Seminari
Kitengo 23: Siku ya 4, Helamani 15–16


Kitengo 23: Siku ya 4

Helamani 15–16

Utangulizi

Wakati Samweli Mlamani alipowahutubia Wanefi kutoka juu ya ukuta katika Zarahemla, alibashiri kwamba isipokuwa watubu, Mungu “atawaangamiza kabisa”(Helamani 15:17). Alitangaza kwamba Walamani walikuwa wenye haki zaidi kuliko Wanefi na kwamba Bwana ataongeza muda wa siku za Walamani. Wanefi wengine waliamini mafundisho ya Samweli na wakabatizwa na Nefi. Wengine, ambao hawakuamini Samweli, walijaribu kumuua. Alilindwa kwa nguvu ya Mungu, naye akarudi mpaka nchi yake mwenyewe.

Helamani 15

Samweli anaonya Wanefi na kuelezea kwa nini Walamani walikuwa watu wa ahadi

Yafuatayo ni hali za kubuni za watu wawili vijana:

Kijana mmoja alilelewa na wazazi ambao hawakuwa waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho na hawakusisitiza mafundisho ya Yesu Kristo. Waliruhusu mwanao kijana kunywa pombe, mazoea aliyoendeleza katika chuo. Baadaye alikutana na baadhi ya wamisioari Watakatifu wa Siku za Mwisho. Baada ya kukutana na wamisionari mara chache, aliahidi kuachana na pombe. Siku chache baadaye alikuwa pamoja na kundi la marafiki. Wakampa kinywaji cha pombe.

Kijana mwingine alilelewa katika familia ya Watakatifu wa Siku za Mwisho. Wazazi wake walifanya jioni ya familia nyumbani na masomo ya familia ya maandiko mara kwa mara. Alikuza tabia ya kujifunza maandiko kila siku na sala ya binafsi. Alihudhuria “ masomo ya” Watoto, kuhudumu katika akidi za Ukuhani wa Haruni, na kuhitimu kutoka seminari. Alijua na kuelewa injili ya Yesu Kristo na amri za Mungu. Alipokuwa akihudhuria chuo alikuza urafiki upya. Usiku moja baadhi ya marafiki wakampa kinywaji cha pombe.

Fikiria kiwango cha uwezo wa kiroho ambao unaweza kutarajiwa kutoka kwa mojawapo wa vijana hawa wawili katika hali zao na jinsi inavyolinganishwa na Walamani na Wanefi unaojifunza kuhusu katikaHelamani 15.

  1. ikoni ya shajaraJibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Kulingana na Helamani 15:3, 17, hali ya kiroho ya Wanefi ilikuwaje?

    2. Kulingana na Helamani 15:4–8, hali ya kiroho ya Walamani ilikuwaje? (Neno uangalifu katika Helamani 15:5 ina maana ya “kuonya” au “uangalifu.”)

Ingawa Walamani walikuwa na historia ndefu ya uovu “kwa sababu ya uovu wa desturi ya babu zao,” Walipofikia ufahamu wa ukweli, walitubu na wakawa “imara na thabiti katika imani”(Helamani 15:4, 8). Wanefi, kwa tofauti, wakajawa na kiburi na kukataa ukweli wa injili.

Soma kwa makini Helamani 15:7–8, na ujaze pengo katika taarifa ifuatayo: Ujuzi wa ukweli na imani katika maandiko matakatifu inaelekeza kwa na , ambayo inaleta ; kwa hivyo, vile wengi wamekuja kwa ukweli huu .

Wakati Walamani walipojifunza ukweli kwa kusoma na kuamini maandiko, walikuza imani katika Yesu Kristo na wakaongozwa kwa toba. Waliona mabadiliko ya moyo na wakawa imara na thabiti katika imani.

kijana akiandika katika shajara
  1. ikoni ya shajaraJibu moja ya maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Ni lini mafunzo yako ya maandiko yamekusaidia kufanya mabadiliko zinazohitajika katika maisha yako?

    2. Je unafikiri ni kivipi tabia ya masomo aminifu ya maandiko inaweza kusaidia mtu kupokea mabadiliko ya moyo?

Mafundisho ya Samweli hutusaidia kuelewa umuhimu wa kubakia kweli kwa ujuzi na imani ambayo tumepokea. Soma Helamani 15:14–17, na uangalie vishazi vinavyoeleza kanuni za injili zifuatazo: Ikiwa watu watakuwa wasioamini baada ya kupokea utimilifu wa injili, watapata laana kubwa. Unaweza kutaka kuandika ukweli huu katika maandiko yako karibu na mistari. Pia unaweza kutaka kuandika M&M 82:3 kama marejeleo mtambuko kwenye ukingo wa maandiko yako.

Ni mafunzo gani ambayo kanuni hii itakuwa nayo katika maisha yako? Je kumekuwa na nyakati ulipotenda kwa kujua dhidi ya kile ulichojua kuwa cha kweli? Je, unahitaji kufanya nini ili kuimarisha imani yako katika Mwokozi, kutubu, na kuwa imara na thabiti katika kweli za injili?

Helamani 16

Wale ambao wanaamini Samweli wanabatizwa, wengine wanakaza mioyo yao

Tafakari jinsi kwa kawaida wewe huitikia maneno ya manabii hai na mitume. Wanefi walipewa fursa ya kupokea maneno ya nabii Mlamani Samweli. Tumia yale unayojifunza kutoka Helamani 16:1–7 ili kujaza chati ifuatayo ili kutambua ni watu gani waliamini na jinsi Wanefi walifanya.

Helamani 16

Je kundi hili la Wanefi waliamini?

Hawa watu walijibu kivipi maneno ya nabii Samweli?

Ndiyo

La

Mstari 1

Mstari 2

Mstari 3–5

Mstari 6–7

  1. ikoni ya shajaraJibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Kwa nini unafikiri baadhi ya vijana wanaweza kupata hasira na kukataa mashauri ya manabii leo?

    2. Ni lini umeona mtu akichagua kufuata ushauri wa nabii hata ingawa wengine wakiukataa?

    3. Ni lini ulipoamua kufuata ushauri wa nabii hata ingawa wengine karibu na wewe wakiukataa?

    4. Unajifunza nini juu ya maneno ya manabii katikaHelamani 16:13–14?

Rais Ezra Taft Benson

Tafakari taarifa ifuatayo kutoka kwa Rais Ezra Taft Benson kuhusu jinsi watu wa dunia husikia manabii wa siku za kisasa: “Nabii siyo lazima awe maarufu kwa dunia au na kidunia. Wakati nabii anapofunua ukweli, huwagawa watu. Mwaaminifu katika moyo hutii maneno yake, lakini mwovu hupuuza nabii au kupigana naye. Wakati nabii anapoonyesha dhambi za ulimwengu, walimwengu, badala ya kutubu dhambi zao, hutaka kufunga kinywa cha nabii au pengine kutenda kama kwamba nabii hayupo. Umaarufu kamwe si mtihani wa ukweli. Manabii wengi wameuawa au kutupwa nje. Tunapokaribia ujio wa pili wa Bwana, unaweza kutarajia kwamba jinsi watu wa dunia wanavyokuwa waovu zaidi, nabii atapoteza umaarufu kwao” (The Teachings of Ezra Taft Benson [1988], 133).

Soma Helamani 16:16–21 ili kugundua jinsi wasioamini walitetea kukataa kwao kwa utimilifu wa unabii na ishara kutoka mbinguni. Pengine unaweza kuwekea alama katika maandiko yako ni ipi kati ya sababu hizi na hoja dhidi ya manabiii unaoaamini ni ya kawaida katika siku zetu.

Soma Helamani 16:23, na uandike katika maandiko yako au shajara yako ya kujifunza maandiko madhara yanayofuata wale wanaokataa mashahidi wa Bwana. Taarifa yako inaweza kufanana na kanuni ifuatayo: Tunapokataa mashahidi wa Bwana, tunaruhusu Shetani kupata umiliki wa nyoyo zetu.

Na Rais Henry B. Eyring

Soma taarifa ifuatayo kutoka kwa Rais Henry B. Eyring ya Urais wa Kwanza, na alama yoyote ya maneno yake kwamba kuthibitisha kile ulichojifunza kutoka Helamani 16: “Tunapokataa ushauri utokao kwa Mungu, hatuchagui kuwa huru kutokana na ushawishi wa nje. Tunachagua ushawishi mwingine. Tunakataa ulinzi wa mwenye upendo mkamilifu, mwenye nguvu zote, Baba wa Mbinguni mwenye kujua yote, ambaye kusudi lake lote, kama lile la Mwanawe Mpendwa, ni kutupatia uzima wa milele, kutupatia yote anayo, na kuturudisha nyumbani tena katika familia kwa mikono ya upendo Wake. Katika kukataa shauri Lake, tunachagua ushawishi wa nguvu nyingine, ambao lengo lake ni kutufanya duni na ambao lengo lake ni chuki. Tuna wakala wa kimaadili kama karama ya Mungu. Badala ya haki ya kuchagua kuwa huru ya ushawishi, ni haki thabiti kujiwasilisha wenyewe kwa namna yoyote ya nguvu hizo tunazochagua” (“Finding Safety in Counsel,” Ensign, May 1997, 25).

Ni nini Rais Eyring alisema hutokea tunapokataa ushawishi wa Mungu katika maisha yetu? Kwa nini ni muhimu kuelewa kwamba tunapokataa ushawishi wa Mungu, tunapitia chini ya ushawishi wa Shetani?

Fikiria kama kuna njia yoyote kwa ambayo umekaza moyo wako dhidi ya ushauri uliotolewa na manabii na mitume. Inaweza kuwa na manufaa kuchambua kijitabu cha Kwa Nguvu ya Vijana unapofikiria juu ya kile vinavyofundisha na jinsi unavyokubali ushauri wao. Amua kile utafanya leo ili kuwa imara na thabiti katika kuishi injili na katika kutii ushauri wa manabii wa Bwana.

  1. ikoni ya shajaraAndika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza Helamani 15–16 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu: