Kitengo cha 5: Siku ya 3
2 Nefi 2
Utangulizi
Katika 2 Nefi 2, Lehi alimfunza Yakobo mwanawe kwa nini Baba wa Mbinguni amewaweka watoto Wake katika ulimwengu ambako mateso, huzuni, dhambi, na mauti yapo. Ili kumsaidia Yakobo kuelewa madhumuni ya maisha ya mauti, alielezea mafundisho ya kimsingi kuhusu mpango wa ukombozi—ikijumuisha wakala, Anguko la Adamu, na Upatanisho wa Yesu Kristo. Kujifunza kweli zilizofundishwa katika 2 Nefi 2 kunaweza kukusaidia kuthamini kikamilifu zaidi jinsi Upatanisho wa Yesu Kristo hushinda madhara ya Kuanguka na kumwezesha kila mmoja wetu kufanya chaguo ambazo zitatuelekeza kwenye uzima wa milele.
2 Nefi 2:1–25
Lehi anafunza kuhusu Kuanguka kwa Adamu na Upatanisho wa Yesu Kristo.
Fikiria kuhusu baadhi ya changamoto zilizokukabili hivi karibuni. Je! Umewahi kushangaa kwa nini maisha yana changamoto kama hizi? Unaposoma 2 Nefi 2:1, unaweza kutaka kuyaweka alama maneno au vishazi ambavyo Lehi alitumia kuelezea miaka ya mwanzoni ya Yakobo. Kisha soma 2 Nefi 2:2, na uweke alama kile Lehi alimwahidi Yakobo kingekuwa matokeo ya kuteseka kwake. Maana moja ya neno kuweka wakfu ni kutoa kwa kusudi jema au kufanya kuwa takatifu. Lehi anaonekana kumwahidi Yakobo kwamba Bwana atatoa kwa kusudi jema majaribu ya Yakobo kwa faida yake ya mwisho.
Lehi alimfunza Yakobo kuhusu umuhimu wa Kuanguka kwa Adamu na haja yetu ya Upatanisho wa Yesu Kristo katika mpango wa Baba wa Mbinguni. Alitaka Yakobo ajue kwamba Anguko na Upatanisho hutuwezesha sisi kutumia wakala wetu ili kwamba tuweze kukua na kuendelea hata uzima wa milele. Soma 2 Nefi 2:15–18, na uandike majibu mafupi kwa maswali yafuatayo:
-
Mungu alitoa nini kwa Adamu na Hawa katika Bustani ya Edeni ambacho kiliwaruhusu kutumia haki ya kujiamulia wao? (Ona 2 Nefi 2:15–16.)
-
Shetani alikuwa anatafuta nini katika Bustani ya Edeni? (Ona 2 Nefi 2:17–18.) Je! Unamwonaje Shetani akifuatilia kusudi hiyo hiyo leo?
-
Chora chati iliyo chini hapa katika shajara yako ya maandiko. Pekua 2 Nefi 2:19–25, na utambue ni matokeo gani ambayo yangekuwa kama Adamu na Hawa hawangekula tunda lililokatazwa na kuanguka, pamoja pia na matokeo ambayo yalitokea kwa sababu ya Kuanguka.
Kama Adamu na Hawa hawangeanguka (2 Nefi 2:22–23) |
Kwa sababu Adamu na Hawa walianguka (2 Nefi 2:19–20, 25) |
---|---|
Baada ya kukamilisha chati, fikiria kwa nini Kuanguka kwa Adamu na Hawa ni sehemu muhimu ya mpango wa furaha wa Baba wa Mbinguni.
-
Tuseme rafiki anakuambia kwamba Adamu na Hawa walifanya makosa kwa kula tunda lililokatazwa. Ukitumia kile ulichojifunza katika 2 Nefi 2:19–25, andika aya katika shajara yako ya maandiko ukielezea kwa nini Kuanguka kulikuwa muhimu katika mpango wa Baba wa Mbinguni kwa wokovu wetu.
Ilhali Kuanguka kwa Adamu na Hawa kulifungua njia kwetu ya kuendelea, pia kulileta matokeo mengine. Kabla ya Kuanguka, Adamu na Hawa walikuwa katika uwepo wa Mungu katika Bustani ya Edeni; baada ya kula tunda lililokatazwa, iliwabidi waondoke kutoka kwa uwepo Wake.
Soma 2 Nefi 2:5, na utambue kishazi ambacho kinaonyesha kutengana kwa Adamu na Hawa kutoka kwa Mungu baada ya Kuanguka. “Sheria ya muda” inalenga sheria za kimwili ambazo zilianza kutumika kama matokeo ya Kuanguka. Kwa hivyo, “kutengwa” kulingana na “sheria ya muda” hulenga hali ya maisha ya muda hapa duniani ambayo tunarithi kama wazao wa Adamu na Hawa. Kwa sababu ya sheria hizi, sisi hutengana kimwili kutoka uwepo wa Mungu na tunakuwa wenye kupatwa na huzuni, maumivu, mateso, na kifo kimwili. “Kutengwa” kulingana na “sheria ya kiroho” hulenga kutenganishwa kutoka kwa uwepo wa Mungu kwa sababu ya dhambi zetu.
Tafakari jinsi wewe binafsi umepatwa na matokeo haya ya Kuanguka kwa kuakisi maswali yafuatayo:
-
Ni mateso gani, machungu gani, na huzuni gani wewe umepata katika maisha haya?
-
Ni nani unayemjua ambaye amekufa? Je! Kifo cha mtu huyu kimekuathiri vipi?
-
Ni wakati gani umehisi kutenganishwa kiroho na Mungu?
Unaposoma 2 Nefi 2:6–10, unaweza kutaka kuweka alama kwenye maneno au vishazi muhimu ambavyo vinaonyesha kwamba kupitia kwa Upatanisho, Yesu Kristo hutukomboa kutokana na madhara ya Kuanguka na kutoa ukombozi kutoka kwenye dhambi zetu. Katika 2 Nefi 2:9–10, neno kuomba dua humaanisha kutenda kwa manufaa ya mwingine.
Umahiri wa Maandiko—2 Nefi 2:25
Lehi alipokuwa akimfundisha Yakobo kuhusu Kuanguka kwa Adamu na ukinzani ambao tunapata katika maisha ya mauti, alisisitiza matokeo chanya ya Kuanguka kwa wanadamu wote.
-
Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
-
Kutokana na kile ambacho umejifunza kuhusu Kuanguka, inaletaje furaha kwa wanadamu?
-
Ni lini umejihisi na furaha kwa sababu ya matokeo chanya ya Kuanguka?
-
2 Nefi 2:11–18, 26–30
Lehi anafundisha kuhusu haki ya kujiamulia na matokeo ya chaguo zetu
Fikiria kuhusu chaguo muhimu ilikubidi ufanye hivi majuzi na yale matokeo ya muda mrefu ya chaguo hilo yanaweza kuwa. Lehi alifundisha watu wake umuhimu wa msingi wa haki ya kujiamulia katika mpango wa wokovu wa Baba wa Mbinguni. Ili kukusaidia kuelewa kwamba sisi tuna uhuru wa kuchagua uhuru na uzima wa milele au utumwa na kifo (ona 2 Nefi 2:27), kamilisha shughuli hii.
-
Andika kila taarifa ifuatayo inayotoka katika For the Strength of Youth ([kijitabu, 2011], 2–3) katika shajara yako ya kujifunza maandiko. Kisha, unaposoma kila mstari katika 2 Nefi 2:11–18, 26–29, tua na uandike nambari ya huo mstari baada ya taarifa unayofikiri inayohimili. Kila moja ya nambari ya mstari inafaa kuandikwa baada ya kila taarifa moja. Taarifa inaweza kutumika kwa zaidi ya mstari mmoja, na mstari unaweza kuhusiana na zaidi ya taarifa moja. Kama mfano, mstari umeandikwa katika taarifa ya kwanza—ukweli mmoja Lehi alifundisha katika 2 Nefi 2:16 ni kwamba sisi tumepewa uwezo wa kujitendea wenyewe.
-
“Baba wa Mbinguni amekupatia wakala, uwezo wa kuchagua baina ya kile kilicho sahihi na kilicho kibaya na kujitendea mwenyewe.” 2 Nefi 2:16
-
“Ukiwa hapa duniani, unatathiminiwa ili kuonekana kama utatumia wakala wako ili kuonyesha upendo wako kwa Mungu kwa kushika amri Zake.”
-
“Ingawa wewe una uhuru wa kuchagua njia yako ya kutenda, wewe hauna uhuru wa kuchagua matokeo.”
-
“Chaguo za dhambi huchelewesha maendeleo yako na hukuletea machungu na mfadhaiko.”
-
“Chaguo za haki huelekeza kwa furaha ya kudumu na uzima wa milele.”
-
Soma 2 Nefi 2:26–27. Una uhuru wa kuchagua nini? Soma 2 Nefi 2:28, na uweke alama kile kingine Mungu amekupatia ili kukusaidia “kuchagua uzima wa milele.” Tafakari chaguo ambazo umezifanya katika maisha yako mwenyewe ambayo yanaonyesha umechagua uzima wa milele.
Umahiri wa Maandiko—2 Nefi 2:27
Fanya bidii kukariri 2 Nefi 2:27, mstari wa umahiri wa maandiko. Uusome mara kadhaa, na kisha ufunge maandiko yako na utumie herufi ya kwanza ya kile neno katika mstari huu uliyopo chini na kujaribu kuukariri mwenyewe au kwa mshiriki wa familia. Rudia zoezi hili mpaka utakapohisi kwamba unaweza kulifanya vyema.
K h, w w u w; n w v v a n m k m. N w h k u n u w m, k y M m w w w, a k u n k, k n u n n z i; k a w w w n d k y.
-
Ukitumia tu herufi ya kwanza ya kila neno katika 2 Nefi 2:27 hapo juu, andika hiki kifungu cha umahiri wa maandiko katika shajara yako ya maandiko. Hakuna kuchungulia!
-
Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi za leo katika shajara yako ya maandiko:
Nimejifunza 2 Nefi 2 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).
Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningependa kushiriki na mwalimu wangu: