Seminari
Kitengo 4: Siku ya 4, 1 Nefi 18–19


Kitengo 4: Siku ya 4

1 Nefi 18–19

Utangulizi

Kufuatia maelekezo ya Bwana, Nefi na familia yake walimaliza kujenga merikebu na kusafiri kwenda nchi ya ahadi. Wakati wa safari yao, wengi kwenye merikebu, wakiongozwa na Lamani na Lemueli, waliasi. Kama matokeo, Liahona ilisita kufanya kazi na dhoruba kali ilitishia maisha ya kila mmoja kwenye chombo. Baada ya waasi kutubu na Nefi kuomba kwa imani, Liahona ilianza kufanya kazi na Bwana akaituliza dhoruba na tena kuelekeza safari yao. Baada ya kuwasili katika nchi ya ahadi, Nefi aliwasihi familia yake kumkumbuka Mwokozi na kulinganisha maandiko na wao wenyewe. Unapojifunza 1 Nefi 18–19, fananisha uzoefu wa Nefi wa kukabiliana na majaribio na changamoto za kukabiliana na majaribio yako. Tafuta kufuata mfano wa Nefi.

1 Nefi 18:1–8

Familia ya Lehi inajiandaa kusafiri hadi nchi ya ahadi

Kwa nini ni muhimu kufanya kazi kwa bidii na kutafuta maelekezo kutoka kwa Bwana? Nefi alionyesha vipi sifa hizi zote wakati alipokuwa akijenga merikebu? Soma 1 Nefi 18:1–8.

  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, orodhesha maneno yote na vishazi katika 1 Nefi 18:1–8 vinavyoonyesha jitihada iliowekwa na Nefi na familia yake. Kisha tambua maneno yote na vishazi vinavyoonyesha jinsi Bwana alivyowaelekeza na kuwasaidia. Ni uhusiano gani unaona kati ya Juhudi za Nefi na usaidizi aliopata kutoka kwa Bwana?

Uzoefu wa Nefi unatuonyesha kwamba ili kutimiza kile ambacho Bwana ameamuru, tunahitaji kutafuta usaidizi Wake na kuweka mbele juhudi zetu.

  1. Fikiria kuhusu hali yako sasa ambapo unahitaji usaidizi wa Mungu. Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko kile unaweza kufanya ili kutafuta mwongozo wa Bwana na juhudi ambayo unaweza kuhitaji kufanya.

1 Nefi 18:8–25

Lamani na Lemueli waliongoza uasi kwenye merikebu ambao ulitatiza safari hadi nchi ya ahadi

Tunapopitia majaribio na matatizo katika maisha, ni kawaida kushangaa ni kwa nini tunapitia matatizo kama hayo. Pengine wewe au mtu mwengine unayemjua ameuliza “Kwa nini?” wakati wa hali ngumu.

Mzee L. Whitney Clayton wa Urais wa wale Sabini aligundua vyazo vitatu vya matatizo tunayopitia. Unaposoma, weka mstari chini ya vyanzo anazoelezea.

Picha
Mzee L. Whitney Clayton

“Katika hali ya kawaida, mizigo yetu huja kutoka kwa vyanzo vitatu. Mizigo fulani ni matokeo ya asili ya hali za ulimwengu tunamoishi. Ugonjwa, ulemavu wa kimwili, tufani, na mtetemeko wa nchi huja kutoka wakati hadi wakati kupitia makosa ambayo si yetu wenyewe. …

“Mizigo ingine inawekwa juu yetu kwa sababu ya makosa ya wengine. Udhalimu na uteja unaweza kuifanya nyumba kuwa chochote bali si mbinguni hapa ulimwenguni kwa wanafamilia wasio na hatia. Dhambi, desturi potovu, ugandamizaji, na jinai inatapaka kwenye waathiriwa katika mapito ya maisha. Hata makosa madogo kama masengenyo na ukatili yanaweza kuwaletea wengine mateso halisi

“Makosa na upungufu wetu wenyewe huzaa shida zetu nyingi na kuweka mizigo mzito kwenye mabega yetu wenyewe. Mzigo mzito [mgumu] sana tunaojitweka wenyewe ni mzigo wa dhambi. Sote tunajua majuto na uchungu ambao hakika hufuata kukosa kwetu kutii amri” (“That Your Burdens May Be Light,” Ensign or Liahona, Nov. 2009, 12–13).

Picha
Nefi alifungwa kwenye mlingoti

Baada ya Nefi na familia yake kuanza kusafiri hadi kwenye nchi ya ahadi, walipata matatizo mengi. Unapojifunza 1 Nefi 18, angalia aina moja ya mateso ambayo Mzee Clayton alieleza. Soma 1 Nefi 18:9–11, na utambue mifano ya chaguo baya zilizofanywa na watu wengine kwenye merikebu.

Ingawa sio vibaya kucheza densi, kusikiliza muziki, au kujiburudisha, 1 Nefi 18:9inaonyesha kuwa walifanya vitu hivi “kwa ujeuri mwingi” Neno ujeuri humaanisha lugha kali, chafu, au upotovu Shetani anaweza kutumia kucheza densi, muziki, au jinsi tunavyoongea ili kupotosha mioyo na akili zetu na kutufanya sisi kupoteza wenzi wa Roho Mtakatifu.

Kulingana na 1 Nefi 18:10, Nefi alihofia ni nini kingefanyika kama wale walioasi hawangetubu? .

Nefi alifanya nini kuihusu? Utafanya nini kama mwanafamilia au kiongozi wa Kanisa atakuuliza kubadilisha muziki unaosikiliza, njia unayocheza densi, au kukoma kutumia lugha chafu? Je, utakuwa tayari kusikia na kubadilika?

Soma 1 Nefi 18:12–14, 17–19, na utafute matokeo ya uasi wao. Ni kwa jinsi gani Nefi na wana familia wengine waliteseka kama matokeo ya matendo ya wengine? Tazama jinsi matendo ya waasi ya wengine yanaweza kuathiri uwezo wa kundi lote wa kupokea mwongozo kutoka kwa Mungu.

Matendo ya wale waasi yanatuonyesha kwamba dhambi huelekeza katika kuteseka kwetu wenyewe na wakati mwingine kwa wengine pia.

  1. Majaribio ya kawaida ambayo vijana wanapitia leo inajumuisha kukosa heshima kwa wazazi na viongozi, kudang’anya shuleni, kusengenyana, kuvalia vibaya, kuvunja amri ya usafi, kuvunja Neno la Hekima (sigara, pombe, na madawa), na kutazama ngono. Chagua moja au mawili ya majaribio hayo, na uandike katika shajara yako ya kujifunza maandiko jinsi kila moja linaweza kuathiri familia na marafiki wa mtu anayeruhusu majaribu.

Sehemu iliyobakia ya 1 Nefi 18 inatufunza jinsi tunaweza kufanya wakati matatizo yanapokuja, hata yakitokana na kufanya chaguzi mbaya au kutokana na kosa lisilo letu wenyewe. Soma 1 Nefi 18:15–16, 20–23, na uweke alama kwenye vishazi vinavyofunza kile kinapaswa kufanywa katika hali zote.

Kuna baadhi ya mafundisho na kanuni zilizoelezwa katika mistari hii. Baada ya kila taarifa zifuatazo, andika idadi ya mstari au mistari kutoka 1 Nefi 18:15–16, 20–23ambayo unahisi inaonyesha mfano wa ukweli huo:

  • Tunaweza kutegemea Mungu na kubakia waaminifu wakati wa majaribu yetu.

  • Maombi yanaweza kutusaidia kupata imani wakati wa majaribu yetu.

  1. Chagua mojawapo wa mistari uliotumia katika zoezi liliopita ambayo ni muhimu sana kwako, na ueleze katika shajara yako ya kujifunza maandiko kwa nini unaipenda. Jumuisha kile ulijifunza kutoka kwa mstari na kile ilikufundisha kuhusu kutatua matatizo. Ikiwa umeona mfano wa kile mstari huu unafundisha kwa maisha yako mwenyewe au maisha ya mwengine, andika juu yake vile vile.

Picha
Lehi na Watu Wake Wakiwasili katika Nchi ya Ahadi

licha ya matatizo yaliyowakabili, Nefi na familia yake hatimaye walifika nchi ya ahadi. Unapotafuta maelekezo ya Bwana na kufanya bidii kuyafuata, wewe pia unaweza kufanikiwa kukamilisha safari ambayo Bwana alikutuma duniani kutimiza.

Mzee L. Whitney Clayton alitoa ushuhuda huu:

“Bila kujali mizigo yetu tunayokabiliana nayo katika maisha kama matokeo ya hali za asili, makosa ya wengine, au makosa na upungufu wetu wenyewe, sisi sote ni watoto wa Baba wa Mbinguni wenye upendo, ambaye alitutuma hapa ulimwenguni kama sehemu ya mpango Wake wa milele kwa ukuaji na maendeleo yetu. Uzoefu wetu wa kibinafsi na kipekee unaweza kutusaidia sisi kujitayarisha kurudi Kwake. Taabu na mateso ambayo ni yetu, hata kama ni vigumu kustahimili, mwishowe, kwa mtazamo wa mbinguni, kwa ‘muda mfupi; na halafu, kama[tukistahimili] vyema, Mungu ata[tu]inua juu’[M&M 121:7–8]. Ni sharti tufanye kila kitu tunachoweza ili kubeba mizigo yetu ‘vyema’ bila kujali urefu wa ‘muda wetu mfupi’ wa kuibeba utadumu. …

“… Najua kwamba kama tutazishika amri za Mungu na maagano yetu, Yeye atatusaidia na mizigo yetu. Yeye hutuimarisha Wakati sisi tunatubu, Yeye hutusamehe na hutubariki kwa imani ya dhamiri na shangwe” (“That Your Burdens May Be Light,” 13–14).

1 Nefi 19

Nefi anaandika unabii kuhusu Yesu Kristo ili kutushawishi kumkumbuka Yeye.

Baada ya kuwasili katika nchi ya ahadi, Nefi alitoa unabii kuhusu ujio wa Mwokozi na jinsi atakavyopokelewa na watu Wake. Soma 1 Nefi 19:8–10, na utambue vishazi vinavyofundisha kuhusu asili na hulka ya Yesu Kristo.

  1. Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko jinsi kile ulichojifunza katika 1 Nefi 19:8–10kinaongeza upendo wako kwa Mwokozi.

Hitimisha somo la leo kwa kusoma 1 Nephi 19:18–19, 23 na uweke mstari chini ya kile Nefi alitamani kuwashawishi watu wake na wale wote wanaosoma Kitabu cha Mormoni kufanya. Tafuta fursa leo ya kushiriki ushuhuda wako wa Mwokozi na rafiki au mwanafamilia, au toa ushuhuda wako katika mazingira ya Kanisa. Kwa kufanya hivyo, unaweza kuwasaidia kukumbuka na kuamini katika Mkombozi wao.

  1. Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko njia ambayo kwayo unaweza kufuata mifano ya Nefi katika maisha yako mwenyewe.

  2. Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza1 Nefi 18–19 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha