Utangulizi waHelamani
Kwa nini Ujifunze Kitabu Hiki?
Katika masomo yako ya kitabu cha Helamani, utajifunza kutoka kwa mifano na mafundisho ya watu wakuu kama vile Helamani, Nefi, Lehi, na Samueli Mlamani ambao walitii Bwana kwa ushujaa na kushuhudia kuhusu Yesu Kristo. Utume wa wanaume hawa unaonyesha kuwa Mungu hupeana uwezo ili kuwasaidia watumishi Wake kutekeleza matakwa Yake na kwamba jitihada za watu wenye haki zinaweza kuleta baraka kwa maelefu. Utajifunza pia kuhusu madhara yatakayofuata kiburi, uovu, na makundi ya siri.
Nani Aliandika Kitabu Hiki?
Mormoni alikusanya na kufupisha rekodi kutoka kwa mabamba kubwa ya Nefi ili kutengeneza kitabu cha Helamani. Kitabu kimeitwa Helamani, mwana wa Helamani na mjukuuu wa Alma Mdogo. Helamani alipokea rekodi kutoka kwa mjomba wake, Shibloni, na alihudumu kama jaji mkuu wa haki wa Wanefi. Aliwafundisha wanawe Nefi na Lehi kukumbuka Mkombozi wao, Yesu Kristo (ona Helamani 5:9–14). Mafundisho haya baadaye yaliwavutia Nefi kuacha wadhifa wake kama jaji mkuu ili kuhubiri toba kwa Wanefi na Walamani. Baada ya maelfu ya Walamani kuogoka, nabii Mlamani aliyeitwa Samueli alivutiwa kuhubiri toba na kutoa unabii miongoni mwa Wanefi wakati huo huo kama Nefi. Kitabu cha Helamani kimeandikwa kutoka kwa rekodi zilizowekwa wakati wa utawala na uchungaji wa Helamani (Helamani 1–3) na Nefi (Helamani 4–16). Rekodi za Nefi zilijumuisha utabiri na mafundisho ya Samueli Mlamani.
Kiliandikwa lini na wapi?
Rekodi asili zilizotumiwa kama vyanzo vya kitabu cha Helamani yawezekana kuwa ziliandikwa kati ya 52 Kabla ya Kristo. na 1 Kabla ya Kristo. Mormoni alizifupisha rekodi hizo wakati fulani kati ya Baada ya Kristo. 345 na Baada ya Kristo 385. Mormoni hakuelezea mahali alikuwa alipounganisha kitabu hiki.