Seminari
Alma


Utangulizi wa Alma

Kwa nini ujifunze Kitabu Hiki?

Kwa kujifunza kitabu cha Alma, utajifuza kuhusu Yesu Kristo na umuhimu wa Upatanisho Wake na Ufufuo katika mpango wa furaha wa Baba wa Mbinguni. Utajifunza pia kuhusu nguvu za neno la Mungu za kushinda ukuhani wa uongo, mafundisho ya uongo, dhambi, chuki, na uasi wakati unapowaongoza watu kupokea mabadiliko makuu ya moyo na kuzaliwa tena. Utajengwa kiroho unaposoma kuhusu jitihada za kimisionari za wana wa Mosia na uongofu na uaminifu uliofuata wa watu wa Amoni, au Anti-Nefi-Lehi. Aidha, unapojifunza sura zinazoelezea kwa kina mapambano kati ya Wanefi na Walamani, unaweza kujifunza kanuni ambazo zitakuongoza katika nyakati za shida ambapo unaishi na kukusaidia kufaulu katika vita vyako binafsi dhidi ya adui.

Nani Aliandika Kitabu Hiki?

Mormoni alikusanya na kufupisha kumbukumbu kutoka kwa mabamba makubwa ya Nefi ili kutengeneza kitabu cha Alma. Kitabu kinaitwa Alma, ambaye alikuwa mwana wa Alma na mara nyingi anaitwa Alma mdogo. Wakati Mfalme Mosia alipoweka utawala wa waamuzi miongoni mwa Wanefi, Alma akawa mwamuzi mkuu wa kwanza na pia kumrithi baba yake kama kuhani mkuu wa Kanisa (ona Mosia 29:42). Hatimaye alijiuzulu nafasi yake kama mwamuzi mkuu ili kujitolea mwenyewe “kabisa kwa ule ukuhani mkuu” na “kuwatolea watu neno la Mungu” katika nchi yote ya Wanefi (Alma 4:20; 5:1). Mormoni alitumia kumbukumbu za huduma ya Alma (Alma 1–44) na maandishi ya wanawe Helamani (Alma 45–62) na Shibloni (Alma 63) ili kutunga kitabu cha Alma.

Kiliandikwa Lini na Wapi?

Kumbukumbu asili zilizotumiwa kama vyanzo vya kitabu cha Alma inawezekana ziliandikwa kati ya 91  Kabla ya Kristo na 52  Kabla ya Kristo Mormoni alizifupisha kumbukumbu hizo wakati fulani kati ya miaka 345 Baada ya Kristo.na 385 Baada ya Kristo . Mormoni hakuandika mahali ambapo alikuwa wakati alipofanya ufupisho wake.

Chapisha