Seminari
3 Nefi


Utangulizi wa3 Nefi

Kwa nini ujifunze Kitabu Hiki?

Unaposoma 3 Nefi, utajifunza kuhusu maneno ya Mwokozi na vitendo wakati wa huduma Yake miongoni mwa watu wa Kitabu cha Mormoni. Viongozi wa kanisa wametaja 3 Nefi kama “Injili ya tano” ya Bwana wetu kwa sababu, kama vile Injili nne za Agano Jipya, inalenga mafundisho ya moja kwa moja na huduma ya Yesu Kristo (ona Gordon B. Hinckley, “The Cornerstones of Our Faith,” Ensign, Nov. 1984, 52). Rais Ezra Taft Benson alifundisha kwamba “3 Nefi ina vifungu vingine vya kuvutia na vyenye nguvu katika maandiko yote. Inashuhudia juu ya Yesu Kristo, manabii Wake, na mafundisho ya wokovu” (“The Savior’s Visit to America,” Ensign, Mei 1987, 6). Katika kuona jinsi Yesu Kristo alivyoonyesha huruma kwa watu “mmoja mmoja” (3 Nefi 11:15; 17:21), unaweza kuelewa vyema haja Yake kwako kama mtu binafsi. Unaweza pia kujifunza masomo muhimu kwa kubainisha jinsi watu wengine walivyojitayarisha ili kukutana na Mwokozi wakati wengine wakijizuia kukutokana na kupitia baraka kubwa.

Nani Aliandika Kitabu Hiki?

Mormoni alifupisha rekodi kutoka kwa mabamba kubwa ya Nefi ili kutengeneza kitabu cha 3 Nefi. Kitabu kimeitwa kwa ajili ya Nefi, mwana wa Nefi, ambaye huduma yake iliendelea kwa vipindi kabla, wakati wa, na baada ya kutokea kwa Mwokozi kwa watu. Wakati wa uovu mkuu iliotangulia ziara ya Yesu Kristo, Nefi alifundisha “kwa uwezo na mamlaka” (3 Nefi 7:17). Hata hivyo huduma ya Nefi ilikuwa tu mwanzo wa huduma ya Yesu Kristo, ambaye maneno na matendo Yake yanajumuisha lengo kuu la 3 Nefi. Wakati akifanya ufupisho wake wa rekodi ya Nefi, Mormoni pia aliongeza ufafanuzi wake na ushahuda kwa kitabu hiki (ona 3 Nefi 5:8–26; 26:6–12; 29–30).

Kiliandikwa lini na wapi?

Rekodi asili zilizotumiwa kama vyanzo vya kitabu cha 3 Nefi yawezekana kuwa ziliandikwa kati ya 1 Kabla ya Kristo. na 34  Kabla ya Kristo. Mormoni alizifupisha rekodi hizo wakati fulani kati ya Baada ya Kristo. 345 na Baada ya Kristo  385. Mormoni hakuandika pale alipokuwa alipotunga kitabu hiki.