Seminari
Etheri


Utangulizi wa Etheri

Kwa nini ujifunze Kitabu Hiki?

Unaposoma kitabu cha Etheri, utajifunza kuhusu Wayaredi—kikundi cha watu waliosafiri hadi Ulimwengu wa Magharibi na kuishi huko kwa karne nyingi kabla ya kufika kwa watu wa Lehi. Kitabu hiki kitakusaidia ujifundisha kanuni muhimu kuhusu maombi, ufunuo, na uhusiano kati ya kuweka imani katika Yesu Kristo na kupokea ufahamu wa kiroho. Kitakusaidia pia kuelewa jukumu la manabii katika kuwashawishi watu watubu na matokeo yanayokuja kwa wale wanaomkataa Yesu Kristo na manabii Wake.

Nani Aliandika Kitabu Hiki?

Moroni alifupisha kitabu hiki kutoka mabamba 24 ya dhahabu yaliyoitwa mabamba ya Etheri. Kimeitwa kwa ajili ya nabii Etheri, aliyekuwa nabii wa mwisho wa Wayaredi na aliyeunda kumbukumbu ya historia yao (ona Etheri 15:33–34). Katika siku za Mfalme Mosia, baadhi ya watu wa Limhi waligundua mabamba ya Etheri walipokuwa wakitafuta nchi ya Zarahemla (ona Mosia 8:7–11; Etheri 1:2). Manabii Wanefi na wawekaji kumbukumbu walikabiahi mabamba ya Etheri hadi yakaja katika umiliki wa Moroni. Moroni alisema kwamba hakujumuisha “ile sehemu moja kwa mia” ya kumbukumbu katika ufupisho wake (Etheri 15:33).

Kiliandikwa Lini na Wapi?

Vyenzo hasili vilivyotumiwa kuunda kitabu cha Etheri viliandikwa karne nyingi kabla ya Moroni kutengeneza ufupisho wake. Kumbukumbu ya kwanza ya Wayaredi iliundwa wakati kaka ya Yaredi aliandika ono alilopokea kabla watu wake wavuke bahari (ona Etheri 4:1). Hakuna wawekaji kumubukumbu wengine miongoni mwa Wayaredi wanatajwa hadi Etheri (ona Etheri 13:3; 15:33). Moroni alifupisha kitabu cha Etheri (ona Mormoni 8:3–6; Moroni 10:1). Moroni hakusema alikuwa wapi alipotengeneza ufupisho, ingawa aliandika kwamba Wayaredi walikuwa wameangamizwa katika “nchi hii ya kaskazini”(Etheri 1:1), ikionyesha huenda alikuwa katika nchi ambapo waliangamizwa.

Chapisha