Seminari
Kitengo 4: Siku ya 3, 1 Nefi 17


Kitengo 4: Siku ya 3

1 Nefi 17

Utangulizi

Baada ya kusafiri nyikani kwa miaka minane, familia ya Lehi iliwasili katika eneo la pwani. Waliita eneo lile Neema. Nefi alitii amri ya Bwana ya kujenga chombo. Pia aliwakemea ndugu zake kwa uovu wao ambao uliwazuia kupokea maongozi kutoka kwa Bwana. Unapojifunza 1 Nefi 17 na mfano wa Nefi, utaona kuwa kupitia kwa utiifu unaweza kutimiza yote ambayo Mungu ameamuru. Utajifunza pia kumtambua vyema Bwana anapoongea nawe kupitia kwa ile sauti tulivu, na ndogo.

1 Nefi 17:1–51

Familia ya Lehi inasafiri hadi Neema, pale Nefi aliamriwa kujenga merikebu

Unaweza kuelezea maisha yao sasa kama rahisi au magumu? Kwa nini? Soma 1 Nefi 17:1, 4, 6, na uweke mviringo kwenye maneno yanayoonyesha kama wakati Nefi na familia yake walikuwa nyikani ilikuwa rahisi au mgumu.

Soma 1 Nefi 17:3, na utambue sababu alizopeana Nefi kwa kubarikiwa kwa familia yake wakati huu mgumu—inaanza na neno na kama.Weka alama kwenye kanuni hii katika maandiko yako.

Kanuni za injili mara nyingine husemwa katika maandiko kwa mbinu ya “kama-basi” Hii mbinu ya “kama-basi” inaweza pia kuonekana katika mwelekeo wa maisha ya mtu, vile vile familia na taifa zima. Neno kama linaelezea matendo yetu, na basi linaelezea matokeo au baraka tutakayopata kwa ajili ya kitendo hicho. Wakati ambapo 1 Nefi 17:3 haina neno basi, inaelezea kitendo na baraka zitakazofuata. Utaelezea kivipi kanuni ambayo Nefi anashuhudia kuhusu katika maneno yako mwenyewe? kama , basi .

Tambua jinsi kanuni hii imeelezwa katika 1 Nefi 17:2, 12–13. Unaposoma mistari hizi, weka alama njia zingine ambazo Bwana aliimarisha na kumbariki Nefi na familia yake walipotii amri. Tafuta ushahidi wa ziada wa ukweli wa kanuni hii unapoendelea kujifunza uzoefu wa Nefi.

  1. Chukua muda ili kujibu vilivyo swali lifuatalo katika shajara yako ya kujifunza maandiko. Zoezi hili litakusaidia kuona kwamba Nefi aliendelea kuishi kanuni aliyoeleza katika 1 Nefi 17:3, wakati wanafamilia wengine walikosa kuitii. Kumbuka kufikiri jinsi kanuni hii inatumika katika maisha yako mwenyewe.

    1. Bwana alimwamuru Nefi kufanya nini? (Ona 1 Nefi 17:7–8.) Ni nini ambacho kilikuwa kigumu kuhusu kutii amri hii?

    2. Ni nini kinachokuvutia kuhusu majibu ya Nefi kwa amri hii? (Ona 1 Nefi 17:9–11, 15–16). Ndugu zake walijibu vipi? (Ona 1 Nefi 17:17–21.) Unaweza kujifunza nini kutokana na majibu haya.

    3. Nefi aliwajibu ndugu zake kwa kuwakumbusha uzoefu wa Musa. Bwana alimsaidia vipi Musa kutimiza kazi ile alikuwa ameamriwa kufanya? (Ona 1 Nefi 17:23–29.) Ndugu za Nefi walikuwa kama watoto wa Israeli kwa njia gani? (Ona 1 Nefi 17:30, 42.)

    4. Je, kuna amri zingine ambazo ni ngumu kwako? Unaweza kufanya nini kwa kazi au amri ngumu kutoka kwa Mungu kama vile Nefi na Musa walivyofanya?

Wakati umemaliza zoezi la hapo juu, soma onyesho la imani la Nefi katika1 Nefi 17:50.

Soma 1 Nefi 17:51, na utumie mstari huu kwako mwenyewe kwa kuongeza jina lako baada ya neno “mimi” na kubadilisha kishazi “nijenge merikebu” na amri uliotambua katika swali la d hapo juu.

  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika kuhusu uzoefu (wako mwenyewe au wa mtu unayemjua) ambao ulikusaidia kujua kuwa kama wewe ni mwaminifu kwa Mungu, atakusaidia kutimiza chochote Yeye atakuuliza.

Kanuni ambayo Nefi `alionyesha katika 1 Nefi 17 na kote maishani mwake ni kwamba tunaposhika amri, basi Bwana atatuimarisha na kutupatia njia ili kutimiza mambo Yeye ametuamuru.

1 Nefi 17:45–55

Nefi aliwakemea Lamani na Lemueli kwa ajili ya uovu wao.

Soma 1 Nefi 17:48, 53–54, na utambue ni kwa nini Nefi “alinyosha mkono [wake] tena kwa kaka [zake]

Kulingana na 1 Nefi 17:53, ni nini Bwana alifanya kwa ndugu za Nefi? Kwa nini?”

Picha
Nefi Akiwadhibiti Nduguze Waasi

Mshtuko waliopewa ndugu za Nefi ilikuwa ni mojawapo wa njia nyingi Bwana alitaka kuwasiliana nao. Soma1 Nefi 17:45, na utambue baadhi ya njia Bwana alikuwa amejaribu kuwasiliana nao.

Picha
Rais Boyd K. Packer

Tafakari dondoo ifuatayo kutoka kwa Rais Boyd K. Packer wa Akidi ya Wale Mitume Kumi na Wawili: “Roho Mtakatifu husema kwa sauti ambayo wewe utahisi zaidi ya wewekusikia. Inasemekana kama ‘sauti ndogo tulivu’ [M&M 85:6]. Na hali tunaongea juu ya ‘kusikiliza’ mnong’ono wa Roho, mara nyingi mtu huelezea msukumo wa kiroho kwa kusema, ‘mimi nilipata hisia …’” (“Personal Revelation: The Gift, the Test, and the Promise,” Ensign, Nov. 1994, 60).

Unaweza kutaka kuweka alama1 Nefi 17:45na uandike kanuni ifuatayo karibu nayo:Roho Mtakatifu huongea kwa sauti tulivu, ndogo ambayo tunahisi kuliko kusikia.

  1. Andika majibu kwa maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Ni wakati gani ulihisi Bwana akiongea nawe kupitia sauti tulivu, ndogo?

    2. Unaweza kufanya nini kuhisi na kutambua sauti tulivu, ndogo?

Weka alama kwenye kishazi kifuatacho katika 1 Nefi 17:45: “amewazungumzia kwa sauti ndogo tulivu, lakini mlikuwa mmekufa ganzi, kwamba hamkupata yale maneno yake.” ‎ Tazama mara nyingine sentensi ya kwanza ya 1 Nefi 17:45, na utambue ni kwa nini ndugu za Nefi walikuwa “wamekufa ganzi.”

Dhambi zinawezaje kutuzuia kuhisi Roho Mtakatifu? Ni mambo mengine gani yanaweza kutupotosha kwa kuhisi Roho Mtakatifu?

Rais James E. Faust wa Urais wa Kwanza alitumia analojia kutambua baadhi ya njia dhambi inaweza kutuzuia kuhisi Roho Mtakatifu:

Picha
Rais James E. Faust

“Simu za rununu zinatumika kwa mawasiliano mengi katika nyakati zetu. Mara kwa mara, hata hivyo, tunapata sehemu tupu ambapo signali inayokuja kwa simu ya rununu hazifiki. Hii inaweza kufanyika wakati mtumiaji wa simu ya rununu yuko ndani ya upenyo chini ya ardhi au korongo kuu au pale palipo ukinzani wa signali.

“Hivyo ndivyo ilivyo na mawasiliano matakatifu. Sisi mara nyingi tunajiweka kwenye sehemu tupu kiroho—sehemu na hali ambazo zinazuia jumbe takatifu. Kati ya hizi sehemu tupu hujumuisha ghadhabu, picha za ngono, kutenda dhambi, uchoyo, na hali zinazoudhi Roho” (”Did You Get the Right Message?” Ensign or Liahona, May 2004, 67).

  1. Tafakari jinsi umesikia vyema jumbe ambazo Bwana amejaribu kuwasilisha kwako hivi majuzi Orodhesha katika shajara yako ya kujifunza maandiko “sehemu tupu za kiroho” ”zozote—hali na sehemu ambazo zinaweza kukuzuia kupokea sauti tulivu, ndogo— na kile utakachofanya kuepukana nazo.

Unaweza kupata mawasiliano kutoka kwa Bwana kupitia sauti tulivu, ndogo unapotafuta kuwa mstahiki na msikivu wa huu mvuvio ororo.

  1. Andika yafuatayo mwisho wa kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza1 Nefi 17 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe)

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha