Seminari
Kitengo 23: Siku ya 2, Helamani 11–12


Kitengo cha 23: Siku ya 2

Helamani 11–12

Utangulizi

Helamani 11–12inajumuisha miaka 14 ya historia ya Wanefi na inaonyesha watu wakipitia mzunguko wa haki na uovu. Sababu ya kiburi chao, watu walikataa kutubu uovu wao. Nefi alifunganisha mbingu, kusababisha ukame na njaa. Ukame na njaa uliwanyenyekeza watu, na walitubu na kumgeukia Bwana. Kwa sababu hawakuchagua kuwa wanyenyekevu, watu walianza kwa urahisi kusahau Bwana Mungu wao mpaka walipoletwa kwa utambuzi wa kiasi gani walihitaji msaada wake. Katika huruma Yake, Mungu huwarudi watu wake ili kuwaleta katika toba na wokovu.

Helamani 11

Wanefi wanapita “katika” mzunguko wa haki na uovu

  1. Chora mzunguko ufuatao wa haki na uovu katika shajara yako ya kujifunza maandiko. Mzunguko huu mara nyingi hujulikana kama “mzunguko wa kiburi.” Tambua kuwa kipengele nambari 4 ya mzunguko imepotea kutoka kwa mchoro. Unafikiri itahitaji nini kutoa watu kutoka kwenye uharibifu na mateso hadi kwenye haki na ustawi? Unapojifunza Helamani 11, angalia habari ya kukusaidia kujaza hatua hii katika mzunguko.

    Picha
    Rightous Cycle

Ulivyosoma katika Helamani 10, watu hawangesikiliza neno la Mungu lililotolewa na nabii Nefi. Chambua Helamani 10:18, na utambue kule unafikiri Wanefi walikuwa kwenye mzunguko wa kiburi wakati huo (mwisho wa mwaka wa 71 wa utawala wa majaji).

Shughuli zifuatazo za maandiko zitakusaidia kuona mzunguko huu wa haki na uovu kati ya watu wa Kitabu cha Mormoni miaka yote 14 ya historia yao. Katika chati ifuatayo, soma marejeo ya maandiko kutoka Helamani 11,andika maelezo mafupi ya hali ya Wanefi, na uandike katika nambari ukionyesha mahali ambapo ungewaweka kwenye mzunguko wa kiburi. Mifano miwili zimetolewa kwa ajili yako. Angalia maneno ya kukusaidia kujaza hatua ya nne inayokosekana kwenye mzunguko uliyochora katika shajara yako ya kujifunza maandiko.

Mwaka wa Utawala wa Majaji

Helamani 11

Ufafanuzi mfupi wa Hali ya Wanefi

Msimamo kwenye Mzunguko

72–73

mistari ya 1–2

Ubishi na vita viliongezeka; bendi ya siri ya wezi zilienedeleza kazi ya uharibifu.

2, 3

73–75

mistari ya 3–6

75

mistari ya 7, 9–12

76–77

mistari ya 17–18, 20–21

Watu walifurahi na kumtukuza Mungu; walikuwa wenye haki na kufanikiwa tena.

4, 1

78–79

mistari ya 22–23

80

mistari ya 24–26

80–81

mistari 27–30, 32–35

82–85

mistari 36–37

Kama inavyoonekana katika shughuli ya andiko, kipengele 4 katika mzunguko wa kiburi ni “unyenyekevu na toba.” Andika hii katika chati katika shajara yako ya kujifunza maandiko.

  1. Mzunguko wa kiburi si tu picha ya jamii. Pia inaweza kuonekana katika familia au katika maisha ya mtu binafsi. Kuelewa jinsi inafanya kazi inaweza kutusaidia kuepuka hilo. Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko kile unafikiri ni muhimu kwako ili kuepuka kuingia katika “kiburi na uovu” au “uharibifu na mateso” awamu ya mzunguko.

Unaweza kutaka kuandika kanuni ifuatayo katika maandiko yako katikaHelamani 11: Kwa njia ya unyenyekevu na toba, tunaweza kuepuka kiburi na uharibifu. Unaweza kutaka kuwekea alama katika Helamani 11:4 kile Nefi alitarajia ukame utatendea watu wake.

Fikiria kuhusu majibu ya maswali yafuatayo:

  • Je, jamii, familia, au mtu binafsi anahitaji kufuata mzunguko wa kiburi?

  • Ni nini unafikiri jamii, familia, au mtu binafsi anahitaji kufanya ili kuepuka kupatikana katika mzunguko wa kiburi?

Mzee Richard G. Scott wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alisema yafuatayo kuhusu sala ya Nefi: “Bwana alisikia maombi ya mtumishi Wake [katika Helamani 11:10–14] na kusababisha ukame kuisha, lakini sio mpaka mwaka uliofuata. Tukio hili linaeleza kwamba Bwana anasikia maombi yetu mara moja lakini kisha anajibu wakati, katika hekima Yake, tutafaidika zaidi kutokana na majibu Yake” (“Nephi, Son of Helaman,” in Heroes from the Book of Mormon [1995,] 154.)

Rais Ezra Taft Benson alifundisha juu ya kile tunaweza kufanya ili kuepuka kupatikana katika mzunguko wa kiburi:

Picha
Rais Ezra Taft Benson

“Mungu atakuwa na watu wanyenyekevu. Ama tunaweza kuchagua kuwa wanyenyekevu au tunaweza kulazimishwa kuwa wanyenyekevu. Alma alisema, ‘Heri wale ambao hunyenyekea bila kulazimishwa kunyenyekea.’ (Alma 32:16.)

“Acha tuchague kuwa wanyenyekevu.

“Tunaweza kuchagua kujinyenyekeza kwa kushinda uadui [chuki] kwa ndugu na dada zetu, kuwaheshimu kama sisi wenyewe, na kuwainua juu au juu zaidi kuliko sisi. …

“Tunaweza kuchagua kujinyenyekeza kwa kupokea ushauri na adhabu. …

“Tunaweza kuchagua kujinyenyekeza kwa kuwasamehe wale ambao wametukosea. …

“Tunaweza kuchagua kujinyenyekeza kwa kutoa huduma ya upendo. …

“Tunaweza kuchagua kujinyenyekeza kwa kuhudumu katika misheni na kuhubiri neno ambayo inaweza kuwanyenyekeza wengine. …

“Tunaweza kuchagua kujinyenyekeza kwa kuingia hekaluni mara nyingi zaidi.

“Tunaweza kuchagua kujinyenyekeza kwa kukiri na kuziacha dhambi zetu na kuzaliwa kwa Mungu. …

“Tunaweza kuchagua kujinyenyekeza kwa kumpenda Mungu, kuwasilisha mapenzi yetu Kwake, na kumweka kwanza katika maisha yetu. …

“Acha tuchague kuwa wanyenyekevu. Tunaweza kufanya hivyo. Najua tunaweza” (“Beware of Pride,” Ensign, May 1989, 6–7).

Helamani 12

Mormoni anaelezea kwa nini Bwana huwarudi watu

Fikiria ungekuwa nabii Mormoni na ulikuwa umemaliza kuandika kuhusu miaka 14 ya historia Nephite kupatikana katikaHelamani 11. Jinsi gani ungekamilisha taarifa ifuatayo: “Na hivyo tunaweza kutazama .”

Soma Helamani 12:1, na utambue kile Mormoni alitaka tuone. Kufikiri juu ya kile Mormoni huenda alimaanisha kwa “kutoaminika kwa mioyo ya watoto wa binadamu.”

Soma Helamani 12:2–3, na utambue masomo mengine ambayo Mormoni alitaka tujifunze. Makini sana maneno “tunaweza kuona”(mstari 2) na “hivyo tunaweza kuona” (verse 3).

  1. Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Kwa nini unafikiri ni rahisi sana kwa wale ambao wanafanikiwa kusahau Bwana?

    2. Ni mifano gani ya raha na mafanikio katika siku zetu zinaweza kusababisha mtu kusahau Mungu?

    3. Ni hali gani ni unafahamu ambapo mtu au kikundi kimemesahau Bwana katika mafanikio yao?

Baadhi ya mafunzo ambayo Mormoni alitaka wasomaji wake kujifunza ni: Tusipokuwa makini, mafanikio yanaweza kutusababisha kusahau Bwana, na Bwana huwarudi watu Wake kuwavutia kwa ukumbusho Wake.

Picha
Mzee D. Todd Christofferson

Mzee D. Todd Christofferson wa Akidi ya Mitume kumi na wawili alifundisha ni kwa nini Bwana huturudi:

“Ingawa ni vigumu kuvumilia, kwa kweli tunafaa kufurahia kwamba Mungu hutufikiria kuwa wastahiki wa muda na wagumu kukosoa.

“Adhabu ya Mungu ina angalau makusudi matatu: (1) ili kutushawishi kutubu, (2) kuboresha na kututakasa, na (3) wakati mwingine kuelekeza njia yetu katika maisha ili kujua kile Mungu anajua ni njia bora zaidi” (“As Many as I Love, I Rebuke and Chasten,” Ensign or Liahona, May 2011, 98).

Ni makusudi gani kati ya haya unahisi inaonyesha nia ya Bwana katika kuwaadhibu Wanefi na Walamani katika Helamani 11–12? Ni katika makusudi gani ambayo ametumia adhabu katika maisha yako?

  1. Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Soma Helamani 12:4–6, na uangalie maelezo ya ziada ya wale wanaosahau Mungu. Je, ni mitazamo gani za binafsi zinazozuia watu kumkumbuka Mungu?

    2. Soma Helamani 12:7–13. Kwa nini Mormoni alisema “watoto wa watu wako hafifu kuliko mavumbi ya dunia”? Je mavumbi hufanya nini ambayo watu wakati mwingine hawataki kufanya?

Picha
Yehova Anaumba Dunia
Picha
Rais Joseph Fielding Smith

Rais Joseph Fielding Smith alifundisha: “Sasa huyu nabii [Mormoni] hakunuia kusema kwamba Bwana anajali sana na anapenda mavumbi ya dunia kuliko anavyofanya kwa watoto Wake. Anachomaanisha ni kwamba mavumbi ya dunia ni tiifu. Inazunguka huku na huko kwa amri ya Bwana. Mambo yote yanawiana na sheria zake. Kila kitu katika ulimwengu kinatii sheria kilichopewa, kama nijuavyo, isipokuwa mwanadamu. Popote unakoangalia unakuta sheria na utaratibu, wale wanaotii sheria waliopewa, wakweli kwa wito wao. Lakini mwanadamu anaasi, na katika jambo hili mwanadamu ni hafifu kuliko mavumbi ya dunia kwa sababu anakataa mashauri ya Bwana” (in Conference Report, Apr. 1929, 55).

Mormoni alielewa kwamba watu ambao watakuwa na Mungu kama kiongozi wao ni wakubwa kuliko mavumbi ya dunia. Ulinganisho wake ulikuwa ni kuvutia usikivu wa wale wenye kiburi na wanaokataa sauti ya Bwana na wenye mioyo isioaminika. Kama ilivyoandikwa katika Helamani 12:9–20, Mormoni alitukumbusha juu ya uwezo mkubwa wa Bwana dhidi ya vitu vya kidunia —vyote hutenda kwa amri Yake. Chukua muda kutafakari kiwango chako mwenyewe cha utii kwa amri ya Bwana. Jinsi gani nia yako ya kutii maagizo Yake inaonyesha unyenyekevu? Jinsi gani kutumia wakala wetu kutotii maneno Yake unaonyesha kiburi?

  1. Andika na ukamilishe vishazi vifuatavyo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Na hivyo nikaona katikaHelamani 11–12 …

    2. Kwa hiyo, Nita …

Tunapokumbuka Bwana, kuisikiliza sauti Yake, na kutubu, tunaonyesha unyenyekevu wetu na imani yetu Kwake. Kwa upande wake, Anaweka ahadi Yake kubariki na kutufanikisha, hatimaye kutupatia uzima wa milele.

  1. Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza Helamani 11–12 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha