Seminari
Kitengo 25: Siku ya 2, 3 Nefi 13


Kitengo cha 25: Siku ya 2

3 Nefi 13

Utangulizi

Kama ilivyoandikwa katika 3 Nefi 13, Mwokozi aliendeleza mahubiri Yake katika hekalu, katika nchi ya Neema. Aliwaonya watu dhidi ya unafiki na kuwafundisha kwamba matendo yao ya haki itampendeza Baba wa Mbinguni. Pia alielekeza umati kujiwekea hazina mbinguni na kisha kuelekeza wanafunzi Wake kumi na wawili kutafuta ufalme wa Mbinguni kwanza kabla ya kuhofia juu ya masuala yao ya dunia.

3 Nefi 13:1–18

Mwokozi anaonya Wanefi dhidi ya unafiki na kuwafundisha kufanya matendo ya haki yanayompendeza Baba wa Mbinguni

Kamilisha tathmini binafsi yafuatayo katika akili yako kwa kuchagua ni kishazi gani ambayo inafafanua bora motisha yako kwa kutoa sadaka (kutoa kwa wengine), kuomba, na kufunga:

Natoa sadaka kwa sababu:

  1. Napaswa kutoa.

  2. Nampenda Bwana na kufurahia kusaidia watu wengine.

  3. Nataka wengine kufikiri vizuri juu ya yangu.

Naomba kwa sababu:

  1. Sitaki kusema “la” mbele ya watu wengine ninapoitwa kuomba.

  2. Ni sehemu tu ya mpangilio wangu wa kila siku.

  3. Nataka kuwasiliana na Baba yangu wa Mbinguni.

Nafunga kwa sababu:

  1. Kufunga kunanisaidia kumkaribia Bwana.

  2. Watu wengine watadhani mimi ni mbaya ikiwa sitafanya.

  3. Wazazi wangu hawanani ruhusu kula wakati napaswa kufunga.

Katika 3 Nefi 13, Yesu Kristo alifundisha umati wa Wanefi kuhusu umuhimu wa nia ya mtu kwa kutoa sadaka, kuomba, na kufunga. Majibu yaliotajwa katika tathmini binafsi hii yanaonyesha nia tofauti tulizo nazo kwa kufanya matendo haya au mengine ya ibada za kidini.

  1. Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Je, inajalisha ni kwa nini tunafanya matendo ya haki? Kwa nini au kwa nini haijalishi?

  2. Nakili chati ifuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko, na ikamalishe kwa kusoma kila marejeo ya maandiko na kujibu maswali mawili. Unaposoma, inaweza kuwa na manufaa kujua kwamba mnafiki ni mtu ambaye anavalia sura bandia ya haki au anayesema jambo moja na kufanya nyingine.

    Shughuli

    Ni nia gani ambayo Bwana alionya dhidi tunapofanya shughuli hii?

    Jinsi gani Bwana alisema tunapaswa kufanya shughuli hii?

    Toeni sadaka (3 Nefi 13:1–4)

    Omba (3 Nefi 13:5–6)

    Funga (3 Nefi 13:16–18)

Fikiria kuuliza maswali yafuatayo:

  • Jinsi gani nia yetu ya kufanya matendo ya haki huathiri jinsi tunavyoyafanya?

  • Ni nia gani za haki ambazo zinaweza kuvutia mtu kutoa sadaka, kuomba, au kufunga kwa siri?

Nia moja ya haki kwa kufanya mambo haya ni kumpendeza Baba wa Mbinguni. Soma 3 Nefi 13:4, 6, 18, na uangalie kile Bwana anaahidi wale ambao hutenda kwa haki faraghani.

Kanuni muhimu ambayo Mwokozi alifundisha katika mistari hizi ni: Tunapotenda haki kwa sababu tunampenda Baba wa Mbinguni, Atatuzawaia hadharani.

  1. Katika shajara ya kujifunza maandiko, andika kuhusu wakati ulipohisi kubarikiwa kwa kutafuta kufanya kitu ili kumpendeza Baba wa Mbinguni badala ya kuonekana na wengine.

Kwa ufupi hakiki utathmini yako binafsi mwanzoni mwa somo na tathmini nia yako kwa kutoa sadaka, kuomba, na kufunga. Fikiria jinsi unavyoweza kutumia mafundisho ya Mwokozi kuboresha nia yako kwa kufanya matendo haya au mengine ya ibada kwa Bwana.

Mwokozi alitoa mafundisho ya ziada kwa Wanefi kuhusu maombi. Soma 3 Nefi 13:7, na uangalie jinsi Bwana alivyoeleza vishazi vinavyorudiwa au vilivyofafanuliwa ambavyo vinaelezwa bila uaminifu katika maombi. Neno bureina maanisha tupu, bila mawazo au hisia. Marudio ya bure inaweza pia kumaanisha kurudia maneno yale yale ovyoovyo au kuomba bila imani.

  1. Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Kwa nini unafikiri ni muhimu kuepuka marudio ya bure katika sala zetu kwa Baba wa Mbinguni?

    2. Ni mambo gani unaweza kufanya ili kuepuka marudio ya bure unapoomba?

Soma 3 Nefi 13:8, na uangalie kanuni ambayo Yesu Kristo alisema juu ya Baba wa Mbinguni. Unaweza kutaka kwekea alama kanuni hii katika maandiko yako. Lengo moja la maombi yetu ni “kujipatia wenyewe na wengine baraka ambazo Mungu tayari anatoa ikiwa tutamwomba kwa imani” (Bible Dictionary, “Prayer”).

Picha
kijana akiomba

Soma 3 Nefi 13:9–15, na utafakari kile Bwana angetaka ujifunze juu ya maombi yako. Fikiria kuhusu njia za kuboresha maombi yako kwa kutumia yale uliyojifunza kutoka katika mafundisho ya Mwokozi.

3 Nefi 13:19–24

Yesu Kristo anafundisha umati kujiwekea hazina mbinguni

Umewahi kusoma au kusikia hadithi juu ya hazina iliopotea au kuzikwa? Wakati mwingine katika hadithi hizi wawindaji hazina hatimaye wafikia lengo lao kisha kugundua kwamba hazina haipo au haijakuwepo kamwe. Soma 3 Nefi 13:19–20, na utambue aina mbili ya hazina Bwana alizungumza kuhusu. Ni gani ya hazina hizo alisema itapatikana kwetu daima ikiwa tutaitafuta?

  1. Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Kuna tofauti gani kati ya “hazina duniani” na “hazina mbinguni”?

    2. Kutokana na kile ulichojifunza katika 3 Nefi 13:21–24, ni kweli gani ambazo Mwokozi alifundisha kuhusu kutafuta hazina ya duniani na hazina ya mbinguni? (Inaweza kukusaidia kuelewa zaidi mistari hizi ili kujua kwamba neno malini neno la kuipenda dunia au utajiri.)

    3. Jinsi gani kutafuta hazina hapa duniani kunaweza kutuvuruga kwa kutafuta hazina ya mbinguni?

Mwokozi hakufundisha kwamba fedha au mali ya kidunia ni maovu. Lakini alisisitiza umuhimu wa kuweka mioyo yetu juu ya hazina ya mbinguni ambayo itadumu na si juu ya utajiri wa kidunia.

Kanuni moja tuyonaweza kujifunza kutoka 3 Nefi 13:19–24ni: Ili kuwa na Mungu kama Bwana wetu, ni lazima tumpende na kumtumikia Yeye kuliko mambo ya dunia.

Ni baadhi gani ya mifano ya kujaribu kumtumikia Mungu na mali wakati moja? Ni kwa nini inaweza kuwa vigumu kumpenda na kumtumikia Mungu daima badala ya mambo ya dunia? Kwa nini kuweka Mungu kwanza inastahili juhudi?

  1. Soma mifano yafuatayo. Katika shajra yako ya kujifunza maandiko, onyesha ni bwana gani mtu anatumikia: Mungu au mali (ulimwengu).

    1. Kijana anakataa kazi ambayo itamhitaji kukosa mikutano yake ya Jumapili na badala yake anachagua kazi ya malipo ya chini isiomhitaji kufanya kazi siku za Jumapili.

    2. Msichana mara nyingi analalamika kwa wazazi wake kwa ajili ya haja yake ya nguo mpya. Mavazi anazotamani zinagharimu zaidi ya familia yake inaweza kumudu.

    3. Kijana analipa zaka yake mara kwa mara kwa pesa alizopata kutokana na kazi yake. Lakini anatumia mabaki ya mapato yake kununua vitu vya burudani, ikiwemo baadhi ya sinema na nyimbo zisizofaa, na hajahifadhi pesa za kulipa misheni au elimu.

    4. Msichana mara nyingi anatumia sehemu ya mapato yake kununua zawadi ndogo ndogo ili kuonyesha upendo wake kwa wengine.

3 Nefi 13:25–34

Mwokozi anaelekeza wanafunzi kumi na wawili kutafuta ufalme wa Mungu kabla ya matatizo yao ya kidunia

Picha
Wanefi Watatu

Walipoenda kuhudumu miongoni mwa watu, Yesu Kristo aliwaelekeza wanafunzi Wake kumi na wawili Wanefi wasiwe na wasiwasi juu ya mahitaji yao ya kidunia kwa chakula na mavazi (ona 3 Nefi 13:25–31). Soma 3 Nefi 13:32–33, na uangalie kile Mwokozi aliwaambia wanafunzi Wake juu ya mahitaji yao ya kidunia. Aliahidi nini wale ambao huweka Mungu na ufalme Wake kwanza katika maisha yao?

Kanuni tunayoweza kujifunza kutoka kwa mistari hizi inaweza kuwa: Tukitafuta ufalme wa Mungu kwanza, atatusaidia kukimu mahitaji yetu.

  1. Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Jinsi gani mtu “hutafuta kwanza ufalme wa Mungu”? 3 Nefi 13:33).

    2. Ni katika njia gani ambapo Bwana amehudumia mahitaji yako ulipomweka kwanza katika maisha yako?

Rais Ezra Taft Benson alishuhudia juu ya baraka zinazotokana na kuweka Mungu kwanza katika maisha yetu (unaweza kutaka kuandika dondoo hii kwenye karatasi na kuitunza katika maandiko yako ili kuipitia au kushiriki katika siku zijazo):

Picha
Rais Ezra Taft Benson

“Tunapoweka Mungu kwanza, mambo mengine yote huingia katika nafasi yao sahihi au kutoka nje ya maisha yetu. Upendo wetu wa Bwana utaongoza madai yetu ya upendo, mahitaji ya siku zetu, maslahi tunazotafuta, na utaratibu wa vipaumbele vyetu. …

“Tunapaswa kumpa Mungu, Baba wa roho zetu, utawala wa kipekee katika maisha yetu” (“The Great Commandment—Love the Lord,” Ensign, May 1988, 4–5).

Tafakari jinsi wewe au wale unajua wamebarikiwa kwa kuweka Mungu kwanza katika maisha yenu.

  1. Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza 3 Nefi 13 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha