuhusishwa vipi? (Zingatia uhusiano kati ya toba, kulipiza kisasi, na hukumu za Mungu.)
-
Tafakari kile Bwana angekutaka ufanye ili kutumia kweli hizi.
Mormoni 5–6
Mormoni aamua kuongoza jeshi la Wanefi, lakini Walamani wanashinda; Mormoni anaomboleza maangamizo ya watu wake.
Je, kuna tofauti kati ya huzuni inayoweza kuambatana na kifo cha mtu aliyekuwa anaishi maisha ya haki na mtu aliyekufa akiwa anaishi maisha ya uovu? Unafikiria tofauti ni nini?
Baada ya zaidi ya miaka 13 akiwa amekataa kuongoza majeshi ya Walamani, Mormoni alichukua tena uongozi. Lakini, aliwaongoza bila tumaini kwa sababu watu walikataa kutubu na kumwita Bwana awasaidie. Baada ya kuzuia mashambulizi kadhaa ya Walamani, Wanefi walikimbia. Wale ambao hawakuweza kutoroka kwa haraka vya kutosha waliangamizwa. Mormoni aliandika barua kwa mfalme wa Walamani akiomba kwamba aruhusu muda ya Wanefi kujikusanya kwa ajili ya vita moja ya mwisho (ona Mormoni 5:1–7; 6:1–6).
Soma Mormoni 6:7–11, na ujaribu kuelewa huzuni ya Mormoni alipokuwa akiona maangamizo ya watu wake. Kwa nini unafikiria kifo kinaweza kuwa cha kuogofya kwa wale wanaoishi maisha ya uovu?
-
Soma Mormoni 6:16–22, na ujibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
-
Kwa nini manabii, viongozi, na wazazi hutuhimiza kwa bidii tutubu?
-
Tumaini la kukumbatiwa na Bwana linakusaidia vipi kutubu? (ona Mormoni 6:17).
-
Tafakari ikiwa kuna chochote ambacho Bwana anataka utubu kuhusu hivi sasa katika maisha yako. Unaweza kuamua kuandika kukihusu katika shajara yako ya kibinafsi na uweke malengo kukitekeleza.
-
Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
Nimejifunza Mormoni 3–6 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).
Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningetaka kushiriki na mwalimu wangu: