Utangulizi wa Enoshi
Kwa nini ujifunze Kitabu Hiki?
Kitabu cha Enoshi kinaonyesha uwezo wa Upatanisho wa Yesu Kristo wa kutakasa watu kutoka kwenye dhambi na kuwafanya wawe wazima. Enoshi alishindana mbele za Mungu katika maombi makuu kabla ya dhambi zake kusamehewa. Kisha aliomba kwa ustawi wa kiroho wa Wanefi na Walamani. Alitumia salio la maisha yake akifanya kazi kwa ajili ya wokovu wao. Unapojifunza kitabu cha Enoshi, unaweza kugundua masomo muhimu kuhusu maombi, toba, na ufunuo. Pia unaweza kujifunza kwamba watu wanapopokea baraka za Upatanisho, watakuwa na hamu ya kushiriki hizo baraka na wengine.
Nani Aliandika Kitabu Hiki?
Enoshi, mwana wa Yakobo na mjukuu wa Lehi na Saria, aliandika kitabu hiki. Enoshi aliandika kwamba baba yake alimfundisha “katika malezi na maonyo ya Bwana” (Enoshi 1:1). Karibu na mwisho wa maisha yake, Enoshi aliandika kwamba yeye alikuwa ametangaza “neno kulingana na ukweli ulio katika Kristo” (Enoshi 1:26) katika siku zake zote. Kabla ya kifo chake, Enoshi aliyakabidhi mabamba madogo ya Nefi kwa mwanawe Yaromu. Enoshi alihitimisha kumbukumbu yake kwa kufurahia katika siku ambayo angesimama mbele za Mkombozi wake. Alitangaza, “Kisha nitaona uso wake kwa furaha, na ataniambia: Njoo kwangu, heri wewe, umetayarishiwa mahali katika nyumba za Baba yangu” (Enoshi 1:27).
Kiliandikwa lini na wapi?
Enoshi alifunga kumbukumbu yake kwa kutangaza kwamba miaka 179 ilikuwa imepita tangu Lehi aondoke Yerusalemu (ona Enoshi 1:25). Hiyo inaweka tarehe ya kuandika kwake katika ya miaka 544 Kabla Kristo (wakati Yakobo alifunga kumbukumbu yake) na miaka 420 Kabla Kristo Enoshi aliandika kumbukumbu hii wakati akiishi katika nchi ya Nefi.