Seminari
Kitengo cha 9, Yakobo 3–4


Kitengo cha 9: Siku ya 4

Yakobo 3–4

Utangulizi

Yakobo 3 ina hitimisho la mahubiri Yakobo aliyoyatoa kwa watu wake. Katika hitimisho ili, Yakobo alitoa kwa ufupi maneno ya faraja na ahadi kwa walio wasafi katika moyo. Pia aliwakemea wenye kiburi na wazinzi miongoni mwa watu wake, akiwaonya juu ya matokeo kama hawangetubu. Yakobo 4 ina maneno ambayo Yakobo alipata maongozi kuandikia watu ambao siku moja watasoma kumbukumbu yake. Alishuhudia juu ya Upatanisho wa Yesu Kristo na kuwasihi wasomaji wake kujipatanisha (kurejesha kwenye uwiano) wenyewe na Mungu Baba kupitia Upatanisho. Kwa sauti ya onyo, aliwaambia Wayahudi ambao walimkataa Yesu Kristo na uwazi wa injili Yake.

Yakobo 3

Yakobo anawatia nguvu wale walio wasafi katika moyo, na kuwahimiza wengine watubu.

Fikiria kuhusu ushauri unaoweza kutoa kwa mvulana au msichana katika hali zifuatazo:

  • Msichana ambaye anajitahidi kuishi kwa wema anateseka kwa sababu ya uteja wa ulevi wa baba yake.

  • Mvulana ambaye anafanya vyema kuishi injili anasumbuka kwa sababu ya talaka ya wazazi wake.

  • Msichana anayejaribu kwa bidii kupenda familia yake, lakini anasumbuka nyumbani kwa sababu ya uchoyo na matendo ya kutofikiria wengine ya dada yake.

Tafakari wakati wewe ulipata majaribio hata ingawa wewe ulikuwa unajitahidi kuishi kwa haki. Yakobo alitufundisha nini cha kufanya katika hali kama hizi. Soma sentensi ya kwanza ya Yakobo 3:1, na utambue ni nani Yakobo anahutubia kwanza katika sura ya 3.

Yakobo alisema kwamba kwa sababu ya kiburi cha wengine na ukosefu wa maadili (ambayo alionya hapo mapema dhidi yake kama ilivyoandikwa katika Yakobo 2) wale walio wasafi katika moyo walipatikana nayo. Soma Yakobo 3:1–2, na ujaze katika chati ifuatayo:

Yakobo aliwahimiza wale walio wasafi katika moyo wafanye nini?

Mungu anaahidi nini kwa wale walio wasafi katika moyo?

  1. ikoni ya shajaraRejea maswali yako katika safu ya kwanza. Ili kukusaidia wewe kufikiria zaidi kanuni hii, jibu mawili ya maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Unafikiri ni vipi kijana anaweza “kumtazamia Mungu kwa uthabiti wa akili”?

    2. Unafikiri inamaanisha nini kuomba kwa Mungu “kwa imani ya kuzidi” wakati wa majaribio?

    3. Unafikiri kijana anaweza kufanya nini ili “kupokea neno la kupendeza la Mungu”?

  2. ikoni ya shajaraRejea majibu yako katika safu ya pili. Aya hizi zinafunza kwamba Mungu atawafariji wale walio wasafi katika moyo katika mateso yao. Ili kukusaidia kufikiria zaidi kanuni hii, jibu moja au zaidi ya maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Mungu amekufafiji vipi katika mateso yako ulivyojaribu kumfuata Yeye?

    2. “Kuomba kwa imani ya kuzidi” kumekusaidia vipi wakati wa majaribio?

    3. Ni lini kupokea neno la Mungu kumekusaidia kuhisi upendo Wake?

Baada ya kuongea na wale walio safi katika moyo, Yakobo aliwahuburia wale wasio wasafi katika moyo. Soma Yakobo 3:3–4, 10–12, na utambue kile Yakobo aliwahimiza watu hawa wafanye. Inaweza kusaidia kujua kwamba kishazi “amsheni fahamu” humaanisha kuamusha uwezo wetu na hisia, na maneno uzinzi na ukware yanalenga dhambi za zinaa na ashiki.

Katika Yakobo 3:3–4, 10–12, sisi pia tunasoma maonyo ya Yakobo kuhusu nini kingetokea kama watu wake hawangetubu. Baada ya kujifunza aya hizi, weka mviringo vishazi ambavyo vinaelezea matokeo yafuatayo: (a) Walamani wangewaangamiza. (b) Mfano wao ungewaelekeza watoto wao kwenye maangamizo. (c) Wangepatwa na kifo cha pili, au kwa maneno mengine, utenganisho kutoka kwa Mungu.

Fikiria kwa dakika jinsi maonyo ya Yakobo yanaweza kufikiriwa kuwa baraka kuu kwa watu wake.

Kama ilivyoandikwa katika Yakobo 3:5–7, Yakobo kwa uthabiti alitangaza kwamba Walamani walikuwa “watakatifu zaidi” kuliko Wanefi kwa sababu “mabwana zao wanawapenda wake zao, na wake zao wanawapenda mabwana zao; na mabwana zao na wake zao wanawapenda watoto wao.” Wanefi walihitaji kutubu dhambi zao zote, hasa zile ambazo zilipelekea upungufu wa upendo na uaminifu katika familia zao.

Tafakari Yakobo 3:11–12, na ufanye muhtasari wa ujumbe huu kwa maneno yako mwenyewe.

Chukua dakika ufikirie kuhusu majaribu yanayokukabili na matokeo mabaya sana unayoepuka unapotubu makosa yako.

Yakobo 4

Yakobo anawasihi watu wake wapate tumaini kwamba wanaweza kurudi katika uwepo wa Mungu.

Ili kujitayarisha kujifunza Yakobo 4, inua kalamu au penseli yako angalau futi mbili au mita moja juu ya kitabu cha kiada chako, na jaribu kuiangusha ili igonge katikati ya shabaha —“alama.” Unaweza kutaka kujaribu hivi mara kadhaa. Fikiria kuhusu jinsi kungekuwa hakuna ufanisi katika juhudi zako kama ungekuwa unaangalia mahali pengine badala ya shabaha. Je! Unafikiria watu wangefanya vyema kiasi gani katika upigaji mishale kama kamwe hawangetazama shabaha, au alama, wakati wakipiga mishale au kama wangetazama kilicho zaidi ya lengo? Soma Yakobo 4:14, na utambue silka za watu Yakobo alitoa unabii wangetazama “zaidi ya lengo?

miviringo ya shabaha

Unaweza kutaka kuandika katika maandiko yako karibu na Yakobo 4:14 kwamba “lengo ni Kristo” (Neal A. Maxwell, “Jesus of Nazareth, Savior and King,” Ensign, May Vivyo hivyo, Paulo alifunza, “Nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu.( Wafilipi 3:14).

Nabii Yakobo alikuwa anamaanisha Wayahudi ambao walikosa kuelewa sheria ya Musa na dhamira yake ya kuwaelekeza wao kwa Mwokozi. Wengi wa Wayahudi walikuwa wanatafuta aina tofauti ya ukombozi kuliko aina Yesu, Masiya, alitoa kwao—walikuwa wanatafuta ukombozi kutoka kwa utawala wa kigeni na dhuluma.

  1. ikoni ya shajaraJibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Je! Unafikiria inamaanisha nini kutazama mbali na lengo (Yesu Kristo)?

    2. Ni mitazamo na matendo gani yaliyoorodheshwa katika Yakobo 4:14 yaliyowapofusha Wayahudi na kuwazuia wao kumpokea Yesu Kristo?

    3. Ni ipi inayoweza kuwa baadhi ya mifano ya kutazama mbali na lengo, au kushindwa kuzingatia Mwokozi leo?

Yakobo alitaka wale ambao wangesoma kumbukumbu yake wapate mtazamo tofauti kabisa na mtazamo wa Wayahudi ambao walikosa lengo. Soma Yakobo 4:4, na utambue kile Yakobo alitaka wote wale ambao wangesoma kumbukumbu yake wajue. Pia soma Yakobo 4:12, na uweke alama kishazi “kwa nini usizungumziwe upatanisho wa Kristo.” Kama ilivyoandikwa katika Yakobo 4:4–12, Yakobo alitoa sababu kadhaa kwa nini yeye aliamini katika Yesu Kristo na kwa nini alihisi ilikuwa ni muhimu kuwajulisha wengine Upatanisho.

  1. ikoni ya shajaraAndika marejeo ya maandiko yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko, na kisha uandike muhtasari mfupi wa kile Yakobo alifunza kuhusu Yesu Kristo au Upatanisho katika kila rejeo.

    1. Yakobo 4:4–6

    2. Yakobo 4:7–8

    3. Yakobo 4:9–10

    4. Yakobo 4:11

Ni maneno au vishazi gani katika Yakobo 4:4–6 vinavyoonyesha watu wa Yakobo walielewa asili ya Uungu?

Inaweza kusaidia kujua kwamba “mkabidhiwe kama malimbuko ya Kristo kwa Mungu” (Yakobo 4:11) inamaanisha kusimama mbele za Mungu wastahiki kuingia katika ufalme wa selestia. Pia, ni muhimu kuelewa kwamba ikiwa tuna “matumaini ya utukufu wa [Mwokozi]” (Jacob 4:4), ni sharti tuamini kwamba Yesu Kristo ametoa njia kwetu ya kukombolewa kutoka kwa dhambi zetu na kufufuliwa ili tuweze kurudi katika uwepo wa Baba yetu wa Mbinguni.

Ukweli mmoja tunaoweza kujifunza katika Yakobo 4 ni huu: Kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo, tunaweza kujazwa na matumaini na kujipatanisha wenyewe na Mungu.

  1. ikoni ya shajaraAndika majibu mafupi kwa yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Rejelea kweli kuhusu Yesu Kristo ulizojifunza katika Yakobo 4:4–12, na uchague mmoja ambao hasa unakupatia motisha wewe utake kuongea kuhusu Upatanisho. Andika ukweli huo, na elezea kwa nini umeuchagua.

    2. Ni sababu gani zingine za kibinafsi zinazokupatia motisha utake kusema kuhusu Yesu Kristo na Upatanisho”

Unapohitimisha somo hili, tafakati kwa nini wewe una shukrani kwa Mwokozi. Fikiria kushiriki sababu zako na mwana familia au rafiki wa karibu.

  1. ikoni ya shajaraAndika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi za leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza Yakobo 3–4 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningependa kushiriki na mwalimu wangu: