Seminari
Kitengo cha 31: Siku ya 3, Moroni 6


Kitengo cha 31: Siku ya 3

Moroni 6

Utangulizi

Moroni alikaribia mwisho wa maandiko yake kwenye mabamba kwa kuelezea baadhi ya viwango vya kuhitimu kwa mtu ili kujitayarisha kwa ajili ya ubatizo katika Kanisa. Kisha alieleza majukumu ambayo washiriki wa Kanisa wanayo ya kuwatunza washiriki wengine. Moroni pia alieleza kusudi la mikutano ya Kanisa na akahimiza umuhimu wa mikutano ya Kanisa kuongozwa na ushawishi wa Roho Mtakatifu.

Moroni 6:1–3

Moroni atoa masharti ya ubatizo

kijana akibatizwa

Fikiria una ndugu aliye na umri wa miaka saba ambaye atakuwa na miaka nane katika miezi michache. Wazazi wako wamekuuliza ufundishe somo la jioni la familia nyumbani juu ya jinsi ya kujitayarisha kwa ajili ya ubatizo.

  1. ikoni ya shajaraIkiwa ungefundisha somo hilo hivi sasa, ungefundisha nini ili kumsaidia ndugu yako kujitayarisha kwa ajili ya ubatizo? Andika fikra zako katika shajara yako ya kujifunza maandiko.

Baada ya kujumuisha sala za sakramenti katika kumbukumbu yake (ona Moroni 4–5), Moroni aliongeza maelezo kuhusu agizo la ubatizo. Pekua Moroni 6:1–3 , ukitafuta masharti ya ubatizo. Huenda ukataka kualamisha masharti ambayo umetambua katika maandiko yako.

Unafikiria inamaanisha nini kwamba wale waliotaka kubatizwa walikuwa walete “matunda yapasayo toba”? (Moroni 6:1).

Tafakari kile unafikiria inamaanisha kuwa na “moyo uliopondeka na roho iliyovunjika” (Moroni 6:2) kabla ya kubatizwa. Kama ilivyoandikwa katika Moroni 6:1–3, Moroni alieleza kwamba kupitia ubatizo tunaahidi kuchukua juu yetu jina la Yesu Kristo na kumtumikia hadi mwisho.Unafanya nini ili kudumisha na kuimarisha azimio lako la kumtumikia Yesu Kristo?

  1. ikoni ya shajaraKatika shajara yako ya kujifunza maandiko, elezea baadhi ya njia ambazo umejaribu tangu ubatizo wako kudumisha na kuimarisha azimio lako la kumtumikia Yesu Kristo.

Moroni 6:4

Moroni aeleza jinsi ya kuwatunza na kuwalisha kiroho washiriki wa Kanisa

Baada ya kueleza masharti ambayo watu binafsi wanapaswa kufikia kabla ya kubatizwa, Moroni kisha alieleza jinsi wale ambao walibatizwa hivi karibuni walibaki waaminifu kwa maagano yao. Soma Moroni 6:4, na utafute kile kilichofanywa ili kuwasaidia waongofu wapya kubaki waaminifu.

Fanya muhtasari kile umejifunza kutoka Moroni 6:4 kuhusu majukumu yako kwa washiriki wengine wa Kanisa.

Ni baraka gani Moroni 6:4 inaonyesha itakuja kutokana na kulishwa na neno la Mungu?

Ukweli moja muhimu unaofunzwa katika Moroni 6:4 ni kwamba tunalo jukumu la kuwakumbuka na kuwalisha kiroho waumini wengine wa Kanisa.

Mzee Jeffrey R. Holland wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alishuhudia juu ya umuhimu wa kulishana na neno la Mungu: “Watu wengu huwa hawaji Kanisani wakitafuta tu kweli chache za injili ama kuonana na marafiki wa zamani, ingawa hayo yote ni muhimu. Huwa wanakuja wakitafuta tukio la kiroho. Wanataka amani. Wanataka imani yao iimarishwe na tumaini kufanywa upya. Wanataka, kifupi, kulishwa na neno jema la Mungu, kuimarishwa na nguvu za mbinguni. Wale miongoni mwetu wanaochaguliwa kuzungumza ama kufundisha ama kuongoza wana wajibu wa kusaidia kutoa hayo, vyema tuwezavyo” (“A Teacher Come from God,” Ensign, Mei 1998, 26).

Je, umewahi kufikiria kuhusu idadi kubwa ya watu ambao wamekuombea, wametayarisha masomo kwa ajili yako, wamekuhimiza wewe na ushiriki wako Kanisani, na kukusaidia kupita changamoto?

  1. ikoni ya shajaraKatika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika takribani watu wawili ama watatu ambao wamekukumbuka katika njia ya maana ama kukulisha kiroho.

Hivi karibuni, jadili na mwanafamilia ama rafiki jinsi umebarikiwa kwa sababu mtu alikukumbuka ama alikulisha na neno la Mungu.

Rais Henry B. Eyring wa Urais wa Kwanza alisimulia hadithi ya shemasi katika kata yake ambaye alielewa umuhimu wa kutekeleza jukumu lake kwa washiriki wengine wa jamii yake:

Rais Henry B. Eyring

“Mmoja wa washiriki wa akidi yake aliishi karibu na nyumba yangu. Huyo mvulana jirani hakuhudhuria kamwe mkutano wa jamii ama kufanya chochote pamoja na washiriki wa akidi yake. Babake wa kambo hakuwa muumini wa kanisa, na mamake hakuhudhuria kanisa.

“Urais wa jamiii yake ya shemasi ulikutana katika baraza Jumapili moja asubuhi. Katika mkutano wao wa urais, wachungaji hao wenye umri wa miaka 13 walimkumbuka mvulana ambaye kamwe hakuja. Walizungumza kuhusu vile alihitaji kile walichopokea. Rais alimteua mshauri wake afuate kondoo huyo aliyetanga.

“Nilimjua mshauri huyo, na nilijua alikuwa mwenye haya, nilijua ugumu wa jukumu hilo, hivyo basi nilitazama kwa mshangao kupitia dirisha langu la mbele mshauri akijikokota kupita nyumba yangu, akienda njiani hadi nyumba ya mvulana ambaye kamwe hakuja kanisani. Mchungaji alikuwa na mikono yake mifukoni mwake. Macho yake yalikuwa chini. Alitembea pole pole, jinsi ungetembea ikiwa haungekuwa na uhakika ulikuwa unataka kufika ambapo ulikuwa unaenda. Kwa muda wa dakika 20 hivi, alirudi njiani na shemasi aliyekuwa amepotea akitembea kando yake. Tukio hilo lilirudiwa kwa Jumapili zingine chache. Kisha kijana ambaye alikuwa amepotea na kupatikana alihama.

“ Miaka baadaye, nilikuwa katika mkutano wa kigingi, bara ya mbali na chumba ambapo urais ulikuwa umekutana katika baraza. Mwanaume mwenye nywele za kijivu alinijia na kusema kwa kimya, ‘Mjukuu wangu aliishi katika kata yako miaka iliyopita.’ Kwa upole, aliniambia kuhusu maisha ya kijana yule. Na kisha akauliza ikiwa ningeweza kumpata shemasi yule aliyetembea polepole katika barabara ile. Na aliuliza ikiwa ningeweza kumshukuru na kumwambia kwamba mjukuu wake, sasa akiwa amekuwa mwanaume, alikumbuka bado” (“Watch with Me,” Ensign, Mei 2001, 38–39).

Zingatia watu binafsi ambao Bwana angetaka ‘uwakumbuke’ ama ‘uwalishe.” Panga njia ambayo unaweza kusaidia kuwalisha kiroho. Andika majina yao kwenye kipande cha karatasi, na kiweke mahali ambapo patakusaidia kuwakumbuka.

Moroni 6:5–9

Moroni aeleza madhumuni ya mikutano ya Kanisa na jinsi inapaswa kuongozwa.

Fikiria wewe ni mzazi wa kijana ambaye, kwa wiki chache iliyopita, amesema kwamba hataki kwenda kanisani kwa sababu kunaonekana kutokuwa na maana na kuchosha. Zingatia kile huenda ukasema ili kusaidia kumhimiza mtoto wako ahudhurie kanisa na aelewe sababu sahihi za kuhudhuria kila mara.

Katika kumbukumbu yake, Moroni aliongozwa kueleza sababu za washiriki wa Kanisa kukutana pamoja katika siku zake. Jifunze Moroni 6:5–6, na utafute jinsi unaweza kukamilisha kauli ifuatayo Kama washiriki wa Kanisa, tunapaswa tukutane pamoja kila mara ku .

Mzee Dallin H. Oaks wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alishiriki sehemu ya barua kutoka kwa rafiki aliyeelezea mabadiliko katika mtazamo kuhusu kuhudhuria kanisa:

Mzee Dallin H. Oaks

“Rafiki mwenye hekima aliandika:

“Miaka iliyopita, nilibadilisha mtazamo wangu kuhusu kwenda kanisani. Siendi kanisani tena kwa ajili yangu, ila kuwafikiria wengine. Mimi hujitahidi kuwasalimia watu ambao huketi peke yao, kuwakaribisha wageni, kujitolea kwa kazi yoyote. …

“Kwa kifupi, mimi huenda kanisani kila wiki na nia ya kushughulika, si kuwa baridi, na bali kufanya tofauti mzuri katika maisha ya watu. Kwa sababu hiyo, mahudhurio yangu katika mikutano ya Kanisa yanafurahisha zaidi na yanakamilisha.’

“Haya yote yanaonyesha kanuni ya milele kwamba tunafurahia zaidi na kukamilisha tunapotenda na kuhudumu kwa kile tunachotoa, si kwa kile tunachopata” (“Unselfish Service,” Ensign au Liahona, Mei 2009, 96).

Huenda ukakamilisha kauli iliyo hapo juu na baadhi ya mawazo yafuatayo.

Kama waumini wa Kanisa, tunapaswa tukutane pamoja kila mara ili:

  • Kufunga na kusali.

  • Kuimarishana kiroho.

  • Kupokea sakramenti kwa ukumbusho wa Bwana Yesu Kristo.

Waza juu ya matukio ambayo umekuwa nayo ambayo yalikufunza umuhimu wa kusali ama kufunga pamoja na washiriki wa kata ama tawi lako.

familia katika mkutano wa sakramenti
  1. ikoni ya shajaraJibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Utawezaje kupata mabadiliko kanisani ukihudhuria na nia ya kuimarisha wengine kiroho?

    2. Kwa nini ni muhimu kupokea sakramenti kila mara kwa ukumbusho wa Yesu Kristo?

    3. Kwenda kanisani kwa madhumuni yaliyoorodheshwa hapo awali kunawezaje kusaidia “kukuweka katika njia nzuri”? (Moroni 6:4).

Soma Moroni 6:7–8, na utafute yale ambayo waumini wa Kanisa katika siku za Moroni walikuwa “waangalifu” ama vingine, yale waliyopatia usikivu maalum. Kwa nini unadhani ni muhimu kwamba tufundishane na kuhimizana kuepuka na kutubu dhambi?

Moroni ashuhudia kwamba kwa mara nyingi tunapotubu na kuomba msamaha na kusudi halisi, tutasamehewa. Huenda ukataka kualamisha ukweli huu katika Moroni 6:8.

Moroni alikamilisha mlango huu kwa kufundisha jinsi mikutano yetu ya Kanisa inapaswa iongozwe. Soma Moroni 6:9, na utambue ni nani anapaswa aongoze mikutano yetu Kanisani. Fikiria kuhusu wakati ambapo ulikuwa makini hasa wa mwongozo wa Roho Mtakatifu wakati wa mkutano wa Kanisa.

Kanuni kuwa mikutano ya Kanisa inapaswa iongozwe na nguvu ya Roho Mtakatifu inawezaje kutumika kwako? Ikiwa ungeulizwa kutoa hotuba ama kufundisha somo wakati wa mkutano wa Kanisa, unawezaje kuhakikisha kwamba kile ambacho unasema kinachangia mwongozo na ushawishi wa Roho Mtakatifu wakati wa mkutano huo?

  1. ikoni ya shajaraKatika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika mpango wa jinsi utakavyochukulia mikutano yako ya Kanisa Jumapili hii ijayo. Huenda ukataka kujumuisha njia za kualika Roho Mtakatifu katika kuabudu kwako na jinsi huenda ukaweza kukumbuka na kulisha wengine kupitia kuhudhuria kwako.

  2. ikoni ya shajaraAndika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza Moroni 6 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningetaka kushiriki na mwalimu wangu: