Kitengo cha 9: Siku ya 2
2 Nefi 33
Utangulizi
Nefi alihitimisha kumbukumbu yake kwa kutangaza kwamba maneno yake yaliyoandikwa yanashuhudia Yesu Kristo na yanashawishi watu kutenda mema na kuvumilia hadi mwisho. Alisema kwamba ingawa aliandika “kwa unyonge,” ujumbe wake ulikuwa “wenye thamani kuu” na maneno yake “yatatiwa nguvu” kwa ajili ya wale ambao wangeyasoma (ona 2 Nefi 33:3–4). Alishuhudia kwamba maandiko yake yalikuwa “maneno ya Kristo” na kwamba watu wangewajibika kwa Mungu kwa mjibizo wao kwayo (ona 2 Nefi 33:10–15).
-
Katika somo lililopita, ulialikwa kujaribu “kusali kila mara” kwa masaa 24. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika mawazo na hisia zako kuhusu uzoefu wako.
2 Nefi 33:1–15
Nefi anaelezea madhumuni ya kuandika
Fikiria kwa muda mchache sababu za kwa nini wewe unataka Roho Mtakatifu kuleta ujumbe katika moyo wako.
Kuna tofauti gani kati ya ujumbe kwenda kwa moyo wa mtu na ujumbe kwenda ndaniya moyo wa mtu?
Soma 2 Nefi 33:1, na utafute ni neno gani—kwa au ndani—Nefi alitumia kueleza pale Roho Mtakatifu hubeba ujumbe hadi kwetu. Unaweza kutaka kuweka alama kile umepata.
Kwa nini unafikiri ni muhimu kwamba Roho Mtakatifu hubeba ukweli kwamioyo yetu wala si ndaniya mioyo yetu?
Mzee David A. Bednar wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alitoa kauli ifuatayo kuhusu 2 Nefi 33:1: “Tafadhali angalia jinsi nguvu za Roho hubeba ujumbe kwa bali si lazima ndani ya moyo. Mwalimu anaweza kueleza, kuonyesha, kushawishi, na kushuhudia, na kufanya hivyo kwa nguvu kubwa za kiroho na ufanisi. Hatimaye, hata hivyo, maudhui ya ujumbe na ushahidi wa Roho Mtakatifu hupenyeza ndani ya moyo kama tu mpokeaji anaukubali kuingia. Kujifunza kwa imani hufungua njia ndani ya moyo” (“Seek Learning by Faith,” Ensign, Sept. 2007, 61).
Mzee Gerald N. Lund, ambaye nyakati hizo alikuwa anahudumu kama mshiriki wa Sabini, alielezea kwa nini Roho Mtakatifu atabeba neno kwa, bali si ndani, ya mioyo yetu: “Kwa nini tu kwa moyo? Uwakala wa mtu binafsi ni mtakatifu sana kwamba Baba wa Mbinguni kamwe hataulazimisha moyo wa binadamu, hata kwa nguvu Zake zisizo na mwisho. Mtu anaweza kujaribu kufanya hivyo, bali Mungu hawezi kufanya hivyo. Tusema kwa njia ingine, Mungu huturuhusu sisi kuwa walezi, au walinda lango, wa mioyo yetu wenyewe. Sisi sharti, kwa mapenzi yetu wenyewe, tufungue mioyo yetu kwa Roho, kwani Yeye Hatajilazimisha Mwenyewe juu yetu” (“Opening Our Hearts,” Ensign or Liahona, May 2008, 33).
Unafikiria watu wanahitaji kufanya nini ili kufungua mioyo yao kwa Roho?
Soma 2 Nefi 33:2, na utambue kile hutokea wakati watu wanachagua kufanya mioyo kuwa migumu. Inaweza kusaidia kujua kwamba kishazi “vitu visivyofaa” humaanisha “kitu bure.”
-
Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko ni tabia na mitazamo gani unafikiria mtu aliye na moyo uliofunguka angeonyesha wakati wa kujifunza maandiko kibinafsi, na wakati wa masomo ya nyumbani ya seminari, na wakati wa mkutano wa sakramenti.
Katika 2 Nefi 33:1–2 tunafunzwa kanuni hii: Tunapo fungua mioyo yetu, ujumbe kutoka kwa Roho Mtakatifu zinaweza kuingia katika mioyo yetu.Unaweza kutaka kuandika kanuni hii katika maandiko yako.
-
Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko majibu kwa maswali yafuatayo:
-
Ni lini umehisi kwamba ujumbe wa injili umeingia moyoni mwako? Ilikuwa ni katika mazingira gani, na matokeo yake yalikuwa nini?
-
Je, hii inakuambia nini kuhusu moyo wako wakati huo?
-
Soma 2 Nefi 33:3–7, ukitafuta matumaini ya Nefi kwa wale ambao wangesoma maneno yake. Kisha kamilisha sentensi zifuatazo, ukitumia maneno yako mwenyewe au maneno ya Nefi. Kuwa na tahadhari kwamba vishazi vichache vinaweza kuwa na jibu zaidi ya moja:
2 Nefi 33:3—Nawaombea siku zote .
2 Nefi 33:4—Najua .
2 Nefi 33:6—Nafurahia .
2 Nephi 33:7—Nina .
Unapokamilisha kujifunza 2 Nefi 33, kumbuka kwamba aya hizi ni ushuhuda wa mwisho wa Nefi ulioandikwa katika maandiko. Soma 2 Nefi 33:10–14, na ufikirie unasikia maneno haya kutoka kwa Nefi mwenyewe. Unaweza kuweka mstari vishazi ambavyo vina maana kwako.
-
Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko baadhi ya vishazi hivi kutoka 2 Nefi 33:10–14 ambavyo vilikuwa na maana kwako, na uelezee kwa nini. Pia jibu swali lifuatalo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Ikiwa watu wanaamini katika Kristo watahisi vipi kuhusu Kitabu cha Mormoni? (Ona 2 Nefi 33:10.)
Soma 2 Nefi 33:15, na utafakari maneno ya mwisho ya Nefi: “Ni lazima nitii.” Unaweza kutaka kuandika “1 Nefi 3:7” kama marejeo mtambuko katika maandiko yako karibu na 2 Nefi 33:15. Rejelea 1 Nefi 3:7, na utambue jinsi aya hizi mbili zinavyohusiana.
-
Tumia dakika chache kurejea 1 Nefi and 2 Nefi, ukitambua mifano ya utiifu wa Nefi. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika baadhi ya mifano uliyopata. Pia tafuta kifungu cha kuenziwa au kilicho na maana ambacho kumekushawishi kufanya mema, kuwa bora, au kuamini katika Mwokozi, kama Nefi alivyosema (ona2 Nefi 33:1). Andika kifungu hiki katika shajara yako ya kujifunza maandiko.
Ushuhuda wa mwisho wa Nefi na maonyo yake kwa wale ambao wanaweza kukataa maneno yake yanaongeza uwajibikaji wetu kwa jinsi tunavyochukulia Kitabu cha Mormoni. Rais Joseph Fielding Smith alifunza kwamba, kama waumini wa Kanisa, tuna jukumu la kujifunza Kitabu cha Mormoni:
“Inaonekana kwangu kwamba muumini yeyote wa Kanisa hili kamwe hataridhika mpaka akisome Kitabu cha Mormoni tena na tena, na kukitilia maanani kabisa ili aweze kushuhudia kwamba hakika ni kumbukumbu yenye uongozi wa Mwenyezi juu yake, na kwamba historia yake ni ya kweli” (in Conference Report, Oct. 1961, 18). …
Hakuna muumini wa Kanisa hili anaweza kusimama kuthibitishwa katika uwepo wa Mungu ambaye hajakisoma Kitabu cha Mormoni kwa undani na makini” (in Conference Report, Oct. 1961, 18).
Una nafasi ya kuamua jinsi ya utakavyo yachukulia maneno ya Nefi na Kitabu cha Mormoni.
-
Tathimini juhudi zako za kujifunza Kitabu cha Mormoni, na uandike katika shajara yako ya kujifunza maandiko njia moja unaweza kuboresha kujifunza kwako.
Ili kuhitimisha somo hili, soma ahadi ya Rais Gordon B. Hinckley kwa wale wote ambao wanajifunza Kitabu cha Mormoni kwa bidii, “Bila kujali ni mara ngapi hapo awali umewahi kukisoma Kitabu cha Mormoni, itakuja katika maisha yenu na katika nyumba zenu kipimo cha ziada cha Roho wa Bwana, azimio thabiti la kutembea katika utiifu kwa amri Zake, na ushuhuda thabiti wa uhalisi hai wa Mwana wa Mungu” (“A Testimony Vibrant and True,” Ensign, Aug. 2005, 6).
-
Andika yafuatayo katika sehemu ya chini ya kazi za leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
Nimejifunza 2 Nefi 33na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).
Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningependa kushiriki na mwalimu wangu: