Seminari
Kitengo cha16: Siku ya 3, Alma 13


Kitengo cha16: Siku ya 3

Alma 13

Utangulizi

Alma alifundisha watu waasi wa Amoniha kuhusu makuhani wakuu wa Ukuhani wa Melkizedeki ambao wametawazwa ili kusaidia watu kutubu na kuingia katika pumziko la Bwana. Alitoa mfano wa Melkizedeki, aliyesaidia watu wake kutubu na kuishi kwa amani. Alma alijaribu kufundisha watu wa Amoniha kuwa na imani na matumaini na kuwatia moyo kubadilika ili waweze kujiandaa kuingia katika pumziko la Bwana.

Alma 13:1–12

Alma anafundisha watu wa Amoniha kuhusu wito wa makuhani wakuu

  1. Soma dondoo ifuatayo, na kisha ujibu maswali:

    “Katika ulimwengu wa kiroho, Mungu aliteua roho kadhaa kutimiza kazi fulani wakati wa maisha yao ya duniani. Hii inaitwa uteuzi wa mbele.

    “Uteuzi wa mbele haithibitishi kwamba watu binafsi watapokea miito fulani au majukumu Fursa kama hizo huja katika maisha haya kama matokeo ya matumizi ya haki ya wakala, kama vile uteuzi wa mbele ulikuja kama matokeo ya haki katika maisha kabla ya maisha ya dunia” (True to the Faith: A Gospel Reference [2004], 69).

    1. Kuna uhusiano gani kati ya chaguo ulizofanywa wakati wa maisha kabla ya maisha ya dunia na uteuzi wa mbele?

    2. Ni kwa jinsi gani chaguo zilizofanywa wakati wa maisha ya dunia huathiri uteuzi wa mbele?

Ingawa wamiliki wa ukuhani wanajadiliwa katika Alma 13, Rais Spencer W. Kimball alitukumbusha kwamba kina dada pia walipewa miito bora katika maisha kabla ya maisha ya dunia: “Kumbuka, katika ulimwengu kabla ya kuja hapa, wanawake waaminifu walipewa kazi fulani wakati watu waaminifu waliteualiwa mbele kwa kazi fulani za ukuhani” (“The Role of Righteous Women,” Ensign, Nov. 1979, 102).

Picha
Baraza Kuu

Mzee Neal A. Maxwell ya waumini ya Wale Mitume Kumi na Wawili alifundisha: “Uteuzi wa mbele sio fundisho wa kufurahi. Kwa kila mmoja wetu, kuna chaguo za kufanywa, bila kwisha na kazi gumu za kufanywa, vinaya na majanga za kupitia, wakati wa kutumia vizuri, talanta na vipawa vya kutumika vizuri. Kwa sababu tumechaguliwa tu ‘hapo na hapo,’ hakika haimaanishi kuwa tunaweza kutofautiana ‘hapa na sasa.’ Iwe ni uteuzi wa mbele kwa wanaume, au uteuzi wa cheo kwa wanawake, wale walioitwa na kutayarishwa ni lazima pia wathibitishe kuwa ‘wateule na waaminifu.’ (Ona Ufunuo. 17:14; M&M 121:34–36.)” (“Premortality, a Glorious Reality,” Ensign, Nov. 1985, 17).

Alma aliwafundisha wale ndugu wa Amoniha kwamba watu wengi waliteuliwa mbele katika maisha kabla ya maisha ya dunia ili kupokea ukuhani. Soma Alma 13:1, 8–9, na utambue ukuhani ambao Alma alijadili. Inaweza kusaidia kujua kwamba katika sura hii maneno “mfano mtakatifu” ina maana ya Ukuhani wa Melkizedeki, au “Ukuhani Mtakatifu, kwa Mfano wa Mwana wa Mungu” (M&M 107:3). Fikiria kuweka alama kishazi “mfano mtakatifu” unapojifunza sura hii yote (onaAlma 13:2, 6–7, 10–11, 16, 18). Mzee Bruce R. McConkie wa Akidi ya Wale Mitume kumi na Wawili alisema: “Wanefi, ambao walikuwa waaminifu na wa kweli katika kutunza sheria za Musa, walikuwa na Ukuhani wa Melkizedeki, ambayo inamaanisha walikuwa na utimilifu wa Injili” (The Promised Messiah: The First Coming of Christ [1978], 421). Hii ina maana ya kwamba manabii wa Kitabu cha Mormoni walikuwa na Ukuhani wa Melkizedeki na walijua jinsi ulifanya kazi.

Pekua Alma 13:2–6, 10 kwa majibu ya maswali yafuatayo, na uandike majibu katika kitabu chako cha kiada:

  • Ni sifa gani wale walioteuliwa katika Ukuhani wa Melkizedeki walikuwa nazo? (Ona Alma 13:3–5, 10.)

  • Hawa wamiliki wa Ukuhani wa Melkizedeki waliteuliwa kufanya nini? (See Alma 13:6.)

  • Umeona hii ikifanyika vipi na wamiliki wa Ukuhani wa Melkizedeki unaowajua katika kata yako au tawi, na imebariki vipi maisha yako na maisha ya wengine?

Alma 13 ina majadiliano mazito kuhusu Ukuhani wa Melkizedeki. Inafundisha kwamba wanaume ambao wanapokea ukuhani huu waliteuliwa kabla ili kuupokea (ona mstari 3). Wale walio na ukuhani huu wanapaswa kufundisha amri za Mungu kwa wengine “ili nao pia waingie katika pumziko lake” (mstari 6). Ukuhani ni wa milele (ona mstari 9), na unakabithiwa watu “kwa ajili ya imani yao kuu na toba, na haki yao mbele ya Mungu” (mstari 10). Wamiliki wa ukuhani hutakaswa na Roho Mtakatifu wanapojifunza kuchukia dhambi, na hivyo “kufanywa safi na [kuingia] katika pumziko la Bwana Mungu wao” (mstari 12).

Soma Alma 13:11–12, na utambue athari ya kutakaswa ya Upatanisho wa Yesu Kristo ambao wale wali-o na ukuhani walipokea kwa sababu ya imani yao, toba, na haki.

  1. Jibu swali lifuatalo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Unajifunza nini kutoka kwa mfano wa wamiliki hawa wa Ukuhani wa Melkizedeki kuhusu kile unaweza kufanya ili kupokea athari ya kutakaswa ya Upatanisho katika maisha yako?

  2. Andika ukweli ufuatao katika maandiko yako karibu na Alma 13:1–12 au katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Wanaume ambao ni waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa siku za Mwisho wanaoonyesha imani kubwa na kuchagua haki wanaitwa katika Ukuhani wa Melkizedeki ili kuwaleta wengine kwa Mungu.Kisha andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko kuhusu jinsi kujua kanuni hii ya injili kunaweza kuathiri jinsi unavyoitika kwa viongozi wa ukuhani katika maisha yako.

Alma 13:13–20

Alma anafundisha kuhusu Melkizedeki, kuhani mkuu aliyeimarisha amani miongoni mwa watu wake.

Picha
Melkizedeki Anabariki Abramu

Soma Alma 13:13–18, na utafute maneno ambayo Alma alitumia kuelezea Melkizedeki na kile Melkizedeki aliwafanyia watu wake. Fikiria jinsi maneno haya yanaelezea maisha ya kama Kristo ya Melkizedeki. Alma alifundisha kwamba wamiliki wa Ukuhani wa Melkizedeki ni “kulingana na mpango mtakatifu wa Mwana wa Pekee wa Baba” (Alma 13:9; ona pia M&M 107:2–4), ambaye ni Yesu Kristo, na kwamba wanatuelekeza Kwake kwa mfano wao na mafundisho yao. Mzee Bruce R. McConkie alisema: “Bila shaka kuna matukio mengi katika maisha ya manabii wengi ambayo yanawatenga watu hao wenye haki kama mifano na vivuli vya Masiya wao. Ni safi na sahihi kwa kuangalia mifano ya Kristo kila mahali na kuitumia mara nyingi katika kumweka Yeye na sheria zake kama thamani kuu katika akili zetu” (The Promised Messiah, 453).

Soma Alma 13:19, na uangalie kile aya hii inatuambia kuhusu Melkizedeki. Angalia tena Alma 13:17 ili kuona jinsi Alma alivyoelezea kuhusu watu wa Salemu, wakati Melkizedeki alikuwa mfalme wao. Ona jinsi haya maneno yanaweza pia kuelezea watu wa Amoniha (ona Alma 8:9; 9:28). Watu wa Salemu walifanya nini kama matokeo ya jitihada za Melkizedeki? (Ona Alma 13:18.)

Tambua kile Melkizedeki alitekeleza, kupokea, na kuhubiri katika Alma 13:18. Fikiria juu ya kile ulichojifunza kuhusu jinsi kiongozi wa ukuhani anapaswa kuwa kutoka kwa mfano wa Melkizedeki.

  1. Jibu swali lifuatalo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Ni wakati ambapo wewe au mtu unayemjua alipata amani baada ya kufuatia ushauri wa kiongozi mwenye haki wa ukuhani?

Alma 13:21–31

Alma anawaalika watu kuisikia sauti ya Bwana na kuingia katika pumziko Lake.

Tafuta na uweke alama kwa kishazi kilichorudiwa “pumziko la Bwana” (au kishazi sawa) katikaAlma 13:12, 13, 16, and 29. Alma aliwafundisha watu wa Amoniha kwamba Bwana aliwaita wanaume katika ukuhani ili kuwasaidia watu kuingia katika pumziko la Bwana. Alitumia mfano wa Melkizedeki ili kuwaonyesha kuwa watu waliojawa na dhambi na uovu wanaweza kutubu na kuingia katika pumziko la Bwana (onaAlma 13:17–18; ona pia M&M 84:24).

Rais Joseph F. Smith alisema kwamba kuingia katika pumziko la Mungu “inamaanisha kuingia katika maarifa na upendo wa Mungu, kuwa na imani katika kusudi lake na katika mpango wake, kiasi kwamba tunajua kuwa tu sahihi, na kwamba hatuwindi kwa kitu kingine, hatusumbuliwi na kila upepo wa mafundisho, au kwa ujanja wa watu wanaosema uongo katika kusubiri kuhadaa. Tunajua ya kwamba mafundisho ni ya Mungu” (Teachings of Presidents of the Church: Joseph F. Smith [1998], 56).

Ungetarajia tabia ya mtu iweje kama yeye angeingia pumziko la Bwana katika maisha haya kama vile Rais Joseph F. Smith alieleza?

Mzee Bruce R. McConkie alifundisha: “Watakatifu wa kweli huingia katika pumziko la Bwana katika maisha haya, na kwa kudumu katika kweli, wanaendelea katika hali hiyo yenye baraka mpaka watakapopumzika pamoja na Bwana mbinguni. … Pumziko la Bwana, katika umilele, ni kurithi uzima wa milele, ili kupata ukamilifu wa utukufu wa Bwana” (Mormon Doctrine, 2nd ed. [1966], 633).

Baada ya Alma kuonya watu wa Amoniha kujiandaa kwa ujio wa Kristo (onaAlma 13:21–26), alipeana maagizo ya ziada juu ya jinsi ya kuingia katika pumziko la Bwana…SomaAlma 13:27–29 ili kuona maagizo hayo yalikuwa gani.

Mafundisho ya Alma yanaweza kufupishwa kwa kanuni ifuatayo: Tunavyojibu kwa unyenyekevu mwaliko wa kutubu, Roho hatimaye atatuongoza katika pumziko la Bwana.

  1. Tambua mojawapo ya baraka zilizotajwa katika Alma 13:27–29 ambazo ungependa kupokea. Baada ya kutambua baraka, angalia ushauri ambao Alma alitoa ambao utakusaidia kujiandaa kupokea baraka hiyo. Kisha andika lengo katika shajara yako ya kujifunza maandiko kuhusu jinsi utatekeleza ushauri wa Alma ili uweze kuingia katika pumziko la Bwana katika maisha haya na maisha yajayo.

  2. Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza Alma 13 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha