Seminari
Kitengo cha 12: Siku ya 2 Mosiah 9–10


Kitengo cha 12: Siku ya 2

Mosia 9–10

Utangulizi

Wakati wa utawala wa Mfalme Benyamini, Zenifu aliongoza kundi na Wanefi kutoka Zarahemla kwenda kufanya makazi miongoni mwa Walamani katika nchi Nefi. Kwa sababu mfalme wa Walamani alipanga njama ya kuwaweka watu wa Zenifu katika utumwa, aliwaruhusu wao wakae. Tamaduni za uongo na chuki za Walamani dhidi ya Wanefi hatimaye zilileta vita. Wakati Walamani walitafuta kuwaleta katika utumwa, watu wa Zenifu walimgeukia Bwana, ambaye aliwaimarisha na kuwasidia kuwafurusha Walamani kutoka kwenye nchi yao.

Mosia 9:1–13

Zenifu anaongoza kundi la Wanefi kurudi katika nchi ya Nefi

Je! Umewahi kutaka kitu sana kabisa? Leo utajifunza kuhusu mtu ambaye alitaka kitu sana kabisa na matokeo ya kutenda kwake juu ya tamaa zake.

Angalia ramani ya safari kutoka kwa somo la mwisho. Je! Unakumbuka safari ya Amoni wakati alipompata Limhi na watu wake? Fungua maandiko yako katika Mosia 7–8, na utafute tarehe wakati matukio katika sura hizi yalitokea (yanapatikana aidha hapo mwisho wa ukurasa au katika kichwa cha sura). Linganisha na tarehe zinazohusishwa na Mosia 9:1, Tunarudi nyumba kiasi cha miaka mingapi kati ya Mosia 8 na Mosia 9?

Soma dibaji ya Mormoni ya kumbukumbu ya Zenifu kabla tu Mosia 9.

Zenifu, babu ya Limhi, aliongoza kundi la Wanefi kurudi katika nchi ya Nefi. Alitaka kitu fulani sana kabisa kwamba yeye alishindwa kufikiria pale tamaa zake zingemwelekeza. Soma katika Mosia 9:1–4 kuhusu kile Zenifu alifanya ili apate kile alichotamani. (Kuwa “uharara–” humaanisha kuwa na hamaki au kupendelea kitu sana kabisa.)

Uharara wa Zenifu ilimpelekea kulaghaiwa na mfalme Mlamani. Soma Mosia 9:5–7, 10 ili uone matokeo ya uharara wa Zenifu.

  1. Andika majibu kwa maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Ni nini Zenifu alishindwa kutambua kwa sababu ya hamu zake za uharara za kupata nchi ya Nefi?

    2. Ni ipi baadhi ya mifano ya kisasa ya kile baadhi ya vijana wanaweza kuwa na uharara wapate?

    3. Ni nini undhania kuwa ni hatari za kuzembea kumkumbuka Bwana unapofanya chaguo katika maisha yako?

Baada ya miaka 12, watu wa Zenifu wakawa wamestawi sana. Mfalme Mlamani akaanza kuingiwa na wasiwasi kwamba asingeweza kuwaleta katika utumwa kulingana na mpango wake wa asili, kwa hivyo mfalme aliwatayarisha watu wake kwenda vitani dhidi yao (ona Mosia 9:11–13).

Mosia 9:14–10:22

Walamani wanajaribu kuwaleta watu wa Zenifu katika utumwa

Weka mviringo wa maeneo yoyote katika maisha yako ambayo ungependa kuwa na uhimili zaidi au nguvu: kazi ya shuleni, kushinda majaribu, mahusiano na marafiki, uongozi, ajira, uhusiano na wana familia, kukuza ujuzi, talanta, na uwezo.

Unapojifunza Mosia 9–10, angalia kanuni ambayo inaweza kukusaidia kuelewa kile utakachofanya ili kupokea nguvu zaidi katika maeneo haya ya maisha yako. Mosia 9–10 ina kumbukumbu za nyakati mbili tofauti wakati Walamani walipokuja kupigana vita dhidi ya Zenifu na watu wake.

  1. Nakili chati ifuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko, ukiacha nafasi chini ya kila rejeo la maandiko ya kuandikia jibu. Jifunze aya zilizoonyeshwa, na utafute kile watu wa Zenifu na Walamani walifanya ili kupata nguvu. Jaza katika chati habari unazopata.

Watu walifanya nini ili kujitayarisha?

Walifanya nini ili kuweka imani yao katika Bwana?

Nini yalikuwa matokeo?

Zenifu na watu wake

Mosia 9:14–16

Mosia 9:17

Mosia 9:18

Walamani

Mosia 10:6–8

Mosia 10:11

Mosia 10:19–20

  • Kuna mifanano gani unayoona kati ya jinsi watu wa Zenifu na Walamani walivyo jiandaa kwa vita?

  • Ni tofauti gani unazoweza kuziona kati ya jinsi watu wa Zenifu na Walamani walijiandaa kwa vita?

Somo moja tunajifunza kutoka kwa Mosia 9:17–18 ni kwamba Bwana atatuimarisha tunapofanya yale yote tuwezayo na kuweka imani yetu Kwake .

  1. Jibu swali lifuatalo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Ni katika sehemu gani za maisha yangu ninazoweza kuweka imani katika Bwana zaidi kabisa na kumwomba Yeye aniimarishe?

  2. Weka alama mistari mitatu ya kwanza ya Mosia 9:18. Kisha muulize mtu mzima wa kuaminika (mzazi, kiongozi wa Kanisa, au mwalimu) ashiriki uzoefu pamoja na wewe kuhusu wakati yeye alimuomba Bwana msaada na kuhisi kuimarishwa na Yeye. Sikiliza kile mtu huyu alifanya ili kupokea nguvu za Bwana. Andika kuhusu kile unajifunza katika shajara yako ya maandiko.

Je! Umeshawahi kumkasirikia mtu na ukawa na kinyongo—ukahisi kama hauwezi kumsamehe au kusahau kile mtu huyo alifanya? Je! Umewahi kujua mtu ambaye alionekana kukuchukia? Kabla ya Zenifu na watu wake kwenda vitani mara ya pili, Zenifu aliwafunza watu wake kwa nini Walamani walijawa na chuki dhidi ya Wanefi. Unapojifunza maneno ya Zenifu katikaMosia 10:11–18, inaweza kuwa na msaada kujua kwamba “kukosewa” ni kuhisi kuudhiwa au kutendewa visivyo au katika njia isiyo ya haki na “kukasirika” ni kuwa na hasira sana kupita kiasi. Jifunze Mosia 10:11–18, na utafute kwa nini uzao wa Lamani na Lemueli uliendelea kuchukia uzao wa Nefi. Weka alama maneno kosewa na kasirika unaposoma.

Tafakari juu ya maswali yafuatayo:

  • Kwa nini Walamani waliwachukia Wanefi sana hivyo?

  • Ni nani anayeumia wakati wewe umekasirika au kukataa kusamehe?

  • Je! Kuwa na hasira na kuwa na kinyongo kunaweza kuadhiri vipi familia yako au watoto wako wa siku za usoni?

Soma uzoefu ufuatao kutoka kwa Mzee Donald L. Hallstrom wa Urais wa Sabini, na utafute kile anapendekeza tufanye wakati tunahisi kuudhiwa au kukasirishwa na mtu:

Picha
Mzee Donald L. Hallstrom

“ Miaka mingi iliyopita, niliona kuvunjika moyo—ambako kulifikia kuwa njaga. Wanandoa vijana walikuwa wakikaribia kupata mtoto wao wa kwanza. Maisha yao yalikuwa yamejawa na matarajio na uchangamfu wa tukio hili kuu. Wakati wa kuzaa, matatizo yakatokeza na mtoto mchanga akafa. Kuvunjika moyo kukageuka kuwa huzuni, huzuni ukageuka kuwa hasira, hasira ikageuka kuwa lawama, lawama ikageuka kuwa kisasi dhidi ya daktari, ambaye walimfanya awajibike kikamilifu. Wazazi na wana familia wengine wakaingilia sana, pamoja wakatafuta kuharibu sifa na kazi ya huyu tabibu. Wiki na kisha miezi ya maneno makali [lugha kali, chungu] ilimaliza familia, na uchungu wao wakaelekeza kwa Bwana. “Je, Yeye angekubali jambo hili baya litokee kivipi?’ Walikataa juhudi za kila mara za viongozi wa Kanisa na washiriki za kuwafariji kiroho na kimhemko na, baada ya muda, wakajiondoa wenyewe kutoka Kanisani. Vizazi vinne vya familia sasa vimeadhirika Pale wakati mmoja palikuwa na imani na upendo kwa Bwana na Kanisa Lake, pakawa na hamna shughuli za kiroho kwa mwanafamilia yeyote kwa miongo. …

“Babu zangu upande wa baba walikuwa na watoto wawili, mwana (baba yangu) na binti. [Binti yao] aliolewa mnamo 1946 na miaka minne baadaye alikuwa anatarajia mtoto. Hakuna yeyote aliyejua kwamba alikuwa amebeba mapacha. Cha kuhuzunisha, yeye na mapacha wake walikufa wakati wa uzazi.

“Babu zangu walivunjika moyo. Huzuni wao, hata hivyo, ghafula iliwageuza yao kwa Bwana na Upatanisho Wake. Bila kushikilia juu ya kwa nini haya yangetokea na ni nani angelaumiwa, walizingatia juu ya kuishi maisha ya wema. …

“Uaminifu wa [mababu hawa], hususani wakati walipokabiliwa na matatizo, sasa umeathiri vizazi vinne ambavyo vilifuata. Moja kwa moja na kwa uzito, iliadhiri mwana wao (baba yangu) na mama yangu wakati binti ya wazazi wangu mwenye, mtoto wao mdogo, alikufa kwa sababu ya matatizo yaliyosababishwa na uzazi. Kwa mfano ambao walikuwa wameona katika kizazi kilichopita, wazazi wangu—bila kusita —walimgeukia Bwana kwa faraja. …

“Kama unahisi kuwa umekosewa—na mtu yeyote (mwana familia, rafiki, mshiriki mwingine wa Kanisa, kiongozi wa Kanisa, mwenzi wa biashara) au kwa chochote (kifo cha mpendwa, shida za kiafya, mdororo wa kifedha, udhalimu, uteja wa ulevi)—shughulikia jambo moja kwa moja na kwa nguvu zako zote ulizonazo. Na, bila kuchelewa, mgeukie Bwana. Fanya imani yako yote uliyonayo katika Yeye. Acha Yeye achukue mzigo wako. Ruhusu neema Zake zikurahisishie mzigo wako. Kamwe usiache hali za kilimwengu zikulemaze kiroho” (“Turn to the Lord,” Ensign or Liahona, May 2010, 78–80).

Angalia kwamba katika mfano yote ya Walamani na familia ya wanandoavijana ambao walipoteza mtoto wao wa kwanza, hasira na kuhudhiwa kuliathiri vizazi vya watu.

  1. Fikiria wakati umekuwa na hisia za kukosewa au za hasira dhidi ya mtu? Je, Una baadhi ya hisia hizo kwa sasa? Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Ni kwa jinsi gani niinaweza kupokea usaidizi katika juhudi zangu za kusamehe?

    2. Ninaweza kufuata vipi mfano wa mababu wa Mzee Hallstrom na kutumia ushauri wake katika aya ya mwisho ya dondoo katika maisha yangu leo?

  2. Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi za leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza Mosia 9–10 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningependa kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha